SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Mar 7, 2015

HARRY KANE APIGA ZOTE MBILI SPURS IKIICHAPA 2-1 QPR

Kane gets to the ball first to head home past Rob Green in the QPR goal
Mchezaji wa Tottenham, Harry Kane (kushoto) akiruka juu kupiga mpira kwa kichwa kumfungia kipa wa QPR timu yake ikishinda 2-1 dhidi ya wenyeji wao hao katika mchezo wa Ligi Kuu ya England. Kane alifunga mabao yote ya Spurs, wakati bao la QPR lilifungwa na Sandro.

JONNY EVANS NAYE ‘JELA’ MECHI SITA ENGLAND

BAADA ya Chama cha Soka England (FA) kumfungia mechi saba mshambuliaji wa Newcastle United, Papiss Cisse kwa kosa la kutemeana mate na beki wa Manchester United, Jonny Evans pia chama hicho kimempa adhabu hiyo beki huyo licha ya kukataa kufanya kosa hilo hapo awali.
FA imemfungia mechi sita kama ilivyotarajiwa, Evans baada ya kuthibitisha tukio hilo katika mkanda wa video wa mchezo huo uliopigwa katika dimba la St.James Park jumatano hii huku Manchester United wakiibuka na ushindi wa 1-0 kwa goli lililofungwa na  Ashely Young katika dakika za majeruhi.

Adhabu hiyo itamfanya beki huyo kukosa mechi ya robo fainali dhidi ya Arsenal itakayopigwa kwenye uwanja wa Old Trafford keshokutwa jumatatu na mechi nyingine atakazokosa ni dhidi ya Tottenham machi 15, Liverpool machi 22, Aston Villa April 4 , Manchester City April 12 na dhidi Chelsea itakayopigwa katika uwanja wa Stamford Bridge April 18.
Aidha kwa upande wa Cisse ambaye amekuwa tegemezi katika klabu ya Newcastle United ameongezewa adhabu ya mechi moja kufuatia na kukutwa na adhabu ya kufungiwa mechi 3 mapema msimu huu kwa kosa la kumchezea vibaya beki wa kulia wa Everton Seamus Coleman.

KAVUMBANGU AING’ARISHA AZAM FC CHAMAZI, JKT ALALA 1-0

 Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
BAO pekee la Didier Kavumbangu, limeipa Azam FC ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Ruvu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam jioni ya leo.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Burundi, Kavumbangu alifunga bao hilo dakika ya 17 kwa kichwa akimalizia krosi ya beki wa kulia, Shomary Kapombe.
Kavumbangu sasa anatimiza mabao tisa katika mbio za ufungaji bora, akifuatiwa na Rashid Mandawa wa Kagera Sugar mwenye mabao saba sawa na Abasalim Chidiabele wa Stand United. 
Didier Kavumbangu ameifungia bao pekee Azam FC leo

Na kwa ushindi huo, Azam FC inatimiza pointi 30 baada ya mechi 16, ikizidiwa pointi moja na vinara, Yanga SC ambao hata hivyo wamecheza mechi 15.
Yanga SC itacheza mechi yake ya 16 kesho, itakapomenyana na mahasimu wao wa jadi, Simba SC, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo, refa Kennedy Mapunda aliwatoa nje kwa kadi nyekundu Richard Maranya wa JKT Ruvu na Salum Abubakar ‘Sure Boy’ wa Azam FC dakika ya 59 baada ya kupigana.
Huo ulikuwa ni mchezo wa kwanza Azam FC tangu imfukuze kocha wake, Mcameron, Joseph Marius Omog leo hii timu ikiongozwa na Mganda, George ‘Best’ Nsimbe.    
Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Erasto Nyoni, Aggrey Morris, Serge Wawa, Frank Domayo/Mudathir Yahya dk60, Himid Mao, Salum Abubakar, Didier Kavumbangu, Kipre Tchetche/Kevin Friday dk76 na Brian Majwega. 
JKT Ruvu; Benja Haule, Haruna Shamte, Napho Zuberi, Cecil Efrem, Mohammed Fakhi, Nashin Naftali, Jabir Aziz, Richard Maranya, Samuel Kamuntu/Alex Abel dk69, Ally Bilal/Emmanuel Pius dk72 na Haruna Adolph/Amos Mgisa dk46.
Kavumbangu akimiliki mpira mbele ya mabeki wa JKT Ruvu leo Chamazi

PICHA: ALI KIBA ALIVYO PERFORM MOSHI JANA.#CHEKETOUR

121stgMkoa wa kwanza kufikwa na tour ya Ali Kiba ni Kilimanjaro ambapo Moshi walipata nafasi ya kushuhudia show ya Ali Kiba kwenye stage na wimbo wa Cheketua kwa mara ya kwanza Club La Liga.
Show hii pia ilisindikizwa na Recho kutoka THT,kwa maelezo ya Ali Kiba mbali na kuiperfoam Chekecha kwa mara ya kwanza Moshi pia imekua mara ya kwanza kwake kuperfoam akiwa na live band Moshi,miongoni mwa watu waliokuwepo ukumbini ni pamoja na baba mzazi wa Mwana FA.
4kbbNimeambiwa kwamba leo ni zamu ya watu wangu wa Arusha kucheketua kwa pamoja kwenye viunga vile Triple A.
364stg
Ali Kiba, Abdu Kiba na baba mzazi wa MwanaFA

335stg
289stg
278stg
244stg
228stg
237stg
175stg
121stg
116stg
72stg
6stg
372stg
26stg
337stg
5kbb

MAN CITY YAMUAHIDI MAMBO KIBAO MAZURI YAYA TOURE AONGEZE MKATABA

KLABU ya Manchester City ipo tayari kumpa ofa ya Ubalozi wa klabu, kiungo wake Yaya Toure atakapostaafu soka.
Nahodha huyo wa Ivory Coast, amebakiza miaka miwili na nusu katika Mkataba wake wa sasa, lakini City inafungua mazungumzo ya kumuongezea Mkataba, kwa sasa akiwa analipwa Pauni 220,000 kwa wiki, na pia kumuahidi kazi nyingine atakapostaafu soka.
Akiwa ana umri wa miaka 31, huo unatarajiwa kuwa Mkataba wa mwisho wa fedha nyingi kwa Toure.
Manchester City are ready to offer Yaya Toure a role as a club ambassador when he retires from playing
Manchester City ipo tayari kumopa Ubalozi wa klabu Yaya Toure atakapostaafu soka

CISSE APEWA ADHABU KAMA YA JUMA NYOSSO EPL

MSHAMBULIAJI wa Newcastle United, Papiss Cisse amefungiwa mechi saba kwa kuhusika kutemeana mate na beki wa Manchester United, Jonny Evans.
Evans kwa upande wake, anaweza kufungiwa mechi sita kama atakutwa na hatia baada ya Chama cha Soka England kuwafungulia mashitaka wote wawili.
Tukio hilo liitokea Jumatano usiku wakati Man United ikishinda 1-0 dhidi ya Newcastle katika mchezo wa Ligi Kuu ya England. Hatima ya Evans inatarajiwa kutolewa leo na FA ya England, uwezekano mkubwa ukiwa ni kufungiwa mechi sita.
Evans (left) and Cisse clash near the half-way line at St James' Park following the unpleasant exchange
Evans (kushoto) na Cisse wakigombana katika mchezo huo Uwanja wa St James' Park 

HIZI NI KURASA ZA MWANZO NA ZA MWISHO ZA MAGAZETI YA MICHEZO LEO JUMAMOSI

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

STURRIDGE ASEMA SASA YUKO 'FULL 100'

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Liverpool, Daniel Sturridge amesema yupo fiti kucheza kila mchezo licha ya kocha wake Brendan Rodgers kumpuzisha katika baadhi ya michezo kwa lengo kumlinda
Baada ya Liverpool kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Burnley katikati ya juma hili kocha Brendan Rodgers alisema amekuwa akimpumzisha mshambuliaji huyo katika baadhi ya mechi ili kumlinda kwani amekuwa akisumbuliwa na majeruhi mara kwa mara.
Sturridge alikaa nje ya uwanja kwa muda miezi mitano mwanzoni mwa msimu huu kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya mguu aliyoyapata wakati akiitumikia timu ya taifa ya England.

Hata hivyo mshambuliaji huyo aliyejiunga na majogoo hao mwaka 2013 akitokea klabu ya Chelsea amekuwa moto wa kuotea mbali tangu arejee akitokea majeruhi na kuifanya Liverpool kuvuna pointi nyingi na kushika nafasi ya tano katika msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza.
"Ninajisikia vizuri sana tangu nirudi kutoka majeruhi,na nipo tayari kucheza kila mechi, sitaki niachwe nje lakini inabidi nifuate anachokipanga kocha " alisema Sturridge.
Liverpool ambayo imeshinda michezo minne iliyopita mfululizo katika ligi kuu itashuka dimbani keshokutwa jumapili katika uwanja Anfield kuwavaa Blackburn Rovers ukiwa ni mchezo wa robo fainali katika kombe la FA.

RAIS KIKWETE ASEMA AZAM FC IMEVUNJA UKIRITIMBA WA SIMBA NA YANGA TANZANIA

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ameisifu klabu ya Azam FC kuvunja ukiritimba wa Simba na Yanga katika soka ya Tanzania.
Akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa studio za kisasa za Azam TV, eneo la Tabata Relini, Dar es Salaam, Rais Kikwete alisema mazoea ya bingwa wa Tanzania ama Simba au Yanga sasa yamevunjwa na Azam FC.
Amewasifu mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa kuleta changamoto mpya katika soka ya Tanzania, jambo ambalo anaamini litazifanya na Simba na Yanga, vigogo vya soka nchini viamke.
Rais Kikwete kulia akiwa ndani ya studio za kisasa za Azam TV. Katikati ni Tido Mhando na kushoto Mzee Bakhresa
Rais Kikwete na Mzee Bakhresa na baadhi ya wafanyakazi wa Azam TV 

Pamoja na hayo, Rais KIkwete amesifu uwekezaji wa kituo cha kisasa cha Televisheni, uliofanywa na kampuni ya Bakhresa Group Limited, wamiliki wa Azam FC na Azam Media Limited, ambao waendeshaji wa Azam TV.
Rais Kikwete amesema aina ya studio aliyoishuhudia leo Azam TV ni sawa na zile za kimataifa anapokuwa katika ziara zake nchi za Ulaya na Amerika.
Pamoja na hayo, Rais Kikwete akawasihi viongozi wa Azam TV kuzingatia maadili ya taaluma ya Habari pamoja na kuweka uzalendo wa taifa lao mbele.
“Studio hii ni sawa na zile kubwa za nje, lakini ipo Tanzania na naomba ibaki kuwa ya Tanzania, mtangaze vizuri nchi yetu. Hata CNN ni ya Marekani, inatangaza mambo ya nje, lakini linapokuja suala la Marekani, inabaki kuwa ya Marekani,”.
“Hata BBC, ni ya Uingereza, inatangaza mambo ya nje, lakini linapokuja suala la Uingereza, inabaki kuwa ya Uingereza. Hata Aljazeera ni ya Qatar, inatangaza mambo ya nje, lakini linapokuja suala la Qatar, inabaki kuwa hya Qatar. Kwa hiyo na nyinyi, naomba TV yenu ibaki kuwa ya Tanzania,”alisema Rais Kikwete.
Rais huyo anayemaliza muda wake Oktoba mwaka huu, amesema kwamba amefurahishwa na uwekezaji huo mkubwa, wenye hadhi na thamani, ambao utatoa ajira kwa Watanzania.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa makampuni ya Bakhresa Group, Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa amesema kwamba kwa kipindi cha miongo minne sasa tangu wameanza shughuli za kuwahudumia Watanzania katika nyanja tofauti- ubora, upatikanaji wa uhakika na gaharama nafuu umekuwa muongozo wao katika biashara zao.
Rais Kikwete katika picha ya pamoja na wamiliki, viongozi na wafanyakazi wa Azam Media Limited

“Nyote ni mashahidi kwa namna ambavyo tumeendelea kuwahudumia Watanzania na kwa namna ya kipekee, Mh. Rais tunawashukuru sana Watanzania kwa kuendelea kutuunga mkono na tunawaomba waendelee kutuunga mkono, kwa hakika ubora na unafuu kwetu ni silaha na jambo muhimu tunalolizingatia katika huduma zetu,”amesema.
Alhaj Bakhresa amesema kwamba, hivi karibuni Makampuni yao yalijinyakulia nafasi za juu katika ubora wa viwango, na kwamba dhamira hiyo wanaielekeza pia katika huduma yao mpya ya matangazo ya Televisheni, ili kuendelea kuunga mkono sera za Taifa na mpango wa kusambaza taarifa sahihi na za haraka kwa Watanzania.
Awali ya hapo, Naibu Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Tido Mhando alisema kwamba katika kipindi hiki kifupi, Azam Media Group imefanikiwa kupata ufanisi wa kuridhisha mno hata kuweza kujijengea heshima na kufahamika vyema hasa katika utangazaji wa michezo na hususan soka.
“Pamoja na kuanzishwa kwa timu ya kandanda ya Azam, ambayo nayo kwa kipindi kifupi sana imeweza kupaa hadi kunyakua ubingwa wa kandanda wa nchi hii, hivi sasa ndiyo klabu bingwa ya kandanda Tanzania, uongozi wa SSB ukaonea uimarishe ari hiyo ya kuendeleza michezo nchini kwa kwenda hatua moja zaidi mbele na ndipo ikazaliwa Azam Media Limited ,” amesema Mhando.
Amesema ushirikiano uliofikiwa haraka baina ya Azam Media na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), umefanikisha kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii kuonyeshwa moja kwa moja kwa mechi za Ligi Kuu ya taifa na kuifanya ligi hiyo hivi sasa iimarike sana na kuwa ya kusisimua zaidi.
“Kama ilivyo Ligi Kuu ya England, hivi sasa ligi yetu hii imefikia mahala ambapo haitabiriki. Mfano Mheshimiwa Rais ni hapa majuzi tu ambapo bila ya shaka vijana wapya wa Stand United ya Shinyanga walikufurahisha tena live kwa kuwachakaza watani wako Simba,”alisema huku akicheka akimtazama Rais Kikwete ambaye ni mpenzi wa Yanga SC.  
Mhando amesema mafanikio hayo ni makubwa ambayo ukichanganya na juhudi za Rais Kikwete  kwenye michezo, Watanzania watarajie kwa kipindi kifupi kijacho wataanza kuvuna matokeo ya kufurahisha kwenye michezo. 
“Na kwa kuwa wewe, Mheshimiwa Rais, vile vile ni mshabiki na mpenzi mkubwa wa mchezo wa kikapu, bila ya shaka siku hizi unapopata wasaa hukosi kuangalia “live” zikionyeshwa na Azam TV, kila ijumaa usiku, mechi za michuano ya ligi ya mpira wa Kikapu ya Dar es Salaam,”.
“Naambiwa kutokana na hatua hii, ule ushindani uliokuwepo zamani ya klabu za Pazi na Tan Blacks umeanza tena kwa kasi kubwa na hivyo kuufanya mchezo wa kikapu kupata maendeleo ya haraka sana,”ameongeza Tido.
Amesema uwekezaji huo wenye thamani ya zaidi ya dola za Kimarekani Milioni 500 umefanywa kwa mpangilio wa kiwango cha juu na wawekezaji wazalendo kwa nia na ari kama ile ile, ya kuifanya Azam TV kuwa BBC ya Tanzania, CNN ya Afrika Mashariki na Al Jazeera ya Afrika,”.
“Tunafahamu ya kwamba wewe ni muumini wa kila jambo kufanywa kwa weledi na ubunifu wa kiwango cha juu Tunakuahidi ya kwamba katika muda siyo mrefu utaweza kuuona weledi huo na kushuhudia ubunifu wa kiwango cha juu sana hapa hapa Azam TV,”.
“Tumejipanga vizuri na tuna mipango mikubwa sana ya kufika kileleni na kuwa Televisheni namba moja nchini hapa katika kipindi kifupi sana kijacho kwani kama ulivyoona tunavyo na kutumia vifaa bora na vya kisasa kabisa vya utangazaji na kuwa hivi sasa tunaimarisha mno idara yetu ya rasilimali watu kwani tunaelewa ya kwamba bila ya wao hatutaweza kutimiza ndoto yetu hii kubwa,”alisema kumuambia Rais Kikwete. 
Viongozi mbalimbali wa dini, siasa na taasisi mbalimbali zikiwemo za vyombo vya Habari pamoja na wasanii nyota walihudhuria zoezi hilo lililofana, likichombezwa na burudani za wasanii wa nyumbani.

MATAJIRI YANGA SC 'WAWATIA MIZUKA' WACHEZAJI WAUE MNYAMA JUMAPILI TAIFA

Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
KIKOSI cha Yanga kimeendelea kujifua kwa mazoezi makali kabla ya kuwavaa watani wao Simba lakini jana jioni kikapokea ugeni ambao ukaachia mshiko wa maji.
Yanga ambayo imeweka kambi Bagamoyo katika hoteli ya Kiromo huku wakifanya mazoezi katika Uwanja wa Chuo cha Uvuvi Mbegani ambapo viongozi wao wa kamati ya mashindano walitinga na kushuhudia maandalizi hayo.
Wakiongozwa na mwenyekiti wao Isaac Chanji aliyeambatana na wajumbe wake Musa Katabaro,Said Ntimizi na Ndama mara baada ta mazoezi hayo walikutana na kikosi hicho katioka hoteli yao na kuwaachia kiasi cha sh milioni 6 ikiwa ni fedha za vocha.
Viungo Nizar Khalfan mwenye mpira mbele ya Haruna Niyonzima mazoezini leo
Said Juma 'Kizota' akimtoka Hassan Dilunga
Matajiri wa Yanga SC, Mussa Katabaro kulia na Rashid Ntimizi kushoto

Akizungumzia maandalizi yao Kocha Mkuu wa timu hiyo Hans Pluijm amefarijika na morali ya wachezaji wae ambapo amesema wanataka kupata ushindi katika mechi zao.
"Unaona jinsi wachezaji wanavyojituma hii ni ishara kwamba tunataka kupata mafanikio katika mechi zetu kuanzia hii ya Jumapili,"amesema Pluijm.

KOPUNOVIC: MBINU ZA PLUIJM ZIPO KWENYE KIGANJA CHA MKONO WANGU

Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
SIMBA SC ipo Zanzibar wakati wowote kuanzia leo usiku inaweza kurejea tayari kwa mchezo wao dhidi ya Yanga lakini kocha wao Goran Kopunovic ametamka kwamba hana wasiwasi na mbinu za mwenzake wa Yanga Hans Pluijm.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY, Kopunovic raia wa Serbia amesema wamefanya maandalizi ya nguvu kuelekea mchezo huo ambapo kwake hana wasiwasi na mbinu za kiufundi za Pluijm kwa kuwa dawa anayo.
Kopunovic amesema wataingia katika mchezo kwa kucheza mpira kwa staili yao waliyojiandaa katika kambi yao ya Zanzibar ambayo timu hiyo imekuwa ikijifua katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Chukwani visiwani humo.
Kocha wa Simba SC, Goran Kopunovic amesema mbinu za mpinzani wake, Hans van der Pluijm anazijua

"Hii ni mechi kubwa hapa Afrika,najua kwamba kutakuwa na presha tofauti katika mchezo huu lakini hakuna kingine tunachotaka zaidi ya kutaka kuona ushindi,"amesema Kopunovic.
"Naijua Yanga,najua mbinu za kocha wao Mholanzi,tunawaheshimu lakini tunamalengo na pointi tatu za mchezo huo tutacheza soka letu litakalotipatia ushindi.