SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

May 17, 2015

ARSENE WENGER HANA MPANGO NA PETR CECH…HIKI NDICHO ALICHOSEMA

cech
Petr Cech amehusishwa sana na tetesi za kujiunga na Arsenal kipindi cha usajili kikifika. Cech anategemewa kuondoka Chelsea na kutafuta timu nyingine baada ya msimu huu kuisha.
Lakini manager wa Arsenal amesema maneno ambayo yamefanya uwezekano wa Cech kwenda Arsenal kuwa ni ndoto.
“Hilo ni swali gumu kwasababu hivi sasa hatuna interest na mtu yoyote, tutaanza mambo ya uhamisho mwishoni mwa msimu. Lakini sisi tuna makibo bora wa level ya juu. Wapo watatu”
Kitendo hicho cha Arsene Wenger kukwepa kabisa kumzungumzia Cech na kuwasifia makipa wake watatu. Kimeonyesha wazi kabisa Wenger hana mpango na Cech

FIFA IMEWA-FORCE BARCELONA KUMRUDISHA MESSI MPYA KWAO JAPAN

messi
Kama alivyolelewa Messi na kuja kuwa mchezaji tegemezi wa Barcelona ndivyo hivyo inavyojaribiwa kwa Kubo ambae tayari ameshapewa jina la Japanese Messi. Kubo mwenye miaka 13 amelazimika kurudi kwao Japan na kujiunga na timu ya FC Tokyo kwa na kuendelea kucheza soka. Kubo alikua La Masia academy ya Barcelona lakini FIFA iliiambia Barca wamevunja sheria kwa kusaini wachezaji wadogo.
Kilichotokea ni kwamba kutokana na Barcelona kuvunja sheria za usajili, hivyo basi Kubo atacheza huko hadi akifika miaka 18 anaweza kujiunga tena na Barcelona. Manchester city na Arsenal ni club ambazo zimeonyesha kumuhitaji mchezaji huyu.
Cheki hii video ya Kubo akiwa kwenye action