SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Feb 10, 2015

SASA NI ALI KIBA NA CHRIS BROWN

Uongozi wa muziki nchini marekani unao muongoza msanii wa R&B Chris Brown umetoa taarifa kwa uongozi wa muziki Tanzania unao muongoza msanii kutoka Tanzania ALI KIBA msanii ambae yupo chini ya uongozi wa Kampuni za SAMSUNG. Kwa taarifa zilizopo katika mtandao wa VIP Beats nchini marekani zinaeleza kua tarehe 24 mwezi wa 11 mwaka 2014 uongozi wa msanii Chris Brown ulipokea maombi ya muungano wa wasanii wawili kufanya wimbo wa pamoja kati ya msanii Ali kiba na Chris Brown maombi hayo yaliambatanishwa na Softcopy zilizobeba nyimbo tatu za msanii Ali kiba ikiwemo SINGLE BOY, MWANA pamoja na wimbo aliofanya katika project ya ONE 8. Uongozi wa Chris Brown umethibitisha kupokea taarifa za maombi hayo na umeonesha kupenda sauti ya msanii Ali kiba na kutoa tamko kua wapo tayari kusimamia kazi ya pamoja itakayofanywa na wasanii hawa. Upande wa msanii Chris Brown amesema hana tatizo yupo tayari kushirikiana na msanii Ali kiba kwani alipata nafasi ya kutazama project ya One 8 na ameona kiwango cha msanii Ali kiba kinaridhisha japokua anahitaji marekebisho madogo sana. 

Tunampongeza msanii Ali kiba kwa juhudi zake tunamtakia kila lakheri katika kazi hii, kuipata habari hii kamili tembelea mtandao wa VIP Beats, Channel 0 au unaweza kuipata katika American Spring news.

PICHA; SIMBA YAENDELEA KUJIFUA

CHINI YA KOCHA GORAN KOPUNOVIC, SIMBA IMEENDELEA KUJIFUA KATIKA KAMBI YA JESHI IKIWA NI MAANDALIZI KABLA YA KUIVAA TIMU NGUMU YA POLISI MORO, JUMAPILI.





HII INAIHUSU VIDEO MPYA YA DIAMOND

.
.
Video ya Nitampata wapi ya Diamond Platnumz baada ya kupitishwa kuchezwa kwenye kituo cha TV cha kimataifa   cha Trace Urban cha Ufaransa,  bado imeendelea kufanya vizuri mpaka kupewa nafasi ya kuchezwa kama Smash Hit kwenye kituo hicho.
Hizi ni baadhi ya picha kutoka zikionesha video hiyo ikichezwa kama #SmashHit
.
.
.
.
.
.
DSC_0620
.

.

BEKI KISIKI YANGA KUWAKOSA WA BOTSWANA

YANGA SC itamkosa beki wake mahiri chipukizi, Edward Charles Manyama katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya BDF XI ya Botswana mwishoni mwa wiki.
Edward alitoka nje dakika ya 39 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bada jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya Mtibwa Sugar baada ya kuumia enka na nafasi yake ikichukuliwa na Juma Abdul.
Na leo Daktari wa Yanga SC, Juma Sufiani amesema mlinzi huyo wa pembeni kushoto atakuwa nje kwa siku 10 akiuguza maumivu yake, maana yake Jumamosi atakosekana.
Edward Charles jana baada ya kuumia

Lakini hapana shaka kuumia hadi kukosekana kwa beki huyo aliyesajiliwa msimu huu kutoka JKT Ruvu si pigo sana, kwa sababu yupo beki chaguo la kwanza katika nafasi hiyo, Oscar Fanuel Joshua.
Kuna uwezekano Charles akaukosa hata mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho, lakini hakuna shaka mapema Machi atakuwa fiti kabisa kuanza tena kufanya kazi Jangwani.

AZAM ,MTIBWA PATACHIMBIKA KESHO

AZAM FC kesho watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, mchezo ambao utafanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Azam FC, itahitaji ushindi katika mchezo huo ili kurejea kileleni mwa Ligi Kuu, baada ya juzi, wapinzani wao wakuu katika mbio za ubingwa, Yanga SC kushinda 2-0 dhidi ya hao hao Mtibwa.

MECHI ZIJAZO LIGI KUU

Feb 11, 2P15
Azam vs Mtibwa Sugar
Feb 14, 2015
Ndanda vs Mtibwa Sugar
Coastal Union vs Mbeya City
Stand United vs Mgambo Shooting
Feb 15, 2015
Polisi Morogoro vs Simba
Kagera Sugar vs JKT Ruvu
Feb 21, 2015
Mbeya City vs Yanga
Kagera Sugar vs JKT Ruvu
Ndanda vs Coastal Union
Mgambo Shooting vs Mtibwa Sugar
Feb 22, 2015
Stand United vs Simba
Azam vs Tanzania Prisons
Feb 25, 2015
Mbeya City vs Ruvu Shooting

Ushindi wa Jumapili umeipeleka kileleni Yanga SC baada ya kufikisha pointi 25 kutokana na mechi 13, ikiishushia nafasi ya pili Azam yenye pointi 22 za mechi 12.
 
Azam FC imecheza mechi tano bila kushinda, tangu iliposhinda mara ya mwisho dhidi ya Kagera Sugar mabao 3-1 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza Januari 20, mwaka huu.
Baada ya ushindi huo uliotokana na mabao ya mawili Mrundi Didier Kavumbangu na Kipre Tchetche wa Ivory Coast, Azam FC ilitoa sare ya 1-1 na Simba SC.
 
Kutoka hapo, ikachukua mapumziko ya wiki moja katika Ligi Kuu ili kwenda Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa michezo ya kirafiki kujiandaa na mchezo wa kwanza Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika, dhidi ya El Merreikh mwishoni mwa wiki.
 
Wakiwa Lubumbashi, Azam FC walifungwa mechi mbili 1-0 mara zote dhidi ya wenyeji TP Mazembe na Don Bosco ya Kinshasa, wakati mchezo mwingine walitoa sare ya 2-2 na ZESCO United ya Zambia, mabao yao yote yakifungwa na kiungo Frank Domayo.    
Waliporejea kutoka Lubumbashi, mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu, walitoa sare ya 2-2 na wenyeji Polisi Jumamosi mjini Morogoro na sasa kesho, kocha Mcameroon Joseph Marius Omog atakuwa anawania ushindi wa kwanza baada ya mechi tano. 
 
Mara ya mwisho, timu hizo zilikutana katika Robo Fainali ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar mwezi uliopita na Mtibwa Sugar ikashinda kwa penalti 7-6 katika Robo Fainali baada ya sare ya 1-1.

MAN CITY WAMTAKA DIEGO SIMEONE

KLABU ya Manchester City inaendelea kumfuatilia kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone kwa ajili ya kumchukua.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England, wameachwa pointi saba na vinara Chelsea baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Hull City.
 
Timu hiyo ya Manuel Pellegrini sasa ipo kwenye hatari ya kumaliza msimu bila taji baada ya kutolewa kwenye mashindano yote ya nyumbani katika hatua za mwanzoni. Mbali na mbio za ubingwa wa Ligi Kuu, zaidi Man City itajaribu bahati yake kwenye hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Diego Simeone is being monitored by Manchester City as their season continues to falter
Diego Simeone yuko kwenye rada za Manchester City 

SUPER SIMEONE 

7- Baada ya miaka tisa ya ukocha, Simeone tayari ameshinda mataji saba — yakiwemo La Liga, the Copa del Rey na Europa League.
64.3 ndiyo wastani wa asilimia za ushindi wake kwa misimu yake mitatu na nusu
4- Mara kadhaa, Simeone amewafunga wapinzani wake kama Real, na pia wametoa sare mbili
Februari 24, mwaka huu, Manchester City itamenyana na Barcelona kwa mara ya pili mfululizo na kipigo kingine kwa Pellegrini kitaibua maswali juu ya mustakabali wa Mchile huyo.
Simeone aliiongoza Atletico kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Hispania,maarufu La Liga pamoja na kufika fainali ya Ligi ya 
 
Mabingwa Ulaya, ambako walifungwa na mahasimu wao, Real. 
Lakini Simeone akalipa kisasi cha kufungwa kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa, kwa kuitandika 4-0 timu ya Carlo Ancelotti Jumamosi.
Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 44 ndiye anaonekana mtu aliye tayari zaidi kumrithi Pellegrini. Wote Ancelotti na koca Bayern Munich, Pep Guardiola hawategemewi kuondoka katika klabu zao, wakati Jurgen Klopp amekuwa  na msimu mbaya

NGASSA YANGA WAMEKIUKA MAKUBALIANO

MSHAMBULIAJI wa Yanga SC, Mrisho Ngassa amesimulia machungu ya kimkataba anayokutana nayo ndani ya Yanga, lakini akawaambia viongozi wa klabu hiyo kumlipia deni alilolazimishwa kukopa ili aisaidie klabu hiyo.
 
Akizungumza mchana huu katika makao makuu ya klabu ya Yanga Ngassa amesema awali wakati anajiunga na Yanga akitokea Azam alipata ofa kubwa kutoka kwa El Merreikh ya Sudan, lakini hakuweza kusaini nao mkataba kutokana na tayari alishasaini mkataba na Yanga na kuamua kuwatosa Waarabu hao.
Mrisho Ngassa kushoto akizungumza na Waandishi wa Habari leo

Ngassa amesema mara baada ya kujiunga na Yanga akitokea Simba alikokuwa kwa mkopo kuliibuka deni la Sh Milioni 45 alilotakiwa kuwalipa Simba na uongozi wa Yanga ulimtafutia mkopo ambao alitakiwa kusaini ili umsaidie kulipa deni jambo ambalo hakukubaliana nao.
"Sikuwa tayari kusaini mkopo ule, niligoma kabisa lakini wakanilazimisha wakiniahidi kwamba klabu nayo itanisaidia kulipa lakini baadaye mambo hayakuwa hivyo, nilikatwa peke yangu,"alisimulia Ngassa.
"Kuna kipindi ambacho wakati nakatwa hizo fedha kumbe benki zilikuwa hazifiki, sikuwa najua zilikuwa zinaenda wapi lakini katika mshahara wangu zilikuwa zinakatwa."
 
Mshambuliaji huyo mwenye mabao mawili katika Ligi Kuu Bara huku pia akishikilia rekodi ya mfungaji Bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita, ameitaka Yanga kumlipia deni lake na endapo watafanya hivyo anaweza kuifungua mabao mengi zaidi kwa kuwa uwezo wa kufanya hivyo anao.
Awali akizungumzia sakata hilo la Ngassa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Yanga ,Jerry Murro ametamka kwamba klabu yake haina mgogoro wowote a mchezaji huyo na tayari wameanza mazungumzo ya kuongeza mkataba