Diamond Platnumz akimbusu mpenzi wake Zari katika usiku wa Zari All White Party ndani ya Mlimani City. Zari na Diamond katika pozi ndani ya Mlimani City. Zari na Diamond wakati wakiingia ukumbini. Wasanii wa Yamoto Band wakiwa wametulia tayari kwa shoo. Mpiga Picha Mkuu wa Global Publishers, Richard Bukos (kati) akipozi na watangazaji Sauda Mwilima wa Star TV(kulia) na Khadija Shaibu 'Dida' wa Times FM. Wanausalama wakiwaondoa baadhi ya watu waliokosa tiketi. Baadhi ya mabango waliyokuwa nayo mashabiki wa Diamond. (PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPL)
AZAM
TV, Televisheni namba moja Tanzania ya michezo na burudani- leo
inatarajiwa kuonyesha moja kwa moja mchezo kati ya Yanga SC dhidi ya
wenyeji Etoile du Sahel nchini Tunisia. Mchezo huo
utaanza Saa 1:00 usiku kwa Saa za Kaskazini mwa Afrika na Saa 3:00 usiku
kwa Saa za Afrika Mashariki Uwanja wa Olimpiki mjini Sousse na Azam TV
wataanza Saa 2:00 kutoa maelezo ya utangulizi kupitia chaneli ya Azam
Two. Etoile du Sahel wamethibitisha kufikia makubaliano na Azam TV kurusha mchezo huo ‘Live’ leo. Aidha, kamera za Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) zimezuiwa Uwanja wa Ndege wa Tunis. Watangazaji wa TBC wakiongozwa na Enock Bwigane walizuiwa kutoka na kamera na wakalazimika kuziacha kwenda kuripoti mechi hiyo. Hakuna
tatizo kwa Waandishi wa Habari kuingia Tunisia, bali kamera za video
ndizo zimezuiwa na wakati wafanyakazi wa TBC wanarejea nyumbani
watakabidhiwa vifaa vyao.
WINGA wa Dar Young Africans,
Simon Happygod Msuva amefurahia hali ya hewa ya Tunisia na kusema
wanaweza kuwafunga Etoile du Sahel.
Mchezo huo wa marudiano wa
hatua ya 16 ya kombe la shirikisho utapigwa kesho jumamosi katika dimba
la Olympique de Sousse katika mji wa Sousse kuanzia majra ya saa 3
kamili usiku kwa saa za Afrika Mashariki na Kati.
Katika mchezo wa awali
uliofanyika wiki mbili zilizopita jijini Dar es salaam, Young Africans
ilitoka sare ya bao 1- 1 na Etoile na mshindi wa jumla atacheza hatua
ya mtoano (Play-off) dhidi ya timu zitakazokuwa zimetolewa kwenye Ligi
ya Mabingwa (CL) kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi.
kuelekea katika mechi Msuva
amesema: “Sisi tunashukuru Mungu hali ya hewa iko vizuri, tunaamimi
kesho tunaweza kufanya chochote. Kama wao waliweza kupata goli moja
kwetu nasisi tunaweza kupata kwao”.
Msuva ndiye kinara wa mabao
Yanga na ligi kuu Tanzania bara kwa sasa akiwa ameshafumania nyavu mara
17 akifuatiwa na mchezaji mwenzake wa Yanga Amissi Tambwe mwenye magoli
14.
Mshambuliaji wa klabu ya Azam FC,
Didier Kavumbagu, amefunguka ya moyoni juu ya muenendo wa ligi kuu ya
Vodacom Tanzania bara ambayo inaelekea ukingoni na kusema kuwa
inaendeshwa kwa kujuana zaidi.
Akizungumza na Shaffihdauda.com Mshambuliaji huyo
ambaye alijiunga na Azam FC mwaka jana akitokea Yanga SC, amesema kuwa
kutokana na mchango ambao anauonyesha katika klabu yake hasa pale
mwanzoni mwa ligi, alikuwa anastahili kupewa tuzo ya mchezaji bora wa
mwezi Septemba 2014, lakini anadai kuwa kujuana ndio kulipelekea
akanyimwa na kupewa mchezaji wa Mbeya City Antony Matogolo licha ya timu
yake kufanya vibaya kwa wakati huo.
“Unaweza kusema ligi inaenda kwa
kujuana, ilitakiwa nipewe tuzo ya mchezaji bora mwezi Januari lakini
akapewa wa Mbeya City, Ukiangalia Muda huo nilikuwa ninafunga katika
kila mechi huku timu yangu ikifanya vizuri lakini nikanyimwa akapewa
yeye wakati timu yake ilikuwa inafanya vibaya” Amesema Didier Kavumbagu.
Wadhamini wakuu wa Ligi hiyo ambao ni kampuni ya Simu za mkononi
Vodacom, Mwaka jana walikuja na wazo la kutoa tuzo kwa mchezaji bora wa
mwezi kufatia kazi nzuri na mchango wao katika timu, zoezi ambalo
lilipokelewa vizuri na kusimamiwa vyema na TFF wakishirikiana na Bodi ya
ligi ambao waliteua watu maalumu (Makocha) ili kuhakikisha mshindi
anapatikana kwa haki na kwakuzingatia vigezo husika, Kigezo kimojawapo
kikiwa ni Mchezaji awe ameisaidia timu yake kufanya vizuri ndani ya
mwezi husika.
Hadi Matogolo anakabidhiwa tuzo hiyo ikiwa ni kabla ya Mbeya
city kumpeleka Panone FC kwa mkopo, Wagonga Nyundo hao wa jiji la Mbeya
tayari walikuwa wamepoteza michezo minne mfululizo huku Azam FC
ikichanja mbuga katika kutetea Ubingwa ilioupata msimu uliopita bila
kufungwa pamoja na Mtibwa Sugar, Tukio ambalo lilifanya wachambuzi wengi
wa soka Tanzania kushangaa na kujiuliza ni vigezo gani ambavyo TFF na
Bodi ya Ligi walitumia hadi kumpatia mchezaji huyo tuzo na kuwaacha watu
kama Kavumbagu na Ame Ally ambao kwa muda ule ndio waliokuwa wanafanya
vizuri sana.
Michezo ambayo Mbeya City ilipoteza Antony Matogolo akicheza ni
dhidi ya Ruvu Stars zilitoka sare tasa Septemba 20, Septemba 27 Mbeya
City 1-0 Coastal Unon. Oktoba 4, Ruvu Shooting 0-0 Mbeya City. Oktoba
18, Mbeya City 0-1 Azam FC. Oktoba 26, Mbeya City 0-2 Mtibwa Sugar.
pamoja na ule mchezo wa mwanzoni mwezi Novemba ambapo City walikutana na
JKT Mgambo wakapoteza kwa bao 2-1 Mkwakwani Tanga.
Kavumbagu ameiambia Shaffihdauda.com kuwa kama kweli
haki na sheria zote zingefatwa basi yeye ndio angeibuka kinara wa tuzo
hiyo ambayo inathamani ya Pesa za Kitanzania Milioni Moja.
Mbali na Antony Matogolo kunyakua tuzo hiyo baadhi ya wachezaji
wengine ambao wamewahi kuchukua tuzo hiyo ni pamoja na Salum Abubakar
‘Sure Boy’ wa Azam FC (Oktoba), Rashid Mandawa wa Kagera Sugar
(Novemba), Mahundi (Desemba), Said Bahanunzi wa Polisi Moro (Januari) na
Godfrey Wambura wa Coastal Union (Februari).
Bondia
Floyd Mayweather Jr akiwa kwenye mzani wakati wa kupima uzito ukumbi wa
MGM Grand usiku wa kuamkia leo kuelekea pambano lake na Manny Pacquiao
usiku wa kuamkia kesho kwenye ukumbi huo. Mayweather 'alibalanasi' uzito wa pambano (Paundi za 147 za Welter), tena akiwa amepungua Paundi moja.
Pacquiao naye amepungua Paundi mbili za uzito kamili wa Welter