SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Feb 28, 2015

SAMATTA :SINA FURAHA TP MAZEMBE


samatta_cska_2
Samatta alikwenda kufanya majaribo CSK Moscow ya Urusi, lakini hakufanikiwa baada ya kupata majeruhi ya kifundo cha mguu
Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
 Mshambulizi wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta ameweka wazi kuwa ataachana na mabingwa mara nne wa kihistoria wa Afrika, TP Mazembe mara baada ya kumalizika kwa mkataba wake. Akizungumza na mwandishi wa mtandao wa www.shaffihdauda.co.tz muda mfupi uliopita mshambulizi huyo wa Taifa Stars amesema kuwa hana furaha katika timu hiyo ya Congo.

 Samatta ambaye alipata nafasi ya kufanya majaribio katika klabu ya CSKA Moscow ya Urusi mwezi uliopita amepewa ofa nyingi barani ulaya na kama ataendelea kuchezea TP basi atakuwa ni mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi barani Afrika. Hivi karibuni kuna vyombo vya habari ambavyo viliripoti kuwa mchezaji huyo ana furaha kuendelea kuichezea TP lakini amesema huo ni uzushi mkubwa.


 ” Sina furaha hapa ( TP Mazembe) nitaondoka wakati wa majira ya usajili katikati ya mwaka na sitaongeza mkataba” anasema Samatta. Ni wapi anakwenda, nini kinachomuondoa TP Mazembe, tafadhaLi endelea kufuatilia mtandao huu wa www.shaffihdauda.co.tz... na www.hajibalou.blogspot.com Utapata kujua wapi mchezaji huyo anakwenda. Je, tayari ameruhusiwa na Katumbi Moies mmliki wa TP?…..

WALICHO FANYIWA AZAM FC SUDAN KABLA YA MECHI YA LEO


Azam FC leo saa mbili usiku itajitupa kwenye uwanja wa AlMerrikh kukwaana na Al Merrikh SC.
Azam FC ambayo ilitua hapa Khartoum Jumanne 24/2/2015 imekuwa katika hali nzuri tangia kuwasili. Vijana wa kitanzania wanaosoma hapa Khartoum wamekuwa wenyeji wetu.
Azam FC imekodi Apartment nzima, tumekuwa tukiishi kama nyumbani, tunapika wenyewe, tuna ulinzi wa kutosha wa kambi, na walinzi wetu ambao tumesafiri nao toka Dar es Salaam wakiongozwa na afisa wa usalama wa Taifa wamekuwa wakifanya doria masaa 24.
Tulipowasili Khartoum, wapinzani wetu walijaribu kucheza mchezo mchafu wa kutuchanganya kisaikolojia kwa kuleta mabasi mawili mabovu kutupolea lakini walishangazwa kuona Azam FC ikiachana na basi lao na kupanda basi lingine zuri lililoandaliwa na viongozi wa Azam FC waliotangulia siku tatu kabla.
Jana wakati timu inaenda kufanya mazoezi uwanjani mashabiki wa Merrikh walijipanga barabarani na kurusha vumbi, makopo, mawe nk lakini polisi waliokuwa kwenye magari maalum wakisaidiwa na wanajeshi walifanikiwa kuwadhibiti.
Wenyeji wanasema mashabiki wa Merrikh ni wakorofi na wamekuwa na kawaida ya kufanya fujo kwa timu ngeni.
Benchi la ufundi la Azam FC linaloongozwa na Joseph Omog limesema hawana wasiwasi kabisa kwani wamewaandaa vijana kwa ajli ya mchezo wa leo.
CHANZO AZAM FC PAGE

DI MARIA AJUTA KUJIUNGA MAN UNITED

Mchezaji wa Manchester United Angel Di Maria
Mchezaji nyota ambaye pia ni kiungo wa kati wa Manchester United Angel Di Maria amesema kuwa alifanya makosa kujiunga na Kilabu ya Manchester United msimu uliopita.
Raia huyo wa Argentina amejaribu kuingiana na maisha ya ligi ya Uingereza na majuto yake yataongeza uvumi kwamba anapanga kuondoka katika kilabi hiyo miwshoni mwa msimu huu.
Mwandishi wa Uhispania Manolete Esteban anadai kwamba mchezaji huyo wa zamani wa kilabu ya Real Madrid ambaye amekosolewa kwa uchezaji wake amewaambia marafiki zake kwamba anajuta kuondoka katika kilabu ya Real Madrid.
Esteban aliiambia runinga ya Uhispania katika kipindi cha La Goleada kwamba Di maria alikiri kwa rafikiye katika kilabu ya Real Madrid kuwa anajuta kujiunga na Manchester United.

SIMBA YATAKATA TAIFA AJIBU APIGA HAT-TRICK


simba ushindiNa Richard Bakana, Dar es salaam
Klabu ya Simba ya Jijini Dar es salaam leo imefanikiwa kutoa dozi ya msimu kwa maafande wa Tanzania Prisons, baada ya kuwafunga mabao 5-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara uliopigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
 Katika mchezo huo mshambuliaji wa Simba Ibrahim Ajib ndio aliibuka kinara wa kufumania nyavu baada ya kutupia kambani bao 3 (Hat trick) ambapo katika kipindi cha pili alipumzishwa baada ya kupewaa kadi njano.
Simba walijipatia ushindi huo kupitia kwa Ibrahim Ajib dakika ya 15, dakika 21 na dakika ya 42 kwa mkwaju wa penati, na kufanya muamuzi wa mchezo huo Odongo ampatie mpira wake kwa kazi nzuri aliyoifanya.
Baada ya kutengeneza nafasi nyingi za mabao Okwi naye akaiandikia Simba bao la nne katika dakika ya 74 kabla ya Ramadhan Singano kumaliza kazi kwa kufunga bao la tano katika dakika ya 82 kufatia kazi nzuri ya Emanuel Okwi.
Kwa ushindi huo Simba inakuwa imeweka rekodi nzuri ya kufunga mabao mengi katika mchezo huku ikiwa ni salamu kuelekea mchezo na Yanga wiki kesho Machi 8.

VAN GAAL ATAJA TATIZO LA MAN UNITED


Kilabu ya Manchester United haiwezi kushinda taji la ligi kwa kuwa haina mshambuliaji mwenye uwezo wa kufunga mabao 20 kwa msimu.
Meneja Luois Van Gaal amesema kuwa mshambuliaji mwenye mabao mengi katika klabu hiyo ni Van Persie mwenye mabao 10 pekee ikilinganishwa na Diego Costa na Sergio Aguerro ambao wamefunga mabao 17 kila mmoja wao.
Radamel falcao
''Ni kweli'',alisema Van Gaal.
''Robin van Persie hawezi kukataa,Falcao naye hawezi kupinga na Rooney hachezi katika safu ya mashambulizi.
Van Persie
MKufunzi huyo wa Old Trafford amekuwa akikosolewa kwa kumchezesha Wayne Rooney katika kiungo cha kati,huku Radamel Falcao akipewa fursa chache kwa madai kwamba hayuko shwari.
Van Gaal alisema:''Kwa sasa hatuna mshambuliaji ambaye anaweza kufunga mabao 20''.

KAPTENI JOHN KOMBA ALIYEIMBA 'MGENI' AFARIKI DUNIA


MBUNGE wa Mbinga Magharibi na mkurugenzi wa Tanzania One Theatre (TOT) Kapten John Komba amefariki dunia muda huu.
Katibu mipango wa TOT, Gasper Tumaini ameithibitishia BIN ZUBEIRY jioni hii kwamba, Komba amefari na taarifa zaidi zitatoka hapo baadaye.
Kwa muda mrefu tangu amestaafu jeshi, Komba amekuwa Mkurugenzi wa kikundi cha sanaa cha Chama cha Mapinduzi (CCM), kiitwacho TOT na miaka ya karibuni amekuwa akitamba na wimbo Mgeni, unahusu ugonjwa hatari wa Ukimwi.

Feb 27, 2015

MESSI WA MBEYA CITY AREJEA DIMBANI


Messi-Wall1-630x360
BAADA ya kuwa nje kwa majeruhi muda mrefu, kiungo mshambuliji  wa Mbeya City Fc, Alex Seth ‘Messi’ amerejea kikosini tayari kuendeleza mapambano katika kindumbwendumbwe cha ligi kuu ya soka Tanzania Bara.
Seth amekaririwa na Tovuti ya Mbeya City fc akisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kupona majereha yaliyokuwa yanamsumbua kwa kipindi kirefu na kumfanya kuikosa ligi  kwa kipindi kirefu.
“Nashukuru nimepona,nilikosa ligi kwa kipindi kirefu mara ya mwisho nilicheza dhidi ya Tanzania Prison msimu uliopita,narudi kuongeza nguvu kwenye kikosi, kama timu tulikuwa na wikiendi mbaya baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Yanga lakini jumamosi  hii  naimani itakuwa ni sehemu nyingine ya furaha  kwetu hasa  kwa kuongeza pointi tatu muhimu dhidi ya Ruvu Shooting” alisema.
Akiendelea zaidi Seth alisema, hivi sasa kwenye kikosi imani ya kila mchezaji ni kucheza kwa nguvu ili kutafuta matokeo kwenye mchezo ujao huku akiamini kuwa hilo linawezekana hasa ukizingatia morali iliyopo hivi sasa miongoni mwa nyota wa City bila kujali nini kilikuwepo juma lililopita.
“Naomba mashabiki wawe na timu yao, bado iko vizuri na kwa uwezo wa mwenyezi mungu naimani tutashinda jumamosi, tunajua walikosa furaha baada ya mchezo uliopita lakini huu ni wakati wao na waamini kwenye soka inawezekana kushinda mchezo unaofuata  hata kama ulipoteza mchezo uliopita” alimaliza.

AZAM WAZIPOTEZA FITINA ZA WASUDANI

 10403629_918481188192238_6973291696561800103_n
MABINGWA watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara na wawakilishi wa nchi katika michuano ya ligi ya mabingwa Afrika, Azam fc wanaendelea kujifua nchini Sudan kuelekea mechi ya marudiano dhidi ya wenyeji Al Merrick itayopigwa kesho jumamosi usiku uwanja wa Odmarman, mjini Khartoum.
Azam fc wataingia katika mechi ya kesho wakiwa na faida ya mabao 2-0 waliyovuna februari 15 mwaka huu uwanja wa Azam Complex, Dar es salaam.
Mabao hayo yalifungwa na Didier Kavumbagu na Nahodha John Raphael Bocco ‘Adebayor’.
 Licha ya kufanyiwa fitina za hapa na pale, kocha mkuu wa Azam, Mcameroon, Joseph Marius Omog ameendelea na programu yake ya mazoezi leo.
Azam wanahitaji sare ya aina yoyote ile au kufungwa si zaidi ya goli 1-0 ili kusonga mbele.

MCHEZAJI SERBIA ATISHIWA KUUAWA KWA BUNDUKI KISA KUKOSA PENALTI

MCHEZAJI wa klabu ya Ligi Kuu ya Serbia, Novi Pazar ametishiwa kupigwa bastola na mashabiki baada ya kukosa penalti, taarifa ya chama cha Umoja wa Wachezaji Duniani, FIFPro imesema jana.
Ikiliita tukio hilo kama sheria mpya katika soka ya Serbia, FIFPro imesema kwamba mchezaji wa Novi Pazar, Zarko Udovicic alipaisha mkwaju wake wa penalti juu ya lango dakika ya 85 Jumamosi iliyopita katika mchezo dhidi ya FK Rad.
Siku mbili baadaye, mashabiki kadhaa wenye hasira walivamia chumba cha kubadilishia nguo cha wachezaji na kwenda kumuonyeshea mtutu wa bunduki usoni Udovicic, imesema taarifa ya FIFPro. Baada ya hapo, mchezaji huyo ameondoka kwenye klabu hiyo.
Zarko Udovicic has left Serbian club Novi Pazar after  fans threatened him with a gun for missing a penalty
Zarko Udovicic ameondoka Novi Pazar ya Serbia baada ya kutishiwa mtutu wa bunduki kwa kukosa penalti

Mirko Poledica, Rais wa Chama cha Wachezaji wa Kulipwa Serbia, Nezavisnost, amesema hakuna aliyechukua hatua baada ya tukio hilo kati ya Chama cha Soka Serbia au bodi ya Ligi.
"Nchini Serbia, hakuna shabiki aliyewahi kuchunguzwa au kutiwa hatiani baada ya kuwafanyia fujo wachezaji. Ndiyo maana wachezaji wanaogopa. Kila siku wanaishi kwa matumaini ifike wakati wasiwe na mashaka ya kugongewa milango na kupigwa na mashabiki, au kuchomewa moto gari zao,".
FIFPro imesema; "Kama ilivyo kwa mfanyakazi yeyote kitaaluma, kila mchezaji anastahili kuwekewa mazingira salama ya kufanyia kazi. Ni juu ya mamlaka za soka kuweka mazingira hayo salama,".
Udovicic had missed a penalty for Novi Pazar against FK Rad two days before the incident
Udovicic alivyopaisha penalty ya Novi Pazar dhidi ya FK Rad kabla ya kutishiwa mtutu wa bunduki siku mbili baadaye

PLUIJM AWAPA UHAKIKA YANGA SC WANALING’OA JESHI LA BOTSWANA AFRIKA

Na Mwandishi Wetu, GABORONE
KOCHA Mkuu wa Yanga SC, Mholanzi Hans van der Pluijm amewatoa hofu wapenzi wa timu hiyo kuelekea mchezo wa leo dhidi ya BDX XI, akisema kwamba; “tiketi ya kusonga mbele ipo”.  
Yanga SC wanatarajiwa kuwa wageni wa timu hiyo ya Jeshi la Botswana katika mchezo wa marudiano, Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika utakaofanyika Uwanja wa Lobetse kuanzia Saa 1:00 usiku kwa saa za huko na Saa 2:00 kwa saa za Afrika Mashariki.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana mjini hapa katika mahojiano maalum kuelekea mchezo wa leo, Pluijm amesema kwamba vijana wake wako tayari kwa kazi nzuri leo. 
Hans van der Pluijm akiwa na Msaidizi wake, Charles Boniface Mkwasa

Kocha huyo ambaye jana asubuhi alifanya mazoezi na kikosi chake katika Uwanja wa Lobetse utakaotumika kwa mcheo huo wa leo, amesema wataingia na akili ya kutaka kuthibitisha ubora wa timu yao.
Pluijm amesema wameuona Uwanja wa mchezo na kwake hauna sababu ya kuifanya timu yake kukosa ushindi na akawaambia wachezaji wake kufanya kweli kwa kupata ushindi lengo likiwa kuthibitisha ubora wa timu yao.
Pluijm amesema wataingia katika mchezo huo kupigana kwa nguvu zao zote ili wapate ushindi mzuri na kusonga mbele.
"Tunataka kuthibitisha ubora wetu kuwa sisi ni Yanga, nimewaambia vijana watulie wacheze kama tulivyokubaliana, kama tutadumisha nidhamu ya mchezo, ushindi upo,"amesema Pluijm.
Yanga SC inahitaji hata sare leo ili kusonga mbele, baada ya awali kushinda mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

WAZIRI WA KIKWETE ATUA SUDAN KUIPA ULINZI AZAM FC


Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Vijana na Michezo, Alhaj Juma Nkamia (kushoto) akizungumza na wachezaji wa Azam  FC mazoezini Uwanja wa Jeshi mjini Khartoum, Sudan usiku wa jana. Anayezungumza naye kulia ni mshambuliaji Mrundi, Didier Kavumbangu. Azam FC watacheza na wenyeji El Merreikh kesho mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika. Mechi ya kwanza, Azam FC ilishinda 2-0 Dar es Salaam.
Wachezaji wa Azam FC wakifanya mazoezi mepesi Sudan jana
Kocha wa makipa, Iddi Abubakar kulia na vijana wake wakifanya dua
Wachezaji wa Azam FC wakiteremka kwenye basi wanalotumia mjini Khartoum ambalo wanajilipia wenyewe baada ya kukataa basi walilopewa na wenyeji wao

KURASA ZA MWANZO NA ZA MWISHO MAGAZETI YA MICHEZO LEO 27 FEB

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

NTAMPATA WAPI YA DIAMOND YASHIKA NAMBA 1 UFARANSA


.
.
Kama wewe ni shabiki wa muziki wa Africa unaweza kuwa na hamu ya kufahamu ni single gani ambayo iko juu kwenye chati za muziki huu duniani…. kwa sababu kazi yangu ni kukusogezea zote muhimu, nakusogezea na hii kwamba video ya ‘Nitampata wapi’ ya Diamond Platnumz kupitia kituo cha TraceTV ya Ufaransa imeicheza video hiyo kama namba 1.
.
.
Mbali na video hiyo kuchezwa kama namba 1 kwenye kituo hicho cha Trace TV, Diamond Platnumz ana sababu nyingine ya kufurahi mafanikio ya kuwa msanii wa kwanza wa Tanzania kupitia video yake ‘Nitampata wapi’  kufikisha views milioni 2 tangu iwekwe Nov 20, 2014.
.
.
.
.
.
.

INTER MILAN NAYO YASONGA MBELE EUROPA LEAGUE

Van Dijk contests for the ball alongside Inter Milan striker Mauro Icardi in the Europa League game
Van Dijk wa Celtic akigombea mpira na mshambuliaji wa Inter Milan, Mauro Icardi katika mchezo wa Europa League usiku huu mjini Milan. Inter walishinda 1-0 ma kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-3, baada ya sare ya 3-3 awali nchini Scotland.

MCHEZAJI WA CHELSEA AIADHIBU SPURS NA KUITUPA NJE ULAYA

Former Basle forward Salah was booked after taking his shirt off in celebration of his goal on Thursday
Mshambuliaji wa Chelsea, Mohammed Salah anayecheza kwa mkopo Fiorentina ya Italia, akishangilia baada ya kuifungia timu yake ya mkopo bao la pili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Totenham Hotspur usiku nchini Italia katika mchezo wa Europa League. Bao la kwanza la Fiorentina lilifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Bayern Munich, Mario Gomez na hivyo wameitoa Spurs kwa jumla ya mabao 3-1, baada ya sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza.

LIVERPOOL YATUPWA NJE YA MICHUANO YA ULAYA

LIVERPOOL imetupwa nje ya michuano ya Europa League, baada ya kufungwa kwa penalti 5-4 na Besiktas kufuatia sare ya jula ya 1-1.
Tolgay Arslan alitokea benchi na kuifungia Besiktas bao dakika ya 72 Uwanja wa Ataturk, Istanbul nchini Uturuki akimalizia ‘pande’ la Demba Ba na kufanya sare ya jumla ya 1-1 baada ya Liverpool kushinda 1-0 katika mchezo wa kwanza England.
Ba angeweza kufunga bao la ushindi dakika ya  92, kama asingegongesha mwamba akiwa umbali wa mita sita.
Baada ya dakika 120, penalti za Besiktas zilifungwa na Ba, Lambert, Tore, Lallana na Kavlak, wakati zilifungwa na Can, Hutchinson, Allen na Arslan huku Lovren akikosa.
Kikosi cha Besiktas kilikuwa; Gonen, Opare, Franco, Uysal, Kurtulus, Hutchinson, Kavlak, Tore, Sosa/Arslan dk61, Sahan/Frei dk105 na Ba.
Liverpool: Mignolet, Toure, Lovren, Skrtel, Moreno, Can, Allen, Sterling, Ibe/Manquillo dk76, Sturridge/Lambert dk106 na Balotelli/Lallana dk82.
Liverpool failed to repeat their 2005 Champions League final heroics in Istanbul as they were dumped out of the Europa League by Besiktas
Wachezaji wa Liverpool wakisitika baada ya kutolewa Europa League na Besiktas, kulia Demba Ba akishangilia


Feb 26, 2015

AZAM TV ‘KURUSHA LIVE’ MECHI YANGA NA BDF BOTSWANA KESHO



Rhys Torrington (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Azam Media Group Limited, Yussuf Bakhresa (kushoto)
TELEVISHENI ya kisasa ya kulipia kwa gharama nafuu, Azam TV itaonyesha moja kwa moja mchezo wa marudiano wa Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika, kati ya wenyeji BDF XI na Yanga SC ya Tanzania.
Mchezo huo utakaofanyika Uwanja wa Lobatse mjini Lobatse, kuanzia Saa 11:30 jioni kwa saa za Afrika za Mashariki utaonyeshwa moja kwa moja na Azam Two.
Mtendaji Mkuu wa Azam Media Group, Muingereza Rhys Torrington ameiambia BIN ZUBEIRY jioni hii kwamba, mipango yote ya kuonyesha mchezo huo imekamilika.
“Kila kitu kimekamilika na tunayo furaha kuwaambia wateja wetu kwamba kesho tutakuwa na zawadi nzuri kwao, ambayo ni mchezo wa Yanga na BDF XI, watautazama kupitia Azam TV,” alisema Torrington.
Katika mchezo huo wa kesho, Yanga SC inahitaji hata sare ili kuweza kusonga mbele, baada ya awali kushinda mabao 2-0 nyumbani, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

CANNAVARO AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIEZI 10 JELA

NAHODHA wa kikosi cha Italia kilichobeba Kombe la Dunia mwaka 2006 nchini Ujerumani, Fabio Cannavaro amehukumiwa kifungo cha miezi 10 jela kwa kukiuka amri ya kutofika katika nyumba yake iliyozuiliwa na Mamlaka.
Cannavaro mwenye umri wa miaka 41, amekuwa akichunguzwa kwa tuhuma za kukwepa kodi na Oktoba Mamlaka mjini Naples ilizuia mali za karibu Pauni 732,737 zinazohusishwa na mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid na Juventus pamoja na mkewe.
Kaka wa Cannavaro, Paolo mwenye umri wa miaka 33, ambaye anachezea timu ya Ligi Kuu Italia, Sassuolo, naye amehukumiwa kifungo cha miezi sita na mkewe Daniela Arenoso mwenye umri wa miaka 40 miezi minne.
Watatu hao wamekata rufaa na kifungo chao kimesitishwa hadi mwisho wa rufaa yao.
Cannavaro won 136 caps for Italy and claimed two La Liga titles while at Real Madrid
Cannavaro amehukumiwa miezi 10 jela, ingawa kifungo chake kimesitishwa kupisha rufaa yake
Beki na Nahodha wa Yanga SC, Nadir Haroub Ali (kulia) anafahamika kwa jina la utani Cannavaro akifananishwa kiuchezaji na Nahodha wa zamani wa Italia, Fabio Cannavaro

Ndugu hao akina Cannavaro na Arenoso waliponzwa na kwenda kutembelea nyumba hiyo wakati ipo kizuizini. 
Cannavaro alishinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia, Ballon d'Or mwaka 2006 baada ya kuiongoza Italia kutwaa Kombe la Dunia. Akahamia Real Madrid baada ya hapo, ambako alikwenda kutwaa mataji mawili ya La Liga na vigogo hao wa Hispania.
Beki wa klabu ya Yanga SC ya Tanzania, Nadir Haroub Ali, amepewa jina la utani Cannavaro kutokana na Mtaliano huyo aliyeichezea mechi 136 Azzuri. 

JULIO AANZA MANENO COASTAL UNION

Na Oscar Assenga, TANGA
KOCHA Msaidizi wa Coastal Union, Jamhuri Kiwelu “Julio”amesema kuwa timu hiyo itapata matokeo mazuri katika mechi zake zilizosalia katika michuano ya Michuano ya Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kutokana na ubora wa kikosi hicho
Julio alitoa wito huo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa mara kumalizika mazoezi ya timu hiyo ambapo alisema kuwa lengo la kujiunga na timu hiyo ni kuongeza nguvu ili kukiwezesha kikosi hicho kurudisha makali yake.
Jamhuri Kihwelo 'Julio' kushoto amesema Coastal Union itatisha

Alisema kuwa atahakikisha anatoa mchango wake mkubwa kwenye timu hiyo ili kuiwezesha kufanya vizuri katika michezo mbalimbali ya Ligi kuu soka Tanzania bara hapa nchini.
“Mimi niliwahi kuifundisha Coastal Unionna kuiwezesha kupata mafanikio hivyo ni matumaini yangu kukiwezesha kikosi hichi kurejesha makali yake kwani timu hii ni kubwa na inaheshima yake kwenye soka “Alisema Kocha Julio.
Kocha huyo alisaini mkataba wa muda mfupi mpaka ligi kuu soka Tanzania mzunguko wa pili utakapomalizika ambapo atatumia nafasi hiyo kukipa makali kikosi hicho.
Alisema kuwa malengo makubwa yake ni kuhakikisha timu hiyo inachukua ubingwa wa Michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara ikiwemo kuwataka wachezaji kushikamana na kuwa watulivu kila mechi ili kupata mafanikio.
Hata hivyo alisema kuwa hatasita kuwafukuza kwenye kikosi hicho wachezaji watakaokuwa watovu wa nidhamu na watakaojiona mastaa na kushindwa kuendana na kasi yake katika mazoezi.
“Nashukuru kutua Coastal Union sasa ni kazi tu tutahakikisha tunapambana kufa na kupona ili kuweza kupata matokeo mazuri kila mechi zilizosalia kwenye Ligi hiyo “alisema Julio.

HIKI NDIO KIKOSI BORA LIGI YA MABINGWA WIKI HII


IMG_20150226_194709

TAIFA STARS YAPANGWA KUNDI A COSAFA, IKO NA ZIMBABWE, NAMIBIA



Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imepangwa Kundi A katika michuano  ya kombe la COSAFA nchini Afrika Kusini.
Kundi A:
Tanzania, Namibia, Lesotho na Zimbabwe.
Kundi B:
Shelisheli, Madagascar, Mauritius na Swaziland.

Michuano ya kombe la Cosafa inatarajiwa kuanza kutimua vumbi katikati ya mwezi Mei mwaka huu nchini Afrika Kusini.


Katika kila kundi, timu zote zitacheza michezo mitatu na mshindi wa kila kundi ataingia katika hatua inayofuata ya robo fainali itakayozijumuisha nchi za  Afrika Kusini, Botswana, Ghana, Malawi, Msumbuji na Zambia ambazo zimeingia katika hatua ya pili kutokana na nafasi zao kwenye msimamo wa viwango vya FIFA.

SIMON SSERUNKUMA AREJEA KWAO UGANDA


Kiungo Simon Sserunkuma amerejea kwao Uganda kutokana na mafanikio ya kifamilia.


Taarifa kutoka ndani ya Simba zimeeleza Sserunkuma amerudi Uganda kwa ajili ya shughuli ya arobaini ya mmoja wa wazazi wake.

Sserunkuma ameondoka wakati Simba ikijianda akupambana na Prisons, keshokutwa.

Kocha wa Simba, Goran Kopunovic ameonekana kutomuamini sana Simon na mara nyingi amekuwa akimuingiza katika kipindi cha pili.

WAKENYA KUISHANGILIA YANGA BOTSWANA


Mashabiki wa soka wakiwemo Watanzania na raia wa Kenya na Uganda wameungana kuishangilia Yanga ambayo iko jijini hapa kuivaa BDF XI ya Botswana.


Yanga inaovaa BDF XI katika mechi ya Kombe la Shirikisho itakayopigwa leo saa 1:30 kwa saa za hapa na saa 2:30 kwa saa za Afrika Mashariki.

Katika mitaa mbalimbali ya jiji hili, mashabiki wa nchi hizo tatu wameungana na kuishangilia Yanga wakionyesha kudumisha umoja wa Afrika Mashariki.

Ingawa si wengi, jana mchana mashabiki hao wamekiwemo wanafunzi walikuwa wakipanga namna ya kufanya ili kupata usafiri wa uhakika utakaowapeleka Lobatse kwenda kuishangilia Yanga.

Mkuu wa kitengo cha habari cha Yanga, Jerry Muro amesema mashabiki hao, hasa wale wa Tanzania wameonyesha ushirikiano wa hali ya juu.

Botswana ni kati ya nchi Kusini mwa bara la Afrika ambayo Watanzania wengi wanaishi wakiwa wanafanya biashara zao na wengine wakiwa wanafunzi katika vyuo mbalimbali vya jiji hili na katika mikoa mingine.


Yanga ilishinda kwa mabao 2-0 katika mechi yake ya kwanza jijini Dar es Salaam na BDF imepania kushinda na kusonga mbele katika mechi ya leo.

ALICHOSEMA KOCHA YANGA KUELEKEA MECHI YA KESHO BOTSWANA


pluijm
Na Bertha Lumala
Kocha mkuu wa Yanga SC, Hans van der Pluijm amewataka wachezaji wake kuhakikisha wanatikisa nyavu za wapinzani wao BDF XI FC katika mechi yao ya kesho ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Yanga SC, mabingwa mara 24 wa Tanzania Bara, watakuwa na kibarua kigumu mbele ya wenyeji wao hao watakapopamba katika mechi hiyo ya marudiano ya hatua ya awali ya michuano itakayochezwa kuanzia saa 2:00 usiku Uwanja wa SSKB Lobatse uliopo Km 70 kutoka Gaborone, mji mkuu wa Botswana. Uwanja huo upo kwenye kambi ya Jeshi la Ulinzi (BDF) eneo la Lobatse, Botswana.
Katika mahoajino na mtandao huu akiwa Botswana leo mchana, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Jerry Muro amesema benchi lao la ufundi linaloongozwa na Pluijm limewataka wachezaji kuhakikisha wanapata japo goli moja la ugenini huku wakilinda mabao yao mawili waliyofunga nyumbani.
“Tulishinda 2-0 nyumbani, lakini kocha (Pluijm) amewataka wachezaji kutobweteka na ushindi huo. Amesema ni lazima tusakae japo goli moja la ugenini ili tuwe salama zaidi huku tukihakikisha wenyeji wetu hawapati mabao,” amesema Muro.
Pluijm amesema ushindi wa timu hiyo kwenye mechi za Ligi Kuu ni chachu kuelekea mchezo huo wa marudiano dhidi ya BDF
Aidha, mitandao ya michezo ya Botswana imemnukuu Pluijm akitamba kupata ushindi mwingine wakati timu hizo zitakaporudiana kesho.
Pluijm amekaririwa akieleza kuwa, licha ya kucheza ugenini, bado ana uhakika watawafunga wenyeji wao BDF XI FC katika mchezo huo.
“Tumekuja Botswana kucheza kwa kushambulia kama tulivyofanya nyumbani tuliposhinda mabao 2-0, ninajua mchezo utakuwa mgumu kwa sababu wanacheza kwao na watataka kutushambulia, lakini sisi tutacheza kwa malengo huku tukihitaji bao moja ili kuwapa presha wenyeji,” amesema Pluijm.
Pluijm amesema ushindi wa timu hiyo katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara ni chachu kuelekea mchezo huo wa marudiano dhidi ya BDF na kuwataka mashabiki kuiunga mkono timu yao kuelekea mechi hiyo.
Hata hivyo, mashabiki wa Yanga SC waliokuwa wasafiri kwa basi kubwa la klabu hiyo Jumatano alfariji, walikwama kutokana na kile kilichoripotiwa leo kuwa basi hilo halina bima wala kibali cha barabarani.
Yanga SC ambayo kwa muda mrefu imekuwa haifiki mbali katika michuano ya kimataifa ikitolewa kwa matuta dhidin ya Al Ahly ya Misri katika hatua ya pili mwaka jana, inahitaji sare ya aina yoyote au kipigo kisichozidi bao 1-0 kusonga mbele.
Endapo timu hiyo ya Jangwani ikifanikiwa kuwang’oa maafande hao, itakutana na mshindi kati ya Sofapaka FC ya Kenya na Platnum FC katika hatua inayofuata. Wazimbawe walishinda 2-1 dhidi ya Sofapaka katika mechi ya kwanza iliyochezwa jijini Nairobi wiki mbili zilizopita.

BAADA YA KIPIGO, OZIL AISUSA JEZI YAKE KWA MCHEZAJI WA MONACO

WAKATI KIUNGO BERNADO WA AS MONACO ALIMFUATA MESUT OZIL WA ARSENAL WABADILISHANE JEZI BAADA YA MECHI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA KWENYE UWANJA WA EMIRATES, LONDON. ALIJIKUTA AKISUSIWA JEZI HIYO NA OZIL WALA HAKUTANA KUCHUKUA YA BENADO, HALFU HUYOOO AKAONDOKA ZAKE. ARSENAL ILILALA KWA MABAO 3-1.

ATLETICO MADRID YALALA BAO 1-0 DHIDI YA WAJERUMANI

.
FERNANDO TORRES (KULIA) AKIKIMBIA KUMLALAMIKIA MWAMUZI BAADA YA KIKOSI CHAKE KUFUNGA BAO LILILOKATALIWA. ATLTETICO MADRID IKIWA UGENINI IMELALA KWA BAO 1-0 DHIDI YA WENYEJI WAKE BAYER LEVERKUSEN.




ZIPO HAPA KURASA ZA MWANZO NA ZA MWISHO ZA MAGAZETI YA MICHEZO LEO FEB 26

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.