SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Mar 5, 2015

PAPIS CISSE, JONNY EVANS KAMA 'MCHANGANI' WATEMEANA MATE....

Beki Jonny Evans wa Man United na mshambuliaji wa Newcastle, Papiss Cisse wameonyesha utoto utafikiri wachezaji wachanga wa mchangani tena Bongo.

Wachezaji hao wawili wamefikia hatua ya kutemeana mate wakati wa mechi ya Ligi Kuu England timu zao zilipokutana na Man United kushinda kwa bao 1-0.

BILIONI 56 ZATUMIKA KUJENGA STUDIO ZA AZAM TV, RAIS JK KUZIZINDUA KESHO

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
JUMLA dola za Kimarekani Milioni 31 (zaidi ya Sh. Bilioni 56 za Tanzania) zimetumika kutengeneza studio mpya za kisasa za Azam TV, zilizopo eneo la Tabata Relini, Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa na Naibu Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Tido Mhando wamiliki wa Azam TV leo mchana katika Mkutano na Waandishi wa Habari, Tabata, Dar es Salaam. 
Mhando mwenye uzoefu wa kuongoza kampuni kubwa za vyombo vya habari zikiwemo Idhaa ya Kiswahili BBC, Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) na Mwananchi Communication Limited (MCL), amesema studio hizo zina ubora kuliko nyingine zote nchini.
Naibu Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Tido Mhando akizungumza na Waandishi wa Habari leo

“Ni studio ambazo labda unaweza ukazifananisha na studio za kampuni kubwa kama CNN, Aljazeera BBC, na kwa kuwa za kwetu ni mpya, zinaweza kuwa na ubora kuliko hizo,”amesema.
Tido amesema baada ya kukamilika kwa ujenzi wa studio hizo, zoezi la uzinduzi wake rasmi litafanyika kesho, asubuhi mjini Dar es Salaam.
Mhando ambaye alikuwa mtangazaji maarufu wa mpira wa miguu enzi zake nchini kupitia Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD), alisema mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.
“Azam TV imeanza kufanya shughuli zake kwa zaidi ya mwaka sasa, lakini tumekuwa tukiboresha mambo kadha wa kadha kuelekea siku ya kesho, ambayo tunaweza tukasema ndiyo mwanzo rasmi wa Azam TV,”alisema Tido.   

FIFA; TUNASHUGHULIKIA SUALA LA OKWI

???????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????Na Sanula Athanas
FIFA imesema inaushughulikia utata uliojitokeza kuhusu usajili wa kiungo mshambuliaji wa Simba, Mganda Emmanuel Okwi katika klabu za Tanzania na Tunisia.
Katika taarifa yake kwa NIPASHE jana saa 8:04 alasiri, Ofisa Habari wa FIFA, Cilla Duncan, alisema tayari shirikisho hilo lenye mamlaka ya juu kisoka ulimwenguni, limeshaanza kuchukua hatua za kinidhamu kuhusu suala hilo.
“Tunathibitisha kwamba, kesi ya kinidhamu (kuhusu Okwi) imeshafunguliwa. Kesi inaendelea na hivyo, hatuwezi kueleza zaidi kuhusu kesi hiyo kwa muda huu,” alisema Duncan.
Februari 11, shirikisho hilo la kimataifa la soka liliitaka SC Villa ya Uganda kutolea ufafanuzi sakata la uhamisho wa mshambuliaji Emanuel Okwi katika klabu za Tanzania (Simba na Yanga) na Etoile du Sahel ya Tunisia.
Huku likiipa wiki mbili SC Villa kuwasilisha utetezi wao FIFA (kuanzia Februari 11-25, mwaka huu), shirikisho hilo lilisema imebaini dosari juu ya kumbukumbu za uhamisho wa Okwi ambazo zimekuwa na utata mwingi tangu alipohamia klabu za Simba, Yanga na Etoile du Sahel.
Shirikisho hilo lilisema kuwa, wakati Okwi anahama kutoka klabu moja kwenda nyingine, pesa pia zilikuwa zinalipwa kwa klabu ambayo Okwi alikuwa anaihama. 
Lakini, FIFA ilisema kuwa takwimu zilizopo katika mfumo wake wa uhamisho wa wachezaji (TMS), zinaonyesha kwamba, Okwi alihama kutoka SC Villa kwenda SC Villa, kitu ambacho si cha kawaida, na baadaye SC Villa kwenda Yanga ilhali alikuwa mali ya Etoile du Sahel.
Okwi alihama kutoka SC Villa iliyomkuza kwenda klabu ya Simba mwaka 2010 kabla ya kuhamia klabu ya Etoile du Sahel miaka mitatu baadaye.
Mganda huyo akarudi tena kwenye klabu yake ya zamani ya SC Villa 2013, suala lililozua utata, lakini akajiunga na klabu ya Yanga mwaka huo huo.
Imeripotiwa kuwa kuna baadhi ya watu ndani ya klabu ya Villa walikuwa wanaficha ukweli wa mambo wakati wa uhamisho wa baadhi ya wachezaji. 
CHANZO: NIPASHE

UFAFANUZI KUHUSU SUALA LA "AJIBU" HUU HAPA


DSC03036
Na Baraka Mbolembole,
Nani anayejitoa kusaidia kwa dhati mpira wa Tanzania?. TFF hakuna ‘ watendaji’, katika klabu kubwa ‘ wameshikili ‘ Mafionso’, na Chombo kilichopiganiwa sana ‘ Bodi ya Ligi’ kumejaa watu ‘ wababaishaji’ wasio na ufahamu wa kandanda. Wakati ‘ Hoja ya msingi’ inapojitokeza, hakuna aliye tayari kujadili katika ‘ misingi ya kimpira’. Umefikia wakati sasa wa klabu ‘ kukataa kuendeshwa katika utumwa’ na TFF. TFF imekuwa dhaifu mno kiutendaji na wakati ipojulikana makosa yao huwa si wazungumzaji wazuri, kwa maana kwamba mazungumzo mengi ya msingi hugeuzwa na kuwa ‘ fimbo’ ya kuuchapa upande mwingine.

Majuzi, Ofisa mkuu wa kitengo cha habari wa klabu ya Yanga SC, Jerry Muro aliweka wazi kuwa Simba imefanya makosa kumchezesha kumchezesha mshambulizi Ibrahimu Ajibu katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons kwa kuwa mchezaji huyo tayari alikuwa na kadi tatu za njano na kwa mujibu wa kanuni zilizo wazi, mchezaji anapopata kadi tatu za njano atakosa mchezo mmoja hivyo Ajibu hakustahili kutumika katika mchezo huo ambao Simba ilishinda mabao 5-0, magoli matatu ‘ Hat-trick’ yakifungwa na mshambulizi huyo kinda.

TFF ilijibu haraka kuwa, kanuni tayari zilikuwa zimeshafiwa marekebisho huku baadadhi ya klabu tu zilipata barua kuhusu marekebisho hayo mapya yaliyofanywa na Bodi ya Ligi. Kanuni za sasa ni nzuri, kwa kuwa zitaruhusu klabu kumchagulia mechi ya ‘ kumiss’ mchezaji ambaye atakuwa na kadi tatu. Simba ni kati ya klabu zilizopata barua ya marekebisho hayo na tayari walishaitumia dhidi ya Abdi Banda wiki mbili zilizopita wakati kiungo mwenye kadi tatu za njano Abdi Banda alipotumika katika mchezo huo ambao Simba walipoteza kwa bao 1-0 katika uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Inawezekana Yanga wasiwe na ‘ hitaji la pointi za Simba kupunguzwa’  lakini kama timu ambayo inaweza kutumia kanuni hiyo Yanga wana hoja ya msingi kwa kuwa hawana taarifa hadi sasa. Bodi ya Ligi tayari wamekiri kuwa Yanga wana hoja ya msingi, kuhoji ni kwanini hawajapata taarifa rasmi ya mabadiliko hayo tangu Januari 8. Lakini katika hilo Bodi inaweza isihusike sana kwa kuwa walitoa maagizo hayo mapema kwa Shirikisho la soka, TFF.

 Kwanini Yanga hawana taarifa ya mabadiliko hayo?. TFF imefanya uzembe mkubwa nap engine sababu muhimu kama hii inapaswa watu wawajibike kwa kuwa hawana umakini ama hawafahamu majukumu yao. Simbailiwasilisha barua TFF wakiomba AJIBU atumike katika michezo dhidi ya Prisons na Yanga ili adhabu yake ifanye kazi katika gemu dhidi ya Mtibwa Sugar, na hilo liliwezekana na Ajibu akatumika katika mchezo huo kwa ruhusa ya TFF.

 Labda pia tujiulize ni kwani mambo yote hayo yanafanyika bila klabu nyingine kufahamu kama kuna kanuni mpya zinatumika katika ligi?. Katika suala la Banda hakukuwa na malalamiko, labda kwa kuwa Simba ilipoteza mchezo, lakini ili la Ajibu limefumuka wakati zikiwa zimebaki siku chache kwa mpambano wa mahasimu wa soka nchini Simba na Yanga. Unaweza kujiuliza ni kwanini Yanga wamevalia ‘ njuga’ jambo hili na kupata majibu yako.

Sababu ya mechi ya Jumapili hii, Yanga wanajaribu kuichanganya Simba nje ya uwanja ‘ game mind’ huku pia wakifichua ‘ udhaifu mkubwa wa kiutawala ndani ya TFF’. Yanga wako mbele ya Simba kwa alama nane hivyo si lazima kwao Simba wapoteze pointi tatu za Prisons, wanachohoji Yanga ni kwanini klanbu nyingine ikiwemo wao hawana taarifa rasmi za mabadiliko ya kanuni ya ‘ kadi tatu za njano’. Makau mwenyekiti wa Bodi ya ligi anasema kuwa TFF na Bodi ya ligi ndiyo waendeshaji wakuu wa mpira nchini hivyo klabu hushirikishwa katika vikao muhimu ikiwa kuna umuhimu tu wa kufanya hivyo kama hakuna havitaitw

MANYIKA JUNIOR YUKO FITI KUIVAA YANGA JUMAPILI

MANYIKA KATIKA MAZOEZI YA SIMBA MJINI ZANZIBAR, JANA JIONI.
Kipa Peter Manyika yuko fiti yuko fiti na hivyo Kocha Goran Kopunovic atakuwa na kazi ya kuchagua, nani aanze Jumapili.


Jumapili ni siku inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini kwa kuwa watani wa jadi, Simba na Yanga watakutana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Simba iko kambini mjini Zanzibar wakati Yanga imechichimbia mjini Bagamoyo, kwa kifupi zote zimekimbia jijini Dar es Salaam zilipozaliwa.
Kinda huyo, yaani Manyika ambaye ni mtoto wa kipa nyota wa zamani wa Yanga, Manyika Peter, alionekana yuko fiti na kufanya kazi yake kwa usafasaha mkubwa katika mazoezi ya Simba leo mjini Zanzibar.

Manyika alikuwa kivutio kutokana na alivyoifanya kazi yake kwa ufasaha, alivyokuwa akiokoa hatari kadhaa na kudaka kwa ustadi mkubwa.

Hii itamfanya kocha huyo Mserbia awe na wakati mgumu wa kuchagua katika kinda huyo au kipa mkongwe Ivo Mapunda.

Mapunda naye alionekana kuwa fiti katika mazoezi hayo yaliyokuwa ya nguvu na kasi.

05 Mar 2015
Next

YANGA SC KUMKOSA COUTINHO DHIDI YA SIMBA JUMAPILI

Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
YANGA SC itaendelea kumkosa wake Mbrazil, Andrey Coutinho katika mchezo dhidi ya mahasimu wa jadi, Simba SC Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga SC ilifikiria kumpeleka India Mbrazil huyo kwa matibabu zaidi, lakini baada ya vipimo katika hospitali moja jijini, imebainika anaweza kupona bila kwenda huko.
Kiungo huyo aliyeumia wiki iliyopita akiichezea timu yake katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Mbeya City, Yanga SC ikishinda mabao 3-1 amefanyiwa vipimo leo.
Coutinho akizungumza na kocha wake, Hans van der Pluijm kambini, Mbegani leo

Mbrazil huyo aliumia goti lake la kulia wakati akisaidia Yanga kuibuka na ushindi huo ambapo kufuatia majibu ya vipimo hivyo hataweza kusafirishwa tena India badala yake matibabu yake yatafanyika hapahapa nchini.
"Tulikuwa tunahofia kwamba anaweza kupelekwa India, alionekana kama maumivu yake ni makubwa, lakini leo tulimpeleka hospitali akiwa na daktari wetu Yomba (Richard) na kuonekana maumivu aliyonayo yatatibiwa hapahapa,"alisema bosi mmoja wa Yanga.
Kiungo huyo leo alifanikiwa kufanya mazoezi ya peke yake nje ya Uwanja kwa kukimbia taratibu katika kambi ya timu hiyo iliyopo Mbegani, Bagamoyo mkoani Pwani, lakini imethibitishwa hatacheza dhidi ya SImba SC.

MAXIMO APATA TIMU BRAZIL

ALIYEKUWA kocha wa Yanga SC, Mbrazil Marcio Maximo (pichani juu) amefanikiwa kupata ajira mpya nchini kwao Brazil.
Maximo aliyetemwa na Yanga Desemba 19 mwaka jana akidumu kwa miezi sita, amefanikiwa kupata kibarua kipya kwa kuinoa timui ya Parana ambayo inafanya vibaya katia ligi ya jimbo moja huko Brazil.
Katika kibarua hicho Maximo anakabiliwa na shughuli pevu ya kuibakisha timu hiyo isishuke daraja wakati ikiwa mkiani mwa msimamo wa ligi ya huko.
Maximo alifungwa mara baada ya Yanga SC kufungwa mabao 2-0 na mahasimu, Simba SC katika mchezo wa Nani Mtani Jembe.