SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Apr 13, 2015

YANGA YACHEMSHA KUIPIKU AZAM

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
“Azam ilitwaa ubingwa wa Bara msimu uliopita ikikusanya pointi 62 huku ikimaliza msimu bila kupoteza mechi hata moja.’
WAMECHEMSHA! Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na ukweli kwamba Yanga SC licha ya kuwa na moto mkali msimu huu, haitaweza kuzifikia pointi ambazo Azam FC walizipata msimu huu hata kama ikitwaa ubingwa msimu huu na kushinda mechi zote tano zilizobaki.
jam
Yanga SC, mabingwa mara 24 wa Tanzania Bara, kwa sasa wanaoongoza msimamo wa Ligi Kuu ya Bara wakiwa na pointi 46 baada ya mechi 21, zikiwa zimebaki mechi tano kabla ya msimu huu kufikia tamati Mei 9, mwaka huu.
Azam FC walitwaa taji la kwanza kwao la ligi hiyo msimu ulioipita wakiifikia rekodi ya Simba SC ya kumaliza msimu bila kupoteza mechi hata moja, kikubwa wakikusanya pointi 62 baada ya mechi zote 26.
Kwa mantiki hiyo, Yanga SC yenye pointi 46 kwa sasa ikishinda mechi zote tano zilizobaki itatwaa ubingwa ikiwa na pointi 61, moja pungufu ya pointi za Azam FC za msimu uliopita.
Wakiwa na Mcameroon Joseph Omog, aliyerithi mikoba ya Muingereza Stewart Hall katikati ya msimu, walishinda mechi 18, sare nane. Wakafunga mabao 51 na kuruhusu nyavu zao kutikiswa mara 15.

MAN UNITED WALA ZA USO KWA CAVANI, BILIONEA WA KIARABU AWAAMBIA; "HATUMUUZI NG;O"

DILI la Manchester United kumnasa Edinson Cavani kama linaelekea kubuma, baada ya leo asubuhi klabu yake, Paris Saint-Germain kukanusha kwamba wana mpango wa kumuuza mshambuliaji huyo.
United imekuwa ikimfukuzia nyota huyo wa Uruguay katika jitihada za kuiongezea makali ya safu yake ya ushambuliaji, huku ikitaka kumrejesha Radamel Falcao klabu yake Monaco ilipomchukua kwa mkopo, na kumtema mkongwe Robin van Persiealiyeoteza makali.
Lakini mmiliki wa PSG, Nasser Al-Khelaifi amesema mabingwa hao wa Ufaransa wana dhamira ya kumbakiza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 na hawafikirii kumuuza. 
The Uruguayan forward is a target for Manchester United but looks set to stay in Paris 
PSG imesema haina mpango wa kumuuza Edinson Cavani, maana yake Manchester United hawawezi kumpata mshambuliajin hyo tena

"Edinson Cavani ni mchezaji ninayempenda haswa,"amesema tajiri huyo. "Naweza kukuambia kwamba yuko sana nasi, na swali la kuondoka kwake halijatokea. Paris inampenda, naye anaipenda Paris,".
PSG ina shaka na mshambuliaji mwingine nyota, Zlatan Ibrahimovic anaweza kuondoka, ndiyo maana haifikirii kumuuza Cavani iliyemsajii kwa Pauni Milioni 50 kutoka Napoli mwaka 2013.

TAMBWE AWAAMBIA MBEYA CITY; “BAHATI YAO”

Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI wa Yanga SC, Amissi Tambwe amesema kwamba haikuwa bahati yake jana kushangilia bao dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga SC iliifunga Mbeya City mabao 3-1 Uwanja wa Taifa katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, lakini Tambwe mfungaji bora wa Ligi Kuu msimu uliopita hakufunga.
Tambwe angekuwa mchezaji wa kwanza kuwainua mashabiki wa Yanga vitini jana, kama si refa Mathew Akrama wa Mwanza kukataa bao lake safi dakika ya sita, alilofunga akiwa amedhibitiwa na kipa na mabeki wa Mbeya City kwa kupiga kichwa cha kudundisha.
Haikuwa bahati yake; Moja ya mabao ya wazi ambayo Amissi Tambwe alikosa jana baada ya kupiga kupiga nje akiwa amebaki yeye na kipa


“Kwa kweli, ndiyo vile tuseme na marefa ni binadamu nao, ila sioni kwa nini alikataa lile bao, lilikuwa zuri tu. Nilipiga mpira nikiwa nimebanwa na mabeki wa Mbeya City na kipa wao,”.
“Kwanza niliposikia filimbi nikadhani refa anataka kutupa penalti, kumbe ananipigia mimi. Sasa sijui nilikuwa nimeotea au nilicheza rafu, sijui,”amesema Tambwe.
Aidha, baada ya bao hilo la mapema la Tambwe kukataliwa, Kpah Sherman, Salum Telela na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kila mmoja akafunga katika ushindi wa 3-1, ambao unazidi kuipaisha Yanga SC kileleni mwa Ligi Kuu.
Yanga SC sasa ina pointi 46 baada ya kucheza mechi 21, ikifuatiwa na mabingwa watetezi, Azam FC wenye pointi 38 za mechi 20, wakati Simba SC yenye pointi 35 za mechi 21, ni wa tatu.   

MSUVA SASA AMTAMBIA KAVUMBAGU, AMUAMBIA KIATU CHA DHAHABU MALI YAKE

Baada ya kumzidi kwa idadi ya mabao matatu, kiungo mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva, amemwambia mshambuliaji wa kutegemewa wa Azam FC, Didier Kavumbagu asahau ufungaji bora kwenye msimu huu wa Ligi Kuu Bara.


Msuva jana aliiongoza timu yake kuvaana na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Msuva alisema kuwa, kamwe hatakubali kuona mshambuliaji huyo anampita kwenye mbio hizo za ufungaji bora.

Alisema kuwa, bado anaendelea kushika maelekezo na mafunzo anayoyapata kutoka kwa kocha wake Mholanzi, Hans van Der Pluijm na msaidizi wake Charles Mkwasa kuhakikisha anafunga na anawatengenezea wenzake nafasi za kufunga mabao.

“Sitaki kuondoka hapa nilipo katika orodha ya wafungaji bora, lengo kubwa likiwa ni kumaliza ligi kuu nikiwa mfungaji bora msimu huu, ninaamini hilo linawezekana kabisa.

“Hivyo, nitahakikisha ninaitumia vyema kila nafasi ninayoipata ndani ya uwanja kwa kufunga mabao ili niipe timu yangu ubingwa kwenye msimu huu na ufungaji bora.


“Ninafurahia ushirikiano mkubwa ninaoupata kutoka kwa wachezaji wangu katika kufanikisha malengo yangu kwa kunitengenezea nafasi nzuri za kufunga mabao,” alisema Msuva.