SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Nov 11, 2014

KIKOSI BORA CHA WIKI CHA EPL KWA WIKI YA 11.

Ligi Kuu ya Uingereza itaendelea tena tarehe 22 kwa michezo ya mzunguko wa 12 kufuatia kuwa na michezo ya kimataifa itakayopigwa wikiendi hii.
 
Wikiendi iliyopita baadhi ya timu zilifanya vizuri huku nyingine zikipata matokeo yasiyoridhisha aidha kwa kutoka sare au kufungwa. 
 
Nyota kadhaa walionyesha juhudi binafsi katika kutoa mchango kwa timu zao kufanya vizuri hivyo kuchaguliwa kuunda kikosi bora cha wiki ya 11 tangu Ligi Kuu hiyo maarufu ianze mwezi Agosti.
  
Kifuatacho ni kikosi bora cha EPL cha wiki ya 11:
 
#
Mchezaji
Timu
1
Brad Guzan
Aston Villa
2
Daryl Janmaat
Newcastle United
3
Cesar Azpilicueta
Chelsea 
4
Ryan Shawcross
Stoke City
5
Fabricio Coloccini 
Newcastle United
6
Emre Can 
Liverpool
7
Remy Cabella
Newcastle United
8
Oscar
Chelsea
9
Sergio Aguero 
Manchester City
10
Charlie Austin 
QPR
11
Jefferson Montero 
Swansea City

MAXIMO KUSAJILI VIUNGU KATIKA DIRISHA DOGO.

Baada ya kuona timu yake inasua sua sehemu ya viungo kocha mkuu wa Yanga Marcio Maximo amepanga kusajili viungo mahili katika dirisha dogo ili kuboresha sehemu hiyo.
Yanga tayari imeshapoteza mechi mbili msimu huu, sare moja na kushinda nne ikiwa nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo yenye timu 14.
Akizungumza baada ya mchezo wao wa juzi walioshinda 2-0 dhidi ya Mgambo Shooting katika uwanja wa Taifa Maximo alisema ana orodha ndefu ya viungo ambao kwa sasa wanahitajika Yanga.
Katika michezo 7 Yanga wameweza kuchapwa mabao 9 na hiyo ni ishara ya wazi kuwa kuna tatizo kubwa katika sehemu ya kiungo.

SIRI YA IVO NA MABAO YAKE.


KIPA wa Simba, Ivo Mapunda, juzi Jumapili aliingia uwanjani kucheza dhidi ya Ruvu Shooting huku akiwa amevalia kaushi iliyoandikwa kwa Kiingereza ‘Why us?’ Pia ilikuwa na maandiko ya Biblia ‘Math7:7’ ambayo aliyatolea ufafanuzi.
Ivo ambaye aliibukia kwenye mchezo huo baada ya kuwa benchi kwa kipindi kirefu akiuguza mkono na nafasi yake ilichezwa na chipukizi, Peter Manyika.
Aliandika ujumbe huo ili kuonyesha hisia zake ambapo ule wa ‘Why us?’ ulikuwa na maana ya ‘Kwa nini sisi?’ na ule wa Math7:7(Mathayo 7 mstari wa 7) ni maneno yaliyopo kwenye Biblia yanayosema: “Ombeni, nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtapata, bisheni nanyi mtafunguliwa.”
Alipoulizwa na Mwanaspoti kwa nini aliandika hivyo, aliyatolea ufafanuzi huku Manyika akimuunga mkono kwa msisitizo akisema: “Nimeamua kuandika haya namna nilivyoguswa, hivi kwa nini sisi tu, kwa nini?
“Lakini pia maneno ya Biblia yalikuwa yakinipa moyo na kuamini ndiyo utakuwa mwisho, kumbe anayeomba na kutafuta hupata ni hivyo tu.”
Simba iliifunga Ruvu Shooting bao 1-0 ukiwa ni ushindi wao wa kwanza baada ya kutoa sare sita mfululizo tangu Ligi Kuu Bara msimu huu ilipoanza.

ANGALIA MAJINA YA WALIOFAULU USAILI WA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI TANZANIA.


 

 Wahitimu wa kidato cha sita mwaka 2014 na kidato cha nne mwaka 2013 waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi baada ya usaili kukamilika.

Maelekezo Muhimu.
Wahitimu wa kidato cha sita mwaka 2014, kidato cha nne mwaka 2013 na JKT Mafinga, Mlale, Ruvu, Mgambo, Bulombola, Kanembwa, Itende, Nachingwea, Mbweni, Maramba, Chita, Makutupola, Mtabila, Msange, Mgulani, Oljoro, Rwankoma na Kimbiji wamechaguliwa kujiunga na mafunzo ya awali ya Jeshi la Polisi.
Wahitimu hawa waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti tarehe 28/11/2014 kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa kama ilivyooneshwa kwenye jedwali hapa chini ili waandaliwe usafiri wa kuwapeleka Shule ya Polisi Tanzania tarehe 30/11/2014.
Zoezi la usajili litaanza shuleni hapo tarehe 01/12/2014 hadi tarehe 15/12/2014. Atakaefika kuanzia tarehe 16/12/2014 hatapokelewa.
Atakaeamua kuripoti kwa Kamanda wa Polisi ambako hakupangiwa atalazimika kujigharimia usafiri hadi Shule ya Polisi Tanzania mjini Moshi.

Vijana hawa watalazimika kufika shuleni wakiwa na mahitaji yafuatayo:

Vyeti vyao vyote vya masomo( original Academic Certificates/Result slip pamoja na Leaving certificates) kidato cha Nne/Sita, Vyeti vya kuzaliwa (Original Birth certificates). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.

Mashuka mawili rangi ya Bluu Bahari (light blue)

Chandarua chenye upana futi tatu

Nguo za michezo(Track suit nyeusi,Tshirt blue na Raba)

Pasi ya Mkaa

Ndoo moja

Pesa za kulipia bima ya afya kiasi cha shilingi elfu hamsini na mia nne tu (50,400/=).

Pesa kidogo ya kujikimu.

Kwa mujibu wa kanuni za shule ya Polisi ni marufuku kufika shuleni na simu ya mkononi. Atakayepatikana na simu atafukuzwa shuleni hapo.

Angalia orodha ifuatayo: BOFYA HAPA KUANGALIA MAJINA

SOCIEDAD WAMWITA MOYES.

David Noyes
Kocha wa zamani wa timu ya Manchester United David Moyes ametajwa kuwa meneja mpya wa timu ya kutoka Hispania,Real Sociedad.
Kocha huyo mwenye miaka 51, hii ni kazi yake ya kwanza baada ya kutimuliwa kwenye kilabu cha Man U mwezi wa nne mwaka huu, .
Moyes anachukua nafasi ya Jagoba Arrasate ambaye pia ametimuliwa na Sociedad baada ya matokeo mabaya na kusababisha timu hiyo kuangukia nafasi ya 15 katika ligi kuu nchini humo, maarufu kama La Liga.
Mkataba wa Moyes na Real Sociedad ni mpaka june mwaka 2016 na kwama mara ya kwanza ataonekana katika mechi ya Deportivo November 22.

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI




.
.