SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Jan 31, 2016

HII NDIO SABABU YA SAMATTA KUVAA JEZI NAMBA 77

Mbwana Samatta ambaye kwasasa ni mchezaji wa kulipwa wa klabu ya Genk ya Ubelgiji amezungumza na shaffihdauda.co.tz kwanini
ameamua kuchagua kuvaa jezi yenye namba 77 mgongoni.

Samatta amesema alitokea kuipenda jezi namba saba tangu akiwa TP Mazembe ikafikia wakati
akaanza kuushawishi uongozi wa klabu hiyo umbadilishie jezi lakini ilikuwa ngumu kwasababu tayari kulkikuwa na mchezaji akiivaa
jezi hiyo.

Jan 28, 2016

MAYANJA AMTAJA KIPA NAMBA MOJA SIMBA

Na Haji balou
Dar es salaam
Siku chache baada ya kuanza kibarua cha kukinoa kikosi hicho, Kocha Mkuu wa Simba
Mganda, Jackson Myanja, amemtangaza Muivory Coast, Vincent Angban kuwa kipa
namba moja kwenye kikosi chake.
Kocha huyo aliitoa kauli hiyo, hivi karibuni kabla ya mechi ya Kombe la FA dhidi ya Burkina Faso iliyochezwa Uwanja wa Jamhuri Morogoro, mchezo uliomalizika kwa Simba
kushinda mabao 3-0 yakifungwa na HamisvKiiza (mawili) na Said Ndemla.

Kocha huyo, tangu ameanza kibarua hicho amekuwa akimtumia Angban katika kikosi cha kwanza katika mechi mbili za Ligi Kuu Bara
dhidi ya Mtibwa Sugar waliyoshinda bao 1-0 na JKT Ruvu ambayo waliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Mayanja anaona ni sahihi kumtangaza Angban kuwa kipa namba moja kutokana na
kutoruhusu nyavu zake kutikiswa kwenye michezo mitatu.

KOCHA SIMBA AMTAJA KIPA BORA LIGI KUU BARA

Ligi Kuu Bara imekuwa na ushindani mkubwa, mastraika wakisaka kiatu cha dhahabu makocha wakitafuta ushind VPL, Makipa nao hawapo nyuma, Je! kipa bora msimu huu
nani? Kipa wa Azam FC, Aishi Manula, ametajwa kuwa ndiye kipa bora katika Ligi Kuu Bara msimu huu mpaka sasa akiwapiku makipa Deogratius Munishi ‘Dida’ wa Yanga na JumabKaseja wa Mbeya City.

Goal kinatambua mchango wa Aishi Manula katika kikosi chake cha Azam FC, hali kadhalika amekuwa akionyesha jitihada katika
timu ya Taifa ya Tanzania lakini bado
hajafanikiwa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Charles Mkwasa.

Kwa mujibu wa aliyekuwa kocha wa zamani wa makipa wa Simba, Mkenya, Iddi Salim, kwa kipindi cha miezi sita alichokaa Tanzania
kufundisha soka, amemuona Manula kuwa ndiye bora huku akisisitiza kama ataendelea kulelewa kwenye misingi bora, bila shaka atakuja kuwa msaada mkubwa kwa timu ya
taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Akizungumza na waandishi wa habari Iddi Salim alisema “Kwa miezi sita niliyokaa Tanzania, naweza kusema nimewaona makipa wengi katika Ligi Kuu Bara, lakini kipa
wa Azam, Manula, kwangu ndiye ni bora zaidi kuliko mwingine kutokana na mambo anayoyafanya uwanjani ikiwemo kucheza penalti nyingi.

“Lakini pia ukiangalia kwa makipa vijana, Manula anashika namba moja akifuatiwa na Manyika Jr., na kama watazidi kukomaa basi
watakuja kuwa makipa wazuri siku za usoni,”
alisema kocha huyo aliyewahi kuinoa Gor Mahia na timu ya taifa ya Kenya 'Harambee Stars' .
Akizungumzia kipa mwingine bora, Idd alisema Peter Manyika wa Simba, kama atapata matunzo mazuri, mafunzo mazuri na
kuthaminiwa, ndiye atakuwa tegemeo la Tanzania hapo baadaye.

Jan 27, 2016

TETESI KUHUSU KOCHA MPYA MAN UNITED NA CHELSEA


Taarifa kutoka Manchester United zimedai kwamba uongozi wa klabu hautakata tamaa kufuatilia saini na na huduma za meneja Pep
Guardiola anayemaliza muda wake katika Bayern Munich, ingawa habari zilitependekeza kwamba atajiunga na mahasimu Manchester City.

Mtendaji Makamu Mwenyekiti Ed-Wood Ward anataka kumuajiri meneja wa Barcelona wa
zamani na atafanya hivyo kwa nguvu hadi dakika ya mwisho.

Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Uongozi wa Chelsea umemtangaza meneja wa Tottenham Hotspur Mauricio Pochettino katika
orodha ya mameneja wanaoweza kumrithi meneja wa mpito Guus Hiddink mwishoni mwa
msimu. Diego Simeone, Didier Deschamps na Jorge Sampaoli wako pia katika orodha hiyo ya
ushindani. (Source: The Times)

KIPRE AIOKOA AZAM DAKIKA ZA JIONI DHIDI YA ZESCO

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC imeanza kwa sare katika harakati zake za kuwania ubingwa wa michuano maalumu nchini Zambia baada ya jioni ya leo kupata matokeo ya bao 1-1 dhidi ya wenyeji wao Zesco United ya huko.

Kocha wa Azam FC, Stewart Hall, aliingia kwenye mchezo huo kwa kukifanyia marekebisho matano
kikosi chake kwa kuwajumuisha mabeki David Mwantika, Pascal Wawa, Wazir Salum, kiungo
Frank Domayo na mshambuliaji Kipre Tchetche, ambao hawakucheza mchezo uliopita wa Kombe la FA dhidi ya African Lyon.
Mchezo huo uliathiriwa kwa kiasi kikubwa na mvua inayoendelea kunyesha jijini Ndola, Zambia,
baada ya Uwanja wa Levy Mwanawasa kusimamisha maji jambo ambalovlilifanya soka la
pasi kutotumiwa sana na timu hizo kufuatia mpira kunasa kwenye maji kila unapoburuzika.

Walikuwa ni Zesco United walioweza kuziona nyavu za Azam FC katika dakika ya kwanza tu ya mchezo huo, bao lililofungwa na mshambuliaji
mpya wa timu hiyo, Jesse Were, aliyeibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Kenya msimu uliopita akiwa na Tusker FC akifunga mabao 22.

Azam FC iliamka baada ya kufungwa bao hilo na kufanya mashambulizi kadhaa langoni mwa
Zesco United, lakini hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Wazambia hao waliondoka kifua mbele kwa bao hilo.
Kipindi cha pili kilianza kwa Azam FC kufanya mabadiliko akiingia kiungo Michael Bolou kuchukua nafasi ya Nahodha Msaidizi Himid Mao
'Ninja'. Mabadiliko hayo yaliweza kuisaidia sana Azam
FC baada ya kutawala kwa kiasi kikubwa eneo la
kiungo na kuanza kulishambulia kwa kasi lango la wapinzani wao.

Dakika 67 Azam FC ilipata pigo baada ya kuumia kwa nahodha wake John Bocco 'Adebayor' na
nafasi yake ilichukuliwa na Allan Wanga huku pia akitoka beki Wazir Salum na kuingia Ramadhan
Singano 'Messi'.

Kuingia kwa wawili hao kukizidi kuongeza kasi kwenye eneo la ushambuliaji la Azam FC na
katika dakika ya 70 beki Shomari Kapombe aliyeachiwa kitambaa cha unahodha na Bocco, almanusura aipatie bao la kusawazisha timu hiyo
baada ya kupiga shuti kali umbali ya mita 30 lililogonga mwamba wa juu na kutoka nje ya lango la Zesco United.

Azam FC ilizidi kuweka kambi katika lango la wapinzani wao dakika 15 za mwisho na hatimaye
ikajipatia bao safi la kusawazisha dakika ya 90 lililofungwa na Kipre Tchetche kwa kichwa
akimalizia kona safi iliyochongwa na Messi upande wa kulia.

Kona hiyo iliyozaa bao ilikuwa ni ya tatu kupigwa na Messi ndani ya dakika hiyo baada ya
wachezaji wa Zesco United kuokoa mara mbili za
mwanzo alizopiga kabla ya tatu haijazaa bao.
Hadi dakika 90 za mchezo huo wa kwanza
zinamalizika timu hizo zilitoka uwanjani zikiwa
nguvu sawa kwa mabao hayo.
Hiyo ni sare ya pili mfululizo baina ya timu hizo kwani katika michuano ya mwaka jana iliyofanyika jijini Lubumbashi DR Congo na
wenyeji TP Mazembe kuibuka mabingwa, zilitoka
sare ya mabao 2-2.

Azam FC itateremka tena dimbani Jumamosi Ijayo kucheza na mabingwa wa Zimbabwe
Chicken Inn kabla ya kumaliza michuano hiyo kwa kukipiga na Zanaco FC ya huko Jumatano
ijayo.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa hivi
Aishi Manula, Shomari Kapombe, Wazir Salum/
Ramadhan Singano 'Messi' dk67, Erasto Nyoni,
David Mwantika, Pascal Wawa, Jean Mugiraneza
'Migi', Himid Mao 'Ninja'/Michael Bolou dk46,
Frank Domayo 'Chumvi', John Bocco 'Adebayor'/
Allan Wanga dk67, Kipre Tchetche

ALICHOSEMA SUAREZ KUHUSU YEYE KUCHEZA TENA ENGLAND

Mshambuliaji hatari wa Barcelona, Luis Suarez amezungumzia uwezekano wa yeye kurudi
nchini England na kuichezea klabu yake ya zamani ya Liverpool, huku akisema kuwa ndio klabu pekee anayoweza kurudi England kwa ajili
yake.

Suarez ambaye aliichezea Liverpool kwa kipindi cha miaka 2 na nusu kabla ya kusajiliwa na
Barcelona ya nchini Hispania ameiambia ESPN kuwa kila mchezaji ambaye alipata kuichezea Liverpool anajua umuhimu wa mashabiki wa
Liverpool Anfield.

Suarez anasema kuwa mashabiki wa Liverpool ni wa pekee zaidi duniani, na kwamba anawakumbuka kila wakati kitu kinachomfanya
awe na ndoto za siku moja kurudi tena Merseyside kufurahia tena maisha na mashabiki hao.

Mchezaji huyo wa zamani wa Ajax alijiunga Liverpool mwaka 2011 kwa ada ya uamisho wa pauni 22m na katika kipindi cha miaka 2 na nusu
aliifungia Liverpool magoli 94 kabla ya kusajiliwa na Barcelona kwa dau kubwa la pauni 75m.

HUYU NDIYE MCHEZAJI ANAYEMZIDI MESSI KWA MAGOLI

Mashabiki wengi wa kilabu ya Athletic Bilbao wangecheka iwapo ungetaja miaka ya nyuma
kwamba Aritz Aduriz angelinganishwa na Lionel
Mesii,Cristiano Ronaldo na Luiz Suarez.

Mchezaji huyo anayekaribia miaka 35 ameingia katika kumbukumbu za daftari lenye wachezaji
wenye mabao mengi pamoja na
Messi,Suarez,Karim Benzema na Neymar msimu huu.
Wale wasiofutilia ligi ya Uhispania huenda wasimtambue Aritz Aduritz ni nani.Aduriz
alifunga mabao mawili katika mechi ya ushindi dhidi ya Eibar na kufikisha mabao yake kuwa 25 katika michuano yote msimu huu.

Nyota wa Real Madrid,Ronaldo ni mchezaji pekee anayesakata soka yake nchini Uhispania
aliyewahi kufunga mabao zaidi,ijapokuwa Messi,Suarez,Benzema na Neymar wana mabao
mengi ukilinganisha na mechi walizocheza dhidi ya Aduriz.

Lakini sio mabao mengi ya Aduriz yaliowavutia wengi,kasi yake ya kuweza kufunga mabao ya
'bicycle kick' dhidi ya Eibar imempa uwezo wa kupigania nafasi ya bao zuri msimu huu na kuweka jina lake katika midomo ya wapenzi
wengi wa ligi ya Uhispania.

Ungana na mchezaji wa Atletico Bilbao Aduriz
ambaye amefunga mabao mengi zaidi ya Messi.
Aduriz, ambaye atafikisha miaka 35 mnamo tarahe 11 mwezi Februari,amefunga mabao 25
katika michuano yote ya Athletico Bilbao msimu huu.

Mchezaji mwenye mabao mengi nchini Uhispania.Bao katika kila mechi.Cristiano Ronaldo 27 27 1.00Aritz Aduriz 25 34 0.74Luis
Suarez 24 28 0.86Karim Benzema 21 20 1.05Neymar 20 24 0.83Lionel Messi 19 23 0.83 Lakini ni vipi Aduriz ameweza kuingia katika
orodha ya wafungaji bora katika ligi ya Uhispania?

Kupitia uvumilivu na ubarakala .
Alirudi katika kilabu ya Atletico Bilbao kwa mara
ya 3 mwaka 2012,baada ya kufeli kuvutia
alipokuwa kijana,ambapo alihudumu misimu
miwili na nusu akichezea Burgos na Real
Valladolid kabla ya kurudi mwaka 2005 na 2008
ambapo alizuiliwa na uwepo wa Fernando
Llorentes.
Athletico ilimchezesha sana Llorentes kuwa
mshambuliaji wa pekee hatua iliomaanisha
kwamba Aduriz alipatiwa nafasi chache,na
baadaye akaelekea Mallorca na Valencia ili
kutafuta fursa hiyo.

Jan 26, 2016

MAKOCHA KUMI WA KIHISTORIA LIGI KUU ENGLAND

Makocha 10 bora katika historia
ya Ligi Kuu ya England
Ligi Kuu ya England huchukuliwa kama ligi bora katika ulimwengu wa soka, ambapo utakuta vilabu kabambe kama Manchester United,
Chelsea, Liverpool na Arsenal na nyingine zenye uwezo katika mchuano. Ni ligi ya kupendeza kwa
watu wengi duniani ambapo kila klabu yaweza kuipika ingine.
Hapa kuna mameneja 10 walioweza kuvutia mioyo ya watazamaji wa soka katika ligi ya
England.

10. Roy Evans( Liverpool)
Ni mwingereza aliyefunza Liverpool tangu 1994 hadi 1998, licha ya kushinda Ligi Kuu ya England
katika awamu ya yake akiwa Anfield, Evans alisaidia klabu ya Merseyside kumaliza katika timu nne za kwanza mara nne mfululizo.

Mechi alifunza: 244
Michezo aliyoshinda: 123
Michezo aliyoshindwa: 58
Michezo aliyotoka sare: 63
Kiwango cha ushindi: 50.41%
Mataji aliyoshinda:
League Cup(1): 1994–95

9. Gerard Houllier ( Liverpool )
Mfaransa alichukuwa klabu mnamo 1998 baada
ya Roy Evans kustaafu alipopigwa kimbwa 3-1 katika League Cup na Tottenham Hotspur katika
Anfield.
Houllier alifurahia mafanikio aliyopata kwa
kushinda mataji 4 muhimu katika misimu mitano
kama meneja wa Liverpool.
Mechi alifunza: 307
Michezo aliyoshinda: 160
Michezo aliyoshindwa: 74
Michezo aliyotoka sare: 73
Kiwango cha ushindi: 52.12%

Mataji aliyoshinda:
FA Cup (1): 2000–01
League Cup (2): 2000–01, 2002–03
FA Community Shield (1): 2001
UEFA Cup (1): 2000–01
UEFA Super Cup (1): 2001

8. Rafael Benitez ( Liverpool and
Chelsea )
Mhispania alikuwa katika Liverpool tangu mwaka 2004 hadi 2010 ambapo alishinda mataji mawili
muhimu likiwemo la Ligi ya Mabingwa baada ya kushinda AC Milan kwa mikwaju ya penalti.
Alirudi tena katika England kama meneja wa Chelsea mnamo 2012, na kusaidia klabu kushinda
Kombe la Europa League.
Mechi alizofunza: 350 (Liverpool)
Michezo aliyoshinda: 196
Michezo aliyoshindwa: 79
Michezo aliyotoka sare: 75
Kiwango cha ushindi: 56%

Mataji aliyoshinda:
FA Cup: 2005–06
FA Community Shield: 2006
UEFA Champions League: 2004–05
UEFA Super Cup: 2005

7. Carlo Ancelotti( Chelsea )
Mwitaliano mwenye uzoefu katika kazi ya ukufunzi alichukua Chelsea kwa muda kumrithi meneja Guus Hiddink mwaka 2009. Baada ya
miezi miwili tu katika West London, Ancelotti aliinua kombe la Community Shield baada ya
kumpiga Sir Alex Furguson wa Manchester United kwa mikwaju ya penalti, baada ya kumaliza dakika za kawaida kwa sare ya 2-2.
Pia aliongoza klabu ya Stamford Bridge kwa ushindi wa Ligi Kuu ya England na Kombe la FA
katika msimu wake wa kwanza katika klabu hiyo.

Michezo aliyofunza: 109
Mechi alizoshinda: 67
Mechi alizoshindwa: 22
Michezo aliyotoka sare: 20
Kiwango cha ushindi: 61.47%
Mataji aliyoshinda:
Premier League: 2009–10
FA Cup: 2009–10
FA Community Shield: 2009

6. Kenny Dalglish (Blackburn
Rovers, Liverpool and Newcastle
United )
Raia wa Scotland alifanya kazi ya ukufunzi katika
klabu tatu tofauti, awamu mbili katika Liverpool,
miaka minne katika Blackburn Rovers tangu 1991
hadi 1995 na kumrithi Kevin Keegan katika
Newcastle mnamo 1997.
Kenny Dalglish aliongoza Blackburn Rovers
kwenye taji la Ligi Kuu ya England mnamo
1994/95, na kusaidia Newcastle United kumaliza
msimu ikiwa kwenye nafasi ya pili mnamo
1996/97. Lakini hakufanikiwa katika awamu yake
ya pili katika Liverpool.

5. Manuel Pellegrini ( Manchester
City )
Raia wa Chile alitangazwa kama meneja wa
Manchester City mnamo 2013 baada ya Roberto
Mancini kuondoka. Manuel Pellegrini alipata
kuwa kocha wa kwanza kutoka nje ya Ulaya
aliyeshinda Ligi Kuu ya England katika msimu wa
kwanza katika Etihad Stadium.
Mechi alizofunza: 112
Mechi alizoshinda: 73
Mechi alizoshindwa: 24
Michezo aliyotoka sare: 15
Kiwango cha ushindi: 65.18%
Mataji aliyoshinda:
Premier League (1): 2013–14
Football League Cup (1): 2013–14

4. Roberto Mancini ( Manchester
City )
Kocha Mwitaliano alikuja kumrithi Mark Hughes
katika Manchester City tangu 2009 hadi 2013.
Katika msimu wake wa kwanza, Mancini
aliisaidia City kumaliza msimu katika nafasi ya
tano, nafasi nzuri kwa mara ya kwanza katika
miaka 44.
Alishinda pia FA Cup na FA Community Shield
kwa Manchester City wakati wa awamu yake
katika Ligi Kuu ya England.
Mechi alizofunza: 119
Mechi alizoshinda: 113
Mechi alizoshindwa: 40
Michezo aliyotoka sare: 38
Kiwango cha ushindi: 59.16%
Mataji aliyoshinda:
Premier League: 2011–12
FA Cup: 2010–11
FA Community Shield: 2012

3. Arsene Wenger ( Arsenal)
Kocha Mfaransa aliwasili katika
Arsenal mnamo 1995, lakini tangu wakati huo
klabu Kasikazini mwa London haijashindwa
kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa.
Mechi alizofunza: 1,071
Mechi alizoshinda: 616
Mechi alizoshindwa: 205
Michezo aliyotoka sare: 250
Kiwango cha ushindi: 57.52
Mataji aliyoshinda:
Premier League (3): 1997–98, 2001–02,
2003–04
FA Cup (6): 1997–98, 2001–02, 2002–03,
2004–05, 2013–14, 2014–15
FA Community Shield (6): 1998, 1999, 2002,
2004, 2014, 2015

2. José Mourinho (Chelsea)
Kocha Mreno ni mmoja wa mameneja wachache
walioweza kuchinda vikombe vitatu vya Ligi Kuu
ya England katika misimu 5 ya awamu mbili,
huchukuliwa kama mmoja wa mameneja bora wa
sasa katika ulimwengu wa soka, alishinda mataji
ya ligi katika nchi nne tofauti.
Kiwango cha ushindi: 70%
Mataji aliyoshinda:
Premier League(3): 2004–05, 2005–06, 2014–15
FA Cup(1): 2006–07
Football League Cup(3): 2004–05, 2006–07,
2014–15
FA Community Shield(1): 2005

1. Sir Alex Furguson ( Manchester
United )
Mskoti mwenye historia ndefu tena ya ajabu
katika ulimwengu wa soka, alidumu miaka 27
katika Manchester United kati ya 1986 na 2013,
aliandika rekodi ya kushinda Ligi Kuu ya England
mara 13 vile vile na mataji mengine ya Ulaya na
vikombe kadhaa vya England.
Ferguson, aliyestaafu kutoka soka mnamo 2013,
ndiye kocha pekee aliyewahi kushinda mataji 3
ya Ligi Kuu ya England kwa mfululizo. Alivifanya
kati ya 1998/99 na 2000/01, alivifanya tena kati
ya 2006/07 na 2008/09.
Mechi alizofunza: 1500
Mechi alizoshinda: 895
Mechi alizoshindwa: 267
Michezo aliyetoka sare: 338
Kiwango cha ushindi: 59.67
Mataji aliyoshinda:
Premier League (13): 1992–93, 1993–94, 1995–
96, 1996–97, 1998–99, 1999–2000, 2000–01,
2002–03, 2006–07, 2007–08, 2008–09, 2010–
11, 2012–13
FA Cup (5): 1989–90, 1993–94, 1995–96, 1998–
99, 2003–04
League Cup (4): 1991–92, 2005–06, 2008–09,
2009–10
FA Charity/Community Shield (10): 1990
(shared), 1993, 1994, 1996, 1997, 2003, 2007,
2008, 2010, 2011
UEFA Champions League (2): 1998–99, 2007–08
UEFA Cup Winners' Cup (1): 1990–91
UEFA Super Cup (1): 1991
Intercontinental Cup (1): 1999
FIFA Club World Cup (1): 2008

Jan 24, 2016

HILI NDIO GOLI AMBALO KAPOMBE HAWEZI KULISAHAU AKIWA AZAM FC

Kapombe amesema kuwa
hataweza kulisahau bao alilofunga dhidi ya Ndanda goli ambalo liliipa ushindi wa bao 1-0 timu yake ya Azam fc katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Nangwanda
Sijaona, Mtwara.

“Kwa kweli mimi nalifurahia sana bao nililofunga
dhidi ya Ndanda dakika za mwisho, lilikuwa ni
bao muhimu sana kwa timu yangu kwani tuliweza
kuondoka na pointi tatu katika mchezo huo
uliokuwa mgumu,” alisema.

Jan 23, 2016

NDEMLA ANUKIA TP MAZEMBE

Kiungo kinda wa Simba, Said Ndemla,
anatarajia kwenda kufanya majaribio
kwenye kikosi cha TP Mazembe ya DR
Congo ili kusaka nafasi ya kucheza soka
katika klabu hiyo.

Hivi karibuni, Watanzania, Abuu Ubwa na
Haruna Chanongo walienda kufanya
majaribio Mazembe ambapo kwa sasa
hatua iliyobaki ni makubaliano kati yao na
Stand United inayowamiliki wachezaji hao.
Jamali Kisongo ambaye ni meneja wa
Mbwana Samatta, amesema kuwa,
ataendelea kuwasaidia wachezaji wa
Tanzania kupenya kwenye soka la
kimataifa kama Samatta.
“Nimewapeleka Ubwa na Chanongo
kufanya majaribio TP Mazembe,
kinachoendelea sasa ni mazungumzo kati
ya Stand na Mazembe kwa ajili ya usajili.

“Ndemla naye nitampeleka akafanye
majaribio kule, lengo ni kuwasaidia
wachezaji wengi wa hapa nyumbani
kupata fursa ya kucheza soka nje ya
mipaka ya nchi yetu.
“Mbali na Ndemla, pia kiungo wa Mtibwa
(Sugar), Mohammed Ibrahim, naye
anahitajika kule baada ya awali safari
yake kushindikana,” alisema Kisongo.

Jan 22, 2016

KUMBE KIPRE KWAO ANAJULIKANA NA MAJIRANI TU

Unaweza kudhani ni utani, lakini ukweli ni
kwamba kati ya Waivory Coast
wanaocheza soka hapa nchini ni Pascal
Wawa (Azam FC) na Vincent Angbani
(Simba) wanaojulikana kuwa wanacheza
soka Tanzania, lakini upande wa
mwenzao fowadi wa Azam, Kipre
Tchetche kuna kitu ambacho
kinashangaza kidogo.

Kwa hapa nchini Kipre ni staa mkubwa
tangu mwaka 2011 alipojiunga na timu
hiyo na ndiyo maana ndiye straika
anayelipwa fedha ndefu zaidi nchini
akipokea dola 12,000 (Sh milioni 24) kwa
mwezi.

Angbani amesema kuwa utapotea njia
iwapo utafika Ivory Coast na kuulizia kina
Tchetche kwani hawajulikani, zaidi ya
umaarufu wao kuishia kwa majirani zao
tu.
“Mara ya kwanza nilishangaa sana kukuta
Kipre ni staa kiasi hiki hapa Bongo, ujue
kwetu tofauti na majirani hakuna anayejua
kuwa anacheza soka huku, wao wanamjua
Wawa na mimi,” alisema kipa huyo.
Akifafanua zaidi alisema umaarufu wake
na Wawa ni kutokana na kuwahi
kuichezea timu ya taifa ya vijana ya nchi
yao.
SOURCE: CHAMPIONI

Jan 20, 2016

SAMATTA ARUDI MAZEMBE KUMALIZIA MKATABA, KATUMBI HOI

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa
Tanzania, Mbwana Ally Samatta
anaondoka asubuhi ya leo kwenda
Lubumbashi, Jamhuri ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC),
kujiunga na klabu yake, TP Mazembe
wakati sakata la uhamisho wake
likiendelea.

Samatta anaondoka na Maofisa wa
Wizara ya Michezo walioteuliwa
kwenda kuzungumza na Rais wa TP
Mazembe, Moise Katumbi
kumshawishi amruhusu mchezaji huyo

kujiunga na KRC Genk ya Ubelgiji.
Lakini iwapo Katumbi ataendelea
kusistiza msimamo wake wa kutaka
Samatta aende Nantes ya Ufaransa,
basi mchezaji huyo ataamua kubaki
Mazembe amalizie miezi yake mitatu
ya Mkataba wake ili aondoke kama
mchezaji huru Aprili.

Jan 19, 2016

MAYANJA ATOA NENO KUHUSU MAKIPA SIMBA

Kocha Mkuu wa muda wa Simba, Jackson
Mayanja amewataka makipa Peter
Manyika na Vicent Agbani raia wa Ivory
Coast kuwa katika utimamu wa asilimia
mia kwa fitnesi.

Mayanja raia wa Uganda amewataka
makipa hao kuongeza mazoezi
kuhakikisha wanakuwa walinzi sahihi
katika kila dakika 90 za mechi.
“Kwa mchezaji wakati wote anatakiwa
kuwa fiti kwa asilimia mia, kipa ni mlinzi
namba moja. Akipitiwa yeye, maana yake
mmefungwa, hivyo anatakiwa kuwa fiti
kamilifu.

“Mchezaji anapokuwa timilifu kwa maana
ya kuwa fiti sana, basi uhakika wa
kufanya anachotaka iwe ni kwenye kuokoa
au kushambulia unakuwa juu sana. Hivyo
nimewasisitiza na wao wanalijua hilo,”
alisema.
MAYANJA

Kwa sasa Simba haina kocha wa makipa
baada ya Iddi Salim raia wa Kenya
kutupiwa virago na uongozi wa Simba na
tayari ameisharejea kwao Nairobi, Kenya

Jan 17, 2016

NIYONZIMA AOMBA MSAMAHA KWA MASHABIKI YANGA

KIUNGO Haruna Hakizimana Fadhil
Niyonzima ameomba msamaha Yanga
SC na kuahidi kutorudia kuikwaza
klabu kwa namna yoyote.
Mwezi uliopita, Yanga SC ilitangaza
kuvunja Mkataba na Nahodha huyo
wa Rwanda kwa tuhuma za kukiuka
vipengele vya Mkataba wake.
Lakini leo katika Mkutano na
Waandishi wa Habari makao makuu
ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam,
Niyonzima ameomba msamaha ili
arejeshwe kundini.

“Ninapenda kuchukua fursa hii
kuomba msamaha kwa uongozi,
benchi la ufundi na wachezaji
wenzangu pamoja na wanachama na
wapenzi. Ninaipenda timu yangu na
ninapenda kuendelea
kuitumikia,
”amesema.
Aidha, Niyonzima amesema kwamba
kulitokea kutoelewana kimawasiliano
na ofisi ya Katibu Mkuu, Dk Jonas
Tiboroha kiasi cha kulifikisha suala
hilo kwenye hatua hiyo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya
Habari na Mawasiliano ya Yanga SC,
Jerry Muro amesema kwamba suala la
Niyonzima limefika katika uongozi
mkuu wa klabu na lipo katika hatua
nzuri.

Ingawa Muro hakuweza wazi, lakini
inavyoonekana muda si mrefu Yanga
itatangaza kuzika tofauti zake na
mchezaji huyo na kumrejesha kundini
rasmi.

MKUDE ATOA YA MOYONI BAADA YA KUFUKUZWA KERRY

KIUNGO wa Simba, Jonas Mkude,
ameonyesha masikitiko yake kwa mtindo
ulioanza kuzoeleka ndani ya Simba wa
ingia toka ya makocha kila uchao, akidai
inawavuruga, licha ya kwamba
wachezaji ni kama wanajeshi na katu
hawapaswi kuchagua pori la kupigania
vita.

Mkude alisema wachezaji wa Simba
wapo kwenye wakati mgumu, ingawa
jukumu lao ni kusimama imara ili kuona
timu yao inajenga heshima katika soka
la Bongo.
“Ukisikia utu uzima na kujielewa ndiyo
kipindi hiki ambacho tunakipitia
wachezaji wa Simba, kwani
kubadilishiwa makocha katikati ya
mechi ni mtihani kitu cha ziada ni kutoa
ushirikiano wa haraka kwa kocha
anayekabidhiwa kwetu kwa wakati
husika,” alisema.

Mkude alisema utakuwa msimu mgumu
kwao hasa wakiwa na nia ya kutimiza
kiu ya mashabiki wao wanaolilia
ubingwa. Lakini kwa kitendo cha
kuingia na kuondoka kwa makocha
kunawaumiza na kujikuta muda mwingi
wanatumia kuzoea makocha badala ya
kusonga mbele.

“Sisi tutakuwa tunafanya kazi ya
kuwakumbuka makocha wanapoondoka
na kuwazoea wanaoingia kama
binadamu inatugharimu, hata hivyo
tutapambana na tunaamini tutamzoea
Jackson Mayanja kama ambavyo
tuliwazoea makocha kina Patrick Phiri
na wenzake waliopishana Msimbazi,”
alisema. Mkude pia aliwataka
wanachama na kila mdau wa Msimbazi
kushirikiana pamoja ili kuivusha Simba
katika kipindi hiki ikiusaka ubingwa wa
Ligi Kuu baada ya kuukosa kwa misimu
mitatu iliyopita.

NIYONZIMA KUFANYAKIKAO NA WANACHAMA WA YANGA LEO

Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima
atazungumza na wanachama na
mashabiki wa Yanga jijini Dar es Salaam,
leo.
Niyonzima anatarajia kufanya hivyo katika
mkutano wa waandishi wa habari
uliopangwa kufanyika jijini Dar.
Mpashaji mmoja amesema huenda
Niyonzima akafanya mkutano huo makao
makuu ya klabu ya Yanga.

"Sina uhakika sana, lakini mkutano huo
unaweza kufanyika palepale klabuni na
Niyonzima ndiye atakuwa mzungumzaji
mkuu," alitoa taarifa hiyo, mpashaji.
Taarifa zinaeleza, Niyonzima ambaye ni
nahodha wa timu ya taifa ya Rwanda
ameamua kufanya hivyo kwa lengo la
kumaliza mgogoro.

Hadi sasa, klabu ya Yanga imeishatangaza
kuvunja mkataba na Niyonzima kwa madai
ya utovu wa nidhamu.
Lakini taarifa zinaeleza, hadi sasa bado
uongozi wa Yanga haujampa barua ya
kuvunja mkataba huo hadi sasa.

Jan 16, 2016

LEICESTER CITY YABANWA MBAVU NA ASTON VILLA

Leicester City imelazimishwa sare ya goli 1-1 ugenini dhidi ya Aston villa katika mchezo wa ligi kuu nchini England. Goli la Leicester City limefungwa na Okazaki katika dk ya 28 na goli la kusawazisha kwa upande wa Aston Villa limefungwa na Gestede dk ya 75. Kwa matokeo hayo  Leicester City inapanda kileleni mwa ligi hiyo kwa kufikisha point 44 nyuma ya Arsenal na Man City wenye point 43

AZAM YALAZIMISHWA SARE NA AFRICAN SPORTS

AZAM FC imelazimishwa sare ya
kufungana bao 1-1 na African Sports
ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu
ya Vodacom Tanzania Bara usiku huu
Uwanja wa Azam Complex, Chamazi,
Dar es Salaam.
Sare hiyo inaiongezea Azam FC pointi
moja na kufikisha 36 baada ya mechi
14, ikiwazidi pointi tatu mabingwa
watetezi, Yanga SC walio katika
nafasi ya pili, ingawa wana mechi
moja mkononi.

Katika mchezo uliochezeshwa na refa
Jonesia Rukyaa wa Kagera
aliyesaidiwa na Ferdinand Chacha na
Julius Kasitu, hadi mapumziko Azam
FC walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Bao hilo lilifungwa na kiungo wa
zamani wa Yanga SC, Frank Raymond
Domayo dakika ya 28 kwa shuti la
umbali wa takriban mita 20, baada ya
kupokea pasi ya Nahodha John
Raphael Bocco.

Pamoja na kumaliza dakika 45 za
kwanza, wakiwa nyuma, lakini African
Sports walionyesha upinzani kwa
Azam FC na mara mbili walikaribia
kupata bao.

Kipindi cha pili, Sports iliyo chini ya
kocha wa zamani wa Simba SC,
Ramadhani Aluko iliongeza bidii na
kufanikiwa kusawazisha bao hilo
dakika ya 59 kupitia kwa Hamad
Mbumba aliyemalizia mpira wa
adhabu uliopigwa na Mwaita Gereza.
Baada ya bao hilo, timu hizo
ziliendelea kushambuliana kwa zamu
na kosakosa zilikuwa za pande zote
mbili.

Matokeo hayo yanaipunguza kasi
Azam FC katika mbio za ubingwa na
sasa, mabingwa watetezi, Yanga SC
wanaweza kurejea kileleni iwapo
watashinda dhidi ya Ndanda FC
kesho.
Kwa African Sports, sare hiyo ya
ugenini inakuwa ahueni katika
harakati zao za kujiepusha na balaa la
kushuka daraja.

Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi
Manula, Shomary Kapombe, Waziri
Salum/Farid Mussa dk62, Abdallah
Kheri, Serge Wawa, Erasto Nyoni,
Jean Baptiste Mugiraneza, Salum
Abubakar ‘Sure Boy’, John Bocco
‘Adebayor’, Frank Domayo/Mudathir
Yahya dk65 na Kipre Herman
Tchetche.

African Sports; Zakaria Mwaluko,
Mwaita Gereza, Khalifa tweve, Rahim
Juma, Juma Shemvuni, Ally
Ramadhani/James Mendi dk86,
Mussa Chambega, Pera Ramadhani,
Hamad Nathaniel, Hassan Materema/
Mohammed Mtindi dk47 na Rajab
Isihaka/Hussein Issa dk70.

MAN CITY YAUA CHELSEA HOII

Timu ya Manchester City imeibuka na ushindi wa goli 4-0 dhidi ya Crystal palace katika mchezo wa ligi kuu nchini England magoli ya City yamefungwa na Delph  dk 22 Aguero 41,68 Na goli LA mwisho lilifungwa Na David Silva dk 84
Matokeo mengine.
Chelsea imetoka sare ya goli 3-3 dhidi ya Everton magoli ya Chelsea yamefungwa Na Costa 64, Fabregas 66 Na Terry 90 Na magoli ya Everton yamefungwa Na Millarlas 55, More 90 Na goli LA kujifunga la Terry 50.

Bournemouth 3-0 Norwich

Southampton 3-0 West brom

Newcastle 2-1 West ham

TOTTENHAM YAITANDIKA SUNDERLAND BILA HURUMA

Kiungo wa Tottenham
Hotspur, Christian Eriksen akiteleza
chini Uwanja wa White Hart Lane
kushangilia baada ya kuifungia mabao
mawili timu yake katika ushindi wa
4-1 dhidi ya Sunderland leo. Mabao
mengine ya Spurs yamefungwa
na Mousa Dembele na Harry Kane
kwa penalti, wakati la Sunderland
limefungwa na Patrick van
Aanholt

MATOKEO YOTE YA LIGI KUU TANZANIA BARA LEO YAPO HAPA

Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara imeendelea hii Leo katika viwanja tofauti tofauti. Jijini Dar es salaam Simba imeibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Mtibwa sugar goli la timu ya Simba limefungwa na Hamisi kiiza mwanzoni mwa kipindi cha kwanza.
Matokeo mengine.
Coastal union 1-1 Maji Maji
Stand united 1-0 Kagera sugar
Jkt ruvu 1-5 Mgambo jkt
Mbeya city 1-0 Mwadui fc
Toto Africans 0-1 Prisons

KINACHOFANYA SAMATTA ACHELEWE KWENDA ULAYA NI HIKI HAPA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
RAIS wa klabu ya Nantes ya
Ufaransa, Waldemar Kita
amesikitishwa mno na kitendo cha
mshambuliaji wa kimataifa wa
Tanzania, Mbwan Ally Samatta
kukataa ofa ya kujiunga na klabu
yake, lakini hajakata tamaa kwa
sababu kijana huyo bado ni mali ya
TP Mazembe.
“Tungependa kumpata.
Inavyoonekana amesaini (KRC Genk).
Lakini ni mali ya klabu gani? Atakuwa
huru mwishoni mwa msimu? Mawakili
wangu wanalishughulikia hilo suala
kwa siku mbili, au tatu,”.
“Kama itakuwa poa, au hapana, vizuri,
mbaya sana, yote maisha,” amesema
katika safu ya Ocean Press.
Wakati huo huo, tovuti ya Gazeti la
Lequipe la Ufaransa limeandika,
Samatta mwenye umri wa miaka 24
sasa, amekwishasaini Mkataba wa
awali na KRC Genk ya Ubelgiji.
Na lakini akiwa na Mkataba na TP
Mazembe hadi Aprili 30, Mwanasoka
huyo Bora Anayecheza Afrika hawezi
kuruhusiwa kwa dau la chini ya Euro
Milioni 1.
Na wakati Samatta tayari amepatiwa
viza na Ubalozi wa Ubelgiji kwenda
kusaini klabu ya KRC Genk, Rais wa
Mazembe, Moise Katumbi amegoma
kusikikiliza kuhusu klabu hiyo ya Ligi
Kuu ya Ubelgiji.
Rais wa Nantes ya Ufaransa,
Waldemar Kita amesikitishwa na
Samatta kukataa ofa ya kujiunga na
klabu yake
BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE
inafahamu Katumbi anataka Samatta
aende Nantes FC ya Ligi Kuu ya
Ufaransa, ambayo amekwishafikia
makubaliano nayo.
Na wiki iliyopita Nantes FC ilituma
mwakilishi wake Dar es Salaam,
ambaye alifanya mazungumzo na
Meneja wa Samatta, Jamal Kisongo
mbele ya Ofisa mmoja wa Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF).
Katika mazungumzo, Kisongo alifikia
makubaliano ya maslahi binafsi na
Samatta ikiwemo dau la kusaini,
mshahara, masharti na marupurupu
mengine.
Kisongo alitaka kiwepo kipengele cha
mchezaji kutorejeshwa Afrika iwapo
hatapata nafasi ya kucheza Nantes,
bali auzwe klabu nyingine ya Ulaya na
ikakubaliwa.
Nantes ilionyesha nia ya dhati kabisa
ya kumchukua Samatta na Kisongo
aliinuka kwenye meza ya
mazungumzo akiwa amekubali na
kusema anakwenda kuzungumza na
mchezaji.
Hata hivyo, inaonekana Samatta
mwenyewe ndiye anayetaka kwenda
Ubelgiji na si Ufaransa, kwani kitendo
cha Kisongo kutorejesha majibu kwa
Nantes kinaashiria ameshindwa
kumshawishi mchezaji wake akubali
ofa hiyo.
Wakati huo huo, Rais wa Mazembe
hayuko tayari kumuuza Samatta
Ubelgiji na yuko tayari kuona Samatta
anabaki Mazembe kumalizia Mkataba
wake ili aondoke kama mchezaji huru
Aprili, hali ambayo itamlazimu kusubiri
hadi Agosti kusaini Genk.
Kwa sasa, kambi ya Samatta inajaribu
kuomba msaada kwa viongozi wa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, wakazungumze na Katumbi
ili akubali kumuacha mchezaji aende
klabu aliyochagua.
Rais Mstaafu, Dk Jakaya Mrisho
Kikwete ambaye kwa sasa ni
Mwenyekiti wa chama tawala, CCM,
Waziri wa Michezo, Nape Nnauye kwa
pamoja wameahidi kumsaidia Samatta
katika suala la kumlainisha Katumbi
akubali kupokea ofa ya Genk.
Wakati huo huo, Nantes wamekuwa
wakimpigia simu Kisongo wakisema
wanamsubiri mchezaji aende kusaini,
lakini Meneja huyo anakosa majibu ya
uhakika.
Inaonekana tayari Katumbi anaujua
mchezo wote unaoendelea naye
ameamua kukaa kimya akiamini
Samatta hawezi kufanya chochote
kwa sasa bila baraka zake.
Na wazo la kusema Samatta asubuhi
hadi Aprili atakapomaliza Mkataba
wake ili asaini kama mchezaji huru
Agosti halifurahiwi hata na Kisongo
mwenyewe.
Samatta aliyejiunga na TPM mwaka
2011 akitokea Simba SC aliyoichezea
kwa nusu msimu, akitokea African
Lyon, hadi sasa ameichezea klabu
hiyo mechi 103 na kuifungia mabao
60.
Ndani ya mechi hizo, kijana huyo wa
umri wa miaka 24, ameshinda taji la
Ligi ya Mabingwa Afrika na Mazembe,
huku naye akiibuka mfungaji bora wa
michuano hiyo na kutwaa tuzo ya
Mchezaji Bora Anayecheza Afrika.

ALI KIBA: SIO KWELI KUWA DIAMOND PLATNUMZ NDIE ANAEPITISHA VIDEO ZA BONGO KWENYE KITUO CHA MTV

Siku kama mbili zilizopita kulikuwa na habari
iliyokuwakuwa maarufu sana, ni kuhusu kauli ya
Diamond Platnumz akisema kuwa video yoyote
ya Bongo haipigwi katika Kituo cha MTV bila
yeye kushirikishwa, leo Ali Kiba kaamua kumjibu
kwa kusema kuwa hana uhakika na kauli hiyo
ya Diamond Platnumz.
Katika kipindi cha XXL katika kipengele cha 255
Ali kiba amesema “ Nitawaambia ukweli ambao
unawahusu, kama ni kweli watakuwa wanakosea
(MTV), haikai sawa na sidhani kama ni
kweli….Yaani haikai sawa na sidhani kama ni
kweli, kwasababu watakuwa hawako fair, ndio
hivyo hawako fair, hajabeba talent ya kila mtu
(Diamond), kila mtu ana kipaji chake na kila mtu
ana haki ya kuonesha kipaji chake kazi yake.
Unajua kila mtu anafanya biashara ya muziki
saizi, sio mtu anafanya masihara unapoona mtu
anafanya video yake anagharamikia unajua
haipendezi, kwahiyo sidhani kama ni kweli……. “.

ALICHOSEMA KOCHA MATOLA BAADA YA SIMBA KUMFUKUZA KOCHA

Matola, amesema Simba imechelewa
kumtimua Kocha Dylan Kerr kwani alianza
muda mrefu kutibua mambo.
Hivi karibuni Matola aliamua kuondoka
mwenyewe Simba na kujiunga na Geita
Gold Sports ya Ligi Daraja la Kwanza kwa
kile kilichoelezwa kuwa ni kutoelewana
kwake na Kerr ambaye ni raia wa
Uingereza.
Simba mapema wiki hii ilitangaza rasmi
kuvunja mkataba na Kerr kwa
kilichoelezwa kutoridhishwa na mwenendo
wa kikosi hicho katika mechi zake za
michuano mbalimbali.
Matola alisema: “Kerr ni kocha mzuri ila
nilishawaambia viongozi mapema kuwa
hafai ndani ya timu kutokana na yeye
kutaka kufuata kile anachokiamini bila ya
kushirikiana na wenzake hata kama
anakosea.
“Simba imechelewa kumtimua kwani
ameiweka timu mahali pabaya na kama
angeondoka mapema usikute klabu
ingekuwa pazuri sasa,” alisema Matola.

AZAM FC NA AFRICAN SPORTS NI USIKU LEO CHAMAZI

MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara kati ya vinara, Azam
FC na African Sports ya Tanga
itachezwa kuanzia Saa 1:00 usiku
Uwanja wa Azam Complex, Chamazi,
Dar es Salaam.
Leo kutakuwa na jumla ya mechi tatu
za Ligi Kuu, Dar es Salaam, moja
Uwanja wa Karume kati ya JKT Ruvu
na JKT Mgambo na nyingine Uwanja
wa Taifa, kati ya Simba SC na Mtibwa
Sugar.
Na ili kuwapa fursa watu kuona mechi
zote mbili kubwa za leo kupitia Azam
TV, ndiyo maana mchezo mmoja wa
Dar es Salaam umepelekwa usiku.
Ikumbukwe Azam FC iliyo kileleni
mwa Ligi Kuu kwa pointi zake 35
baada ya kucheza mechi 13,
ikifuatiwa na mabingwa watetezi,
Yanga SC wenye pointi 33 za mechi
13 pia, imepania kushinda mechi hiyo
ili kuzidi kupiga kasi katika mbio za
ubingwa.
Baada tu ya kutolewa katika Kombe
la Mapinduzi visiwani Zanzibar wiki
iliyopita, Azam FC ilirejea Dar es
Salaam mapema kuanza maandalizi
ya mechi dhidi ya Sports.
Na katika kipindi hiki kifupi
wamefanya hadi mazoezi ya ufukweni
kuhakikisha wachezaji wake
wanakuwa fiti kikamilifu.
Mechi nyingine za Ligi Kuu leo ni
baina ya mabingwa wa zamani wa ligi
hiyo, Simba SC na Mtibwa Sugar
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
kuanzia Saa 10:00 jioni.
Mabingwa hao wa zamani wa Ligi
Kuu, wanakutana Jumamosi ya leo
ikiwa ni wiki moja tangu wakutane
katika Nusu Fainali ya Kombe la
Mapinduzi visiwani Zanzibar, Mtibwa
Sugar ikiilaza Simba SC 1-0, bao
pekee la Ibrahim Rajab ‘Jeba’.
Na baada ya kipigo hicho, Simba SC
iliwafukuza makocha wake,
Muingereza, Dylan Kerr na Mkenya
Iddi Salim na sasa Mganda, Jackson
Mayanja ndiye yupo na timu.
Mtibwa Sugar nao wataingia katika
mchezo wa kesho wakiwa na
kumbukumbu ya kufungwa mabao 3-1
na URA ya Uganda katika fainali ya
Kombe la Mapinduzi Jumatano.
Mechi nyingine za ligi hiyo leo ni kati
ya JKT Ruvu na Mgambo JKT Uwanja
wa Karume, Dar es Salaam, Toto
Africans na Prisons Uwanja wa CCM
Kirumba, Mwanza, Stand United na
Kagera Sugar Uwanja wa Kambarage,
Shinyanga, Mbeya City na Mwadui FC
Uwanja wa Sokoine, Mbeya na
Coastal Union na Majimaji wa Uwanja
wa Majimaji, Songea.
Ligi Kuu itaendelea kesho kwa mechi
moja tu, mabingwa watetezi, Yanga
SCwakiikaribisha Ndanda FC Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga SC nayo inarejea kwenye Ligi
Kuu baada ya kutolewa katika Nusu
Fainali ya Kombe la Mapinduzi,
wakifungwa kwa penalti 4-3 na URA
kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika
90.

Jan 15, 2016

ALICHOSEMA KOCHA MPYA SIMBA NA ALICHOSEMA KOCHA MPYA COASTAL UNION

MAMBO mengine ukiyasikia unaweza
kucheka sana, yaani ni kama muvi
fulani ya kichekesho. Jackson Mayanja
alikuwa Kocha wa Coastal Union mpaka
juzi kati, lakini sasa ametua Simba.
Coastal wakamchukua Ally Jangalu
kuziba nafasi yake.
Mayanja kwenye mazoezi yake ya
kwanza kabisa alipowaangalia wachezaji
wa Simba akashika mdomo. Akashangaa
na kujisemea: “Mbona hawa wachezaji
hawako fiti kabisa? Hapa nina kazi
ngumu kwelikweli ya kufanya.”
Alienda mbali zaidi kwa kusema
kwamba wasingefanya lolote msimu
huu.
Sikia sasa. Jangalu akatoa naye ya
mwaka akamwambia: “Mbona hii
Coastal uliyoiacha ndiyo iko unga
zaidi?”

Jangalu amesema anachokifanyia kazi
kikosini humo kwa sasa ni kukijengea
ukakamavu, kwani anasema kikosi
kilikuwa hakina mwelekeo.
“Nimewakuta wachezaji hawana fitinesi,
hawana pumzi na hilo ndilo
ninalopambana nalo kwa sasa, naamini
watarejea kwenye ligi na kasi kubwa
tofauti na walivyoanza,” alisema.
Jangalu ambaye amepokea mikoba ya
Mganda Mayanja aliongeza: “Coastal
itakuwa timu yenye mfano hapa Tanga,
nimejipanga kuiweka kwenye ushindani
mkali.”
Alisema tayari ameishaona wachezaji
wameanza kurejea kwenye ari ya
kujituma na hilo ndilo inalompa
matumaini.
“Wachezaji wameanza kurejea kwenye
mstari na wapinzani wajiandae kwa
upinzani si kama walivyokuwa
wamezoea kuwa ni daraja la kupatia
pointi,” alisema.

FARIDI MUSSA APATA DILI CELTIC

WINGA wa kimataifa wa Tanzania,
Farid Malik Mussa anaweza kwenda
Celtic FC ya Ligi Kuu ya Scotland au
Athletic Bilbao ya Ligi Kuu ya
Hispania kwa majaribio.
Hiyo inafuatia wakala mmoja mwenye
mahusiano mazuri na klabu hizo
kuwasiliana na Azam FC, inayommiliki
Farid akisema Celtic na Bilbao ndizo
klabu ambazo zinahitaji mchezaji aina
ya Farid.
Na wakala huyo amefanikiwa
kuishawishi Azam FC iachane na ofa
ya wakala aliyekuwa anataka
kumpeleka Farid klabu ya FC Olimpija
Ljubljana ya Slovenia.
Taarifa ambazo BIN ZUBEIRY
SPORTS – ONLINE imezipata kutoka
Azam FC zinasema kwamba wakala
huyo anayetaka kumpeleka Farid
Celtic au Bilbao, tayari ametuma
fedha nchini ili mchezaji huyo apate
kozi za masomo ya lugha ya
Kiingereza.
Hata hivyo, mpango wa Slovenia
ulikuwa ni wa mapema zaidi kwa
Farid kwamba kama angekwenda
Hispania kukutana na klabu hiyo kwa
majaribio na kufuzu angesajiliwa
katika diridha hili dogo la Januari.

Lakini haijulikani mpango wa Celtic au
Bilbao kama unaweza kukamilika
katika dirisha hili la usajili au
baadaye.
Na Mtanzania ambaye aliwaunganisha
Azam FC na wakala wa timu ya
Slovenia anaamini klabu hiyo
inayomilikiwa na Alhaj Sheikh Said
Salim Awadh Bakhresa na familia
yake imegoma kumuuza mchezaji
huyo ili abaki kuwasaidia katika Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Ingawa, ndani ya Azam FC wanasema
wanachoangalia ni sehemu ambayo
Farid akienda atapata mafanikio zaidi,
lakini ukweli ni kwamba mchezaji
huyo kwa sasa yuko njia panda.
Baada ya kuzilinganisha ofa za
mawakala wote wawili, Azam FC
imevutiwa zaidi na yule ambaye
anataka kumpeleka Farid Celtic au
Bilbao.
Lakini kutokana na mipango ya Celtic
na Bilbao kuwa bado haijaiva, Farid
anaonekana kutamani aruhusiwe
aende FC Olimpija Ljubljana, ambako
tayari mwaliko upo mezani Azam FC.
Ikumbukwe Farid alitarajiwa kuondoka
wiki iliyopita kwenda Hispania
kuungana na klabu hiyo bingwa ya
Slovenia, FC Olimpija Ljubljana
iliyoweka kambi huko ambako alipewa
siku 10 za majaribio.
Mabingwa hao wa Slovenia waliweka
kambi nchini Hispania kujiandaa na
Ligi ya kwao na Farid alitarajiwa kuwa
nao kwa siku zote 10 akifanya nao
mazoezi kabla ya kuamua
kumununua.

Jan 13, 2016

SAMATTA KUTIKISA ZANZIBAR LEO


MWANASOKA Bora Anayecheza
Afrika, Mbwana Ally Samatta kesho
atatambulishwa kwa Wazanzibari
wakati wa mchezo wa fainali ya
Kombe la Mapinduzi, kati ya Mtibwa
Sugar na URA ya Uganda.
Katibu wa Kamati ya Kombe la
Mapinduzi, Mwinyimvua Khamis
ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS –
ONLINE leo kwamba Samatta
atawasili kesho Uwanja wa Amaan na
kusalimia mashabiki pamoja na kuinua
tuzo yake kuinoyesha.
Samatta, mshambuliaji wa kimataifa
wa Tanzania na klabu bingwa Afrika,
TP Mazembe ya DRC, anatarajiwa
kuketi pamoja na viongozi wakuu wa
serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kesho wakati mchezo huo ukiendelea.

Ikumbukwe ni jana tu Samatta
amepatiwa viza ya kwenda Ubelgiji
kujiunga na klabu ya KRC Genk ya
Ligi Kuu ya nchini humo.
Ingawa bado klabu yake, TP Mazembe
haijatangaza rasmi, lakini taarifa
zinasema mwishoni mwa mwaka jana,
Rais wa klabu hiyo ya DRC, Moise
Katumbi alifikia makubaliano na klabu
hiyo ya Ubelgiji juu ya biashara ya
mchezaji huyo.
Na kwa Samatta kwa kupatiwa viza
ya kwenda Ubelgiji, maana yake
anahitimisha miaka yake minne ya
kuishi Lubumbashi, yalipo makao
makuu ya TPM, klabu bingwa ya
Afrika mara ya tano.
Samatta aliyejiunga na TPM mwaka
2011 akitokea Simba SC aliyoichezea
kwa nusu msimu, akitokea African
Lyon, anaondoka Mazembe baada ya
kuichezea mechi 103 na kuifungia
mabao 60.
Kijana huyo wa umri wa miaka 24,
anaondoka Mazembe akiiachia taji la
Ligi ya Mabingwa Afrika, huku naye
akiibuka mfungaji bora wa michuano
hiyo na kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora
Anayecheza Afrika.
Ikumbukwe ni jana tu Samatta
amepatiwa viza ya kwenda Ubelgiji
kujiunga na klabu ya KRC Genk ya
Ligi Kuu ya nchini humo.
Ingawa bado klabu yake, TP Mazembe
haijatangaza rasmi, lakini taarifa
zinasema mwishoni mwa mwaka jana,
Rais wa klabu hiyo ya DRC, Moise
Katumbi alifikia makubaliano na klabu
hiyo ya Ubelgiji juu ya biashara ya
mchezaji huyo.
Na kwa Samatta kwa kupatiwa viza
ya kwenda Ubelgiji, maana yake
anahitimisha miaka yake minne ya
kuishi Lubumbashi, yalipo makao
makuu ya TPM, klabu bingwa ya
Afrika mara ya tano.
Samatta aliyejiunga na TPM mwaka
2011 akitokea Simba SC aliyoichezea
kwa nusu msimu, akitokea African
Lyon, anaondoka Mazembe baada ya
kuichezea mechi 103 na kuifungia
mabao 60.
Kijana huyo wa umri wa miaka 24,
anaondoka Mazembe akiiachia taji la
Ligi ya Mabingwa Afrika, huku naye
akiibuka mfungaji bora wa michuano
hiyo na kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora
Anayecheza Afrika.