SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Dec 28, 2015

AVEVA AFUNGUKA SUALA LA KUIBINAFSISHA SIMBA

Image result for RAISI AVEVA SIMBA

Rais wa Simba, Evans Aveva amesema suala la kuibinafsisha klabu hiyo linahitaji ungalifu mkubwa katika mambo kadhaa.

Aveva amesema kuwa Simba inaweza kubinafsishwa lakini lazima uongozi uhakikishe na kujua thamani ya klabu  hiyo ikiwa imeishajiridhisha kama ubinafsishaji kweli una faida.

“Ni suala la kitaalamu, lazima kuliangalia na kutathmini. Kama tutapata uhakika basi ni suala la thamani ya klabu ya Simba. Hapa si kuangalia majengo, sijui magari na uwanja ambao tunataka tuanze kuujenga.

“Lakini kuna suala la maana ya thamani ya Simba kama klabu, hili linahitaji wataalamu waliotulia na kufanya tathmini ya uhakika. Baada ya hapo, litafuatia suala la wanachama kuelimishwa kuwa nini kinafanyika, zipi faida zake.

“Wanachama ndiyo wamiliki wa klabu, lazima waelimishwe na baada ya hapo kuna suala la katiba ambayo inasema wamiliki wa Simba ni wanachama. Ukiangalia hapa utaona hili si jambo dogo,” alisema Aveva.

Mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji maarufu kama Mo alikuwa ameeleza wazi nia yake ya kutaka kuinunua Simba kwa asilimia 51 na zilizobaki 49 zitaachwa kwa wanachama wengine wa Simba. Lakini uongozi wa Simba umekuwa ukisema unalisikia suala hilo kwenye vyombo vya habari tu.

BAADA YA MECHI ZA LEO JUMATATU MSIMAMO LIGI KUU ENGLAND UPO HIVI


HUU NDIO MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA



Rnk
TeamMPWDLGFGA+/-Pts

1
Young Africans1310303052533

2
Azam1210202681832

3
Simba SC127321991024

4
Mtibwa Sugar11731147724

5
Mwadui136431612422

6
Stand United137151411322

7
Tanzania Prisons136341314-121

8
Toto African134541215-317

9
Mgambo JKT12345710-313

10
JKT Ruvu133371520-512

11
Mbeya City132561115-411

12
Majimaji13328823-1511

13
Ndanda12165914-59

14
Coastal Union13166614-89

15
Kagera Sugar13238416-129

16
African Sports132110314-117

WEGER AANZA KUMFUKUZIA CHICHARITO


Kocha Arsene Wenger wa Arsenal sasa anataka kuimarisha safe take ya ushambuliaji.

Wenger anataka kumsajili mshambuliaji nyota wa zamani wa Manchester United, Javier Harnandez maarufu kama Chicharito.

Chicharito sass anakipiga katika klabu ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani na amekuwa aking’ara katika Bundesliga.

Raia huyo wa Mexico, Chicharito ,27, alijiunga na klabu hiyo ya Ujerumani kwa ada ya pauni million 7 na tayari ametupia mabao 19 katika me chi 21 alizoichezea timu take msimu huu.

Kwa sass safe ya ushambuliaji ya Arsenal in a mshambuliaji mmoja tu wa kati ambaye ni Olvier Giroud aria wa Uafaransa huku wengine kama Danny Welbeck wakiwa majeruhi.


Hata hivyo, Wenger anaangalia upande mwingine kama ataweza kumpata bila ada, mshambuliaji nyota wa Leicester City, Riyad Mahrez raia wa Algeria ambaye hata hivyo tayari anatupiwa macho na klabu kibao zikiwemo Man United na Tottenham.

ALICHOSEMEA ABDALLAH BIN KLEB KUHUSU KUFUKUZWA KWA NIYONZIMA

MILIONEA Abdallah Ahmed Bin Kleb aliyemleta kiungo Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima Yanga SC, ameunga mkono uamuzi wa kufukuzwa kwa mchezaji huyo.
Yanga SC leo imevunja Mkataba na kiungo huyo wa kimataifa wa Rwanda kwa madai ya mchezaji huyo wa Amavubi kukiuka vipengele.
“Mimi kwa kweli ninaunga mkono uamuzi uliochukuliwa na uongozi, kwa sababu suala la nidhamu ni la muhimu mno katika timu. Kama mchezaji ameshindwa kuheshimu Mkataba wake, hii ni hatua sahihi,”amesema Bin Kleb akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE jioni ya leo.
Abdallah Bin Kleb (kushoto) akimkabidhi jezi namba nane Haruna Niyonzima baada ya kukamilisha usajili wake kwa mara ya kwanza mwaka 2011 mjini Kigali, Rwanda

Aidha, Bin Kleb ambaye alisajili nyota wengine kadhaa Yanga SC akiwemo kiraka Mbuyu Twite, amewataka wapenzi na wanachama wa klabu kuunga mkono uamuzi wa uongozi.
“Unajua Haruna ni mchezaji mwenye kipaji, ambaye ana wapenzi wengi pale Yanga SC, ambao najua hawataufurahia uamuzi huu. Lakini mimi napenda nichukue fursa hii kuwaomba wana Yanga wote tuungane na uongozi kuafiki hatua hii,”.
“Mchezaji kama ameshindwa kuheshimu thamani aliyopewa ndani ya klabu, wazi huyo hafai. Haruna tulimchukua kwa Mkataba wa miaka miwili awali, baadaye tukamuongeza miwili. Ikaisha na juzi ametoka kuongezewa mwingine wa miaka miwili,”. 
“Sasa nadhani amekwishajiona mwenyeji kwenye timu anafanya anavyotaka bila kuzingatia Mkataba wake unasemaje. Ni sahihi tu hatua iliyochukuliwa,”amesema Kleb.
Aidha, Bin Kleb amesema anaamini hatua iliyochukuliwa itakuwa fundisho kwa wachezaji wengine, ili waweze kuheshimu mikataba yao wakati wote.
Sakata la kufukuzwa kwa Niyonzima Yanga SC, linaanzia mwezi uliopita baada ya mchezaji huyo kuruhusiwa kwenda kuichezea Rwanda katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki, CECAFA Challenge nchini Ethiopia na akachelewa kurejea baada ya mashindano.
Kufuatia hali hiyo, klabu ilimsimamisha kwa muda usiojulikana Niyonzima kabla ya suala lake kupelekwa Kamati ya Nidhamu, ambayo hatimaye imekuja na maamuzi magumu.
Pamoja na Niyonzima kuwasilisha vielelezo vyote vya kumsafisha, lakini uchunguzi wa Kamati ya Nidhamu ulijiaminisha kiungo huyo amedanganya ili kukwepa hatua za kinidhamu.  Image result for NIYONZIMA
Haruna ni mchezaji kipenzi cha mashabiki Yanga SC kama anavyoonekana hapa akitunzwa fedha baada ya mechi
Ulibaini plasta gumu (PoP) alilofunga baada ya kurejea akiwa amechelewa ilikuwa ni ‘geresha’ na vielelezo vingine alivyowasilisha vilikuwa ‘feki’ pia.
Na ikamnasa kwenye picha za video siku za karibuni ‘akijirusha’ sehemu mbalimbali za starehe ikiwemo kwenye onyesho la mwanamuziki Ali Kiba.
Haruna aliyezaliwa Februari 5, mwaka 1990 Gisenyi nchini Rwanda, alijiunga na Yanga SC mwaka 2011 akitokea APR ya kwao, ambako aliwasili mwaka 2007 akitokea Rayon aliyoichezea kwa misimu miwili baada ya kujiunga nayo akitokea Etincelles iliyomuibua mwaka 2005.

SIMBA KUCHEZA NA URA YANGA NA AZAM FC MAPINDUZI CUP

 Image result for timu ya simba
Mabingwa watetezi, Simba SC wamepangwa Kundi A pamoja na URA, Jamhuri na JKU Na Ali Bakari, ZANZIBAR
MABINGWA watetezi, Simba SC wamepangwa Kundi A katika Kombe la Mapinduzi 2016 pamoja na URA ya Uganda, Jamhuri ya Pemba na JKU ya Unguja.
Katika ratiba iliyotolewa leo na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), mabingwa wa Bara, Yanga SC wamepangwa kundi moja, B pamoja na mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, Mtibwa Sugar ya Morogoro na Mafunzo ya Zanzibar.
Simba SC itafungua dimba na Jamhuri Januari 2, 2016 mchezo ambao utatanguliwa na mechi kati ya JKU na URA Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Yanga SC watashuka dimbani siku inayofuata, Januari 3, 2016 kumenyana na Mafunzo, mchezo ambao utatanguliwa na mechi kati ya Mtibwa Sugar na Azam FC.
Nusu Fainali zinatarajiwa kuchezwa Januari 9, wakati Fainali itachezwa Januari 13, Uwanja wa Amaan katika kilele cha sherehe za Mapinduzi.