SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

May 5, 2015

MAJAJI WALIMPA USHINDI PACQUIAO, 'MC' AKAMTANGAZA MAYWEATHER AMESHINDA, USHAHIDI HUU HAPA!

UTATA mwingine umeibuka kutoka 'Pambano la Karne' baina ya Floyd Mayweather na Manny Pacquiao lililofanyika Alfajiri ya juzi ukumbi wa MGM Grand, Las Vegas, Marekani. 
Karatasi ya kuandika matokeo raundi kwa raundi ya majaji wote watatu, Glenn Feldman, Burt Clements na Dave Moretti inaonyesha bondia aliyekuwa kona nyekundu, Pacquiao ndiye aliyeshinda pambano, wakati mtangazaji 'MC' wa pambano akamtangaza bondia wa kona ya bluu, Mayweather ndiye mshindi.
Inaonekana kama majaji walijichanganya katika kutumia karatasi hizo na pointi za Mmarekani, Mayweather 'Mtu Pesa' wakizihamishia kwa Mfilipino, Pacquiao, lakini kwa nini iwe kwa majaji wote watatu? 
Hii inazidi kuzua shaka kwamba inawezekana Mayweather alipewa ushindi kimakosa- bali kwa mujibu wa karatasi za majaji mshindi ni Pac Man aliyekuwa anatokea kona nyekundu. 
Karatasi halisi za majaji Glenn Feldman, Burt Clements na Dave Moretti zinavyoonyesha na picha inawaonyesha mabondia hao katika kona zao, Mayweather ya bluu (kushoto) na Pacquiao nyekundu (kulia).

SANCHEZ APIGA MBILI ARSENAL YAICHAPA 3-1 HULL CITY

Chilean forward Alexis Sanchez scored twice as Arsenal beat Hull City 3-1 at the KC Stadium on Monday night
Mshambuliaji wa kimataifa wa Chile, Alexis Sanchez (kulia) akishangilia baada ya kuifungia mabao mawili Arsenal katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Hull City mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu Uwanja wa KC. Bao lingine la Arsenal lilifungwa na Aaron Ramsey wakati la Hull lilifungwa na Stephen Quinn.