Uongozi
wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam umesema umefika mbali katika suala
lake na beki wake, Hassan Kessy na una imani kubwa ataendelea kubaki na
kuitumikia klabu hiyo msimu ujao.
Makamu Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema wameanza mazungumzo na Kessy na yako katika hatua nzuri...