SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Jun 4, 2015

NOOIJ ABEBA 23 TAIFA STARS SAFARI YA ADDIS KUFUATA DAWA YA 'KUNYONGA' MAFARAO

Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Mart Nooij ametangaza kikosi cha wachezaji 23 watakaoondoka leo jioni kuelekea Addis Ababa nchini Ethiopia kuweka kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mholanzi huyo amesema watatumia kambi ya Ethiopia kujiandaa na mchezo wa Misri, vijana wapo katika hali nzuri na wameahidi kupambana kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo huo.
Mchezo kati ya Misri na Tanzania unatarajiwa kuchezwa Juni 14, katika uwanja wa Borg El Arab jijini Alexandria, ikiwa ni mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika (AFCON) mwaka  2017.
Kocha Mart Nooij amechukua wachezaj 23 wa kuivaa Misri

Kikosi cha Stars kinaondoka saa 11 jioni kwa Shirika la ndege la Ethiopia ambapo inatarajiwa kuwasili jiji la Addis Ababa majira ya saa 1 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Wachezaji wanaosafiri kuelekea nchini Ethiopia ni Deogratias Munish, Aishi Manula, Mwadini Ali, walinzi Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Erasto Nyoni, Nadir Haroub, Aggrey Morris, Mwinyi Haji, Salum Mbonde na Juma Abdul.
Wengine ni Mwinyi Kazimoto, Abdi Banda, Salum Telela, Frank Domayo, Jonas Mkude, Said Ndemla, washambuliaji Saimon Msuva, John Bocco, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta, Mrisho Ngassa na Juma Liuzio.
Msafara wa Taifa Stars utaongozwa na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji, Vedastus Lufano na Geofrey Irick Nyange “Kaburu”.
Naye mjumbe wa kamati ya Utendaji  ya TFF Vedastus Lufano amesema timu inakwenda kuweka kambi Ethiopia kwa ajili ya kupambana katika mchezo dhidi ya Misri.
Kikosi kingine cha timu ya Taifa kitaondoka nchini siku ya jumamosi kuelekea nchini Rwanda kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya Rwanda katika kumbukumbu ya mauaji ya Kimbali.
Kocha Salum Mayanga ataondoka na kikosi cha wachezaji 18 kuelekea nchini Rwanda kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki, akisaidiwa na kocha Bakari Shime.
Wachezaji watakaondoka kwenda Rwanda ni Peter Manyika, Said Mohamed, Emmanuel Semwanda, Joram Mgeveke, Hassan Isihaka, Gadiel Michael, Hassan Dilunga, Rashid Mandawa, Atupele Green, Kelvin Friday, Hassan Kessy, Ibrahim Hajibu, Malimi Busungu, Mudathir Yahya, Deus Kaseke, Andre Vicent, Amri Kiemba na Mohamed Hussein.

MANCHESTER UNITED IMEWAPIKU BARCELONA NA BAYERN KUMNASA MCHEZAJI HUYU

11a
Usajili ndio mpango mzima hivi sasa huko Ulaya. Manchester united imewashinda Bayern Munich na Barcelona kwenye vita ya kupaya saini ya mchezaji wa Borussia Dortmund.
Mchezaji huyo ambae anacheza sehemu ya midfield amesakubaliana mambo ya msingi na Manchester united. Gundogan anatarajiwa   kutangazwa na Manchester united kuwa mchezaji mpya wa club hiyo.
11

MAKOMBE 24 KABLA YA KUONDOKA, JE BABU XAVI ANAWEZA KUONGEZA MOJA JUMAMOSI?


Wakati Xavi Harnandez ,35, anajiandaa na kustaafu rasmi baada ya kuitumikia Barcelona kwa miaka 17 ya maisha yake, swali je, atafanikiwa kuongeza kombe jingine hapo keshokutwa.

Barcelona inashuka dimbani mjini Berlin, Ujerumani kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Juventus ya Italia.
Utaona katika picha hiyo hapo juu, Xavi akiwa amezungukwa na makongwe 24 aliyowahi kubeba akiwa na Barcelona kwa miaka 17.
Hapo kuna makombe manane ya La Liga, matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, mawili ya UEFA Super Cups, matatu ya Copa del Reys, sita ya Spanish Supercups na mawili ya Kombe la Dunia kwa klabu.


Swali ni kwamba ataweza kubeba kombe lake la 25 kabla ya kuondoka Barcelona?

MWADUI YA JULIO YAIBOMOA TENA MBEYA CITY, YAMTWAA STRAIKA PAUL NONGA

Kama ulidhani Mwadui Football club wanafanya utani, basi ujue unajidanganya maana sasa wamemsajili straika tegemeo wa Mbeya City, Paul Nonga.

Nonga amemsajili Nonga ambaye aliwahi kuichezea ikiwa daraja la tatu klabla ya kuondoka na kujiunga na JKT Oljoro ya Arusha.
Nonga amejiunga leo na Mwadui FC ingawa haijaelezwa mkataba huo utakuwa ni wa muda gani kama ni mwaka mmoja au miwili.
Saa chache zilizopita, Mwadui FC inayofundishwa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ imemsajili beki wa Mbeya City, Anthony Matogolo.
 
Benchi la ufundi la matajiri hao wa Mwadui kutoka mkoani Shinyanga linaonyesha limepania kujiimarisha mara tu baada ya kupanda Ligi Kuu Bara.
Mwadui FC ni kati ya timu zilizokuwa katika daraja hilo katika miaka ya 1980. Sasa imerudi tena na inaonekana imepania kuleta ushindani hasa.