SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Mar 3, 2015

YANGA WAZUA JIPYA KUHUSU AJIBU, WASEMA HAKUPASWA KUCHEZA

Yanga wameibuka na jipya huku wakimtaja mchezaji wa Simba Ibrahim Ajibu hakupaswa kucheza mechi dhidi ya Prisons ambayo alifunga bao tatu au hat trick.


Yanga wamesema Ajibu alikuwa na kadi tatu, lakini Simba walimchezesha kutumia kanuni ambazo bado hazijapitishwa.

Kanuni hizo ni zile zinazoiruhusu timu kuchagua mechi gani mchezaji wake akose na ipi acheze hata akiwa na kadi za njano tatu.

“Kanuni hizo bado hazijapitishwa, lakini Simba wamezitumia. Kama ni haki, basi Ajibu hakupaswa kucheza mechi ile.

“Hilo liko wazi, bodi ya ligi inajua lakini imekaa kimya na Simba wamefanya wanachotaka,” alisema Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Yanga, Jerry Muro.

Katika mechi dhidi ya Prisons, Simba ilishinda kwa mabao 5-0 huku Ajibu akitupia bao tatu peke yake.


Ushindi huo ndiyo mkubwa zaidi kwa Simba msimu huu, hali ambayo angalau imeamsha matumaini kwa mashabiki wake.

KOPUNOVIC AKATAA MECHI YA KIRAFIKI YA USIKU HUKO ZANZIBAR


Kocha wa Simba, Goran Kopunovic amekataa kikosi chake kucheza mechi ya kirafiki usiku.


Wanachama wa Simba walio Zanzibar walikuwa wametafuta mechi ya kirafiki baada ya ombi la kocha huyo lakini ikaonekana inatakiwa kuchezwa usiku.

Kopunovic amechukua uamuzi wa mechi hiyo kwa kusema wao na Yanga Jumapili watacheza jioni, hivyo asingependa kikosi chake kucheza mechi jioni.

Alipozungumza na SALEHJEMBE, Kopunovic alisema mechi ya kirafiki ni maandalizi ya mechi iliyo mbele yao.

"Hauwezi kucheza mechi ya kirafiki usiku halafu ucheze mechi unayojiandaa jioni. Katika uchezaji suala la mazingira pia ni muhimu sana," alisema Kopunovic.

Kocha huyo Mserbia amekuwa akiendelea na mazoezi huku akisaidiana na msaidizi wake, Selemani Matola wakijiwinda kutaka kuitwanga Yanga katika mechi ya Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

SERIKALI YASITISHA MATUMIZI YA TIKETI ZA ELEKTRONIKI TAIFA

Serikali imesitisha matumizi ya tiketi za elektroniki kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia leo (Machi 3, 2015) hadi kasoro zilizopo katika matumizi ya tiketi hizo zitakapoondolewa.
Uamuzi huo umetangazwa leo (Machi 3, 2015) jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Juma Nkamia mbele ya viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na benki ya CRDB.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia (katikati) amesitisha matumizi ya tiketi za Elektroniki katika mechi za soka nchini

YANGA YAGOMEA MECHI YA WANAJESHI

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KLABU ya Yanga imeigeukia kwa sura ya mbogo Bodi ya Ligi Tanzania baada ya kuahirishwa kwa mchezo wao dhidi ya JKT Ruvu na wakasisitiza kwamba hawatakuja uwanjani.
Akizungumza na na waandishi wa habari leo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Yanga Jerry Muro amesema wameshangazwa na mabadiliko ya kila kukicha ya ratiba ya ligi hasa mchezo wao dhidi ya JKT Ruvu ambao walitakiwa waucheze kesho kwa mujibu wa ratiba yao.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Yanga SC Jerry Muro ameshangazwa na mabadiliko ya kila kukicha ya ratiba ya ligi 

Muro amesema bodi ya ligi imeonyesha kwamba haitaki Yanga ifanikiwe katika kampeni zao za kombe la Shirikisho kwa kuitaka kuucheza mchezo huo Machi 11 ikiwa ni siku tatu kabla ya kushuka katika Uwanja wa Taifa kucheza na Plutinum ya Zimbabwe.
"Ratiba tuliyonao inayonyesha kwamba kesho kulitakiwa tucheze dhidi ya JKT Ruvu lakini hawa wenzetu kwa matakwa yao wamebadilisha ratiba pasipo kutuhusisha hii kwetu tunaichukulia kama hujuma,"amesema Muro.
"Tumewaambia tangu jana kama wameufuta mchezo wa kesho na badala yake wakaupeleka Machi 11 Yanga hatutakuja uwanjani kwakuwa huo sio uzalendo hatuwezi kuacha maandalizi ya mechi yetu ya kimataifa kuangalia mechi ya ligi.

SOFAPAKA YAWAPA YANGA SC NJIA MTEREMKO YA KUWANG’OA WAZIMBABWE

Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
YANGA SC imepata msaada mkubwa wa taarifa za wapinzani wao katika kampeni ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika kwa kupata siri nzito juu ya klabu ya Platinum ya Zimbabwe.
Yanga ambayo jana ilirejea nchini ikitokea Botswana ilikokwenda kuwatupa nje ya mashindano BDF ya huko wakiwa njiani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta viongozi wao walikutana na Rais wa Sofapaka Elly Kalekwa ambaye timu yake ilifungwa 4-2  na Platinum.
Mabosi wa Yanga wakiongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Mussa Katabaro, Katibu wa timu hiyo Dk. Jonas Tibohora na kocha wao Hans Pluijm wametakiwa kuwa makini na Plutinum hasa katika mipira ya faulo,krosi na kona kufuatia Wazimbawe hao kuwa wazuri kwa vichwa.

Rais wa Sofapaka Elly Kalekwa (wa pili kulia) akizungumza na viongozi wa Yanga SC Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta jana 

Kalekwa amewaambia Yanga Plutinum ambao wachezaji wao wengi ni warefu kwa maumbo pia wako vizuri katika viungo wa pembeni akiwataka Yanga kuwaanda vyema mabeki wao wa pembeni.
"Jichungeni sana na mipira ya juu mkizubaa wanawafunga lakini pia jiangalieni sana na mawinga wao ni hatari wanachezeshwa na kiungo mmoja ana rasta,"amesema Kalekwa
"Msifanye makosa kama tuliyofanya sisi hakikisheni mnawamaliza nyumbani kwenu kwao hawa ni hatari sana wana fedha za kutosha mkienda kule hakikisheni mnawatuma watu mapema kabla ya timu haijakwenda.

KURASA ZA MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI YA LEO JUMANNE TAREHE 3/3/2015


.


.
.
.
.
.
.
.

Ads by Dynamo ComboAd Options
.
.
.
.
.
.

ALICHOSEMA MPOKI KUHUSU MSIBA WA KAPTENI KOMBA

Mpoki IIMsanii wa Kundi la Orijino Komedi, Mujuni Sylivery aka Mpoki moja ya vitu ambavyo aliwahi kuvifanya katika kazi yake ya uchekeshaji ni pamoja na kuigiza sauti ya marehemu, Kapteni John KOMBA ambaye amefariki February 28.
Leo Mpoki amesikika kwenye Leo Tena @CloudsFM, alianza kuzungumzia namna alivyopokea taarifa za msiba huo; “..Mtu akishatoweka kwenye ulimwengu akifariki dunia inauma kwa sababu mtu unayempoteza leo huwezi kumpata tena.. lakini ukimpoteza mbuzi utaenda Vingunguti utamnunua na sherehe itaendelea.. Kitendo cha kufariki mtu yoyote hata kama hajulikani ni pengo kubwa tu
Imeniathiri kwa kisanii kwa kuwa nilikuwa namuwezea, kidogo alikuwa hapendi lakini ilivyokuja akatulia.. Watu wakamwambia bwana hawa watoto tu.. Ukimuiga mtu ana mazuri huwezi kumuiga kwa mabaya tu.. ana mazuri yake..Ikanipa wigo mpana kwenye kazi yangu ya kubuni sauti yake, vitendo..
mwisho wa siku kaondoka pengo lake halitozibika.. Kama kuna la kufanya kuhusu yeye kwa kumuenzi sitokuwa nyuma, nitafanya ili mradi lisimvunjie heshima Marehemu, familia yake, jamii, viongozi wenzake Bungeni na watu wote ambao kawaacha kwenye jimbo lake sasa hivi wapweke..

SAMATTA ARUHUSIWA KUONDOKA TP MAZEMBE

15922_870694186307442_880608052995095050_n
Samatta (kushoto) alifanya majaribo CSK Moscow ya Urusi
Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
Mshambulizi wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta ameweka wazi kuwa ataachana na mabingwa mara nne wa kihistoria wa Afrika, TP Mazembe mara baada ya kumalizika kwa mkataba wake. 
Akizungumza na mwandishi wa mtandao wa www.shaffihdauda.co.tz muda mfupi uliopita mshambulizi huyo wa Taifa Stars amesema kuwa hana furaha katika timu hiyo ya Congo.

 Samatta ambaye alipata nafasi ya kufanya majaribio katika klabu ya CSKA Moscow ya Urusi mwezi uliopita amepewa ofa nyingi barani ulaya na kama ataendelea kuchezea TP basi atakuwa ni mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi barani Afrika. 
Hivi karibuni kuna vyombo vya habari ambavyo viliripoti kuwa mchezaji huyo ana furaha kuendelea kuichezea TP lakini amesema huo ni uzushi mkubwa.

  ” Sina furaha hapa ( TP mazembe) nitaondoka wakati wa majira ya usajili katikati ya mwaka na sitaongeza mkataba” anasema Samatta, ni wapi anakwenda, nini kinachomuondoa TP Mazembe,
 
Haya hapa mahojiano kati ya Mbwana Samatta na mwandishi wa mtandano huu, Baraka Mbolembole….

www.shaffidauda.co.tz;  Samatta kumekuwa na taarifa kwamba  licha ya baadhi ya vikwazo unavyokutana navyo unapopata fursa ya kucheza Ulaya katika klabu yako ya TP Mazembe bado unafurahia kuwepo ndani ya timu hiyo. Je, ni kweli una furaha kuendelea kuichezea TP?

Mbwana Samatta; Hahaha, ni uongo huo, sina furaha kuendelea kucheza hapa na wala sitaongeza mkataba mpya, nadhani nitaondoka wakati wa usajili ujao wa kiangazi.

www.shaffihdauda.co.tz;  Kwa niaba ya wasomaji wa webisite hii ( www.shaffihdauda.co.tz) ningependa kufahamu nini kilitokea katika majaribio yako CSKA Moscow ya Urusi klabu ambayo ilikupatia nafasi ya kwenda kufanya majaribio. Ni kweli sababu za majeraha ndiyo zimekunyima nafasi?

Mbwana Samatta; Kwa kweli suala la majeraha lilikuwa ni sababu ndogo sana na mahitaji ya CSKA, lakini tatizo lilikuja katika suala la makubaliano kati ya CSKA na TP. Kiukweli Mazembe walihitaji kiasi kikubwa sana ambacho ambacho ni vigumu kwa klabu ya ulaya kutoa kwa mchezaji anayecheza Afrika.

Ukichanganya na sababu za kimkataba ambao umebaki mwaka mmoja kati yangu na TP ilibidi CSKA washindwe kwa sababu hizo na si majeraha kwa kuwa walinihati hivyohivyo. Baada ya hapo nilizungumza na klabu kuhusu ‘ future’ yangu, so nasubiri muda ukifika nitaingia nao makubaliano flani hata kabla muda wangu haujakwisha na TP.

www.shaffihdauda.co.tz; Unamaanisha kuwa bado kuna nafasi kubwa yaw ewe kujiunga na CSKA Moscow?

Mbwana Samatta;  Nafasi ipo ya mimi kujiunga na CSKA pia bosi wa klabu hiyo amekuwa na urafiki na klabu nyingi za ulaya hivyo kuna uwezekano mkubwa akaninunua kwa sababu ya klabu nyingine, nadhani umenielewa.

www.shaffihdauda.co.tz; Kwa nini unaondoka TP Mazembe?

Mbwana Samatta;  Nadhani imetosha kwa sisi kuendelea kucheza barani Afrika, sasa nataka kuishi katika ndoto zangu.

www.shaffihdauda.co.tz; Kila mwanasoka huwa na ndoto kubwa, ndoto yako imeegemea wapi kimpira?

Mbwana Samatta;  Napenda kucheza LIGA BBVA, ndoto yangu ni kucheza ligi kuu ya Hispania, La Liga.

www.shaffihdauda.co.tz; Miaka minne ndani ya klabu kubwa Afrika TP Mazembe imekufunza nini ukizingatia ulitoka Tanzania ukiwa U18?

Mbwana Samatta; Kwa kweli nimepevuka kwa kiasi kikubwa kimpira na kiakili, tayari nimecheza dhidi ya klabu zote kubwa barani Afrika. Nimepata uzoefu mkubwa sana na kujiamini  kwa kiasi kikubwa. Nashukuru kwa kila kitu ambacho TP wamekuwa wakiendelea kufanya dhidi yangu. Nimejiiimarisha kutoka mchezaji kijana hadi kuwa mtu jasiri ndani ya uwanja.

www.shaffihdauda; Je, umezungumza na mmiliki wa TP, Moise Katumbi kuhusu kuondoka kwako kabla ya kumalizika kwa mkataba, amesemaje?

Mbwana Samatta; Nilizungumza naye sana tu na amekubaliana name hivyo muda utakapofika amesema hatokuwa na kipingamizi tena, ataruhusu niondoke.

AZAM WAACHE KULALAMIKA HILI NDIO FUNZO LA KUCHUKUA BAADA YA RABAT, NAMPULA NA KHARTOON....


azammm
Na Baraka Mbolembole, Dar es  Salaam,
AZAM FC walikutana na ‘ matokeo mabaya’ kisha kuondolewa katika michuano ya CAF Champions League. IKicheza kwa mara ya kwanza katika michuano hiyo, huku ikiwa ni mara ya tatu kwa klabu hiyo kucheza michuano ya vilabu Afrika tangu ilipoanzishwa mwaka 2007 na kupanda ligi kuu msimu wa 2008/09, Azam ilikutana na ratiba ngumu mwanzo tu. Ratiba dhidi ya Azam FC vs El Merreikh, na ile ya Al Hilal vs KMKM ilikuwa ni kama ‘ kuwaondoa wawakili wa Tanzania’ na kuzipitisha timu zenye mvuto wa michuano hiyo kutoka nchini Sudan Kaskazini.

Azam walishinda ushindi wa ‘ wastani’ dhidi ya Merreikh katika uwanja wa nyumbani, ushindi wa mabao 2-0 katika uwanja wa Azam Complex wiki mbili zilizopita uliambatana na maandalizi ya hukakika.  Baada ya kufungwa 3=0 katika uwanja wa Al Merreik, Khartoon, Sudan, Azam wameshusha lawama zote kwa waamuzi. Mwamuzi raia wa Zambia analalamikiwa kwa namna alivyokuwa akitoa  uamuzi wa upande mmoja ikiwemo ‘ kiki ya penalti’ iliyochezwa na kipa Aishi Manula katika kipindi cha kwanza.

Umefika wakati sasa wa Azam FC kusahau matokeo hayo na kurudisha akili katika michezo ya ligi kuu ili wafanikiwe kupata nafasi hiyo kwa mara nyingine mwaka ujao. Kucheza dhidi ya Merreik katika michuano yako ya kwanza ya klabu bingwa si ratiba rahisi licha ya wengi kuiweka Azam katika ‘ tawi la klabu shindani Afrika Mashariki na Kati’.  LIcha ya kuondolewa katika michuano, Azam FC wanatakiwa kubaki na funzo ya kile kilichowakuta Khartoon na kuchukulia ni sehemu ya mafanikio kwa klabu zote zenye malengo makubwa Afrika.

Merreikh na mahasimu wao wa soka la Sudan, Al Hilal mtazamo wao katika michuano ya vilabu Afrika ni kucheza walau ‘ Ligi ya Mabingwa’. Kuondolewa katika hatua yoyote ile nje ya nane bora ni kufeli kwa malengo yao. Kabla ya kutoka kwa ratiba ya michuano Azam FC ilikuwa na malengo makubwa, nafikiri walikuwa sawa kabisa kuwa na mtazamo wa kufika nane bora ama hatua ya 16 bora, lakini baada ya ratiba kupangwa matuaimi hayo yalitegemea zaidi matokeo ya gemu mbili dhidi ya Merreikh.

Kuishinda timu hiyo ya Sudan kwa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza ni kitendo ambacho kinaikomoza haraka timu yoyote katika michuano ya kimataifa. Merreikh walikuwa na hofu dhidi ya mabingwa hao wa Tanzania mara baada ya kupangwa kwa ratiba ndiyo maana waliamua kufanya maandalizi ya uhakika kwa zaidi ya mwezi mmoja nchini Qatar huko walicheza na klabu kubwa za Ulaya kama Schalke O4 ya Ujerumani.  Wameacha funzo lingine kwa Azam FC kuwa katika michuano ya kimataifa ni lazima ufanye maandalizi makubwa nay a muda mrefu bila kujali unacheza na timu gani.

AZam wameshindwa kufunga walau goli moja ugenini ikiwa na washambuaji wa kimataifa, Kipre Tchetche, Didier Kavumbagu na Brian Majwega, bado natafakari matokeo yao lakini naendelea kujifunza kuwa klabu za Tanzania zinahitaji kujifunza zaidi kuhusu ‘ fitna za nje ya uwanja’ kama zinahitaji kufanya vizuri barani Afrika . Simba iliifunga Al Ahyl Shandy ya Sudan kwa mabao 3-0 katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Shirikisho mwaka 2012, wakacheza dakika 45 ugenini bila kuruhusu bao lakini baada ya dakika 90 matokeo yakawa Shandy 3-0 Simba na hivyo mechi ikaamuliwa kwa mikwaju ya penalti na Simba ikashindwa na kuondolewa.

Kwa nini walifungwa mabao 3-0 ndani ya dakika 35 za mwisho?. Wakati mwingine waamuzi ni tatizo lakini bado klabu zetu zinashindwa ugenini kutokana na kurudia makosa yale yale tu. Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika Azam FC walikuwa nyuma kwa bao 1-0 lakini baadaye wachezaji wakaanza kupoteza umakini na kujikuta wakifungwa. Michuano ya Tatu Afrika,

Azam FC waendelee kujifunza na kuchukulia vichapo vya Rabat, 2013, Nampula, 2014 na Khartoon, 2015 kama sehemu ya kujiimarisha nag emu muhimu za marejeano. Waliishinda FR Rabat ya Morocco kwa bao 1-0 Dar es Salaam, waliishinda Fereviarrio de Nampula kwa bao 1-0 Dar es Salaam, kisha wameifunga El Merreikh 2-0 Dar es Salaam, lakini walipoteza michezo yote ya ugenini na kuondolewa mashindanoni.

CHANZO SHAFFIHDAUDA.COM

HUYU NDIE ALIYECHUKUA NAFASI YA OMOG AZAM FC

Azam FC imetangaza kumfukuza kazi Kocha Joseph Omog raia wa Cameroon.

Pamoja na Omog, Msaidizi wake, Ibrahim Shikanda ametimuliwa na mikoba amepewa George Best Nsimbe raia wa Uganda ambaye ni msaidizi wake namba moja.
ALIVYOKARIBISHWA NA UONGOZI WA AZAM FC, MWENYEKITI WA AZAM FC, SAID AKIMKARIBISHA.


Best ambaye ameanza kazi Azam FC msimu uliopita, sasa ndiye ataongoza jahazi.

Ingawa uongozi wa Azam FC haujaanika kila kitu, lakini inaonekana Omog anaondoka baada ya Azam FC kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kufungwa mabao jumla ya mabao 3-2.

Azam FC ilianza kwa kushinda 2-0 jijini Dar lakini ikakubali kipigo cha mabao 3-0 jijini Kharthoum.

Omog ndiye aliyeipa Azam FC ubingwa wake wa kwanza wa Ligi Kuu Bara na ushindi wake wa kwanza katika Ligi ya Mabingwa Afrika .

PLUIJM AFURAHIA SIKU SABA ZA MAANDALIZI DHIDI YA SIMBA


Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema wiki moja ya maandalizi kwa ajili ya Simba, itawasaidia sana.

Yanga inaivaa Simba katika mechi ya Ligi Kuu Bara utakayopigwa Jumapili ijayo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Tayari Yanga iko kambini mjini Bagamoyo ambako ilipitiliza moja kwa baada ya kutua nchini ikitokea Botswana.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Pluijm amesema kuwa wiki moja itawasaidia kurekebisha makosa kadhaa.
“Makosa hayaishi katika mpira, lakini wiki moja ya maandalizi itatupa nafasi nzuri.
“Ukiona timu imecheza vizuri ujue mlichojifunza mmekifanyia kazi, mkishindwa kufanya vizuri utaona kuna sehemu mmepungukiwa.
“Soka ni lazima urudie kujifunza, leo, kesho na siku nyingine. Hivyo siku zaidi ya tano, zitasaidia kufanya marekebisho kwa maneno na mafunzo ya vitendo,” alisema.

Yanga imecheza mechi ya mwisho dhidi ya BDF XI ya Botswana na kufanikiwa kuitoa katika Kombe la Shirikisho kwa jumla ya mabao 3-2.

WINGA WA SUNDERLAND AKAMATWA NA POLICE


Winga mwenye kasi wa Sunderland, Adam Johnson amekamatwa kwa tuhuma za kufanya ngono na msichana mwenye umri wa miaka 15.

Kutokana na tuhuma hizo, Sunderland maarufu kama Black Cat imemsimamisha Johnson aliyewahi kukipiga Man City.

Johnson, alikamatwa akiwa kwenye jumba lake la kifahari lenye thamani ya pauni milioni 1.8.


Gazeti la DailyMail la Uingereza limeeleza, Polisi wasio na magwanda alifikika katika nyumba hiyo na kumtia nguvuni Johnson ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya England.