SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Feb 5, 2015

QATAR WAJIPANGA KWA GUARDIOLA

 Qatar Wajipanga Kwa Guardiola
Wenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2022, Qatar wameonyesha kuwa tayari kumuajiri meneja wa klabu bingwa nchini Ujerumani FC Bayern Munich, Josep "Pep" Guardiola i Sala.
Qatar wanatajwa kuwa katika hali ya kuhitaji kufanya kazi na meneja huyo kutokana na kuridhishwa na utendaji wake wa kazi tangu akiwa na FC Barcelona ambapo alipata mafanikio makubwa kwa kutwaa zaidi ya mataji kumi kwa kipindi kifupi.

Hata hivyo bado haijaelezwa viongozi wa shirikisho la soka nchini Qatar watakamilisha mpango huo lini, licha ya Guardiola kuendelea na mkataba wa kuwatumikia mabingwa wa Ujerumani kwa sasa.
Taarifa kutoka huko mashariki ya kati ilipo nchi ya Qatar, zinaeleza kwamba meneja huyo anapigiwa upatu wa kuajiriwa mapema kwa ajili ya kupata nafasi ya kukaa pamoja na wachezaji wa timu ya taifa ya nchi hiyo

kabla ya kuingia katika mikakati ya kuwania ubingwa wa dunia wa mwaka 2022.
Endapo ndoto za Qatar zitakuwa kweli, itakua ni mara ya kwanza kwa Guardiola kufundisha timu ya taifa tangu alipoanza shughuli za ukocha mwaka 2007, kwa kuinoa timu B ya FC Barcelona.

KISIGA ATOA YA MOYONI SIMBA, AWATAJA AMBAO WANAKALIBIA KUACHWA

SHABAN Kisiga amelitumia Mwanaspoti kuwaeleza mashabiki zaidi ya milioni 20 wa Simba ukweli wake wa rohoni wa nini hasa kinachoendelea na kilichomtoa kwenye timu hiyo.
Hata hivyo, alichosisitiza zaidi ni kwamba ilikuwa inamdhalilisha kwa kumkalisha benchi ila Mwanaspoti limepata habari za uhakika kutoka ndani kwamba kuna wachezaji wawili wakongwe nao watamfuata kiungo huyo.


Wachezaji hao ni kipa Ivo Mapunda (pichani) ambaye ndiye mchezaji pekee wa Simba aliyewahi kuwa askari akaacha kazi na beki Nasoro Masoud ‘Chollo’ ambao hata hivyo mikataba yao itamalizika mwishoni mwa msimu, huku Awadh Juma, Elius Maguri na Jonas Mkude wanadaiwa kuwa na nidhamu mbovu na wanachunguzwa kimya kimya.

Kisiga ambaye anaishi Yombo jijini Dar es Salaam, aliliambia Mwanaspoti kuwa alikuwa akivumilia hali hiyo kwa kuamini kwamba mambo yangebadilika, lakini haikuwa hivyo hata pale alipokuja kocha mpya Mserbia Goran Kopunovic ambaye aliendelea kumwingiza akianzia benchi.
Alisema anaamini kama Kopunovic (48), angekuwa ameachwa huru kupanga kikosi huenda angekuwa anapewa nafasi ya kucheza.

“Niliamua kuondoka kwa sababu niliona nadhalilika sana na kwa nini nifikie hatua hiyo? Mimi si mchezaji wa kupewa dakika 10 au tano kucheza, inaumiza sana hasa pale unapojua ni kwa nini hupangwi, yote haya yalikuwa yanatokea kwa chuki ya mtu jambo ambalo mimi huwa sikubaliani nalo,” alisema Kisiga ambaye amewahi kuichezea SC Villa ya Uganda.

“Hivyo ni vyema niondoke ili niwaachie wengine ambao wana nafasi ya kucheza kuliko kwenda kambini unakula na kulala bure halafu huchezi, najua hawaumii juu yangu kwani hata usajili wangu ni wa kawaida sana ukilinganisha na wachezaji wao waliowasajili kwa mamilioni ya fedha, lakini mimi nazingatia heshima yangu.”
Kiungo huyo mtaalamu wa kupiga faulo, alisema kuwa inasikitisha kuona mpira wa Tanzania kwa sasa unaendeshwa kwa fitina na si kuzingatia uwezo wa mchezaji husika ukoje.
“Najua hata kocha alipotua tu Zanzibar aliambiwa watu wa kuanza kuwapanga na wale wa kuanzia benchi, hizo ni fitina mbaya ambazo zinaua viwango vya wachezaji wengi hapa nchini, mpira hautaki majungu, uwezo wa mtu unaonekana uwanjani.

NYONI MAXIMO ALINIBADILISHA

 
MCHEZAJI wa Azam, Erasto Nyoni, amekuwa akicheza nafasi kadhaa kikosini humo na pia timu ya taifa,
Taifa Stars. Unamjua aliyempa uwezo huo ni nani? Amefichua kuwa ni kocha Marcio Maximo, aliyemhamisha kutoka kiungo na kuwa beki.
Nyoni alisema wakati Maximo anaifundisha Taifa Stars kati ya mwaka 2006 na 2010, ndipo alipobadilishwa nafasi kutoka kiungo mkabaji na kupelekwa kucheza beki wa pembeni.

Mchezaji Bora huyo wa Tuzo za Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (Taswa) mwaka jana, amekuwa akicheza beki wa kulia, kushoto, kati na pia kiungo jambo ambalo ni nadra kwa wachezaji wengine.
“Naweza kucheza beki wa pembeni kwa pande zote mbili, pia huwa nacheza beki wa kati na wakati mwingine nacheza kiungo na ninamudu nafasi zote hizo vizuri bila ya wasiwasi,” alisema.
 
“Maximo ndiye alinibadilisha wakati anaifundisha timu ya Taifa, mwanzoni nilikuwa nacheza kiungo mkabaji na sikuwahi kucheza beki,” alisema Nyoni.
Katika hatua nyingine, kocha wa Don Bosco, Kasongo Ngandu, amesema kikosi cha Azam kinacheza vizuri lakini umaliziaji wao ni mbovu jambo ambalo litaigharimu timu hiyo katika mechi kubwa.

Azam ilifungwa bao 1-0 na Don Bosco juzi Jumanne ikiwa ni mechi yake ya mwisho mjini hapa. Kikosi cha Azam kilirejea Dar es Salaam jana kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Morogoro.

Ngandu alisema: “Timu yao ni nzuri lakini ina tatizo katika ufungaji, umaliziaji wao siyo mzuri.
“Viungo wao wanatakiwa kucheza kwa kushambulia zaidi kuliko wanavyocheza sasa, wakiweza kurekebisha itakuwa bora kwao.”

FIFA YA IAGIZA SIMBA KUMLIPA MOSOTI

Simba SC imeagizwa kumlipa beki Donald Mosoti Omanwa takribani dola za Marekani 14 400 kwa kusitisha mkataba wa mchezaji huyo raia wa Kenya mwaka jana.
Kwenye barua ambayo imeandikwa na Shirikisho la Soka duniani, FIFA, Simba imeagizwa kulipa fedha hizo kwa siku thelathini zijazo pamoja na riba ya asilimia tano kwa malipo yake kwa mujibu wa uamuzi uliyoafikiwa na benchi la majaji watatu; Thomas Grimm kutoka Uswizi, Eirik Monsen wa Norway na Zola Majavu kutoka Afrika Kusini.
“Mshitakiwa, Simba SC, afaa kumlipa mdai, Donald Mosoti Omanwa, ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya taarifa ya uamuzi huu, malipo bora kwa kiasi cha USD 600 pamoja na 5% kama riba kwa mwaka kutoka Desemba 12, 2013,” ulisoma ujumbe uliotiwa sahihi na katibu mkuu Jerome Valcke wa korti hiyo (Dispute Resolutions Chamber).
 
“Mshitakiwa pia amlipe mdai ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya taarifa ya uamuzi huu, fidia ya USD 13 800 kwa uvunjaji wa mkataba pamoja na 5% kwa mwaka riba kutoka Septemba 16, 2014hadi tarehe ya ufanisi wa malipo.”
Hii ina maana kwamba beki huyo atatia kibindoni kitita cha zaidi ya shilingi million moja pesa za Kenya na zaidi ya milioni 19 pesa za Tanzania.

TUMBA SWEDI BEKI MZURI INGAWA HAITWI STARS

BEKI wa Coastal Union, Tumba Swedi ‘Mdudu Kiwi’ jana alinusurika kupewa kadi nyekundu timu yake ikimenyana na Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. 

Tumba, alimchezea rafu mshambuliaji wa Yanga SC, Kpah Sherman kipindi cha pili na refa Athumani Lazi wa Morogoro akapiga filimbi mpira utengwe upigwe kuelekezwa lango la Coastal.
Lazi hakuwa na dhamira ya kumpa kadi yoyote Tumba, kwa sababu ilikuwa faulo ya kawaida ya kumzibia njia Mliberia wa Yanga. Hata hivyo, pamoja na kutambua amefanya kosa kimchezo, lakini Tumba alimjia juu refa na kumtolea maneno makali.
Tumba akimtolea maneno makali refa Athumani Lazi jana Uwanja wa Mkwakwani
Tumba akionyeshwa kadi ya njano na Lazi
Faulo iliyosababisha yote hayo ni hii hapa

 
Lazi akamuita Tumba kwa ajili ya kumpa kadi, ambayo wazi ingekuwa ya njano, lakini beki huyo akaendelea kumfanyia ukaidi mwamuzi huyo, huku akimtolea maneno makali.
Ajabu, Lazi alikuwa mpole wakati akifokewa na beki huyo aliyeibukia akademi ya Azam FC, kabla ya kutolewa kwa mkopo Moro United, baadaye Ashanti United na sasa yupo katika msimu wake wa kwanza Coastal.
 
Refa huyo alikuwa ameweka mikono yake nyuma huku akimsikiliza kijana huyo akitoa maneno yake na kurusha mikono kama anayetaka kumuadhibu mwamuzi huyo.
Tukio hilo liliwafanya mashabiki wa Coastal wanyamaze kimya, wakihofia kinachofuatia kwa mchezaji huyo ni kadi nyekundu.
 
Lakini bahati nzuri iliyoje, baada ya vurugu zote Lazi alimpa kadi ya njano tu mchezaji huyo. Hata hivyo, Tumba alirudia kumtolea maneno makali refa huyo baada ya kadi kuashiria kwamba hakujali adhabu hiyo.
Inawezekana kabisa ikawa ni hasira iliyotokana na upinzani wa mchezo huo, lakini ukweli ni kwamba hakuna ambaye angeshangaa kama Lazi angemuonyesha kadi nyekundu beki huyo.
 
Matukio kama haya wamekuwa wakifanya wachezaji wengi katika soka ya Tanzania, lakini bahati mbaya ni kama makocha wao hawawakemei na ndiyo maana wamekuwa wakirudia.
Pamoja na kufundisha, kuongoza mazoezi, walimu wanapaswa kujua wana wajibu pia wa kuwafundisha nidhamu ya mchezo wachezaji wao. Wana wajibu wa kuwandaa kuwa wachezaji kamili katika soko.
 
Mchezaji kama Tumba, ni ambaye ameibukia kwenye mfereji mzuri kisoka, akianzia shule, akademi ya Azam FC ambako alikaribia kupandishwa kikosi cha kwanza chini ya kocha Muingereza Stewart Hall.
Walichoshindwana Tumba na Hall ni juu ya nafasi ya kucheza, kocha Muingereza akitaka kumuhamishia beki ya pembeni, kitu ambacho mchezaji huyo hakutaka na akaamua kuondoka.
 
Lakini Tumba akawa tegemeo la timu za vijana za taifa kuanzia U17 na baadaye U20, ingawa baada ya kutua Ashanti amepoteza bahati ya kuitwa timu za taifa.
Hakuna shaka kuhusu uwezo wa Tumba, ni beki ‘ngangali’, mwenye maarifa na uwezo wa hali ya juu. Anapiga mashuti ya mbali na kufunga na kwa ujumla ni mzuri hata kwenye kusaidia mashambulizi wakati wa mipira ya kona anaweza kufunga hadi kwa kichwa.
 
Lakini kitu kimoja tu, Tumba anapaswa kuangalia nidhamu yake mchezoni, inawezekana kwa namna moja au nyingine, inampunguzia mambo fulani fulani bila yeye mweneywe kujua.
Kwa mfano kwa sasa, pamoja na ubora wake amefungiwa vioo timu za taifa, inawezekana labda kwa tabia zake kama hizi walimu wanaamua kumchunia. 

HILI NDIO GARI JIPYA LA MSANII DIAMOND PLATNUMZ

Diamond 1Katika interview mbili nimewahi kumsikia Diamond Platnumz akitoa msemo mmoja unaofanana lakini katika hizo interview mbili tofauti, akitabasamu alisema ‘kama nafanya kazi kwa bidii ni lazima niishi vizuri pia, nipate ninavyotaka’

Kwa hii picha ya gari aliyopost Diamond kwenye instagram labda ndio anaendelea kutimiza ndoto zake? japokua hakuandika chochote baada ya kuiweka picha hii ya gari jipya lisilo na namba, baadhi ya mashabiki wameanza kumpongeza ila bado millardayo.com inaendelea kumtafuta ili tupate uhakika kama ndio mkoko wake mpy

MASAU BWIRE ASHINDA KESI


Kamati hiyo imeondoa malalamiko dhidi ya Ofisa Habari wa klabu ya Ruvu Shooting, Masau Bwire kwa vile refa Israel Mujuni Nkongo ambaye ni mlalamikaji hakufika kwenye shauri hilo.

Nkongo alimlalamikia Bwire akidai alitoa maneno yenye kuweza kuchochea chuki dhidi yake kwa waamuzi, kwani kupitia redio 100.5 Times FM, Bwire alidai refa huyo ndiye aliyeshinikiza kuondolewa kwa refa Mohamed Theofil kwenye ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).
Pia Kamati hiyo imemkuta bila hatia Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Singida (SIREFA), Gabriel Gunda ambaye TFF ilimlalamikia kuwa akiwa mtendaji mkuu wa chama hicho alishindwa kuhakikisha timu ya Singida inaingia uwanjani kucheza na Dodoma kwenye mechi ya Kombe la Taifa kwa Wanawake.
05 Feb 2015

CHEKI MESSI, SUAREZ, NEYMAR WALIVYONG'ARA KWENYE TANGAZO KIVINGINE


NYOTA WA BARCELONA, LIONEL MESSI, NEYMAR, LUIS SUAREZ, GERARD PIQUE NA ANDRES INIESTA WAMEONEKANA WAKIWA KATIKA MUONEKANO TOFAUTI KABISA KATIKA TANGAZO JIPYA LA BARCELONA WALILOLITENGENEZA. TANGAZO HILO NI LA SHIRIKA LA NDEGE YA QATAR AIWAYS INAYOIDHAMINI BARCELONA.




05 Feb 2015

EXCLUSIVE: BARAKA KIZUGUTO ATUA TFF



Baraka Kizuguto sasa ndiye atakuwa msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).


Mara ya mwisho, Kizuguto alikuwa msemaji wa klabu ya Dar Young African.

Habari za uhakika kutoka ndani ya TFF, zimeeleza Kizuguto amewapiga kumbo zaidi ya wasemaji kumi kushinda nafasi hiyo.

Pamoja na kuwa na taaluma ya uandishi wa habari Kizuguto ni mtaalamu wa masuala ya website.

ALICHOSEMA KOCHA AZAM BAADA YA KUMALIZA ZIARA DR CONGO


 
KOCHA Mkuu wa Azam FC, Mcameroon Joseph Marius Omog (pichani kushoto) amesema ziara ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ilikuwa ya mafanikio. 
 
Akizungumza jana jioni baada ya kurejea Dar es Salaam, Omog alisema kwamba japokuwa hawajashinda mechi, lakini wamepata faida kubwa katika michezo mitatu waliyocheza.
“Tulikuja huku kwa ajili ya kujifunza na tumecheza dhidi ya timu za kiwango cha juu, kilikuwa ni kipimo tosha cha tunavyoweza kucheza na mpinzani mgumu ugenini. Dhamira yetu imetimia,”amesema Omog.
 
Mcameroon huyo amesema sasa vijana wake wapo tayari kwa mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya El Merreikh ya Sudan wiki ijayo, baada ya mazoezi mazuri DRC.  
Azam FC juzi ilihitimisha ziara yake ya Lubumbashi, DRC bila ya ushindi baada ya kufungwa bao 1-0 Don Bosco ya Kinshasa Uwanja wa TP Mazembe mjini humo.
 
Awali, mabingwa hao wa Tanzania Bara, walilazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na ZESCO United ya Zambia mabao yake yakifungwa na kiungo Frank Domayo. Mchezo wa kwanza, Azam FC walifungwa 1-0 na wenyeji wao, TP Mazembe.
 
Baada ya kurejea Dar es Salaam jana, Azam FC watakuwa kambini kwao, Azam Complex, Chamazi hadi Jumamosi watakaposafiri kwenda Morogoro kumenyana na Polisi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Wakitoka Morogoro, Azam FC watarejea nyumbani kucheza mechi nyingine ya Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar na baada ya hapo wataingia kwenye maandalizi ya mwisho kwa ajili ya BDF.  

MAGAZETI YA MICHEZO LEO ALHAMISI FEBRUARY 5



.
.
DSC_0713
.

.
.
.
.
.
.
.
.
.

MAJANGA REAL MADRID


Kikosi cha Carlo Ancelotti kiliifunga Sevilla mabao 2-1 kuendelea kuongoza kwa pointi nne zaidi La Liga, na sasa wanaelekeza nguvu zao kwa wapinzani wao wa jiji la Madrid, wakiwakosa baadhi ya wachezaji muhimu.
James Rodriguez na Sergio Ramos wote walitolewa nje ndani ya dakika 25 Uwanja wa Bernabeu baada ya kuumia. Na taarifa imethibitisha Ramos ameumia nyama za paja, wakati maumivu ya Rodriguez ni makubwa, amevunjika mguu na atahitaji upasuaji. 
Real Madrid were dealt a blow on Wednesday when defender Sergio Ramos (right) seemed to pull a hamstring
Sergio Ramos (kulia) akiwa ameshika nyama za paja wakati anatoka jana

GERRAD APIGA MECHI 700 LIVERPOOL

KIUNGO Steven Gerrard amekuwa mchezaji wa tatu wa Liverpool kutimiza mechi 700 kihistoria baada ya kuichezea timu hiyo jana ikishinda 1-0 dhidi ya Bolton katika mechi ya marudio Raundi ya Nne ya Kombe la FA.
Nahodha huyo wa Liverpool, alirejeshwa kwenye kikosi cha kwanza na kocha Brendan Rodgers, na kuingia kwenye orodha ya Ian Callaghan na Jamie Carragher walioichezea pia mechi 700 klabu hiyo.
Gerrard, ambaye maisha yae yote amecheza Liverpool tu, alifurahia mafanikio yake hayo kwa kuvaa kiatu maalum kilichoandikwa 700 nyuma pamoja na majina ya mabinti zake, Lilly na Lexie.
Steven Gerrard made his 700th Liverpool appearance on Wednesday night in their game against Bolton
Steven Gerrard amecheza mechi ya 700 Liverpool jana
The boots had the No 700 on the back as well as the name of his daughters Lilly and Lexie
Kiatu alichovaa Nahodha huyo jana, No 700 chenye majina ya mabinti zake pia, Lilly and Lexie

WALIOCHEZA MECHI NYINGI LIVERPOOL

1. Ian Callaghan 857
2. Jamie Carragher 737
3. Steven Gerrard 700*
4. Ray Clemence 665
= Emlyn Hughes 665 
(bado anacheza) 
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 34 alibandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram wiki iliyopita kuelezea anavyojiandaa kwa mechi ya 700, lakini hakuwemo kwenye kikosi kilichoifunga West Ham 2-0 Uwanja wa Anfield mwishoni mwa wiki.
Gerrard anaweza kubaki nafasi ya tatu kwa kucheza mechi nyingi Liverpool, nyuma ya  Callaghan aliyecheza mara 857 na Carragher michezo 737, kutokana na kuwa na mpango wa kuhamia LA Galaxy ya Marekani akalizie soka yake huko mwishini mwa msimu.

LIVERPOOL NA BOLTON KATIKA PICHA

Philippe Coutinho's 90th minute strike gave Liverpool a 2-1 lead against Bolton Wanderers on Wednesday nightMM Mfungaji wa goli la pili la Liverpool PhilipCoutinho baada ya kuipatia timu yake goli la ushishindi hapo jana.
The Brazilian midfielder points to the sky after his goal put Liverpool into the FA Cup fifth round

 The 22-year-old prepares to curl a delightful effort off the underside of the bar and into the Bolton netll



vvv
 Alberto Moreno (left) jumps for joy with Coutinho as Liverpool secure an FA Cup fifth round tie against Cyrstal Palacevvv

 Bolton striker Eidur Gudjohnsen celebrates scoring his second half penalty in front of the home crowd against Liverpool nnnMshambuliaji wa Bolton Gudjohnsen akishangilia baada ya kuifungia timu yake kwa nji ya penalty.

MADRID BILA RONALDO INAWEZEKANA

Jese & James put Madrid four points clearWachezaji wa Real Madrd wakishangilia moja ya magoli yao katika mchezo dhidi ya Sevilla, Real Madrid walishinda goli 2-1 magoli ya Janes Rodriguez dakika ya 12 pamoja na Jese dakika ya 36 goli la Sevilla lilifungwa na Iago Aspas dakika ya 80

LIVERPOOL YASHINDA KWA TAABU FA CUP

Timu ya Liverpool imeibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Bolton katika mchezo wa raundi ya nne ya michuanoya Fa Cup. Bolton walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Guojohnsen katika dakika ya 59, Raheem sterling akasawazisha dakika ya 86 kabla ya Philip Coutinho kufunga la ushindi dakika ya 90 ya mchezo.Coutinho completes Liverpool comebackll
Mchezaji Raheem Sterling akishangilia baada ya kuifungia timu yake ya Liverpool katika ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Bolton.

LIVERPOOL MAMBO MAGUMU FA CUP MECHI INAENDELEA

Live: Bolton 1-0 Liverpool
Raheem steling akishuhudia timu yake ya Liverpool ikifungwa dhidi ya Bolton 1-0 dakika ya 73

IVORY COAST YATINGA FAINAL

 Timu ya Ivory Coast imeifunga timu ya Congo DR goli 3-1 shukrani kwa Yaya Toure ambaye alifunga goli la kwanza dakika ya 21,Gervinho alifunga goli la pili dakika ya 41 na Kanon akaihakikishi ushindi Ivory Coast kwa kufunga goli la tatu dakika ya 68 na Goli pekee la Congo DR lilifungwa na Mbokani dakika ya 24 kipindi cha kwanza.Yaya leads Ivory Coast to Afcon final
Mchezaji wa Ivory Coast Yaya Toure akishangilia baada ya kuifungia timu yake katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Congo DR.