SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Jul 1, 2016

PEP GUARDIOLA AMEMSAJILI STAA HUYU HAPA KUTOKA SPAIN

Na Haji balou
TIMU ya Manchester city imekamilisha uhamisho wa Staa wa kimataifa wa Hispania Na Klabu ya Celta Vigo Manuel Agudo Durán "Nolito" Kwa Ada ya Euro million 13.8.

Nolito mwenye umri wa miaka 29 amesaini mkataba wa miaka minne ya kuitumikia Manchester City awali  alikuwa anatakiwa Na Klabu ya Fc Barcelona.

HAYA NDIO MAAMUZI YA BARCELONA KUHUSU NEYMAR

Na Haji balou
Klabu ya Fc Barcelona wamekubali yaishe Na wameamua kukaa pamoja Na mchezaji wao Neymar ili kumbakiza katika kikosini  katika msimu ujao.

Staa huyo wa Brazil alikuwa tayari kuihama klabu hiyo ya katalunya Kama watashindwa kuongeza mshahara wake katika msimu ujao.

Neymar mwenye umri wa miaka 24 anataka kulipwa Euro million 16.5 ili abaki lakini Barcelona hawakuwa tayari kumlipa kiasi hicho cha pesa hata hivyo Manchester United walikuwa tayari kumlipa Neymar kiasi hicho cha pesa Na wakaanza kumfukuzia Staa huyo.