SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Feb 15, 2015

KUTOKA NOU CAMP MAPUMZIKO MATOKEO YAPO HAPA

 Live: Barcelona 2-0 Levante
Timu ya Barcelona inaongoza goli 2-0 dhidi ya Levante na sasa ni mapumziko wafungaji wa Barcelona leo ni Neymar dakika ya 17 na Messi dakika ya 38.

MATOKEO ARSENAL MAPUMZIKO

All the FA Cup action - LIVEKutoka uwanja wa Emirates Arsenal inaongoza goli 2-0 dhidi ya Middlesbrough na sasa ni mapumziko shukran kwa Giroud aliye funga magoli yote mawili

AZAM FC NA EL MERREIKH KATIKA PICHA LEO CHAMANZI COMPLEX


KIPRE TCHETCHE AKIMTOKA NA KUMGARAGAZA BEKI WA EL MERREIKH KATIKA MECHI YA KWANZA YA LIGI YA MABINGWA AFRIKA JIJINI DAR ES SALAAM, LEO. AZAM FC IMESHINDA KWA MABAO 2-0. CHEKI PICHA ZAIDI NDANI YA CHAMAZI.









JULIO AREJEA LIGI KUU BARA


Jamhuri Kihwelo 'Julio' amerejea Ligi Kuu Bara baada ya kuikosa nafasi hiyo msimu uliopita baada ya Stand United ya Shinyanga pia kushinda rufaa yake.



Lakini leo kikosi chake cha Mwadui FC kimeshinda kwa mabao 4-1 dhidi ya Burkina Faso ya Morogoro.

Wakati kikosi hicho cha Mwadui FC chini ya kocha huyo wa zamani wa Simba kinarejea ligi kuu. Toto African nayo imetua tena Ligi Kuu Bara baada ya kuichapa Rhino kwa mabao 2-0.

Mwadui imekuwa kinara wa kundi kwa kufikisha pointi 46, wakifuatia na Toto inayonolewa na John Tegete, baba wa mshambuliai wa Yanga Jerry Tegete ina  pointi 45.

JKT Oljoro iliyokuwa pia ikiwania nafasi hiyo, imebaki katika nafasi ya tatu licha ya kushinda kwa bao 1-0 dhidi ya Polisi Tabora.

JOHN BOCCO AWAPA RAHA AZAM FC CHAMANZI

KAVUMBAGU AKISHANGILIA BAADA YA KUIFUNGIA BAO AZAM FC LEO DHIDI YA VIGOGO BARANI AFRIKA, EL MERREIKH YA SUDAN.
Ingawa ilionekana haitawezekana, Azam FC wamebadili mambo na kuonyesha katika soka kweli linawezekana baada ya kuichapa El Merreikh ya Sudan kwa mabao 2-0 katika mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


Azam FC wameshinda mechi hiyo leo katika pambano tamu na la kuvutia katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar.

Didier Kavumbagu ndiye alikuwa wa kwanza kuioatia Azam FC bao baada ya mabeki wa Wasudan hao kujichanganya.

Haikuwa kazi lahisi kwa kuwa El Merreikh walikuwa wasumbufu na walicheza kwa mipangilio na walionyesha kwamba wana kitu wanatafuta.

Nahodha wa Azam FC, John Bocco ambaye alitokea benchi kama ilivyo kawaida yake siku hizi, aliifungia Azam FC bao la pili.

bocco
Bocco alifunga bao hilo kwa kichwa baada ya mpira wa kichwa kutua kichwani mwa Kavumbagu, halafu ukawapita mabeki wa El Merreikh kabla ya kumkuta mfungaji.

Kwa ushindi huo, Azam FC, inalazimika kwenda kuulinda ugenini wiki mbili zijazo ili iweze kusonga mbele.

BABA YAKE DULLY SYKES AFARIKI DUNIA


Dully Sykes ni mmoja ya mastaa ambao wamekuwa kwenye njia ya safari ya Bongo Fleva kwa muda, huenda mapenzi ya baba yake mzazi kwenye muziki kulifanya Dully awe zaidi ya msanii mwenye kipaji cha kuimba peke yake.
Leo FEB 15 majonzi kwa ndugu, jamaa na watu wa karibu na familia ya mzee Abby Sykes, baba mzazi wa Dully ambaye kwa taarifa niliyoipata muda mfupi uliopita ni kwamba mzee Abby Sykes amefariki.
Abby Sykes akiwa na mtoto wake Dully Sykes
Abby Sykes akiwa na mtoto wake, Dully Sykes
Wengi tulimfahamu kutokana na ukaribu wake na Bongo Fleva, aliwahi kuonekana kwenye video za mastaa kadhaa, ikiwemo video ya Daz Baba “Usiku Huu” pamoja na video ya ROMAKidole cha Mwisho Juu“.

Hivi ndivyo alivyo andika Dully Sykes "KWAHERI BABA YANGU MPENDWA.........KIPENZI CHANGU ...........RAFIKI YANGU............MTANI WANGU .........MWALIMU WANGU..............DAMU YANGU.........KIPENZI CHA WATU..........BABA YANGU MPENZI.........SIAMINI EBBY WANGU!!!!! NAKUPENDA NA NTAKUPENDA MPAKA MWISHO WA MAISHA YANGU R.I.P DAD 1952-2015 Ameandika Dully.

SIMBA YAIFUNGA POLISI MORO

Kikosi cha Simba
WEKUNDU wa Msimbazi Simba SC, wameunguruma katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro baada ya kuitandika mabao 2-0 Polisi Moro katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara iliyomalizika jioni hii.
Bao la kwanza la kikosi hicho cha Mserbia,  Goran Kopunovic limefungwa na Ibrahim Hajib ‘Mido’ katika dakika nya 14’ ya kipindi cha kwanza.
Hadi dakika 45’ za kipindi cha kwanza zinamalizika Simba walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili Simba waliendelea kulisakama lango la Polisi na katika dakika ya 63’ ya kipindi hicho, Elius Maguli aliwanyanyua tena mashabiki wa Simba kwa kuandika bao la pili na la ushindi.
Ushindi huo umeifanya Simba ifikishe pointi 20 baada ya kushuka dimbani mara 14 na sasa inazipumulia Yanga na Azam ambazo zipo juu kwa pointi 5 zaidi.
Kujua nafasi ya Simba katika msimamo tunasubiria matokeo ya Kagera Sugar na JKT Ruvu uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.
Kabla ya mechi ya leo, Polisi Morogoro walikuwa nafasi ya tatu wakijikusanyia pointi 19 kibindoni, wakifuatiwa na JKT Ruvu wenye pointi 19.
Kama JKT Ruvu wamefungwa, basi Simba watapanda mpaka nafasi ya tatu nah ii itakuwa faraja kubwa kwa Wana Msimbazi. Mtandao huu unafuatilia kwa umakini matokeo ya huko na yakipatikana utajulishwa.
Azam wanaongoza katika msimamo wakijikusanyia pointi 25 baada ya kushuka dimbani mara 13 sawa na Yanga wenye pointi 25 kwa mechi 13 walizocheza, lakini wana Lambalamba wana wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.

MTIBWA MAJANGA YANAENDELEA



TIMU ya Stand United imeichapa mabao 4-1 Mgambo Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Kambarage Shinyanga.
Ushindi huo unakuja siku chache baada ya wachezaji wa timu hiyo kupewa mafundisho na kocha Msaidizi wa timu ya taifa ya Uholanzi, Patrick Kluivert.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Barcelona alizuru Shinyanga wiki hii kufungua cha soka cha watoto katika sekondari ya Com na akapata fursa ya kuhudhuria mazoezi ya Stand United Uwanja wa Kambarage na kuwapa mawaidha.

Katika mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Mbeya City imelazimishwa sare ya bila kufungana na wenyeji Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wakati Mtibwa Sugar nayo imetoka 0-0 na wenyeji Ndanda, Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.     

YANGA SAFARI MBEYA MECHI MBILI DABO

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KIKOSI cha Yanga SC kinaondoka Alfajiri ya kesho Dar es Salaam kwa basi lao kubwa, kuelekea Mbeya kwa ajili ya mechi na wenyeji Prisons Alhamisi.
Yanga SC watateremka Uwanja wa Sokoine, Mbeya katikati ya wiki kusaka pointi tatu dhidi ya timu hiyo ngumu inayomilikiwa na jeshi la Magereza katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Baada ya mchezo huo, Yanga SC watashuka tena Uwanja wa Sokoine kumenyana na wenyeji wengine, Mbeya City Jumapili katika mfululizo wa ligi hiyo. 

Yanga SC wanakwenda Mbeya, wakitoka kuanza vizuri mechi ya kwanza Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuifunga BDF XI ya Botswana mabao 2-0 jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Na wakitoka Mbeya tu, wataunganisha safari hadi Gaborone kwa ajili ya mchezo wa marudiano na BDF. 
Kocha wa Yanga SC, Mholanzi Hans van der Pluijm bado na mtihani wa kufanyia kazi mapungufu ya safu yake ya ushambuliaji ambayo inashindwa kutumia nafasi nyingi inazotengeneza.

MALINZI KAMISAA MECHI YA IVORY COAST NA AFRIKA KUSINI FAINALI ZA U17 AFRIKA


FAINALI za Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 zinaanza leo mjini Niamey, Niger, wakati kesho Ivory Coast ikifungua dimba na Afrika Kusini, mechi ambayo Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atakuwa Kamisaa.
Mechi za ufunguzi leo ni kati ya wenyeji Niger dhidi ya Nigeria Saa 9:00 Alasiri kwa saa za huko na Saa 11:00 kwa Saa za Afrika Mashariki, wakati mchezo wa pili utakuwa kati ya Guinea na Zambia Saa 12:00 za huko na Saa 2:00 kwa saa za kwetu.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi (katikati) akiongoza kikao cha kabla ya mechi baina ya Ivory Coast na Afrika Kusini leo katika hoteli ya Gaweye mjini Niamey, Niger
Viongozi wa Afrika Kusini katika kikao cha kabla ya mechi na jezi zao
Viongozi wa Ivory Coast katika kikao cha kabla ya mechi leo

Mchezo wa Ivory na Afrika Kusini, utafuatiwa na mchezo kati ya Mali na Cameroon kesho.
Michuano hiyo ya U17 Afrika itaanza leo hadi Machi 2, mwaka huu na timu zitakazofanikiwa kutinga Nusu Fainali, moja kwa moja zitakuwa zimejikatia tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia nchini Chile baadaye mwaka huu.

KOCHA AWAONYA SIMBA LEO


Kocha wa Polisi Moro, Adolf Rishard amewaambia Simba haitakuwa kazi lahisi leo.


Simba inashuka dimbani Jamhuri mjini Morogoro katika mechi ya Ligi Kuu Bara.

Rishard amesema kikosi chake kimejiandaa na ana imani kubwa kuwa wataonyesha mchezo mzuri.


“Tunajua Simba ni timu nzuri, lakini lazima wakubali haitakuwa kazi lahisi. Lengo letu ni kupata pointi tatu,” alisema.

BOATENG KUWEKA REKODI UJERUMANI

Jerome Boateng sasa anataka kuwa nahodha wa kwanza mweusi wa timu ya taifa ya Ujerumani.


Beki huyo wa kati wa Bayern Munich ameonyesha ujasiri huo na kusisitiza angependa kuipata nafasi hiyo.

Boateng ambaye alionekana si lolote Man United, tayari amepata mafanikio makubwa kwa kuchukua makombe mawili makubwa zaidi katika soka.

Kwanza ubingwa wa Ulaya akiwa na Bayern Munich na ubingwa wa dunia akiwa na Ujerumani.


Mara kadhaa alipitia katika manyanyaso ya ubaguzi wa rangi tokea akiwa na miaka 11.

TAMBWE: TUTAPATA USHINDI UGENINI


Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe amesema wangeweza kufunga mabao mengi zaidi katika mechi yao dhidi ya BDF, jana.


Lakini akasisitiza, hata ugenini Botswana, bado wana nafasi ya kurekebisha na kufunga mabao mengine.

"Kweli tungeweza kupata mabao mengi zaidi na lingekuwa jambo zuri.

"Hata hivyo hatujachelewa, tunaweza kufanya hivi; tukarekebisha makosa na baada ya hapo kufunga mabao hata tukiwa ugenini," alisema Tambwe.

Yanga iliishinda BDF kwa mabao 2-0 katika mechi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho, yote mawili yakifungwa na Tambwe.

LUKAKU KUIHAMA EVERTON

25AD132000000578-2953607-image-a-24_1423930901250
Romelu Lukaku anaweza kuondoka Goodison 
KLABU za West Ham na Tottenham zimeanza mipango ya kumshawishi mshambuliaji wa Everton, Romelu Lukaku ili kuinasa saini yake majira ya kiangazi mwaka huu.
Wiki iliyopita Lukaku alisema yuko tayari kuondoka Goodison ikiwa ni msimu mmoja tu tangu asajiliwe kwa paundi milioni 28 majira ya kiangazi kutokea Chelsea.
 
Nyota huyo alisema kama itawezekana anaweza kurudi hata Chelsea, lakini haitatokea.

SIMBA KAMILI KUIVAA POLISI MORO


okwi-na-simba-jifua
MJI wa Morogoro uko shwari kabisa mpaka muda huu! huku wadau wa soka wakisubiri mechi ya jioni uwanja wa Jamhuri baina ya Polisi Morogoro na Mnyama Simba.
Afisa habari wa Simba, Humphrey Nyasio ameuambia mtandao huu kuwa kikosi cha Simba kipo tayari kuchukua pointi tatu muhimu.
“Sisi tuko poa kabisa. Vijana wanasubiri muda ufike wakafanye kazi ya kuzichukua pointi tatu kutoka kwa Polisi Moro”. Amesema Nyasio.
Polisi nao wametamba kuizima Simba katika mechi ya leo.
Kocha mkuu wa klabu hiyo, Rishard Adolf amesema wanajua Simba wamejiandaa kuchukua pointi tatu, lakini mipango yao haitatimia kwasababu Polisi iko imara idara zote.
“Tumejiandaa vizuri, tuko tayari kwa mechi hii”. Amesema Adolf.
Mechi nyingine jioni ya leoinapigwa uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga ambapo Kagera Sugar wanachuana na JKT Ruvu.

MCHEZAJI WA KITANZANIA APATA TUZO QATAR

TANGAZI 3
Kinda Martin Tangazi ambaye amenyakua tuzo ya mchezaji bora wa Aspire Sports Academy ya nchini Qatar kwa mwezi Januari.
Na. Richard Bakana, Dar es salaam
Mvua ya Neema imezidi kumyeshea Kinda wa Kitanzania, Martin Tangazi anayekipiga kunako Academy ya Aspire nchini Qatar baada ya juzi Ijumaa Februari 13, kufanikiwa kuwaburuza Waarabu, Waivory Coast, Wanigeria na Waghana na kujinyakulia tuzo ya mchezaji Bora wa Academy.
Akizungumza na Shaffihdauda.com  akiwa Qatar, Tangazi ambaye aliondoka nchini enzi za utwala wa Leodegar Tenga, mwaka 2013, amesema kuwa haikuwa vyepesi kwake kuchukua tuzo hiyo ya mwezi Januari kufatia upinzani mkali uliopo ndani ya Academy yao ambayo imejaa vipaji lukuki kutoka kila kona ya Dunia hususani Mataifa ya Afrika.
“Kila mwezi lazima achaguliwe mchezaji bora wa Academy nzima, wachezaji wote wanampigia kura mtu wanaye muona anajua zaidi ya wenzake, wote tunavipaji, lakini jitihada zangu binafsi ndio zimeweza kufanikisha mimi kuchukua tuzo hii ambayo huwa ni heshima kubwa sana mchezaji akiipata” Amesema Tangazi ambaye amefikisha tuzo mbili mfululizo baada ya mwezi Desemba 2014 kuichukua kwa mara ya kwanza.
Tangazi amewataja wapinzani wake katika kinyang’anyilo hicho kuwa walikuwa ni Kalamo Ceesy, raia wa Ivory Coast, Yahuza Idris ambaye ni raia wa Nigeria, Emanuel Asuquo wa Ghana, Coulibay Joseph ambaye pia anatoka Ivory Coast pamoja na yeye mwenye kutoka Tanzania, Watano hao ndio waliingia top 5 ambayo pia ilichujwa na kupata nyota watatu ambao mwisho wa siku Kijana huyo mwenyeji wa Mkoa wa Morogoro akaibuka mshindi.
“Zilipigwa kura na wachezaji wenzetu, Mimi na wenzangu wawil ambao ni Yahuza Idris na Emanuel Asuquo ndIyo tulifanikiwa kuingia fainali” Amesema Tangazi ambaye toka ajiunge na Academy hiyo alikuwa akishika nafasi ya pili naya tatu.
Kinda huyo ambaye yupo kwenye kikosi cha U17 cha Aspire Sports Academy, amesema kuwa jumla ya kura 95 zilipigwa kwa watatu hao likini yeye ndiye akaibuka kidedea kwa kuvuna pointi 40, huku  Emanuel Asuquo  raia wa Ghana akiibuka mshindi wa pili kwa pointi 32 na Mnigeria Yahuza Idris akiwa katika nafasi ya tatu akiambulia alama 23.TAGAZI-5
Tangazi amesema kuwa ujio wa  tuzo hiyo kwake ni kama kufunguliwa mlango wa kujituma zaidi ili aweze kutimiza ndoto zake za kutaka kuitikisa Dunia kama ilivyo kwa Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Lionel Messi wa Barcelona.
“Dah!  Nilikuwa naambulia nafasi ya pili na tatu tu lakini nimefurahi Sana, hii imenipa changamoto zaidi ya kuongeza juhudi zaidi ili niweze kutimiza ndoto zangu” Amesema Tangazi ambaye anamkubali sana Mtanzania mwenzake Mbwana Samatta kutokana na kazi anayoionyesha akiwa TP Mazembe.
Mchezaji huyo wa zamani wa Twalipo Camp ya Jijini Dar es salaam, amesema kuwa Tanzania kuna vipaji vingi sana huku akitoa ushauri kwa vijana kujituma na kusimamia ndoto wanazo jiweke katika maisha.
“Kwanza nakubali Tanzania tuna vipaji vingi sana na tunaweza kupambana, Napenda kuwaambia vijana wenzangu kuwa wajitume sana, hiyo pekee ndio siraha ya maisha” Amemalizia Nyota huyo wa Kesho wa Taifa Stars na Dunia.

AZAM KAZI MOJA TU LEO



10847549_808297752551709_8272495318791573431_o-790072
KILA la kheri Azam fc katika mechi yenu ya raundi ya kwanza ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya El Merreick ya Sudan inayopigwa leo jioni uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Ili kusaka ushindi katika mechi hiyo Mliweka kambi ya wiki mbili nchini Uganda, Mkashiriki michuano ya kombe la Mapinduzi na mkaenda kukaa DR Congo kwa wiki moja kushiriki kombe la Mazembe.
Hayo ni maandalizi makubwa kwenu ninyi na leo Watanzania wapo nyuma yenu kuona mtavuna nini.
Sehemu zote mlizoweka kambi na kushiriki michuano hamkufanya vizuri, timu haikuonekana kucheza kwa kiwango cha juu, lakini haitoshi kujenga imani kuwa leo hamtafanya vizuri.
Merreick waliwatoa robo fainali ya kombe la Kagame kwa mikwaju ya penalti mwaka jana na kuwarudisha Dar, leo mnakutana nao katika michuano mikubwa zaidi ya klabu bingwa Afrika.
Wasudan hao ni miongoni mwa timu bora na zenye uzoefu wa michuano hii ambayo Azam fc mnashiriki kwa mara ya kwanza. Kutokana na hili lazima muingie uwanjani na tahadhari kubwa ili kutowaruhusu kupata goli la ugenini.
Michuano hii inahitaji nidhamu ya mchezo hasa unapokuwa uwanja wa nyumbani. Kinachotakiwa ni kuhakikisha unapata ushindi wa zaidi ya mabao 3-0 uwanja wa nyumbani na ukishindwa sana basi ushindi 2-0.
Hii itakusaidia kujiamini zaidi ugenini kwani kazi yako kubwa itakuwa ni kulinda ushindi huo na unaweza kuingia na mbinu ya kujilinda na kutengeneza mashambulizi ya kushitukiza.
Ingawa mfumo huu ni hatari kwani unawakaribisha zaidi wapinzani langoni kwako na kwa kuwa mpira wa miguu ni mchezo wa makosa, unaweza kuruhusu mabao.
Najua kocha wa Azam fc, Mcameroon, Joseph Marius Omog atatumia mbinu ya kushambulia sana kwasababu anahitaji ushindi nyumbani, sio jambo baya, lakini nidhamu ya ulinzi kuanzia safu ya kiungo na ulinzi lazima iwe kubwa.
Merreick watacheza mpira wa polepole na kujaribu kuwatuliza Azam fc watakuwa na kasi, kinachotakiwa kufanyika ni Azam kucheza kwa kasi na kushambulia zaidi.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Azam fc!!

BAYERN BALAA, MTU AGONGWA 8-0

25AD315700000578-2953639-image-a-188_1423931685313
HII sasa sifa!. Mabingwa watetezi wa Bundesliga, Bayern Munich wameifunga Hamburg SV mabao 8-0 katika mechi ya ligi kuu nchini Ujerumani.
Mabao ya Bayern yamefungwa Thomas Muller (2), Arjen Robben (2), Mario Gotze (2), Frank Ribery na Robert Lewandowski wakifunga goli moja moja.
Katika mechi nyingine, Bayer Leverkusen wamepigwa 5-4 dhidi ya Wolfsburg.
Borussia Moenchengladbach wameitandika 1-0 FC Cologne.
Hoffenheim wameshinda 2-1 dhidi ya VfB Stuttgart, wakati Werder Bremen imeichapa 3-2 Augsburg.