SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Jan 28, 2016

MAYANJA AMTAJA KIPA NAMBA MOJA SIMBA

Na Haji balou
Dar es salaam
Siku chache baada ya kuanza kibarua cha kukinoa kikosi hicho, Kocha Mkuu wa Simba
Mganda, Jackson Myanja, amemtangaza Muivory Coast, Vincent Angban kuwa kipa
namba moja kwenye kikosi chake.
Kocha huyo aliitoa kauli hiyo, hivi karibuni kabla ya mechi ya Kombe la FA dhidi ya Burkina Faso iliyochezwa Uwanja wa Jamhuri Morogoro, mchezo uliomalizika kwa Simba
kushinda mabao 3-0 yakifungwa na HamisvKiiza (mawili) na Said Ndemla.

Kocha huyo, tangu ameanza kibarua hicho amekuwa akimtumia Angban katika kikosi cha kwanza katika mechi mbili za Ligi Kuu Bara
dhidi ya Mtibwa Sugar waliyoshinda bao 1-0 na JKT Ruvu ambayo waliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Mayanja anaona ni sahihi kumtangaza Angban kuwa kipa namba moja kutokana na
kutoruhusu nyavu zake kutikiswa kwenye michezo mitatu.

KOCHA SIMBA AMTAJA KIPA BORA LIGI KUU BARA

Ligi Kuu Bara imekuwa na ushindani mkubwa, mastraika wakisaka kiatu cha dhahabu makocha wakitafuta ushind VPL, Makipa nao hawapo nyuma, Je! kipa bora msimu huu
nani? Kipa wa Azam FC, Aishi Manula, ametajwa kuwa ndiye kipa bora katika Ligi Kuu Bara msimu huu mpaka sasa akiwapiku makipa Deogratius Munishi ‘Dida’ wa Yanga na JumabKaseja wa Mbeya City.

Goal kinatambua mchango wa Aishi Manula katika kikosi chake cha Azam FC, hali kadhalika amekuwa akionyesha jitihada katika
timu ya Taifa ya Tanzania lakini bado
hajafanikiwa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Charles Mkwasa.

Kwa mujibu wa aliyekuwa kocha wa zamani wa makipa wa Simba, Mkenya, Iddi Salim, kwa kipindi cha miezi sita alichokaa Tanzania
kufundisha soka, amemuona Manula kuwa ndiye bora huku akisisitiza kama ataendelea kulelewa kwenye misingi bora, bila shaka atakuja kuwa msaada mkubwa kwa timu ya
taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Akizungumza na waandishi wa habari Iddi Salim alisema “Kwa miezi sita niliyokaa Tanzania, naweza kusema nimewaona makipa wengi katika Ligi Kuu Bara, lakini kipa
wa Azam, Manula, kwangu ndiye ni bora zaidi kuliko mwingine kutokana na mambo anayoyafanya uwanjani ikiwemo kucheza penalti nyingi.

“Lakini pia ukiangalia kwa makipa vijana, Manula anashika namba moja akifuatiwa na Manyika Jr., na kama watazidi kukomaa basi
watakuja kuwa makipa wazuri siku za usoni,”
alisema kocha huyo aliyewahi kuinoa Gor Mahia na timu ya taifa ya Kenya 'Harambee Stars' .
Akizungumzia kipa mwingine bora, Idd alisema Peter Manyika wa Simba, kama atapata matunzo mazuri, mafunzo mazuri na
kuthaminiwa, ndiye atakuwa tegemeo la Tanzania hapo baadaye.