SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Jan 30, 2015

CHELSEA BILA COSTA NA FABREGAS.

FBL-ENG-PR-CHELSEA-SWANSEA

Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa atalazimika kukaa nje ya uwanja akikosa michezo mitatu ya timu hiyo kwenye ligi ya England baada ya kukutwa na hatia ya utovu wa nidhamu kufuatia vitendo kadhaa vya mchezo usio wa kiungwana vilivyoonekana kwenye mchezo dhidi ya Liverpool.
Mshambuliaji huyu wa kimataifa wa Hispania alikutwa na hatia ya kumkanyaga kiungo wa Liverpool Emre Can katika mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Capitol 1 Cup ambao Che;sea ilishinda 1-0 na kufuzu hatua ya fainali .
Kamati ya nidhamu ya FA ambayo iliketi siku ya jumatano ilifikia uamuzi huo wa kumfungia Costa kutocheza michezo mitatu huku akipewa fursa ya kukata rufaa rufaa ambayo hata hivyo imetupiliwa mbali
Hapa Diego Costa anaonekana akimkanyaga kiungo wa Liverpool Emre Can ambapo mshambuliaji huyo amefungiwa kwa kosa hili na atakosa michezo mitatu ya ligi kuu ya England .
Hapa Diego Costa anaonekana akimkanyaga kiungo wa Liverpool Emre Can ambapo mshambuliaji huyo amefungiwa kwa kosa hili na atakosa michezo mitatu ya ligi kuu ya England .
Mshambuliaji huyo alijitetea kuwa hakufanya kitendo hicho kwa kusudi kwani hakuwa ametazama mguu wake umekanyaga sehemu gani na hakuna na lengo la makusudi la kumchezea rafu mchezaji wa Liverpool.
Kwa matokeo haya Chelsea itamkosa Costa kwenye michezo muhimu ya ligi kuu ya England dhidi ya Manchester City , Everton na Aston Villa hali ambayo itakuwa pengo kubwa kwa kocha Jose Mourinho .
Costa hadi sasa amefunga mabao 17 kwenye ligi ya England akiwa anaongoza msimamo wa wafungaji huku akiisadia timu yake kukaa kileleni mwa ligi hiyo huku wakiwazidi wapinzani wao Manchester City kwa pointi 5 .
Cesc ana jeraha la misuli na ataukosa mchezo dhidi ya Manchester City.
Cesc ana jeraha la misuli na ataukosa mchezo dhidi ya Manchester City.
Pengo kubwa kwa Chelsea wikiendi hii litakuwa kumkosa kiungo mshambuliaji Cesc Fabregas ambaye ana jeraha la misuli ya nyuma ya mguu na Chelsea itakuwa kwenye wakati mgumu sasa kucheza na City bila wahispania hawa wawili Cesc na Diego ambao kwa pamoja wanaongoza kwa mabao na pasi za mwisho .

NEYMAR AWA TATIZO LA LIGA

neymar-barcelona-2013-hd-wallpapers-jpg

Kiungo mshambuliaji wa Barcelona Neymar Da Silva Jr vamekuwa kwenye kiwango cha juu msimu huu ambapo amekuwa sehemu muhimu sana ya timu yake katika michezo ya hivi karibuni .
Neymar amedhihirisha ubora wake kwa jinsi ambavyo amekuwa akifunga mabao mfululizo huku akisaidia kwa kutoa pasi za mwisho kwa wenzie na amekuwa akifanya hivyo kwa mwendelezo mzuri ,
Tatizo limekuwa moja tu , jinsi amabvyo mchezaji huyu amekuwa akilaumiwa hasa na wapinzani kwa kuwa mtovu wa nidhamu na mkosefu wa heshima ambapo amekuwa akiwadhihaki wachezaji wa timu pinzani kwenye nyakati tofauti hali ambayo imeonekana kuwakera wengi .
Wapinzani wa Barcelona wamemlalamikia Neymar kwa kitendo chake cha kuwadhihaki anapokuwa uwanjani .
Wapinzani wa Barcelona wamemlalamikia Neymar kwa kitendo chake cha kuwadhihaki anapokuwa uwanjani .
Neymar amekuwa na tabia ya kuwatukana wachezaji wa timu pinzani na wakati mwingine hata kwa vitendo na ndio maana amekuwa kwenye vurugu nyingi ambazo zimekuwa zikitokea kwenye michezo ya Fc Barcelona .
Majuzi wakati wa mchezo war obo fainali ya michuano ya Kombe la Mfalme ambapo Barcelona ilishinda kwa 3-2 Neymar alikuwa kwenye fujo zilizoibuka kati yake na wachezaji wa Atletico ambao ni Gabi , Juan Fran na Raul Garcia.
Ilifikia mpaka kocha Luis Enrique alilazimika kumtoa uwnajani ambapo baadae alikir kufanya hivyo kwa lengo la kumlinda .
Neymar amekuwa akihusika kwneye vurugu zinazotokea uwanjani kutokana na tabia yake ya kuwatukana wachezaji wa timu pinzani .
Neymar amekuwa akihusika kwneye vurugu zinazotokea uwanjani kutokana na tabia yake ya kuwatukana wachezaji wa timu pinzani .
Hivi karibuni Luis Enirque alisikika akisema kuwa Neymar anapaswa kujiheshimu na kuwaheshimu wapinzani na kama asipofanya hivyo huenda akafanywa ‘chambo’ na kuumizwa na wachezaji wa timu pinzani ambao wamejawa na hasira juu yake .
Tabia hii ya Neymar itawakumbusha wengi juu ya kile kilichokuwa kinafanywa na Ronaldinho Gaucho wakati akiwa na klabu hii ya Barcelona ambapo aliripotiwa kuwadhihaki na kuwatusi wapinzani huku akiendelea kuwakera kwa chenga zake za maudhi .

ALI KIBA; AMANI NI MUHIMU

Katika kuelekea kipindi cha Uchaguzi Mkuu nchini Tanzania, amani ikiwa ni somo kubwa linalohubiriwa kwa wananchi kila ngazi, nyota wa muziki Ali Kiba, amesema kuwa yeye pamoja na sanaa yake amekuwa kati ya wadau wanaolitilia mkazo suala hili.
Msanii wa muziki wa bongo fleva nchini, Ali Kiba
Ali Kiba amesema kuwa, Tanzania imekuwa ni nchi ambayo inatambulika kwa amani, changamoto kubwa ikiwa ipo katika nchi za jirani ambapo amekwishaenda si tu kwa kutoa burudani, bali kwa kuhamasisha amani kwa wapenzi wa kazi zake.

WEUSI; TUNAKUJA KIVINGINE

Lile kundi la muziki wa Hip Hop Tanzania ambalo mwaka jana limetamba kwa ngoma kibao kali WEUSI limesema kuwa kwa sasa wanakuja na ngoma nyingine ambayo itafungua mwaka kwa kundi hilo ambayo ni ya tofauti kwani katika wimbo huo
Kundi la Weusi wakiwa na wasanii wengine wa bongo fleva jana usiku studio wakifanya kazi yako mpya.
wamewashirikisha watu ambao wanatengeneza Couples wasanii hao ni pamoja Jux,Vanessa Mdee,Nahreal,Aikamarealle pamoja na Chinbees.
Joh Makini Mwamba wa kaskazini amethibitisha kufanyika kwa kazi hiyo ambayo inakwenda kwa jina la The Indusrty iliyowashirikisha wakali hao wa Bongo fleva ambao kwa sasa wanatamba na ngoma zao mbalimbali katika media,Joh amekiri wazi kuwa katika kazi hiyo iliyofanyika usiku wa jana kuwa ni kazi nzuri sana na haipaswi kusubiri hivyo itavunja ratiba zao ambazo walikuwa wamejipangia kwa mwaka 2015.
Ahsante baba yetu uliye juu kwa hii zawadi usiku huu,kitu ya hatari nathubutu kusema hii haitasubiri itavunja ratiba zetu ni WEUSI feat Couples The Industry vanessa Mdee,Nahreel Gnakowarawara,Juma_jux ,Aika Marealle,Chinbees".
Nae mkali wa kuvunja chorus kutoka katika kundi hilo la Weusi Gnako amefunguka katika ukurasa wake wa Instragram kuhusiana na ujio wao wa wimbo huo mpya uliofanyika jana usiku na yeye amesisitiza kuwa ngoma hiyo haina haja ya kusubiri inapaswa itoke kwani wameifanya kivingine hivyo watu watarajie ujio mwingine wa Weusi kivingine.
"Hivi sasa ni saa nane na robo usiku,tupo office bado the industry yaaaakhaaa watch them black boy flaaaaa,Nikki wapili,vanessa Mdee,Nahreel,Joh Makini,Juma_jux ,Aika Marealle,Chinbees". haisubiri hiii tunakujaa tena!!!
Weusi ni kundi la muziki wa Hip Hop pia ni kampuni ambayo kwa sasa ni moja la kundi ambalo linafanya vizuri katika tasnia ya muziki wa Hip hop Tanzania.

MATOLA AUOMBA UONGOZI SIMBA AONDOKE ZAKE



Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola ameuomba uongozi wa timu hiyo umpunguzie majukumu au umuache ende zake.


Matola ameuambia uongozi wa Simba kwamba ana mambo ya kifamilia yanayomkabili hivyo asingeweza kupambana na presha inayoendelea.

Rais wa Simba, Evans Aveva amesema tayari Matola amewaambia kwa mdomo kuhusiana na hilo na sasa wanalishughulikia.

"Ni kweli amesema hivyo, sasa nimemwambia aandike barua kuhusiana na alichosema," alisema Aveva.

"Baada ya hapo tutakutana na kukaa ili kujua cha kufanya kuhusiana na suala hilo," aliongeza Aveva.

Simba ilipoteza mechi yake ya pili ilipokutana na Mbeya City na kufungwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar,Jumapili. 

Hali ambayo imeamsha jazba kwa mashabiki wa Simba ambao asilimia kubwa waliangua kilio.

YANGA YAIHOFIA NDANDA FC JUMAPILI

IMG_5365
YANGA SC imeendelea kujifua kujiandaa na mechi ya kesho kutwa uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam dhidi ya Ndanda fc.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro amesema katika mazoezi ya leo, kocha mkuu wa klabu hiyo Hans van der Pluijm ameendelea kufanyia marekebisho safu yake ya kiungo na ushambuliaji.
“Tunafanya mazoezi kwa siku kadhaa, nadhani kesho mwalimu atakamilisha programu yake kabla ya mechi ya jumapili, tunaenda kucheza na Ndanda yenye morali kubwa”.
“Wametoka kushinda na Kagera Sugar, nasisi tuliwafunga Polisi Morogoro, kwahiyo tutaingia kwa tahadhari kubwa”

ALICHOSEMA MWANA FA KUHUSU VIDEOYAKE YA KIBOKO YANGU ALIYOMSHIRIKISHA ALI KIBA

BINAMU
Rapper Mwana FA amesema kuwa wakati wanarekodi video ya Kiboko Yangu ilibidi warekodi mara mbili kutokana na Camera kuleta usumbufu baada ya kurekodi sehemu ya Ali Kiba, kwa kuwa alikuwa na ratiba ya kufanya show ilimbidi asafiri kwenda kwenye show kisha akarudi kumalizia sehemu ya video hiyo kitu ambacho kilifanya gharama ziongezeke.
FA amesema video hiyo imepanda ubora ukilinganisha na video zake zote zilizopita, Mike Tee ni mshkaji wake wa karibu ambaye alichangia pia kumpa idea ya kufanya video hiyo.

HABARI NJEMA KWA GERARD PIQUE NA MPENZI WAKE SHAKIRA

EXCLUSIVE: Shakira and Gerard Pique strolling with baby Milan in SpainFamilia ya mwanasoka mahiri Gerard Pique na mkewe Shakira wamepata ugeni mpya ndani ya familia hiyo baada ya mwanamuziki huyo kujifungua mtoto wa pili wa kiume.
bal
Mtoto huyo aliyepewa jina la Sasha likiwa na maana ya Alexander kwa lugha ya Kirussia, alizaliwa katika hospitali iliyopo katika mji wa Barcelona usiku wa kuamkia leo kwa njia ya upasuaji.

PICHA MAANDALIZI YA MWISHO MIAKA 10 YA THT

11idMiaka 10 ya THT inakamilishwa Jumamosi ya January 31 kwenye ukumbi wa Escape One uliopo Mikocheni,maandalizi ya mwisho kabisa kutoka Escape One yamekamilika na baadhi ya wasanii wanaoperfoam kesho wamefika kwa ajili ya mazoezi ya jukwaani  nimeona nikuletee picha hizi mtu wangu.
7id
9id
11id
13id
35id
4id
38id
26id
23id

MANENO YA LINEX KUHUSU MAANDALIZI YA VIDEO YAKE MPYA ALIYO MSHIRIKISHA DIAMONDl PLATNUMPZ

.
.
Msanii wa muziki Linex Sunday Mjenda amefunguka na kusema kesho Jan 31 anatarajia kuingia location kufanya maandalizi ya video mpya ya single yake iitwayo Salima aliyomshirikisha Diamond Platnumz.
Akiongea na millardayo.com alisema; ‘Kesho Jumamosi nitaanza ku shoot video ya wimbo wangu unaitwa Salima nimefanya na Diamond Platnumz, Salima ni wimbo fulani ambao ukiusikiliza vizuri una mafunzo ndani yake.
Ni wimbo ambao tumemuimbia mwanamke ambaye alikuwa na maisha mazuri lakini maisha yalibadilika baada ya wazazi yake kufariki kwa hiyo maisha yalivyobadilika akajikuta ana watoto watatu wenye baba tofauti bila yeye mwenyewe kujielewa lakini mwisho wa siku akafikia point akawa ame give up na ameamua kuishi maisha yake na watoto wake bila kutegemea Mwanaume, kwa hiyo ni wimbo fulani ambao una  mafundisho kwa dada zetu na kaka zetu.
Tuta shoot video na director Adam Juma na hatuta shoot video mjini tuta shoot video kijijini  kwa hiyo watu wenye wataona kitu tofauti kutoka kwangu na kwa Naseeb’--alisema Linex.

WENGER; PAULISTA HAJUI KIZUNGU

Gabriel Paulista
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amekiri kwamba kutojua kizungu kwa beki mpya wa timu hiyo Gabriel Paulista huenda kukaifanya timu hiyo kufungwa mabao.
Beki huyo kutoka Brazil atashirikishwa katika mechi dhidi ya Aston Villa siku ya jumapili baada ya kusajiliwa kutoka Villareal kwa kitita cha pauni millioni 11.2.
''Kwa sasa haongei hata neno moja la kizungu,na hiyo inaweza kukufanya ufungwe mabao ''alisema Wenger.
Paulista
Wenger ameongeza kwamba Gabriel ambaye amekuwa akishirikishwa katika mechi zote za Villareal msimu huu atahitaji mda zaidi ili apate uzoefu katika ligi ya Uingereza.
Kocha huyo pia amesema kuwa mchezaji Francis Coquelin anakaribia kuandikisha mktaba mpya ,lakini nahodha Mikel Arteta bado hajakubali kutia sahihi kandarasi mpya.

ALICHOSEMA IYANYA KUHUSU JAGUAR

jaguar
Mbali na wawili hao kufanya collabo ya pamoja kwenye ngoma ya Jaguar mwenyewe iitwayo “One centimeter rmx” akiwa amemshirikisha Iyanya kutoak Nigeria waliingia kwenye utata baada tu ya kutoa ngoma yao hiyo.Utata huo ulianza baaada ya kusambaa kwa video hiyo ambapo Jaguar alitaka ifike kimataifa lakini hakuonesha juhudi zozote za kui-push video hiyo.Iyanya alisema kwamba Jaguar ni mvivu wa kusukuma ngoma zake zifike kimataifa kama wengine wanavyofanya.Pia alisema hakuona Iyanya nimefanya collaboz na Diamond na Sauti soul laikini wao ndio wanao push ngoma zao kufika vituo mbali mbali lakini kwake Jaguar hafanyi hvyo kwani amekua akitegemea mimi ndio nifanye hivyo.

RAIS SIMBA AZUNGUMZIA SUALA LA MAGURI KUDHALILISHWA NA NYOSSO, AIAMBIA TFF ICHUKUE HATUA



Suala la mshambuliaji wa Simba, Elius Maguri kufanyiwa vitendo vya udhalilishwaji vimepingwa kwa nguvu zote na uongozi wa Simba.

Rais wa klabu hiyo, Evans Elieza Aveva kitendo alichokifanya beki Juma Nyosso dhidi ya Maguri kumshika makalio na kumdhalilisha kwa kumuingiza kidole lilikuwa jambo si la kiungwana.
Nyosso alifanya kitendo hicho cha kulaaniwa katika mechi ya  Ligi Kuu Bara Kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar.
Gazeti maarufu la michezo nchini la Championi, limechapisha picha ikimuonyesha Nyosso akifanya vitendo hivyo vya udhalilishaji dhidi ya Maguri, kitu ambacho wadau wengi wamelaani na kusema Nyosso hakustahili kufanya hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar, Aveva alisema Maguri ambaye amejiunga na Simba msimu huu akitokea Ruvu Shooting, alifanyiwa kitendo cha udhalilishaji na kuitaka TFF kuchukua hatua za kisheria dhidi kwa Nyosso aliyewahi kuichezewa Simba.
“Kuhusiana na suala la tukio hilo kuchapishwa kwenye gazeti la Championi kwamba ni sawa au la, kitaaluma mimi si mtaalamu wa masuala ya habari, lakini tutalijadili na wenzangu.
“Lakini la msingi ninaloweza kusema ni kwamba kitendo alichofanyiwa Maguri si sawa kabisa na tunakikemea vikali, kwani tumesikitishwa sana.
“Pia hii ni changamoto wa viongozi wa klabu na shirikisho. Kwamba huu ndiyo wakati wa kwenda na teknolojia. Tusikatae kw akuwa mambo ndivyo yalivyo.
“Angalia suala la Suarez alipomng’ata  mchezaji wa Italia, Fifa ilimfungia baada ya kutumia teknolojia na haikutumia ripoti ya waamuzi pekee, hivyo na sisi umefika wakati wa kuheshimu teknolojia kwa ajili ya kukomesha vitendo kama hivyo ambavyo tayari vimejionyesha kwa Tambwe, Okwi na Maguri, lakini pia huko daraja la kwanza ndiyo usiseme,” alisema Aveva.

Aidha, Aveva alivishukuru vyombo vya habari kwa kuendelea kuibua mfululizo matukio mabaya ya ukatili na udhalilishaji katika soka ili kuonyesha hali halisi.

OKWI KAMILI GADO KUWAVAA JKT RUVU KESHO TAIFA


s4
KIUNGO mshambuliaji wa Simba Sc, Mganda Emmanuel Anord Okwi anatarajia kuivaa JKT Ruvu kesho uwanja wa Taifa katika mechi ya ligi kuu Tanzania bara.
Afisa habari wa Simba, Humphrey Nyasio amezungumza na mtandao huu dakika chache zilizopita akiwa uwanja wa mazoezi wa JKT Mbweni ambapo Simba inaendelea na mazoezi hivi tunavyoongea na kueleza kuwa Okwi yuko fiti na atacheza mechi ya kesho.
“Nipo hapa uwanjani JKT Mbweni, Okwi anaendelea na mazoezi. Kesho atacheza”. Amesema Nyasio.
Pia Nyasio amesema beki wa pembeni Hassan Ramadhan Kessy yuko fiti kucheza kesho na muda huu unaendelea  na mazoezi.
Hata hivyo, Afisa habari huyo amesema Simba itaendelea kuikosa huduma ya kiungo Said Hamis Ndemla ambaye bado anasumbuliwa na majeruhi.
Okwi, Ndemla na Kessy waliikosa mechi ya jumatano iliyopita uwanja wa Taifa ambapo Mnyama Simba alichapwa 2-1 na Mbeya City.
Nyasio amesema kesho watapambana kupata ushindi, licha ya kukiri kuwepo kwa changamoto katika michuano ya ligi kuu.

DIEGO AFUNGIWA MECHI 3, SCHOLES AMPA TANO ZA UKWELI!!


251F9C4E00000578-0-image-m-4_1422390118302
Mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa (kulia) akiondoka na mpira baada ya kumkanyaga  Emre Can
PAUL Scholes anaamini kuwa Diego Costa anatakiwa kuigwa kwa uvumilivu wake awapo uwanjani na si kukosolewa kwa kosa alilofanya.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England amefungiwa mechi tatu kwa kitendo cha kumkanyaga mchezaji wa Liverpool, Emre Can  wakati wa mechi yao ya pili ya nusu fainali ya kombe la Ligi iliyopigwa jumanne iliyopita uwanja wa Stamford Bridge.
Baadaye Costa alijihusisha katika kosa lingine la kumchezea vibaya beki wa Liverpool Martin Skrtel, lakini FA imesema haitamchukulia hatua yoyote kutokana na tukio hilo.
Costa appears to stamp on Can's right leg during a feisty Capital One Cup semi-final second leg
 
Costa akikanyaga mguu wa kulia wa Can
Licha ya hasira za Costa, gwiji wa Manchester United, Scholes amedai mshambuliaji huyo wa The Blues anatakiwa kuheshimiwa kufuatia kuchukizwa na Skrtel

BAYERN YAMPOTEZEA REUS…MILANGO WAZI KWA CHELSEA, MAN CITY

2501F89B00000578-0-image-a-18_1422618095850
Bayern Munich wameacha na mpango wa kumsajili Marco Reus 
Bayern Munich wameachana na mbio za kumsajili Marco Reus na kuacha milango wazi kwa klabu ya Real Madrid na klabu kubwa za ligi kuu England.
Bayern wamefikia maamuzi ya kutomshawishi Reus wiki kadhaa zilizopita kwa madai kuwa tayari wana viungo washambuliaji wengi na hawataki kuharibu uhusiano wao wa karibu na Borussia Dortmund, hii ni kwa mujibu wa gazeti la Bild. 
Real wanapewa nafasi kubwa ya kumsajili Reus, lakini kutokana na tetesi za klabu za Hispania kufungiwa usajili, anaweza kutua katika timu za ligi kuu England majira ya kiangazi mwaka huu.
Reus is one of the hottest prospects in Europe and will be courted by the Premier League's top clubs
Reus ni miongoni mwa wachezaji wakubwa barani ulaya na atazivutia klabu kubwa.
Taarifa za Bayern kutomsajili zitawashitua Manchester City na Chelsea ambao wanaendelea kutumia pesa kuimarisha vikosi vyao ili kufikia ubora mkubwa wa ulaya.

ALI KIBA KUPIGA SHOO "LIVE" SAUTI ZA BUSARA FEB 12 MWAKA HUU

DSC_0313
Mwenyekiti wa Bodi wa Busara Promotions, wandaaji wa tamasha la Sauti za Busara, Simai Mohammed (katikati) akiongea na wandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa mkutano wa wanahabari Jijini Dar es Salaam, juu ya tamasha la 12 la Sauti za Busara, litakalofanyika, Februari 12 hadi 15, mwaka huu, Ngome Kongwe, Zanzibar. Wengine (kushoto) ni Meneja wa tamasha hilo, Journey Ramadhani. na upande wa kulia ni Mkurugenzi wa tamasha hilo, Yusuf Mahmoud ‘Dj Yusuf, akifuatiwa na msanii wa bongo fleva nchini, Ali Kiba (kulia).
DSC_0409 (1)
Msanii wa Bongo fleva nchini, Ali Kiba akiimba akapela moja ya nyimbo zake wakati wa mkutano huo na wandishi wa habari (Hawapo pichani), katika mkutano huo juu ya ushiriki wake kwenye tamasha hilo linalotarajia kufanyika Februari 12 hadi 15, Ngome Kongwe, Zanzibar. kushoto kwake, ni
Mkurugenzi wa tamasha hilo, Yusuf Mahmoud ‘Dj Yusuf, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Busara Promotions, Simai Mohammed.
??????????
Simai, Dj Yusuf na Kiba wakiwa wameunganisha mikono kwa kusalimiana ikiwa ni ishara ya Umoja na Amani, kama Kauli mbiu ya mwaka huu ya tamasha hilo inavyohimiza amani.
??????????
Ali Kiba katika ‘Selfie’ na Mwenyekiti wa Bodi ya Busara Promotions, Simai Mohammed, muda mfupi baada ya utambulisho wa msanii huyo juu ya kupiga shoo kwenye tamasha la 12 la Sauti za Busara, litakalofanyika Februari 12 hadi 15, Zanzibar.
Na Andrew Chale
Mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ali Kiba ametamba kukonga nyoyo watu mbalimbali watakaojitokeza kwenye tamasha la 12 la Sauti za Busara linalotarajia kufanyika, Februari 12 hadi 15, Ngome Kongwe, Zanzubar.
Ali Kiba alieleza hayo leo Alhamisi, Januari 29. wakati wa mkutano wa ulioandaliwa na Busara Promotions, wandaaji wa tamasha hilo kubwa la Kimataifa linalofanya muziki wa ‘Live’,  ambapo kwa mwaka huu zaidi ya wanamuziki na vikundi 37, watatoa burudani kwenye tamasha hilo kwenye viunga vya Ngome Kongwe, Unguja, Zanzibar.
Akizungumza mbele ya wandishi wa habari, Ali Kiba alisema kwa sasa amejiandaa kutoa burudani ya aina na ambayo itakonga nyoyo kwa watu wote watakaojitokeza kushuhudia tamasha hilo.
“Hii itakuwa ni zawadi kwa watanzania wote kunishuhudia nikiimba ‘live’ bila kutumia ‘cd’ kama wafanyavyo wengine. Mimi ni mwanamuziki na nimesoma muziki hivyo nitapiga muziki wa nguvu jukwaani” alisema Ali Kiba.
Na kuongeza kuwa, kwa sasa yupo kwenye mazoezi ya muda mrefu wa kujifua na bendi maalum  kwa ajili ya shoo hiyo huku akitamba kuwa, yeye ni msanii kwani muziki aliusomea na kujifunza huko nyuma alipokuwa  katika Nyumba ya kuibua vipaji THT, ambapo alijifunza vitu vingi ikiwemo kuimba muziki wa bendi na ‘live’.
Aidha, aliwaomba wapenzi na wadau wa muziki kujitokeza kwa wingi
kushuhudia tamasha hilo kwani wasanii mbalimbali wa ndani na nje watatoa burudani ya kipekee.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa bodi ya Busara Promotion, wandaaji wa tamasha hilo, Simai Mohammed, alisema tamasha limeweza kuongeza ajira na uchumi wa Zanzibar kwani pia limeongeza fursa za utalii.
Kwa upande wake, Meneja wa tamasha  hilo, Journey Ramadhani, alisema tamasha hilo limeweza kuongeza fursa kila mwaka ikiwemo kutoa ajira kwa vijana wa kitanzania kwa asilimia 90, ambapo kwa mwaka huu wanatarajia kuwa na watendaji kazi na wa kujitolewa watakolipwa katika kusaidia tamasha hilo, zaidi ya watu 150.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa tamasha hilo, Yusuf Mahmoud ‘Dj Yusuf’ alisema tamasha hilo limeweza kuibua wasanii mbalimbali ikiwemo kujitangaza kimataifa.
Aidha, Dj Yusuf alieleza kuwa, tamasha la mwaka huu litaendana na kauli mbiu ya kuimiza Amani, pia wameandaa tuzo maalum na zawadi maalum kwa wasanii wa Tanzania watakaoshinda katika kutunga nyimbo za amani.
Mbali na Ali Kiba, Wasanii wengine Isabel Novella kutoka  Msumbiji, Ihhashi Elimhlophe (Afrika Kusini),   Tcheka (Cape Verde),   Diabel Cissokho (Senegal),  Culture Musical Club (Zanzibar),  Msafiri Zawose (Tanzania),   Aline Frazão (Angola),   Tsiliva (Madagascar),   Leo Mkanyia and the Swahili Blues Band (Tanzania),   Mohamed Ilyas & Nyota Zameremeta (Zanzibar),   Thaïs Diarra (Senegal / Mali / Uswisi),   Liza Kamikazi and band (Rwanda),   Erik Aliana (Cameroon),  Mpamanga (Madagascar),   Mgodro Group (Zanzibar),   Rico Single & Swahili Vibes (Zanzibar),   Zee Town Sojaz (Zanzibar),   Ifa Band (Tanzania) na wengine wengi. Maelezo zaidi yanapatikana katika www.busaramusic.org

Huyu ndio beki ambaye Man United wamegoma kukanusha kutaka kumsajili

2501322500000578-2931379-image-a-51_1422537948921Dirisha la usajili barani ulaya limebakiza takribani masaa 48 kabla ya kufungwa, na kama ilivyo ada tetesi za usajili wa wachezaji tofauti zimezidi kushika kasi.
Klabu ya Manchester United ambayo imekuwa na udhaifu kwenye kikosi hasa kwenye maeneo ya kiungo na beki wa kati, leo hii Manchester United wameshindwa kukanusha taarifa kwamba wametuma ofa ya £37m kwa Borussia Dortmund na kuanza mazungumzo kwa ajili ya usajili wa beki  Mats Hummels. Inaaminika ikiwa usajili huo utafanikiwa basi beki wa Dinamo Kiev Aleksandar Dragovic atanunuliwa kurithi mikoba ya Hummels.
United wamekuwa wakihusishwa na usajili wa Mats Hummels tangu wakati wa dirisha la kiangazi lakini walikutana na kizingiti cha Dortmund kugoma kumuuza beki huyo mshindi wa kombe la dunia mwaka 2014, lakini sasa klabu hiyo ambayo ipo kwenye mkia wa msimamo wa Bundesliga inaonekana kuwa tayari kumuuza beki huyo ambaye pia alikuwa akihusishwa na kutakiwa na Arsenal.
Wakati huo huo mchezaji na nahodha msaidizi wa Man United Darren Fletcher anatarajiwa kujiunga na West Ham United kwa uhamisho wa bure na anategemewa kusaini mkataba wa miaka miwili na nusu ikiwa kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa.

Crouch Akataa Kurejea London Kujiunga na Bosi Wake


 


 Mshambuliaji kutoka nchini England, Peter James Crouch amezima ndoto za aliyekua meneja wake Tony Pulis za kutaka kumuhamisha huko Stoke On Trent na kumpeleka jijini London kwa ajili ya kujiunga na klabu ya Crystal Palace.
Crouch, amezima ndoto hizo baada ya kukubali kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu ya Stoke City ambao utamuweka klabuni hapo mpaka mwaka 2017.
Pulis, alitarajia kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 33 kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu, kufuatia mkataba wake wa awali kutarajia kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.
Hata hivyo Crouch aliungana na mchezaji mwingine wa Stoke City, Glenn Whelan ambaye amakubali kuongeza mkataba mpya kwa muda wa miaka miwili ijayo.
Tonny Pulis wakati akiwa mnejea wa Stoke City alimsajili Crouch mwaka 2011 akitokea kwenye klabu ya Tottenham Hostpurs ya jijini London.

SAMATTA AREJEA LUBUMBASHI



 Habari zaidi kutoka lubumbashi zinasema kuwa klabu ya CSKA moscow ya Urusi  iliamua kuachana na Samatta kwa sasa kwa sababu ya kuumia enka akiwa katika wiki ya kwanza ya majaribio.
 kiongozi mmoja wa mazembe ambaye hakupenda kutajwa jina alisema kuwa timu hiyo ya ulaya ilivutiwa na mchezaji huyo wa Tanzania lakini ilishindwa kumtathimini zaidi baada ya kuumia.

Hata hivyo amesema kuwa klabu hiyo (TP MAZEMBE) ipo bega kwa bega na mchezaji huyo ili kutimiza azma yake ya kucheza ulaya.
Samatta ambaye amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake Tp mazembe tangu asajiliwe kutoka simba ya Dar es salaam, alipania mno mwezi huu january kuamia ulaya lakini inaonekana wakati wake bado.

YANGA SC YAIPA POLE SIMBA SC KWA KUPOTEZA MECHI YA PILI TAIFA

Jerry-Muro (1)
Uongozi wa Yanga SC umewapa pole watani waowa jadi, Simba baada ya kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City katika mechi yao iliyopita.
Simba SC iliyokosa huduma ya nyota wake Mganda Emmanuel Okwi, ilipata kipigo hicho cha pili msimu huu na cha kwanza kwa kocha mkuu mpya, Mserbia Goran Kopunovic katika mechi yao ya kiporo ya raundi ya 10 ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) Uwanja wa Taifa jijini hapa jana.
Baada ya kichapo hicho, Mkuu wa Idara ya Habari na Mwasiliano ya Yanga, Jerry Muro, alisema jana kuwa: “Tunawapa pole wenzetu wa upande wa pili (Simba) kwa kupata pancha leo (juzi). Tunaamini wataziba na kurejea katika mapambano.”
Yanga SC na Simba SC zimekuwa timu pinzani tangu hata kabla ya kuanzishwa kwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara 1965, Timu hizo zilianzishwa 1935 na 1936, Yanga SC ikiwa ni ya kwanza.

SIMBA, JKT RUVU KAZI IPO KESHO TAIFA


SIMBA, JKT RUVU NGOMA INOGILE TAIFA
MABINGWA wa kombe la Mapinduzi 2015, Simba SC kesho wanasaka pointi tatu kwa kila namna  ili kupunguza machungu waliyopata kwa kutandikwa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City katika mechi ya ligi kuu iliyopigwa juzi, januari 28 uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Simba watavaana na Maafande wa JKT Ruvu Stars  wanaonolewa na kocha wa zamani wa Yanga, Fredy Minziro, katika mechi ya VPL itayopigwa uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Huu ni mtihani wa tatu kwa kocha wa Simba SC, Goran Kopunovic kwani tayari ameshaiongoza timu hiyo katika mechi mbili za ligi kuu.
Kopunovic alianza ligi kuu kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ndanda fc, Januari 17 mwaka huu, kabla ya kulazimisha sare ya 1-1 na Azam fc, Januari 24 mwaka huu. Juzi wakalala 2-1 dhidi ya Mbeya City.
Tayari baadhi ya wanachama na mashabiki wa Simba wameanza chokochoko wakimtaka Rais wa Simba, Evans Aveva ajiuzulu kutokana na kushindwa kuweka umoja katika klabu hiyo.
Aveva ambaye haamini kama mgogoro wa Simba na wanachama wake wa UKAWA ndio chanzo cha kuboronga kwa timu, amekaririwa mara kadhaa kuwa uongozi wake hauko tayari na hauna mpango wa kukutana na kundi hilo maarufu nchini.
Lakini jana, Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa Simba, Zacharia Hans Poppe ambaye alifungua milango kwa UKAWA kurudi klabuni kama watafuta kesi yao Mahakamani alisema wanasimba hawana haja ya kuwalaumu viongozi kwa matokeo mabaya.
“Mchezaji kukosa penalti (Masoud Nassor Cholo) unamlaumu vipi kiongozi. Labda yeye ndiye aulizwe amekosaje penalti”. Alikaririwa Hans Poppe akiwatetea viongozi kutohusika na matokeo hayo.
Hata hivyo alisema kuna haja ya kufanya uchunguzi ili kubaini kama kuna hujuma klabuni hapo.
Simba inakabiliwa na matokeo mabaya ambapo mpaka sasa wameshinda mechi mbili tu dhidi ya Ruvu Shootings na Ndanda fc katika mechi 11 walizocheza.
Wamefungwa mara mbili dhidi ya Kagera Sugar na Mbeya City na kutoka sare saba.
Tayari kocha Kopunovic ameshatoa kauli ya kuwakatisha tamaa Wanasimba kwamba wasahau kutwaa ubingwa mwaka huu.
Kocha huyo alisema kama Simba wanawaza Ubingwa basi nayeye atafukuzwa kama ilivyotokea kwa makocha wengine waliomtangulia kwani haamini kama ana kikosi cha Ubingwa.
Mpaka sasa Simba wapo nafasi ya 11 wakijikusanyia pointi 13 katika mechi 11 walizocheza.

YANGA YATAFUTA GIA YA KUVUNA USHINDI KWA NDANDA FC


IMG_5570
YANGA yenye kumbukumbu ya ushindi wa goli 1-0 iliovuna mwishoni mwa wiki iliyopita Uwanja wa Jamhuri Morogoro dhidi ya Polisi Moro inawania pointi tatu zingine jumapili, februari 1 mwaka huu itakapocheza na Ndanda fc uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Hiyo itakuwa mechi ya nne ya ligi kuu kwa kocha Hans Van Pluijm ambaye alianza kwa sare ya mabao 2-2 na Azam fc Desemba 28 mwaka jana akirithi mikoba ya Mbrazil, Marcio Maximo.
Baadaye akatoka suluhu (0-0) na Ruvu Shootings, Januari 17 mwaka huu. Mwishoni mwa wili iliyopita alishinda 1-0 dhidi ya Polisi Moro.
Katika mechi tatu alizocheza na kushinda moja, Pluijm ameonekana kufanikiwa kuijenga Yanga inayocheza mpira wa pasi na kushambulia kwa kasi tofauti na kipindi cha Marcio Maximo ambapo Yanga walikuwa wanajihami sana.
Hata hivyo, bado kikosi hicho kilichosheheni nyota wengi akiwemo Mliberia Kpah Sherman, Mrundi Amissi Tambwe, Wanyarwanda Mbuyu Twite na Haruna Niyonzima, Wazawa Danny Mrwanda, Saimon Msuva kina mapungufu ya kucheka na nyavu.
Yanga wanatengeneza nafasi nyingi, lakini umaliziaji ni mbovu na ilifikia hatua uongozi ukaruhusu baadhi ya wanachama wake kuomba dua la kuondoa nuksi klabuni hapo.
Mbali na mechi hiyo ya jumapili, kesho Jumamosi kuna mechi nyingine zitapigwa.
Simba watawakaribisha JKT Ruvu uwanja wa Taifa, Coastal Union watachuana na Mtibwa Sugar uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Ruvu Shootings wataikaribisha Stand United uwanja wa Mabatini, wakati Tanzania Prisons watakuwa nyumbani uwanja wa Sokoine kuchuana na Kagera Sugar.
Polisi Moro watakabiliana na wababe wa Simba, Mbeya City fc.
Mechi ya Mgambo na Azam fc haitakuwepo kwasababu mabingwa  watetezi hawapo nchini kwasasa.
Azam fc ipo nchini DR Congo kushiriki mashindano ya Mazembe yanayoendelea mjini Lubumbashi ikiwa ni maandalizi ya mechi ya ligi ya mabingwa itakayopigwa mwezi ujao dhidi ya El Merreick ya Sudan.

ALICHOKISEMA MCHEZAJI WA ZAMANI WA SIMBA KUHUSU KUBORONGA KWA TIMU HIYO


???????????????????????????????
KUTOKANA na mwenendo mbovu wa Simba SC katika mechi za ligi kuu Tanzania bara, mchezaji wa zamani wa timu hiyo na kiongozi wa TFF, Mtemi Ramadhani amefanya mahojiano maalumu na mtandao huu na kuweka wazi sababu za Mnyama kuzidi kuboronga.
Mwandishi: Mtemi Ramadhani, wewe ni mchezaji wa zamani wa Simba, sasa hivi kumekuwa na malalamiko mengi ya wanachama na wapenzi wa Simba kuhusu mwenendo wa timu yao, kwa uzoefu wako wa kuwa kwenye mpira kwa miaka mingi unafikiri nini kinawasibu Simba saha hivi?
Mtemi: Suala la Simba liko wazi, mwenye kujua mpira anajua kwasababu mpira hauchezwi vyumbani, mpira unachezwa hadharani. Timu ilivyocheza Zanzibar kila mtu aliona, timu inavyocheza hapa kila mtu anaona, tatizo la Simba ni kwamba vijana wa Simba hawataki mazoezi.
Timu ya Simba haina mazoezi magumu, suala lao ni kwamba hawataki mazoezi. Simba wamecheza mechi sita kule Zanzibar, zilikuwa za mfululizo na walikuwa kambini, lakini baada ya pale walirudi kucheza na Ndanda. Nasikia tena wakafanya kambi siku moja kabla ya mpira, huwezi kucheza mpira bila kufanya mazoezi magumu hata siku moja, haiwezekani.
Simba hawajajiandaa vya kutosha, Simba ikicheza na timu yoyote inayofanya mazoezi magumu, ya kukimbia huku na kule, haiwezi kushinda kwa pumzi ile.
Na jambo zuri zaidi ni kwamba mipira inaonekana kwenye ligi nzuri, kama ni Afcon, kama ni Barcelona, Real Madrid,  wanaona duniani kote ambavyo mpira umebadilika, watu wanacheza kwa nguvu, wanakimbia, wanakaba. Simba mpaka mchezaji apate mpira ndio beki anakwenda kukaba, kwahiyo anatoa pasi kwa mwingine ambaye hajakabwa.
Simba hawezi kucheza mpira wa namna hiyo, hata iweje, na wanaweza kushuka daraja hivi hivi, si jambo la kuamini, lakini si la ajabu.
Mwandishi: Lawama kubwa zinatupiwa kwa uongozi, unafikri utawala nao unachangia mwenendo mbaya wa timu?
Mtemi: Naweza nikasema ndiyo! Ingawa si kwa asilimia kubwa. Lakini wanapaswa kusimamia timu, hawa walimu wa kizungu wana tatizo moja, tulikuwa na mzee mmoja alikuwa anaitwa Jan Poulsen pale TFF, timu ikifanya mazoezi asubuhi jioni anasema walale, ukimwabia tufanye hiki, anasema siku mbili wapumzike.
Binafsi niliwahi kuongea na mwalimu yule, akasema unajua mpira wa siku hizi hautaki mbio sana, si unao Barcelona wanavyocheza. Sasa ni jukumu la viongozi kusimamia, mwalimu anaweza kutoka na mambo yake ya ulaya, kamati ya utendaji inatakiwa imuite na kumwambia, “Bwana wachezaji wa Kiswahili wako moja, mbili, tatu na bila kufanya moja, mbili, tatu,hatuwezi kwenda”.
Sasa unamwachia mwalimu wa Kizungu ambaye anakuja na falsafa ya watu wa nje ambako wachezaji wanajitambua, wanalala majumbani kwao, wana mapesa mengi, mtu anatambua wajibu wake.
Hawa wa kwetu sio siri hawajitambui, tunawaona, mtu anatoka mazoezini  na gari yake ndani ana mwanamke, mwingine utasikia nusura apigwe chupa Kinondoni kwasababu ya kugombania mwanamke, hao ni wachezaji wa Simba, huwezi kucheza mpira namna hiyo.

YANGA YATAKA MECHI YAKE DHIDI YA MTIBWA SUGAR ISOGEZWE



Uongozi wa Klabu ya Yanga umesema unatarajia kuwasilisha barua kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jumatatu ijayo kuomba mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar wa Februari 8, usogezwe mbele.

Yanga inatarajiwa kukipiga na BDF XI ya Botswana katika Kombe la Shirikisho mnamo Februari 14 lakini inatakiwa itekeleze majukumu yake katika Ligi Kuu Bara, Februari 8.
Katibu wa Yanga, Jonas Kiboroha amesema hii: “Tumeandaa barua ambayo tutaipeleka TFF siku ya Jumatatu kuomba mchezo wetu dhidi ya Mtibwa usogezwe kwa lengo la kupata muda wa kujiandaa kabla ya kuivaa BDF XI.”
Wakati huohuo, Yanga ipo katika mazungumzo na timu ya Vipers ya Uganda kwa ajili ya kucheza nao mchezo wa kirafiki kabla ya kuvaana na BDF XI.
Mkuu wa Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro, ndiye aliyetoa tamko kwa kusema: “Tupo katika mazungumzo na Vipers lakini hatuwezi kusema lini tutacheza nao rasmi kwa kuwa bado mazungumzo yanaendelea.”