Mashabiki wa soka wakiwemo Watanzania na raia wa Kenya na
Uganda wameungana kuishangilia Yanga ambayo iko jijini hapa
kuivaa BDF XI ya Botswana.
Yanga inaovaa BDF XI katika mechi ya Kombe
la Shirikisho itakayopigwa leo saa 1:30 kwa saa za hapa na saa 2:30 kwa saa za
Afrika Mashariki.
Katika mitaa mbalimbali ya jiji hili,
mashabiki wa nchi hizo tatu wameungana na kuishangilia Yanga wakionyesha
kudumisha umoja wa Afrika Mashariki.
Ingawa si wengi, jana mchana mashabiki hao
wamekiwemo wanafunzi walikuwa wakipanga namna ya kufanya ili kupata usafiri wa
uhakika utakaowapeleka Lobatse kwenda kuishangilia Yanga.
Mkuu
wa kitengo cha habari cha Yanga, Jerry Muro amesema mashabiki hao, hasa
wale wa Tanzania wameonyesha ushirikiano wa hali ya juu.
Botswana ni kati ya nchi Kusini mwa bara la
Afrika ambayo Watanzania wengi wanaishi wakiwa wanafanya biashara zao na
wengine wakiwa wanafunzi katika vyuo mbalimbali vya jiji hili na katika mikoa
mingine.
Yanga ilishinda kwa mabao 2-0 katika mechi yake ya kwanza jijini Dar es Salaam na BDF imepania kushinda na kusonga mbele katika mechi ya leo.
0 maoni:
Post a Comment