SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Feb 6, 2015

ANGALIA SIMBA WALIVYOPOKELEWA TANGA

2
SIMBA inaanza mazoezi leo jioni jijini Tanga kujiandaa na mechi ya keshokutwa dhidi ya Coastal Union itakayopigwa uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga.
Afisa habari wa klabu hiyo, Humphrey Nyasio amezungumza na mtandao huu na kueleza kuwa kikosi kipo salama na wapo tayari kwa mechi hiyo.
Nyasio amefurahishwa na jinsi mashabiki walivyowapokea kwa furaha jijini Tanga na wamejipanga kuwapa furaha zaidi kwa kushinda kipute hicho.
Hata hivyo, Afisa habari huyo ameongeza kuwa beki wa kati Joesph Owino amebaki Dar es salaam akiendelea kufanya mazoezi mepesi na kikosi cha Simba B.

KIONGOZI YANGA ALIA NA MAPRO LIGI KUU BARA

TIBODr. Tibohora (kushoto) akiwa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga,Jerry Muro
Na Richard Bakana, Dar es Salaam
KATIBU mkuu wa Mabingwa wa zamani wa ligi kuu ya Soka Tanzania bara, Dar es salaam Young Africans, Dr. Jonas Tibohora, amesema kuwa wachezaji wengi hasa wa kigeni (Professional Players) wameshindwa kutambua thamani yao wakiwa Uwanjani kitu ambacho kinasababisha kushindwa kuwatofautisha na  wazawa.
Akizungumza na Shaffih Dauda.com juu ya matokeo ya kutoridhisha kwa timu kubwa za VPL licha ya kuwa na uwekezaji wa hali ya juu kwenye ligi, Katibu huyo ambaye alichukua mikoba ya Beno Njovu, amesema kuwa inatakiwa iwepo tofauti kubwa kati ya mchezaji wa Kimataifa na mchezaji wa ndani, lakini kutokana na viwango visivyoridhisha kwa wachezaji wa kigeni imekuwa ngumu kutofautisha kati ya timu kubwa na ndogo zinapokutana kwenye mechi za ligi.
Dr. Tibohora amekili kuwa klabu kubwa za Tanzania bara, Simba, Yanga na Azam, zimewekeza sana kwa kununua wachezaji na makocha wa kigeni lakini bado hazioneshi tofauti na timu nyingine zinazotumia makocha na wachezaji wa ndani pekee wanapokuwa Uwanjani.
“Taaluma na maadili ya wachezaji wetu bado inakuwa sio nzuri, Ukiangalia wachezaji wa timu kubwa wanapocheza na timu ndogo unashindwa kutofautisha timu kubwa ni ipi na ndogo ni ipi” Amesema Dr. Tibohora .
Mrundi Amissi Tambwe (kulia) ni miongoni mwa wachezaji wa kigeni wa Yanga
Timu za Azam FC, Yanga SC, Simba SC ndio timu ambazo zinaongoza kwa kuwa na makocha wa kigeni na wachezaji kutoka nchi za nje lakini matokeo ya Uwanjani hasa zinapokutana na timu kama Ndanda, Stand United na Polisi Morogoro bado unashindwa kutofautisha Kiwango cha wachezaji wa vigogo hao pamoja na hizi timu Changa.
Licha ya kudai kuwa hata uongozi  wa klabu za Tanzania bara zinakosea katika njia za kutafuta na kusajili wachezaji wa kigeni lakini Katibu huyo ametupa zigo la lawama kwa wachezaji wa Kigeni akisema kuwa ni lazima waonyeshe tofauti na thamani yao kama Maprofesional kweli.
Kipre Tchetche ni miongoni wa wachezaji wa kigeni wa Azam fc
“Tatizo ni la wachezaji wetu, Bado hawajaelewa nini maana ya Professionalism, Unapokuwa umepewa kazi lazima ujue  namna gani uwe kama mchezaji wa kulipwa, Ni lazima kuwe na tofauti kati ya mchezaji anayelipwa Milioni tano na yule anayelipwa Laki tatu” Ameongezea Dr. Tibohora.
Kwa upande wake Meneja wa Klabu ya Azam FC, Jemedali Said, amesema kuwa kubweteka kwa wachezaji wa timu kubwa na kukamia kwa timu ndogo ndio kimekuwa sababu ya kufanya utofauti kati ya Simba, Yanga , Ndanda, Ruvu Shooting na Mgambo JKT usionekane pindi wanapokutana katika mchezo.
Jemedali amesema kuwa, Timu ndogo za  VPL zimekuwa na kanuni ya kuzikamia timu kubwa kitu kinachosababisha wachezaji wa timu kubwa washindwe kucheza katika viwango vyao.
Meneja huyo ambaye amewahi kuichezea Yanga amedai kuwa, wachezaji wa timu kubwa wamekuwa na dharau pindi wanapokutana na timu change wakijua muda wowote watapata bao kinyume na wapinzani wao ambao wanakuja kupambana mwanzo mwisho.
“Upinzani uliopo kwa timu hizi tatu kubwa, wachezaji wanaingia Uwanjani wakijua wao ni Nyota, wana viwango vikubwa kitu kinachopelekea washindwe kucheza katika kiwango cha juu, Kwa matokeo yake sasa ukikuta timu ndogo inajituma kwa kiwango kinachotakiwa ndio utaona wanafungwa au kutoa sare” Amesema Jemedali Said Meneja wa Azam FC, huku akiongezea kuwa hata Azam FC kufungwa na Ndanda FC katika ligi ilikuwa ni katika misingi hiyo ya wachezaji kudharau.

WENGER AMTETEA WILSHERE

article-2443651-18840C1700000578-589_636x433
Kocha wa klabu ya washika mitutu wa London Arsenal Arsene Wenger ameibuka na kumtetea kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo na timu ya Taifa ya Uingereza Jack Wilshere, kuwa kiungo huyo sio mvutaji wa sigara licha ya picha zake kusambaa katika mitandao ya kijamii akiwa ameshika sigara jijini London.
Wenger amesema mchezaji huyo inabidi aangalie maisha yake ya baadae katika mchezo wa soka kwani bado ni kijana mdogo mwenye uwezo mkubwa wa kusakata kabumbu la kimataifa, lakini matukio yake ya ajabu yanaweza kumfanya ashindwe kufanya vizuri siku za hapo baadae.
Ni mara ya tatu sasa mchezaji huyo kupigwa picha akiwa anavuta sigara katika maeneo mbalimbali ya starehe na picha zake kusambaa katika mitandao ya kijamii.
 Lakini wenger amekanusha madai kuwa katika klabu ya Arsenal kuna tatizo kubwa la wachezaji wake kuvuta sigara wakiongozwa na kiungo Wilshere.
 
“Hakuna utamaduni wa uvutaji sigara katika kikosi changu, niliongea na Jack kuhusu swala picha zake zinazoonyesha akivuta na kusema yeye sio mvutaji, lakini inabidi aangalie maisha yake,” alisema Wenger.

KESI YA JAJA KUSIKILIZWA ILALA

Uongozi wa Klabu ya Yanga kupitia kwa Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga, Frank Chacha umesema unaendelea kumsubiri mshambuliaji Geilson Santos Santana ‘Jaja’ raia wa Brazil aje nchini kuitikia wito wa kesi waliyomfungulia.

Yanga ilimfungulia kesi mchezaji huyo Mahakama ya Kazi Ilala ambapo imepangwa kusikilizwa Februari 16, ambapo Yanga inadai mchezaji huyo alikiuka vifungu vya sheria wakati alipovunja mkataba wake na timu hiyo.
Wakili Chacha amesema hawatafanya chochote kwa kuwa kisheria mtuhumiwa bado ana nafasi tatu za kuitwa.
“Kwa mujibu wa sheria, ikitokea Jaja hakutokea mahakamani wala kufanya lolote, basi kuna nafasi nyingine tatu za kumwita. Tumeshamtumia e_mail, EMS na kumtumia balozi wake kwa ajili ya kuhakikisha ujumbe wa wito unamfikia kwa wakati ili aweze kuja kusikiliza kesi yake,” alisema.
Yanga iliamua kumfungulia kesi hiyo Jaja aliyejiunga na klabu hiyo Julai 12, 2014 kwa mkataba wa miaka miwili na inamdai faini ya dola milioni mbili (Sh bilioni 3.2), fedha ya usajili dola 20,000 (Sh milioni 32) na dola 3,000 za mshahara wake kwa mwezi mara miezi 12 (jumla Sh milioni 57.6).

KIFARU ATAMBA KUWAFUNGA YANGA JUMAPILI

HIKI NDIYO KIKOSI CHA MTIBWA SUGAR KILICHOIFUNGA YANGA KWA MABAO 2-0. ATAKOSEKANA KESSY AMBAYE AMEJIUNGA NA SIMBA.

Msemaji wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru ametamba kwamba wanakuja jijini Dar es Salaam kuendeleza ubabe wao kwa Yanga.


Yanga inashuka dimbani Uwanja wa Taifa jijini Dar keshokutwa Jumapili kuwakaribisha Mtibwa Sugar ambao waliwatwanga kwa mabao 2-0 katika mechi ya mzunguko wa Ligi Kuu Bara.

Kifaru amesema wana nafasi kubwa ya kuwafunga Yanga katika mechi ya pili kama walivyofanya kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

“Tuliwafunga wakapoteana, tunakuja huko Dar es Salaam na tunatarajia kufika Dar es Salaam, kesho.

“Sisi tumejiandaa sana na hakuna ishu ya mbwembwe au vinginevyo, nakuhakikisha njoo uone tunavyowamaliza Yanga hiyo Jumapili,” alisema Kifaru.


Msemaji huyo ametamba kwamba baada ya kikosi chao kupunguza kasi, kinataka kuanza kuamsha moto katika mechi dhidi ya Yanga.
USIKOSE KUFUATILIA BLOG HII WWW.HAJIBALOU.BLOGSPOT.COM KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI

FA KUCHUNGUZA USAJILI WA CALUM CHAMBERS

 

Chama cha soka cha England - FA kimesema kinauchunguza uhamisho wa Calum Chambers kutoka Southampton kwenda Arsenal - wakitoa ishara kwamba kuna jambo liloenda kinyume na kanuni lakini wamegoma kusema wazi kwanini wanauchunguza uhamisho huo uliofanyika katika dirisha la usajili la kiangazi.

MANYIKA JUNIOR AFUNGUKA KUHUSU BINTI WA MBUNGE ANAYESABABISHA ASHUKE KIWANGO

NIMAA..
Kipa wa Simba, Peter Manyika Jr ameingia kwenye shutuma nzito zinazosababisha kushuka kwa kiwango chake ambapo inadaiwa kuwa uhusiano wa kimapenzi na mrembo mmoja anayejulikana kwa jina la Nima ndiyo sababu.

Manyika Jr amekuwa akionekana sehemu mbalimbali akiwa na mrembo huyo ambaye inadaiwa ni mtoto wa mbunge, pia picha zao hutawala kwenye ukurasa wa Instagram, lakini baada ya kugundua zimeshasambaa kwa watu mbalimbali, mrembo huyo alizifuta picha hizo.
 
PETER MANYIKA...
Inaelezwa kuwa hali hiyo ya kushuka kiwango imewakera viongozi wengi wa Simba pamoja na baba wa mchezaji huyo Manyika Peter ambaye alimuweka chini mwanaye na kumkanya.
Akizungumza kuhusiana na hilo, kipa huyo mwenye umri wa miaka 19, alisema: “Huyo dada ni rafiki yangu wa kawaida na wala sina uhusiano naye wa kimapenzi.  Tatizo letu Watanzania tukiona jambo basi tunalikuza kupita kiasi.”
Kuhusu picha wakiwa pamoja alisema: “Kweli tulipiga picha lakini hiyo siyo sababu ya kusema kuwa ni mpenzi wangu.”
Alipoulizwa kuhusu kukanywa na baba yake juu ya jambo hilo, alisema: “Kweli baba aliniuliza, nilimueleza ukweli kuwa hakuna kitu kama hicho.”
Alipotafutwa baba mzazi wa kipa huyo, Manyika Peter ambaye alikuwa na haya ya kusema: “Sitaki mwanangu apotee, nilipata taarifa hizo na nikamuita na kuzungumza naye kwa kina lakini aliniambia kuwa yule ni rafiki yake, hata hivyo nikiwa kama mzazi nilimkanya na kumpa mwongozo wa nini anatakiwa kukifanya kufika mbali kisoka.
 
MANYIKA SR (KULIA)...
“Kama alidanganya kuwa hayupo na mwanamke huyo, hilo silijui kwa sababu hivi sasa siko naye nyumbani, muda mwingi yupo na timu yake ya Simba lakini nitalifuatilia suala hilo.”
SALEHJEMBE ilimtafuta  Nima ambaye inaelezwa ndiye aliyekuwa mrembo katika wimbo wa Mbagala wa msanii Nasibu Abdul ‘Diamond’, naye alifunguka: “Manyika siyo mpenzi wangu ila ni rafiki yangu, mimi najua ana mtu wake lakini siyo mimi, hiyo video niliyokuwa nimeiweka Instagram tulipiga tukiwa tunatokea mazoezi ya Simba na hata siku hiyo mchumba wa Manyika alikuwa anajua kuwa nipo naye.”

NYOSSO, MORISS WAPEWA ADHABU NA TFF


http://api.ning.com/files/kPWAOYVbPQavo-HAQ0k2Bbl7gIKk70t8Rbfd0VoAZHIpnXBSbtc-1XWCRZ*0pXlYWWzrhKHNT6teFUTmHtfNCbClhQ2vbRv5/Nyosso2.JPG?width=650
TFF imeamka sasa baada ya kuamua kumfungia kitasa wa Mbeya City, Juma Said Nyosso.


Nyosso atakaa nje kwa mechi nane kwa kosa la kumdhalilisha mshambuliaji wa Simba SC, Elius Maguri timu hizo zilipokutana Januari 28, mwaka huu.

Pamoja na Nyosso, beki wa Azam FC, Aggrey Morris naye amefungiwa mechi tatu kutokana na lile sakata la kumpiga kiwiko mshambuliaji Emmanuel Okwi wa Simba.
Morris amefungiwa mechi tatu baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga kwa makusudi kisukusuku mshambuliaji wa SImba SC, Emmnauel Okwi timu hizo zilipokutana Januari 25, mwaka huu.

Okwi alipoteza fahamu baada ya kupigwa na Aggrey na kulazimika kukimbizwa hospitali ya Rufaa ya Taifa, Muhimbili, Dar es Salaam kwa matibabu zaidi na taarifa za Madaktari zilisema Mganda huyo angeweza kupoteza uhai siku hiyo kama si kuwahiwa kwa huduma ya kwanza.

Mechi zote hizo zilifanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba SC ikitoa sare ya 1-1 na Azam FC kabla ya kufungwa 2-1 na Mbeya City.

Katika kikao chake cha awali, Februari 3, mwaka huu Kamati hiyo ya Nidhamu ilitoa adhabu kwa watu tisa wakiwemo viongozi, wachezaji na kocha mmoja kwa kupatikana na hatia ya makosa ya kinidhamu.

Okwi alilazimika kukimbizwa hospitali baada ya kuanguka na kupoteza fahamu na baadaye mikanda ya Azam TV ilionyesha Morris akimpiga.

Kwa upande wa Nyosso, amebainika amefanya hivyo baada ya picha zilizopigwa na gazeti namba moja la michezo nchini kumnasa akifanya vitendo hivyo vya kipuuzi.

Lakini tayari Nyosso ameomba msamaha kwa Maguri na Blog hii ilizungumza na wote wawili lakini Maguri akasisitiza nanachotaka ni sheria kufuata mkondo wake.

LIVERPOOL KUJAZWA NOTI


2557EFF300000578-2940817-image-m-6_1423134983274
Klabu ya Liverpool hii leo imetangaza kuingia mkataba na kmapuni ya kutengeneza vifaa vya michezo ya Marekani ya New Balance mkataba ambao unaweka rekodi ya kuwa mkataba mnono kuliko yote katika historia ya klabu hiyo .
Kampuni hii ambayo makao makuu yake yako huko Boston nchini Marekani inachukua nafasi ya kampuni ya Warrior ambayo imekuwa ikidhamini Liverpool tangu miaka mitatu iliyopita na itaanza rasmi kazi na Liverpool katika msimu wa mwaka 2015/2016.
Thamani ya mkataba ambao New Balance imeingia na Liverpool itakuwa paundi milioni 25 kwa mwaka huku kampuni hiyo ikisimamia utengenezaji wa jezi na vifaa vyote vya maeozi pamoja na nenmbo yake kuonekana kwenye jezi ya timu hiyo.
Liverpool italipwa paundi milioni 25 kwa mwaka na  kampuni ya New Balance ya nchini Marekani .
Liverpool italipwa paundi milioni 25 kwa mwaka na kampuni ya New Balance ya nchini Marekani .
New Balance ndio kampuni mama ya Warrior ambao ndio wadhamini wa sasa wa Liverpool kwa upande wa utengenezaji wa jezi zake na mafanikio yaliyopatikana katika miaka mitatu ya mkataba na Liverpoool umeishawishi kampuni ya New Balance kuingia kwenye soko la mchezo wa soka .

USIKOSE KUFUATILIA BLOG HII HAJIBALOU.BLOGSPORT.COM.KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI

MAN CITY WAMTEMA JOVETIC

KLABU ya Manchester City imemuengua katika kikosi chake cha Ligi ya Mabingwa Ulaya Stevan Jovetic ili kumuingiza Wilfried Bony.
Nyota huyo wa Montenegro, alisajiliwa kutoka Fiorentina kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 22 mwaka 2013, sasa anaweza kuwa anajiandaa kuondoka katika klabu hiyo baada ya kuchaguliwa kumpisha Bony aliyesajiliwa dirisha dogo kwa Pauni Milioni 20 kutoka Swansea City.
Jovetic, ambaye amekuwa akiandamwa na majeruhi tangu atue Man City ameanza katika mechi 18 tu ndani ya miezi 19. 
Stevan Jovetic has been dropped from Manchester City's Champions League squad
Stevan Jovetic ametemwa kikosi cha Ligi ya Mabingwa Manchester CityCity had to make way for £28million signing Wilfried Bony, here in action for the Ivory Coast
Wilfried Bony amechukua nafasi yake katika kikosi hicho

USIKOSE KUFUATILIA BLOG HII WWW.HAJIBALOU.BLOGSPORT.COM KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI

GHANA YAFUZU AFCON, UWANJA WAGEUKA VITA

NDOTO za wenyeji Equatorial Guinea kunyakua Kombe la Mataifa ya Afrika zimeyeyuka usiku huu baada ya kufungwa mabao 3-0 na Ghana Uwanja wa Malabo.
Black Stars inayofundishwa na kocha wa zamani wa Chelsea, Avram Grant ilipata mabao yake kupitia kwa Jordan Ayew kwa penalti dakika ya 42, Mubarak Wakaso dakika ya 45+1 na Andre Ayew dakika ya 75.
 
Baada ya bao la tatu, huku Game wakiendelea kuwashambulia wenyeji, zikiwa zimesalia dakika nane mchezo kumalizika, mashabiki wa Guinea walianza kurusha chupa uwanjani na pia kuwapiga nazo mashabiki wa Ghana, ambao walilazimika kuvamia uwanjani kunusuru maisha yao.
 
Polisi walilazimika kutumia hadi helikopta kuwaondoa uwanjani mashabiki wa Guinea na baada ya nusu saa hali ilipotulia Uwanja ulikuwa kama mtupu na refa Eric Castane akamalizia mchezo.   
Ghana sasa itamenyana na Ivory Coast katika fainali ya AFCON 2015 Jumapili, wakati hatma ya wenyeji na mchezo wa mshindi wa tatu dhidi ya DRC haijajulikana, kwani kuna uwezekano wakapewa adhabu kali na CAF. 
Ghana players celebrate in front of coach Avram Grant en route to the Africa Cup of Nations final
Wachezaji wa Ghana wakishangilia na kocha wao, Avram Grant baada ya kukata tiketi ya Fainali leo
Ghana players are shielded by riot police after being pelted by missiles at half-time
Wachezaji wa Ghana wakiwa wamekingwa na Polisi baada ya kutokea vurugu uwanjani

Mashabiki w Guinea walikasirishwa mapema tu na kitendo cha refa huyo kuwapa penalti ya bao la kwanza Ghana na baada ya bao la tatu, hali ilikuwa mbaya kabisa.
Mashabiki walianza pole pole kurusha chupa kila refa huyo alipopuliza filimbi.  
 
Kikosi cha Ghana kilikuwa; Brimah, Afful, Boye, Mensah, Baba, Acquah, Mubarak, Atsu, Jordan Ayew, Andre Ayew na Appiah.
Equatorial Guinea; Ovono, Evuy/Fabiani Bosio, Mbele, Rui, Belima, Seno, Zarandona/Ganet, Doualla, Balboa, Salvador/Bohale Aqueriaco na Nsue.

KURASA ZA MWANZO NA MWISHO ZA MAGAZETI YA MICHEZO LEO FEB 6 IJUMAA

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.