SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

May 7, 2016

LIKONGOWELE YAICHAPA MNALANI 4-3

Timu ya likongowele fc imeibuka na ushindi wa goli 4-3 dhidi ya Mnalani fc katika mchezo wa ligi ya Mbuzi Vijana Cup uliopigwa katika uwanja Shule ya Msingi Muungano.

Magoli  ya timu ya Likongowele yamefungwa na Twaha Tido katika  dakika ya 39,SelemaniMpoto katika dakika ya 47 na 60 huku goli la mwisho likifungwa Faraji Mayai na kwa upande wa Mnalani magoli yao yamefungwa na Imani Mohammedi aliyefuga goli mbili katika dakika ya 15 na 25 na goli la mwisho likifungwa dakika ya 74.



Katika mchezo wa leo mchezaji Abbuu Matwiko wa Likogowele fc na Abdulai ndandala wa Mnalani wameoneshwa kadi nyekundu katka dakika ya 85 baada ya kurushiaa matusi.

Baada ya mchezo kumalizika kocha wa Mnalani Kasimu Malunga amesema kuwa walizidiwa nguvu na wapinzani wao lakini pia uzembe wa mabeki wake kushidwa kujipanga vizuri umesababisha wao kupoteza mchezo huo na wanajipaga kufanya vizuri katika mchezo ujao.

Pia kocha wa Likongowele Matisho Saidi amesema anamshukuru Mungu kwa kuibuka na ushindi katika mchezo wa leo na vijana wake wamefuata maelekezo aliyowapa mazoezini.

TAARIFA MPYA KUHUSU FARIDI MUSSA KUCHEZA ULAYA

Na Haji balou
Winger wa Azam na timu ya taifa ya Tanzania Farid Musa amefaulu majaribio yake kwenye klabu ya Deportivo Tenerife ya Hispania ambako tayari pia amefaulu vipimo vya afya na kinachosubiriwa ni makubaliano kati ya klabu
hizo mbili ili kukamilisha deal.

Lakini nyuma ya pazia, kuna story kwamba wakalaambaye alitakiwa kusimamia kila kitu Farid anafanya majaribio akiwa nchini Hispania alilala-mbele kwa madai kwamba mteja wake hana vigezo ambavyo
alivitarajia.

Yusuf Bakhresa ambaye yupo Spain na Fafrid ameutonya mtandao huu  kuwa mawakala wengine ni wababaishaji baada ya wakala huyo kutimkia kusikojulikana na
kumuacha faridi kwenye ‘mataa’.

“Wakala John Sorzano aliyetakiwa kumsimamia Farid Musa kufanya majaribio nchini Hispania
alimtelekeza, baada ya Faridi kutua Hispania yule wakala akamtufuta mtu mwingine ili amsimamie Faridi.

Baada ya huyo wakala kumuona Faridi akaema hana viwango kwahiyo wote wakamtelekea”, anasema Yusuf ambay ilibidi avae majukumu ya kuhakikisha Farid
anapata nafasi ya kufanya amajariio kwenye klabu ya Tenerife.

“Kwa bahati nzuri mimi (Yusuf) nilikuwa hapa, ikabidi nianze kumtunza Farid. Nikafanya
mawasiliano na viongozi wa Tenerife wakakubali kumpa nafasi ya kuendelea kufanya majaribio,
baada ya Farid kuonesha uwezo mkubwa wakamkubali.

Wale mawakala wakapata taarifa
kwamba dogo amekubalika, waanza kuja kutaka kusimamia dili”.
“Mimi nimewapiga chini na nimeuambia uongozi wa Tenerife uandike barua rasmi kwa Azam.
Muda wowote watatuma offer kwa klabu ya Azam na kufanya bishara ya kumuuza Farid”.