SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Feb 4, 2015

SANTIAGO BERNABEU; GOOAAAL

Mambo mazuri kwa upande wa Real Madrid sasa ni mapumziko Madrid wanaongoza goli 2-0 dhidi ya Sevila magoli ya James Rodriguez Dakika 13, na goli la Jese Dakika ya 36.

AFCON; GOOAAALLLL

Dakika ya 68 Ivory Coast wanapata goli la 3-1 dhidi ya Congo DR

HAYA HAPA NI MATOKEO KUTOKA SANTIAGO BERNABEU REAL MADRID VS SEVILA

Live: Real Madrid 1-0 SevillaJames Rodrigues ameipatia goli la kuongoza Real Madrid 1- 0 dhidi ya Sevila sasa ni dakika ya 31.

AFCON MAPUMZIKO MATOKEO YAPO HAPA

Democratic Republic of Congo - Cote d'Ivoire Preview: Renard wary of favourites tag
 Wachezaji wa Ivory coast wakishangilia moja ya goli lao usiku huu Ivory coast wanaongoza 2-1 dhidi ya congo dr na sasa ni mapumziko.

WEST HAM WAPIGWA FAINI NA FIFA

KLABU ya West Ham imepigwa faini ya Pauni 71,000 na FIFA baada ya kumtumia Diafra Sakho katika mechi ya Kombe la FA siku 18 tangu ajitoe kikosi cha Senegal kilichocheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.
Sakho alifunga bao pekee katika ushindi wa 1-0 Uwanja wa Ashton Gate dhidi ya Bristol City na bodi hiyo ya soka duniani ikaanza kufanya uchunguzi kama walivunja sheria za majukumu ya kimataifa ya mchezaji.
 
The Hammers walikanusha kufanya jambo lolote baya, wakisema mchezaji huyo alikuwa ana maumivu ya mgongo wakati anaitwa Senegal na akashindwa kujiunga na kikosi, lakini haikuwasaidia kuepuka rungu la FIFA.
West Ham say Sakho was suffering with a back injury and was unable to fly to the Africa Cup of Nations
West Ham imeadhibiwa kwa kumchezesha Sakho aliyegoma kujiunga na timu yake ya taifa

Senegal ilikasirishwa na kitendo cha Sakho kuichezea West Ham saa 48 baada ya kutolewa kwao kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika.

PICHA JUAN CUADRADO ALIVYO ANZA MAZOEZI LEO

Juan Cuadrado (left) has taken part in his first training session since joining Chelsea on Monday




,
Chelsea manager Jose Mourinho (right) talks through tactics with his new arrival Cuadrado (left)

 Cuadrado (right) could make his Chelsea debut when they take on Aston Villa at Villa Park on SaturdayCuadrado (left) plays a pass as his new team-mate Nathan Ake (right) attempts to close him down

YANGA YAKAA KILELENI

Na Mahmoud Zubeiry, TANGA
YANGA SC imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Shujaa wa pointi tatu za Yanga SC leo ni Nahodha Nadir Haroub Ali ‘Cannavaro’, aliyefunga bao hilo pekee mapema tu kipindi cha kwanza, baada ya kupanda kwenda kusaidia mashambulizi. 
 
Yanga SC sasa inatimiza pointi 22 baada ya kucheza mechi 12, moja zaidi ya mabingwa watetezi, Azam FC walioteremkea nafasi ya pili kwa pointi zao 21.
Ilikuwa ni dakika ya 12 ya mchezo, wakati Cannavaro alipomalizia kwa kichwa mpira uliounganishwa kwa kichwa pia na mshambuliaji Mliberia Kpah Sherman kufuatia mpira wa kurushwa wa beki Mbuyu Twite.
Nadir Haroub 'Cannavaro ' akishangilia baada ya kuifungia bao pekee Yanga SC Mkwakwani leo. Kushoto ni kipa Shaaban Kado akiwa ameduwaa

Timu hizo zilishambuliana kwa zamu na hakukuwa na burudani, zaidi ya ‘butua butua’, kushindana nguvu na kasi, kutokana na timu zote kuhofia kucheza ‘kandanda ya kitabuni’ kwa sababu ya hali mbaya ya Uwanja wa Mkwakwani.
Kipindi cha pili, Yanga SC walianza kucheza kwa kujihami kulinda bao lao, huku wakifanya mashambulizi machache ya kushitukiza.
Coastal Union ilikaribia kusawazisha bao dakika ya 82 baada ya Godfrey Wambura kumpa pasi nzuri, Hussein Sued, ambaye licha ya mabeki wa Yanga kumuacha wakidhani ameotea, lakini akapiga nje akiwa ndani ya sita.
Winga wa Yanga SC, Simon Msuva akitafuta maarifa ya kumtoka beki wa Coastal, Sabri Rashid
Kipa wa Coastal, Shaaban Kado akiokoa moja ya hatari langoni mwake leo
Mshambuliaji wa Yanga SC, Kpah Sherman (kushoto) akipambana na beki wa Coastal, Abdallah Mfuko kulia

Kwa ujumla mchezo ulikuwa wa ‘kindava ndava’ na hakukuwa na burudani yoyote- na sifa ziwaendee marefa wa mchezo wa leo kwa kuumudu vyema.
Kipindi cha kwanza mashabiki wa Coastal waliwavurumushia mvua ya mawe mashabiki wa Yanga, hadi Polisi wakaenda kuwasaidia.
Kikosi cha Coastal Union kilikuwa; Shaaban Kado, Mbwana Hamisi, Sabri Rashid, Abdallah Mfuko, Juma Lui, Abdulhalim Humud, Joseph Mahundi/Said Mtindi dk60, Godfrey Wambura, Hussein Sued, Rama Salim na Itubu Imbem. 
Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Rajab Zahir, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Salum Telela, Simon Msuva, Said Juma ‘Kizota’, Kpah Sherman, Amisi Tambwe/Danny Mrwanda dk83 na Andrey Coutinho/Hussein Javu dk65.

YANGA YA NG'AA TANGA

Mpira umeisha uwanja wa mkwakwani Tanga, timu ya Yanga imeibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi Coastal Union shukrani kwa Nadir Haroub "Canavaro" ndiye aliye funga katika mchezo huo.

LULU AAMUA KURUDI SHULE

Hapa Na Pale: Lulu Awa Mtamu Chuoni!!!
Mrembo na mwigizaji wa filamu,  ambae kwa sasa ameamua kupiga kitabu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ,  ambae kwa sasa ameamua kupiga kitabu , anadaiwa kuwafunika kimasomo wanafunzi wenzake katika Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kilichopo Magogoni-Posta jijini Dar.
Akizungumza hivi karibuni chuoni hapo, mmoja wa wanafunzi wanaosoma na mwigizaji huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema Lulu amekuwa akihudhuria vizuri darasani na kufanya vyema kwenye masomo yake mbalimbali zaidi ya wanafunzi wengi anaosoma nao.

“Lulu yupo vizuri sana kimasomo, anawapita hadi wanafunzi wengine. Mahudhurio yake ni mazuri na anafanya mitihani yake na kufaulu.
“Anavaa nguo zinazostahili na hapa chuoni kila mwanafunzi anampenda kwa sababu yupo ‘peace’ ile mbaya,” alisema mnyetishaji huyo na kusisitiza kuwa msanii huyo haishi kama supastaa.
Kwa kifupi unaweza sema Lulu amekuwa mtamu kama Mcharo!!

ALICHOSEMA WAKALA WA DE GEA

 
 Hatimaye wakala wa David De Gea - Super Agent Jorge Mendes amesema mchezaji huyo atabakia Manchester United pamoja na Madrid kuonyesha nia ya kumtaka. Amesema De Gea amebakiza mkataba wa mwaka mmoja, na ana furaha kuongeza mkataba mpya na kuendelea kuwepo Old Trafford.

ALICHOSEMA FEROUZ KUHUSU MGAHAWA WAKE AMBAO UNAFUNGULIWA LEO

 
Baada ya msanii ferooz kuzungumzia ishu yake ya kufungua mgahawa wake wa Hollywood Café msanii huyo amesema kuwa leo ndio siku ambayo amefungua mgahawa huo ambao utakuwa unatoa huduma mbali mbali  za chakula ambao uko maeneo ya Darfree Market na kuwataka mashabiki wake wote wakaribie kumpa support.

KUTOKA MKWAKWANI TANGA GOOOAAALLLLLL

Yanga 1 - 0 Coastal union

SSERENKUMA AWEKA REKODI VPL


Baada ya kufanikiwa kuipa ushindi wa mabao 2-1 klabu yake ya Simba mbele ya JKT Ruvu Jumamosi iliyopita, mshambuliaji wa klabu hiyo, Mganda, Danny Sserunkuma, ameweka rekodi ndani ya klabu hiyo ya kuwa mchezaji pekee aliyepachika bao la mapema zaidi katika mechi za ligi kuu msimu huu.

Sserunkuma ambaye alisajiliwa na Simba katika usajili wa dirisha dogo msimu huu, ameshaichezea klabu hiyo mechi nne na kufanikiwa kupachika mabao matatu, alifunga moja dhidi ya Ndanda na mawili Jumamosi iliyopita kwenye mchezo dhidi ya JKT Ruvu.
Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, Simba walionekana wazi kuupania ili kuibuka na ushindi, kwani walianza kuwashambulia wapinzani wao kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la kwanza katika dakika ya pili kupitia kwa mshambuliaji huyo Mganda.
Licha ya kupachika bao hilo Sserunkuma akafunga bao lingine katika dakika ya 49 ikiwa pia ni bao la mapema kufungwa katika kipindi cha pili kwa timu yao.

TWITE AOMBA MKATABA YANGA


Beki wa Yanga, Mbuyu Twite, raia wa Congo, ameomba kufungwa kitanzi mapema na timu yake hiyo kwa kusema kuwa yupo tayari kuongeza mkataba iwapo uongozi wa timu hiyo utafanya hivyo.


Twite aliyesajiliwa Yanga msimu mmoja uliopita, anatarajia kumaliza mkataba wake na timu hiyo mwishoni mwa msimu huu mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Twite alifunguka kuwa yupo tayari kuongeza mkataba Yanga iwapo watamhitaji na kudai kuwa kuna timu ambazo zinamfuatilia kwa sasa lakini hawezi kuziweka wazi.

“Mkataba wangu na Yanga unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu mara baada ya kumalizika kwa ligi, hivyo nipo tayari kuongeza mkataba mwingine iwapo viongozi watahitaji.

“Yanga ni timu ninayoipenda sana hapa Tanzania lakini siwezi kusema ni timu gani ambazo zinanifuatilia kwa sasa, hiyo ni siri yangu hata kama zipo,” alisema Twite ambaye amekuwa na uwezo mkubwa wa kurusha mipira.

YANGA YAMGEUKA MRISHO NGASSA

 
Uongozi wa Klabu ya Yanga umefunguka kuwa hauhusiki na deni la mshambuliaji wao, Mrisho Ngassa anayedaiwa fedha na Benki ya CRDB kwa kuwa yeye aliomba udhamini katika timu hiyo na si kulipiwa kama anavyodai.

Hivi karibuni, Ngassa alinukuliwa akidai kushindwa kuwa katika kiwango kizuri cha kuitumikia timu yake hiyo kufuatia deni la shilingi milioni 45 alizokopa CRDB kwa ajili ya kuilipa Simba ili ajiunge na Yanga, baada ya kusaini timu mbili kwa madai kuwa uongozi wa timu hiyo ungemsaidia laki tano kila mwezi.

Msemaji wa Yanga, Jerry Muro, alifunguka kuwa Yanga haikuwa na mkataba wa makubaliano na Ngassa wa kumsaidia kumlipia kwa kuwa klabu hiyo ilikubali kumdhamini katika Benki ya CRDB kama mwajiriwa wake tu.

“Ieleweke kuwa Yanga ilimdhamini Ngassa wakati alipokwenda kukopa fedha CRDB kwa ajili ya kulipia deni lake na tulifanya hivyo kama waajiri wake, lakini hakukuwa na makubaliano ya kuweza kumsaidia katika kulipa deni hilo.

“Siku zote taratibu za kukopa zinakuwa kati ya benki na mkopaji na wala hatuhusiki na sisi tulimdhamini tu katika kukamilisha ukopaji wake kwani deni alilokopa ni yeye na CRDB na si Yanga, naomba watu waelewe hivyo,” alisema Muro.

ALICHO JIBU ELIAS MAGULI BAADA YA KUPIGIWA SIMU NA NYOSSO

 
Stori: CHAMPIONI
Beki mkongwe wa Mbeya City, Juma Said Nyosso, amekubali kuwa kitendo alichomfanyia mshambuliaji wa Simba, Elias Maguri na kuonyesha na gazeti la Championi si sahihi, si cha kiungwana na anajuta kupita kiasi.


Kutokana na maumivu ya moyo anayoyapata kutokana na kushiriki katika kitendo hicho, Nyosso amefanya mambo mawili, kwanza ni kumpigia simu Maguri na pili kupiga katika ofisi za gazeti hili.

Nyosso amesema alianza kupiga simu kwa Maguri na kumuomba radhi akimueleza namna anavyojisikia vibaya kutokana na kitendo hicho alichoona si sahihi.
Gazeti la Championi linaloongoza kwa michezo nchini, lilichapisha picha zile zilizoonyesha Nyosso akimtendea vitendo hivyo visivyo vya kiungwana wakati Simba
Akizungumza na Championi Jumatano, Nyosso ambaye ni beki wa zamani wa Simba, alisema kuwa kwa sasa hana tena amani kutokana na kitendo hicho alichomfanyia Maguri na amekuwa akitumia muda mwingi kujikosoa mwenye bila  kupata ufumbuzi wa tatizo hilo.

 “Pamoja na hali hiyo nawaomba viongozi wangu wa Mbeya City na wadau wa soka hapa nchini na duniani kote wanisamehe juu hilo, hakika halikuwa kusudio langu kumdhalilisha Maguri.

“Nikiwa kama binadamu wengine kusema kweli najisikia vibaya na ndiyo maana nimechukua uamuzi huu ambao binafsi nauona kuwa ni wa busara kwa kumtafuta Maguri ili kumuomba radhi kwa kitendo hicho nilichomfanyia.

“Nimetafuta namba yake, halafu nimejitahidi kumpigia simu yake ya mkononi na kuzungumza naye kwa takribani dakika mbili hivi. Lakini hakuonyesha dalili zozote za kunielewa nilichokuwa nikimwambia.

 “Kutokana na hali hiyo imebidi nitumiea njia hii ya kuzungumza na Championi ili kumwomba msamaha yeye pamoja na viongozi klabu yake ya Simba na klabu yangu Mbeya City, wanisamehe kwa kitendo kile.

“Kusema kweli nimejifunza na sitorudia tena kufanya kitendo kama hicho kwa mchezaji yoyote yule kwani hivi sasa najutia na ninajiona mkosefu mbele ya jamii. Nimefanya kosa hivyo nahitaji kusamehewa,” alisema Nyosso.
Gazeti hili lilifanya kazi ya kumtafuta Maguri ili kujua kama kweli aliwasiliana na Nyosso na alikubali ombi la kumsamehe.

 “Sijaongea naye na wala sihitaji kuzungumza naye kwa sababu kitendo alichonifanyia kimenidhalilisha mbele ya ndugu zangu, rafiki zangu pamoja na jamii yangu kwa ujumla.

“Kuna mtu alipingia simu sijui kama alikuwa ni yeye akitaka nimsamehe, lakini nilimkatalia kwani wakati alikuwa akifanya hivyo hakujua kama alikuwa ananidhalilisha?” alihoji Maguri.

“Kama kuna hatua za kuchukuliwa basi atachukuliwa ili liwe fundisho kwa wachezaji wengine wenye tabia kama za kwake ila kusema kweli kwa sasa siwezi kufanya hivyo,” alisema Maguri ambaye amejiunga na Simba msimu huu akitokea Ruvu Shooting.

Nyosso amekuwa mmoja wa wachezaji wa kwanza kuomba radhi baada ya kugundua kosa lake. Lakini Maguri ameshikilia msimamo kutokana na kuumizwa na jambo hilo.

ETO'O AANZA MATATIZO NA KOCHA SAMPODORIA

Etoo 2Ikiwa imepita wiki moja tu tangu asajiliwe na klabu ya Italia ya Sampdoria, mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Cameroon Samuel Eto’o ameripotiwa kuwa kwenye utata wa kutaka kuihama klabu hiyo baada ya kutoelewana na kocha wake.

Kilichotokea ni kwamba Eto’o aliingia kwenye matatizo na kocha Sinisa Mihaijlovic baada ya kocha huyo kumtaka afanye mazoezi ya ziada baada ya mchezo ambao Sampdoria ilifungwa 5-1 na timu ya Torino katika muendelezo wa
ligi ya Italia maarufu kama Serie A.

Kwenye hiyo mechi Eto’o aliichezea klabu yake mpya kwa mara ya kwanza baada ya kuingia akitokea benchi kwenye dakika ya 71 japo uwepo wake haukuweza kuiokoa timu yake na kipigo ilichokipata toka kwa Torino .

Eto’o na kocha wake walifanya kikao cha dharura kuzungumzia kilichotokea baada ya mshambuliaji huyo kuamua kuondoka na kwenda Milan ambako familia yake ipo.
Inasemekana kuwa uhusiano kati ya Eto’o na kocha wake umefikia hatua mbaya kiasi cha klabu hiyo kuwa na wazo la kuvunja mkataba wake wamiaka miwili baada ya kusaini ndani ya wiki moja tu akitokea Everton.
Viongozi wa klabu hiyo ya Sampdoria wamekataa kuzungumzia tukio hilo wakisisitiza kuwa eto’o alikosa mazoezi kwa sababu zake binafasi lakini kocha anasema ‘Club ndio itajua nini cha kufanya ila kwangu mimi mchezaji anapofanya kitu kama hiki ni amenikosea heshima na kunidharau mimi na wafanyakazi wengine, aliondoka mazoezini bila kuniaga au kuomba ruhusa na hakurudi, sijamuona kuanzia asubuhi na sijaongea nae

ALICHO SEMA FID Q KUHUSU HUKUMU YA FRANCIS CHEKA

February 2 2015 bondia Mtanzania Francis Cheka alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani pamoja na faini aliyoitaja kuwa milioni moja na laki sita baada ya kupatikana na kosa la kumpiga meneja aliekua amemuajiri kwenye Bar yake Morogoro.

Ni hukumu ambayo kila mmoja ameipokea kwa muonekano wake ambapo japo Rapper Fid Q hakumtaja mtu kwenye tweet hiyo, imeonekana kama inahusu kilichomtokea Francis Cheka ambacho kimejadiliwa na watu mbalimbali kwenye twitter wiki hii.
Fid aliandika Una muajiri mtu kwa nia nzuri, yeye anakuibia na ukimuhoji anakupa majibu ya dharau wakati anajua wewe ni mbabe, na ukimdunda unaswekwa je

IZO BUSINESS; SIONI UMUHIMU WA KUJIHUSISHA NA SIASA


IZZ

MSANII wa muziki wa Hip Hop, Emmanuel Simwinga ‘Izo Business’, amesema licha ya kushauriwa na rafiki zake kuingia kwenye siasa, bado hajaona umuhimu wa kufanya hivyo.Akizungumza na MTANZANIA jana, Izo Business alisema hakuna umuhimu wa kuingia kwenye siasa, kwani inatakiwa mtu ajitoe kwa ajili ya watu na siyo kuingia ili ujipatie fedha kama yalivyo mawazo ya wasanii wengi.“Siasa kwa upande wangu sijaipa kipaumbele, ingawa nimeshawishiwa na marafiki zangu nigombee nafasi mbalimbali,” alisema Izo Business.
  Alisema wale waliojihusisha na siasa wasisahau kuwatumikia wananchi waliowapa nafasi hizo, kwani wengi wamekuwa wakijisahau na kuishia kufuja fedha za Serikali.

AGGREY MORRIS, NYOSSO WANASHUGHULIKIWA TFF MUDA HUU


_DSC0567
Aggrey Morris (Kushoto)
Na Bertha Lumala
Utovu wa nidhamu wa wachezaji George Michael, Aggrey Morris na Juma Nyosso huenda ukawaponza kwa kupewa adhabu kali na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Kwa nini?
Muda mfupi uliopita mtandao huu umepata taarifa kwamba Kamati ya Nidhamu ya TFF, inaendelea na kikao cha dharura jijini Dar es Salaam kupitia malalamiko yaliyowasilishwa na klabu mbalimbali za Ligi Kuu ya Tanzania Bara na Ligi Daraja la Kwanza.
Januari 17 mfungaji bora wa VPL msimu uliopita, Mrundi Amisi Tambwe alikabwa koo na beki George Michael wa Ruvu Shooting wakati wa mechi yao ya raundi ya 11 ya ligi hiyo msimu huu waliyotoka suluhu.
Beki wa kati Aggrey Morris wa Azam FC, alimpiga kiwiko kiungo mshambuliaji wa Simba kutoka Uganda, Emmanuel Okwi wakati wa mechi yao ya raundi ya 12 ya VPL msimu huu iliyomalizika kwa sare ya bao moja kwenye Uwanja wa Taifa Januari 24. Baada ya kupigwa, Okwi alipoteza fahamu na kulazimika kukimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Nyosso2
Siku nne baada ya tukio la Okwi, beki na aliyekuwa nahodha wa Mbeya City FC katika mechi ya kiporo ya raundi ya 10 ya ligi hiyo msimu huu dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Juma Nyosso alifanya kitendo cha udhalilishaji kwa kumpapasa makalio mshambuliaji Elias Maguli wa Simba.
Matukio yote matatu ambayo yanamtoa mchezaji moja kwa moja uwanjani kwa kuoneshwa kadi nyekundu kwa mujibu wa Sheria Namba 12 ya Soka (Makosa na Tabia Mbaya), hayakuonwa na marefa wa mechi husika.
Hata hivyo, viongozi wa Simba SC na Yanga SC wameshawasilisha malalamiko TFF kuhusu matukio hayo ambayo muda wowote kuanzia kesho adhabu zake zitaanikwa na TFF.
 
Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Boniface Wambura amethibitisha kufanyika kikao cha Kamati ya Nidhamu leo lakini hakutaka kueleza kwa kina yanayojadiliwa katika kikao hicho.
Timu ya Friends Rangers ya Dar es Salaam inayoshiriki FDL msimu huu ikiwa Kundi A, huenda ikakumbwa na adhabu kubwa zaidi kwa kugomea mechi na baadhi ya wachezaji kumtwanga kwa mateke na ngumi refa wa kati wa mechi yake iliyopita dhidi ya Majimaji FC mjini Songea.
Majimaji FC walifunga bao la pili kwa mkono, goli ambalo liliwakwaza zaidi wachezaji wa Friends ambayo imekata rufaa Majimaji FC kupewa pointi tatu za mezani na mabao matatu na TFF ilhali mechi ilichezwa uwanja ukiwa umejaa maji.

VIDEO YA ALI KIBA YAPOKELEWA NA KITUO KIKUBWA CHA TV

.
.
Video ya hit song ‘Mwana‘ ya Ali Kiba Feb 3 2015 imepitishwa na kuoneshwa kwenye kituo kikubwa cha TV cha Trace TV kilichopo Ufaransa ambacho Wasanii wengi wakubwa wa Afrika wamekua wakionyesha furaha yao pindi video zao zinapogongwa kwenye TV hii ambayo imebarikiwa kuwa na nguvu ya kipekee kwenye muziki wa kizazi hiki.

Video ya Mwana ni video nyingine ya Tanzania kwa mwaka 2015 kufanikiwa kuchezwa kama video mpya kwenye kituo hicho baada ya ‘Nitampata wapi‘ ya Diamond Platnumz kuingia kwenye chati yao ya Top 10 hivi karibuni.
Ali KVideo hiyo ya Mwana imeongozwa na director God Father kutoka Afrika Kusini.

MAN UNITED WAPETA FA CUP

KLABU ya Manchester United imetinga Raundi ya Tano ya Kombe la FA baada ya ushindi wa mabao 3-0 Cambridge United Uwanja wa Old Trafford.
Timu ya kocha Mholanzi Louis Van Gaal iliyolazimishwa sare katika mchezo wa kwanza na wapinzani wao hao ugenini, jana ilikuwa tofauti katika mchezo wa pili wa Raundi ya Nne.
 
Juan Mata alianza kuwafungia bao la kwanza Mashetani Wekundu dakika ya 25, kabla ya Marcos Rojo kufunga la pili dakika ya 32 na James Wilson kumalizia la tatu dakika ya 73.
Sasa, Man United itasafiri kuwafuata Preston North End katika Raundi ya Tano Jumatatu ya Februari 16, mwaka huu.
 
Kikosi cha Man Utd jana kilikuwa: De Gea, McNair, Smalling, Evans, Rojo/Young dk81, Blind, Rooney, Di Maria/Herrera dk71, Mata, Van Persie/Wilson dk66 na Fellaini.
Cambridge Utd: Dunn, Tait, Nelson/Miller dk87, Coulson, Greg Taylor, Donaldson, McGeehan, Champion, Chadwick/Morrissey dk51, Elliott na Simpson/KaiKai dk61. 

Juan Mata and Marcos Rojo both scored in the first half as Manchester United sealed their place in the fifth round of the FA CupJuan Mata akipongezana na Marcos Rojo baada ya wote kufunga katika ushindi wa 3-0 wa Manchester United Kombe la FA jana.

MAGAZETI YA MICHEZO LEO FEBRUARY 4


.



.


..
..
..
..
.
.

SALA KWA MESSI, ISIHAKA WAKACHEZE REAL MADRID

 
Endapo watafanikiwa kucheza timu ya vijana ya klabu tajiri duniani, Real Madrid ya Uhispania, basi itakuwa ni habari njema kwa soka la Tanzania, ambayo wachezaji wake kadhaa wamekuwa wakifeli majaribio ya kucheza soka la kulipwa ughaibuni, hasa nchi za Ulaya katika miaka ya nyuma.
Kufuatia tetesi za kutakiwa kwenda kufanya majaribio Real Madrid, mashabiki wa soka wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam wamewaombea wachezaji wao kila la kheri katika majaribio yao ili waweze kusakata kabumbu Ulaya.

Haruna Hamisi, mmoja wa mashabiki na mwanachama wa Simba amesema beki wa kati wa klabu hiyo, Hassan Isihaka na straika Ramadhan Singano anayejulikana kama "Messi" kwa jina la uwanjani wana uwezo wa kucheza soka la kulipwa.

‘Vipaji tunavyo, ila vinakosa nafasi na kuharibiwa na mfumo wetu mbaya wa kutolea wachezaji wakiwa bado wadogo”, alisema Hamisi.
Emmanuel Temaeli, shabiki mwingine amesema endapo watafanikiwa, basi itakuwa faida si tu kwa Simba, bali taifa zima.

“Tukiwa na wachezaji wengi wanaocheza soka nje, tutakuwa na timu ya taifa imara kwa ajili ya michuano mbalimbali kama vile ya Mataifa ya Afrika na michuano ya kufuzu kucheza kombe la dunia”, alisema Temaeli.

Taarifa zinasema kuwa klabu ya Real Madrid ya Hispania, ambayo maofisa wake wamekuja nchini kuingia ubia na shirika la hifadhi ya jamii (NSSF) kujenga kijiji cha michezo kwa ajili ya kulea wachezaji vijana kitakachosimamiwa na klabu hiyo ya Cristiano Ronaldo, wameomba CD (video) ili wawafanyie tathmini kupitia mechi walizocheza hivi karibuni.

Mabosi hao wamevutiwa na wachezaji hao vijana baada ya kuwaona katika mechi ya ligi kuu wakati Simba ilipocheza na klabu tajiri ya Azam na kutoka sare ya 1-1 majuma mawili yaliyopita.
Wachezaji kadha wa Tanzania wamefanikiwa kufanya majaribio kucheza nje bila mafanikio akiwemo mshambuliaji machachari, Mrisho Ngasa (anayecheza Yanga hivi sasa) aliyekwenda kufanya majaribio klabu ya West Ham ya Uingereza mwaka 2009 ikiwa chini ya kocha Gianfranco Zola.

Hivi karibuni, CSKA ya Urusi imemchukua mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na mchezaji wa klabu tajiri barani Afrika ya TP Mazembe ya Congo (DRC), Mbwana Samatta kwa ajili ya majaribio na tetesi zinasema mabosi wa timu wamevutiwa naye licha ya kuendelea kumjaribu

NUSU FAINAL AFCON LEO

 
Michuano ya soka ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON, inaendelea Jumatano katika hatua ya nusu fainali kwa Ivory Coast kupambana na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Katika michezo yao ya robo fainali, Ivory Coast iliwasambaratisha Algeria, kwa mabao 3-1. Algeria ni timu nambari moja kwa viwango vya ubora vya Fifa barani Afrika. Nayo Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo iliwaadhibu majirani zao Congo kwa magoli 4-2.

Kiungo wa timu ya Ivory Coast Cheik Tiote huenda akacheza mechi ya leo baada ya kupona maumivu ya kifundo cha mguu, ambayo yalisababisha akose mechi mbili za mwisho za timu hiyo.
Kocha wa Ivory Coast, Herve Renard amesema: "Tiote ameanza mazoezi mepesi. Itakuwa vigumu kwake kuanza mchezo, lakini ameorodheshwa katika kikosi cha leo."

Naye kocha wa DR Congo Florent Ibenge amesema hatapenda kumfanyia majaribio ya kucheza mechi dhidi ya Ivory Coast, nahodha Youssouf Mulumbu, ambaye kocha wake amesema amepona kwa asilimia "70%".
Mlinzi wa DR Congo Gabriel Zakuani hayumo katika kikosi cha leo baada ya kuumia kifundo cha mguu walipocheza dhidi ya Congo.

Alhamisi ni mtifuano mwingine wa nusu fainali kati ya wenyeji Equatorial Guinea dhidi ya Ghana. Kutinga hatua ya nusu fainali Equatorial Guinea waliwang'oa Tunisia inayoshika nafasi ya pili kwa ubora barani Afrika kwa mabao 2-1, huku Ghana ikiichakaza Guinea magoli 3-0.