Feb 24, 2015
AZAM KUWAFUATA AL MERREIKH LEO USIKU
4:40 PM
MABINGWA watetezi wa ligi kuu ya
Tanzania bara na wawakirikishi kwenye michuano ya klabu bingwa barani
Afrika, Azam FC, leo wanatarajia kukwea pipa moja kwa moja kuwawinda Al
Merreikh katika mchezo wa marudiano huko Sudan.
Akizungumza na Shaffihdauda.com
Afisa habari wa Azam, Jafar Idd Maganga, amesema kuwa kikosi hicho
kitaondo katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere,
jijini Dar e salaam majira ya saa mbili usiku kwa ndege ya Kenya
Airways.
“Mipango imekamilika na leo usiku
tunatarajia kuondoka kwa usafri wa ndege ya Kenya, kikubwa tunajua
tunaenda kucheza mchezo wa marudiano, tumejiandaa tokazamani” Amesema
Jafar Idd.
Kama utakuwa na kumbukumbu,
kwenye mchezo wa kwanza kati y Azam FC na Al Merreikh uliopigwa Februari
15 katika Uwanja wa Chamazi, Dar es salaam, Wanalambalamba waliweza
kuibuka na ushindi wa bao 2-0 mabao yakifungwa na Didier Kavumbagu
pamoja na nahodha John Bocco.
Ili Azam FC iweze kusonga mbele
katika michuano hiyo, siku ya Jumamosi Februari 28 majira ya saa mbili
usiku ambapo mchezo huo ndio utaanza, Watanzania hao itawalazimu wapate
ushindi au sare.
MABINGWA watetezi wa ligi kuu ya
Tanzania bara na wawakirikishi kwenye michuano ya klabu bingwa barani
Afrika, Azam FC, leo wanatarajia kukwea pipa moja kwa moja kuwawinda Al
Merreikh katika mchezo wa marudiano huko Sudan.
Akizungumza na Shaffihdauda.com
Afisa habari wa Azam, Jafar Idd Maganga, amesema kuwa kikosi hicho
kitaondo katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere,
jijini Dar e salaam majira ya saa mbili usiku kwa ndege ya Kenya
Airways.
“Mipango imekamilika na leo usiku
tunatarajia kuondoka kwa usafri wa ndege ya Kenya, kikubwa tunajua
tunaenda kucheza mchezo wa marudiano, tumejiandaa tokazamani” Amesema
Jafar Idd.
Kama utakuwa na kumbukumbu,
kwenye mchezo wa kwanza kati y Azam FC na Al Merreikh uliopigwa Februari
15 katika Uwanja wa Chamazi, Dar es salaam, Wanalambalamba waliweza
kuibuka na ushindi wa bao 2-0 mabao yakifungwa na Didier Kavumbagu
pamoja na nahodha John Bocco.
Ili Azam FC iweze kusonga mbele
katika michuano hiyo, siku ya Jumamosi Februari 28 majira ya saa mbili
usiku ambapo mchezo huo ndio utaanza, Watanzania hao itawalazimu wapate
ushindi au sare.
STAND NA SIMBA ZAINGIZA MIL 31, MBEYA CITY, YANGA MIL 74
4:18 PM
Mchezo
uliokuwatanisha wenyeji timu ya Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage mjini
Shinyanga dhidi ya timu ya Simba umeingiza jumla ya Sh milioni 31.
Juma
la watazamaji 5,439 waliingia uwanjani kushuhudia mchezo huo, ambao timu ya
Stand imepata mgao wa tsh. 6,564,268.22 na Simba wakipata mgao wa tsh.
4,661,581.78.
VAT
(18%) tshs. 4,763,135.59 huku FA mkoa wakipata tsh.665,940.25, FDF tsh.
1,141,611.86, Bodi ya Ligi Sh 1,522,149.15, Gharama za mchezo tsh.
1,617,283.47, Uwanja tsh. 2,854,029.66, Gharama ya tiketi Sh 1,593,000,00,
FDF tsh. 2,921,000.00, TFF tsh.2,921,000.00
Katika
uwanja wa Sokoine mbeya jumla ya Sh 74,600.000.00, zilipatikana kutokana na
watazamaji 14,920 waliokata tiketi kushuhudia mchezo huo, VAT(18%)
tsh.11,379,661.02, CDRB (5%) Sh 3,730.000.00.
FDF Sh 5,222,000,00, TFF Sh 2,238,000.00, Uwanja Sh 7,804,550,85, Gharama za mchezo tsh 4,442,578.81,
Bodi ya Ligi Sh 4,162,427,12. Chama
cha soka mkoa (FA) Mbeya kimepata Sh1,821,061.86, FDF(TFF) Sh
3,121,820.34, wenyeji timu ya Mbeya city wakipata Sh 17,950,466.95 na
klabu
ya Yanga tsh. 12,747,438.98
RONALDO AINGIA KWENYE LIST YA MASHUJAA WA TATU REAL MADRID
4:09 PM
Mreno Cristiano Ronaldo
ni staa wa soka Duniani ambaye kutokana na ubora wake mara nyingi
kwenye kurasa za story za michezo huwa zinaandika kuhusu yeye.
Neema imeendelea kubaki upande wake, siku chache zilizopita ameongoza kikosi cha Real Madrid kwenye ushindi mzuri walioupata, goli 2-0 ambapo walikuwa wakicheza na timu ya Elche, leo Christiano Ronaldo anaingia kwenye taarifa nyingine ya kuwa staa ambaye anashika nafasi ya tatu kwa kuifungia timu ya Real Madrid magoli mengi zaidi katika historia ya soka la Hispania na timu yake pia.
Katika mchezo wa juzi Jumapili Ronaldo alihitimisha ushindi wao kwa kufunga goli la pili na kumfanya kufikisha jumla ya magoli 290.
Ronaldo ambaye pia mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or
ya mchezaji bora wa kiume wa mpira wa miguu kwa mara ya tatu ameshika
nafasi hiyo akiwa amecheza michezo 289 huku nafasi ya pili ikishikwa na Alfredo Di Stefano ambaye alicheza michezo 392 na kuwa na magoli 307 huku nafasi ya kwanza ikishikwa na Raul Gonzalez mwenye magoli 323 katika michezo 741.
MANDAWA, MSUVA WAMBANA MBAVU KAVUMBAGU
3:58 PM
Rashid Mandawa anamfukuzia kwa mabao Didier Kavumbangu |
MBIO za kuwania kiatu cha dhahabu cha ufungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara, zimezidi kunoga ambapo kwa sasa Rashid Mandawa wa Kagera Sugar na Simon Msuva wa Yanga wanamfukuza kwa kasi ya ajabu Didier Kavumbagu anayeongoza mbio hizo.
Kavumbagu hadi sasa ameshafunga mabao nane, wakati Mandawa na Msuva kila mmoja amecheka na nyavu mara saba, hivyo kuonekana kuwa katika nafasi nzuri ya kumpiku Mrundi huyo.
Kwa misimu miwili iliyopita, tuzo hiyo imekuwa ikichukuliwa na wachezaji wa kigeni, Kavumbagu akitaka kuendeleza wimbi hilo msimu huu.
Msimu wa 2012/13, tuzo hiyo ilichukuliwa na Muivory Coast Kipre Tchetche aliyeipora kutoka kwa mzawa John Bocco na msimu uliofuata, 2013/14, Amissi Tambwe wakati huo akiwa Simba (sasa Yanga), ndiye aliyeibuka kidedea.
Na kutokana na kasi ya Mandawa pamoja na Msuva, kuna uwezekano mkubwa wa kutwaa tuzo hiyo msimu huu, lakini iwapo Kavumbagu ambaye ameonekana kutokuwa na mzaha katika kucheak na nyavu, atateleza.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY, Madawa alisema lengo lake kubwa ni kuhakikisha anasaidia timu yake hiyo kufanya vizuri katika ligi pamoja na kuibuka mfungaji bora.
“sitaki kusema mengi lengo langu ni kuhakikisha nasaidia timu yangu inafanya vizuri huku nikiwanyamazisha wale wanaopenda kuzungumza,” alisema.
YANGA SC YAMUACHA COUTINHO SAFARI YA BOTSWANA
3:56 PM
Na Pince Akbarm DAR ES SALAAM
KIUNGO Andrey Coutinho raia wa Brazil hatakuwemo katika kikosi cha kikosi cha Yanga SC kinachoondoka kesho Dar es Salaam kwenda Botswana kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya BDF XI.
Yanga SC wanatarajiwa kuwa wageni wa BDF Ijumaa wiki hii katika mchezo wa marudiano, Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na Mbrazil huyo hayumo safarini kwa sababu ya majeruhi.
Yanga SC inatarajiwa kuondoka na msafara wa wachezaji 20 na viongozi saba mjini Gaborone, tayari kwa mchezo ambao tayari wanaongoza kwa mabao 2-0.
Andrey Coutinho hatakwenda Botswana kwa sababu ni majeruhi |
Maana yake, Yanga SC wanatakiwa japo kulazimisha sare ugenini ili kutinga Raundi ya Kwanza ya michuano hiyo.
Katibu wa Yanga Dk Jonas Tiboroha amesema kikosi chao kitaondoka na wachezaji wote waliopitishwa na kocha wao Hans Pluijm.
Tibohora ambaye pia kitaaluma ni kocha amesema kikosi chao kitaondoka na Ndege ya Shirika la Kenya tayari kwa mchezo huo wa kombe la Shirikisho utakaopigwa Ijumaa nchini humo ambapo Yanga itarejea Jumapili baada ya mchezo huo.
Wachezaji wanaitarajiwa kuondoka kesho ni Ally Mustafa ‘Barthez,’ Deo Munish ‘Dida, Mbuyu Twite, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondani, Rajab Zahir, Pato Ngonyani, Salum Telela, Dilunga, Haruna Niyonzima, Mrisho Ngasa, Simon Msuva,Amissi Tambwe, Kpah Sherman na Danny Mrwanda
ALICHOSEMA KOCHA WA SIMBA BAADA YA KUFUNGWA NA STAND UNITED
8:12 AM
Pamoja na kupoteza nafasi nyingi za kufunga, Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amesema kweli Ligi Kuu Bara ni ngumu.
Kopunovic amekubali hilo baada ya ile mechi waliyolala kwa bao 1-0 mjini Shinyanga dhidi ya wenyeji Stand United.
Ameiambia
SALEHJEMBE kwamba kulikuwa na makosa mengi kwa mwamuzi, pia wachezaji
wake kutotumia nafasi, lakini akasisitiza, ligi ni ngumu.
"Ukiangalia
mechi utaona tulicheza vizuri tu, lakini kuna makosa kadhaa ya sisi
kutotumia nafasi na hata mwamuzi hakuwa mzuri kwetu.
"Lakini bado naweza kusema ligi ni ngumu sana na ushindani uko juu. Kupoteza mechi hiyo na Stand, kweli imeniumiza.
"Najua hata wachezaji wameumia lakini ni suala la kuangalia mechi ipi inafuatia na nini cha kufanya," alisema Kopunovic.
MAMBO KUMI KUHUSU KOCHA WA MTIBWA SUGAR MECK MEXIME
7:35 AM
Jina lake linafanana na aliyekuwa Kocha wa Timu ya Tafa TZ, Marcio Maximo, yeye anaitwa Mecky Mexime,
amesikika kwenye show ya Mkasi, katika aliyoyaongea kuna haya kumi
kutoka kwake, safari yake kwenye soka, uchawi na soka, shule…
Hivi ndivyo safari yake kwenye soka ilivyoanza; “Tangu
shuleni nilikuwa madarasa ya chini lakini timu ya shule nilikuwa
nacheza.. Nikapata bahati ya kwenda Mtibwa, nilikuta watu kibao wako
kwenye majaribio, lakini nilivyofika jioni, asubuhi nimeenda ofisini
wakasema huyu tunamfahamu haina haja ya majaribio.. Asubuhi yake
nikasaini fomu nikapewa chenji kidogo tu, sio kama sasa hivi watu
wanapewa mahela makubwa“
Safari yake ya soka ilianzia Mtibwa kama mchezaji na ikaishia Mtibwa kama kocha; “Viongozi
wa Simba au Yanga tumekuja hivi tunaongea bwana tunakutaka.. lakini
kati yenu watatu mmoja ananipigia simu, ‘Mecky tumekaa kwenye mazungumzo
lakini mi’ naona wewe bora ubaki Mtibwa usije huku”
Kingine ni hiki cha umuhimu wa Makocha kusomea mpira; “Kusoma
ni muhimu zaidi kwa sababu unavyoenda kusoma unaambiwa mazoezi jinsi ya
kufanya.. wachezaji afya zao.. muda wa kupumzika.. Kila hatua unayoenda
na muda wa kupumzika either mrefu au mfupi..”
Nini kilimfanya amekuwa Kocha?; “Sikuwa na wazo la kuja kuwa mwalimu, Maximo ndio
alionipa kipindi kile nacheza timu ya taifa nilikuwa namsaidia mambo
mengi sana, alionna kipaji changu akanishauri akaniambia hapa bado
unacheza zikitokea kozi nenda hata mimi naweza nikakusapoti.
Nilipostaafu timu ya taifa lakini nikawa nacheza Mtibwa kozi zikatoka
nikawa naenda lakini huku bado nacheza”
Ishu ya wachezaji wa TZ kuwa na majina ya wachezaji wa nje; “Haya majina mashabiki ndio wanatoa huwezi kukataa, wewe mwenyewe huwezi tu ukajipa tu kwa mfano Nadir Haroub Cannavaro..”
Nafasi ya makocha wazawa kwenye timu za TZ; “Makocha
sisi wazawa kwanza sisi wenyewe tu hatuaminiani, halafu angalia nani
anaeleta Kocha, ana taaluma ile ya mpira au kwa sababu mtu ana helka
zake basi analeta Kocha.. Jana tu nimesoma gazeti ‘Matola afukuzwa
Simba’, Simba wamefanikiwa kwa sababu wana vijana wengi na yeye ndio
ambaye amewakuza, tunaenda Mapinduzi ‘Mzungu’ kaja sijui mechi tatu za
mwisho sijui.. wakachukua Ubingwa lakini timu alikuwa nayo Matola. Angalia Mbeya City ilifanya vibaya watu wakaleta kelele lakini angalia sasa hivi Mbeya City iko wapi..”
Imani za kishirikina na soka; “Mi’ sizani Mtanzania atokeze hapa hana imani hizo.. zipo watu hela wanaliwa kutokana tu na imani..”
Ana hiki cha kusema kuhusu mpira wa TZ; “Inatakiwa tuimarishe ligi yetu, tuhakikishe wachezaji wanaperform kwenye ligi yetu Tanzania na isiwe ligi ya magumashi.. akina Samatta wanatakiwa wawe wengi hapo tunaweza tukapiga hatua“
Anauchukuliaje utendaji wa viongozi TFF; “Uongozi
unajitahidi, siwezi kuzungumzia sana kwa sababu siko huko.. Mimi
nimechezea timu ya Taifa zamani ilikuwa ina shida sana tunakaa Salvation
army, mchezaji umelala juu wanapita wadudu wale nguchiro”