SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Feb 26, 2015

AZAM TV ‘KURUSHA LIVE’ MECHI YANGA NA BDF BOTSWANA KESHO



Rhys Torrington (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Azam Media Group Limited, Yussuf Bakhresa (kushoto)
TELEVISHENI ya kisasa ya kulipia kwa gharama nafuu, Azam TV itaonyesha moja kwa moja mchezo wa marudiano wa Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika, kati ya wenyeji BDF XI na Yanga SC ya Tanzania.
Mchezo huo utakaofanyika Uwanja wa Lobatse mjini Lobatse, kuanzia Saa 11:30 jioni kwa saa za Afrika za Mashariki utaonyeshwa moja kwa moja na Azam Two.
Mtendaji Mkuu wa Azam Media Group, Muingereza Rhys Torrington ameiambia BIN ZUBEIRY jioni hii kwamba, mipango yote ya kuonyesha mchezo huo imekamilika.
“Kila kitu kimekamilika na tunayo furaha kuwaambia wateja wetu kwamba kesho tutakuwa na zawadi nzuri kwao, ambayo ni mchezo wa Yanga na BDF XI, watautazama kupitia Azam TV,” alisema Torrington.
Katika mchezo huo wa kesho, Yanga SC inahitaji hata sare ili kuweza kusonga mbele, baada ya awali kushinda mabao 2-0 nyumbani, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

CANNAVARO AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIEZI 10 JELA

NAHODHA wa kikosi cha Italia kilichobeba Kombe la Dunia mwaka 2006 nchini Ujerumani, Fabio Cannavaro amehukumiwa kifungo cha miezi 10 jela kwa kukiuka amri ya kutofika katika nyumba yake iliyozuiliwa na Mamlaka.
Cannavaro mwenye umri wa miaka 41, amekuwa akichunguzwa kwa tuhuma za kukwepa kodi na Oktoba Mamlaka mjini Naples ilizuia mali za karibu Pauni 732,737 zinazohusishwa na mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid na Juventus pamoja na mkewe.
Kaka wa Cannavaro, Paolo mwenye umri wa miaka 33, ambaye anachezea timu ya Ligi Kuu Italia, Sassuolo, naye amehukumiwa kifungo cha miezi sita na mkewe Daniela Arenoso mwenye umri wa miaka 40 miezi minne.
Watatu hao wamekata rufaa na kifungo chao kimesitishwa hadi mwisho wa rufaa yao.
Cannavaro won 136 caps for Italy and claimed two La Liga titles while at Real Madrid
Cannavaro amehukumiwa miezi 10 jela, ingawa kifungo chake kimesitishwa kupisha rufaa yake
Beki na Nahodha wa Yanga SC, Nadir Haroub Ali (kulia) anafahamika kwa jina la utani Cannavaro akifananishwa kiuchezaji na Nahodha wa zamani wa Italia, Fabio Cannavaro

Ndugu hao akina Cannavaro na Arenoso waliponzwa na kwenda kutembelea nyumba hiyo wakati ipo kizuizini. 
Cannavaro alishinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia, Ballon d'Or mwaka 2006 baada ya kuiongoza Italia kutwaa Kombe la Dunia. Akahamia Real Madrid baada ya hapo, ambako alikwenda kutwaa mataji mawili ya La Liga na vigogo hao wa Hispania.
Beki wa klabu ya Yanga SC ya Tanzania, Nadir Haroub Ali, amepewa jina la utani Cannavaro kutokana na Mtaliano huyo aliyeichezea mechi 136 Azzuri. 

JULIO AANZA MANENO COASTAL UNION

Na Oscar Assenga, TANGA
KOCHA Msaidizi wa Coastal Union, Jamhuri Kiwelu “Julio”amesema kuwa timu hiyo itapata matokeo mazuri katika mechi zake zilizosalia katika michuano ya Michuano ya Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kutokana na ubora wa kikosi hicho
Julio alitoa wito huo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa mara kumalizika mazoezi ya timu hiyo ambapo alisema kuwa lengo la kujiunga na timu hiyo ni kuongeza nguvu ili kukiwezesha kikosi hicho kurudisha makali yake.
Jamhuri Kihwelo 'Julio' kushoto amesema Coastal Union itatisha

Alisema kuwa atahakikisha anatoa mchango wake mkubwa kwenye timu hiyo ili kuiwezesha kufanya vizuri katika michezo mbalimbali ya Ligi kuu soka Tanzania bara hapa nchini.
“Mimi niliwahi kuifundisha Coastal Unionna kuiwezesha kupata mafanikio hivyo ni matumaini yangu kukiwezesha kikosi hichi kurejesha makali yake kwani timu hii ni kubwa na inaheshima yake kwenye soka “Alisema Kocha Julio.
Kocha huyo alisaini mkataba wa muda mfupi mpaka ligi kuu soka Tanzania mzunguko wa pili utakapomalizika ambapo atatumia nafasi hiyo kukipa makali kikosi hicho.
Alisema kuwa malengo makubwa yake ni kuhakikisha timu hiyo inachukua ubingwa wa Michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara ikiwemo kuwataka wachezaji kushikamana na kuwa watulivu kila mechi ili kupata mafanikio.
Hata hivyo alisema kuwa hatasita kuwafukuza kwenye kikosi hicho wachezaji watakaokuwa watovu wa nidhamu na watakaojiona mastaa na kushindwa kuendana na kasi yake katika mazoezi.
“Nashukuru kutua Coastal Union sasa ni kazi tu tutahakikisha tunapambana kufa na kupona ili kuweza kupata matokeo mazuri kila mechi zilizosalia kwenye Ligi hiyo “alisema Julio.

HIKI NDIO KIKOSI BORA LIGI YA MABINGWA WIKI HII


IMG_20150226_194709

TAIFA STARS YAPANGWA KUNDI A COSAFA, IKO NA ZIMBABWE, NAMIBIA



Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imepangwa Kundi A katika michuano  ya kombe la COSAFA nchini Afrika Kusini.
Kundi A:
Tanzania, Namibia, Lesotho na Zimbabwe.
Kundi B:
Shelisheli, Madagascar, Mauritius na Swaziland.

Michuano ya kombe la Cosafa inatarajiwa kuanza kutimua vumbi katikati ya mwezi Mei mwaka huu nchini Afrika Kusini.


Katika kila kundi, timu zote zitacheza michezo mitatu na mshindi wa kila kundi ataingia katika hatua inayofuata ya robo fainali itakayozijumuisha nchi za  Afrika Kusini, Botswana, Ghana, Malawi, Msumbuji na Zambia ambazo zimeingia katika hatua ya pili kutokana na nafasi zao kwenye msimamo wa viwango vya FIFA.

SIMON SSERUNKUMA AREJEA KWAO UGANDA


Kiungo Simon Sserunkuma amerejea kwao Uganda kutokana na mafanikio ya kifamilia.


Taarifa kutoka ndani ya Simba zimeeleza Sserunkuma amerudi Uganda kwa ajili ya shughuli ya arobaini ya mmoja wa wazazi wake.

Sserunkuma ameondoka wakati Simba ikijianda akupambana na Prisons, keshokutwa.

Kocha wa Simba, Goran Kopunovic ameonekana kutomuamini sana Simon na mara nyingi amekuwa akimuingiza katika kipindi cha pili.

WAKENYA KUISHANGILIA YANGA BOTSWANA


Mashabiki wa soka wakiwemo Watanzania na raia wa Kenya na Uganda wameungana kuishangilia Yanga ambayo iko jijini hapa kuivaa BDF XI ya Botswana.


Yanga inaovaa BDF XI katika mechi ya Kombe la Shirikisho itakayopigwa leo saa 1:30 kwa saa za hapa na saa 2:30 kwa saa za Afrika Mashariki.

Katika mitaa mbalimbali ya jiji hili, mashabiki wa nchi hizo tatu wameungana na kuishangilia Yanga wakionyesha kudumisha umoja wa Afrika Mashariki.

Ingawa si wengi, jana mchana mashabiki hao wamekiwemo wanafunzi walikuwa wakipanga namna ya kufanya ili kupata usafiri wa uhakika utakaowapeleka Lobatse kwenda kuishangilia Yanga.

Mkuu wa kitengo cha habari cha Yanga, Jerry Muro amesema mashabiki hao, hasa wale wa Tanzania wameonyesha ushirikiano wa hali ya juu.

Botswana ni kati ya nchi Kusini mwa bara la Afrika ambayo Watanzania wengi wanaishi wakiwa wanafanya biashara zao na wengine wakiwa wanafunzi katika vyuo mbalimbali vya jiji hili na katika mikoa mingine.


Yanga ilishinda kwa mabao 2-0 katika mechi yake ya kwanza jijini Dar es Salaam na BDF imepania kushinda na kusonga mbele katika mechi ya leo.

ALICHOSEMA KOCHA YANGA KUELEKEA MECHI YA KESHO BOTSWANA


pluijm
Na Bertha Lumala
Kocha mkuu wa Yanga SC, Hans van der Pluijm amewataka wachezaji wake kuhakikisha wanatikisa nyavu za wapinzani wao BDF XI FC katika mechi yao ya kesho ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Yanga SC, mabingwa mara 24 wa Tanzania Bara, watakuwa na kibarua kigumu mbele ya wenyeji wao hao watakapopamba katika mechi hiyo ya marudiano ya hatua ya awali ya michuano itakayochezwa kuanzia saa 2:00 usiku Uwanja wa SSKB Lobatse uliopo Km 70 kutoka Gaborone, mji mkuu wa Botswana. Uwanja huo upo kwenye kambi ya Jeshi la Ulinzi (BDF) eneo la Lobatse, Botswana.
Katika mahoajino na mtandao huu akiwa Botswana leo mchana, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Jerry Muro amesema benchi lao la ufundi linaloongozwa na Pluijm limewataka wachezaji kuhakikisha wanapata japo goli moja la ugenini huku wakilinda mabao yao mawili waliyofunga nyumbani.
“Tulishinda 2-0 nyumbani, lakini kocha (Pluijm) amewataka wachezaji kutobweteka na ushindi huo. Amesema ni lazima tusakae japo goli moja la ugenini ili tuwe salama zaidi huku tukihakikisha wenyeji wetu hawapati mabao,” amesema Muro.
Pluijm amesema ushindi wa timu hiyo kwenye mechi za Ligi Kuu ni chachu kuelekea mchezo huo wa marudiano dhidi ya BDF
Aidha, mitandao ya michezo ya Botswana imemnukuu Pluijm akitamba kupata ushindi mwingine wakati timu hizo zitakaporudiana kesho.
Pluijm amekaririwa akieleza kuwa, licha ya kucheza ugenini, bado ana uhakika watawafunga wenyeji wao BDF XI FC katika mchezo huo.
“Tumekuja Botswana kucheza kwa kushambulia kama tulivyofanya nyumbani tuliposhinda mabao 2-0, ninajua mchezo utakuwa mgumu kwa sababu wanacheza kwao na watataka kutushambulia, lakini sisi tutacheza kwa malengo huku tukihitaji bao moja ili kuwapa presha wenyeji,” amesema Pluijm.
Pluijm amesema ushindi wa timu hiyo katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara ni chachu kuelekea mchezo huo wa marudiano dhidi ya BDF na kuwataka mashabiki kuiunga mkono timu yao kuelekea mechi hiyo.
Hata hivyo, mashabiki wa Yanga SC waliokuwa wasafiri kwa basi kubwa la klabu hiyo Jumatano alfariji, walikwama kutokana na kile kilichoripotiwa leo kuwa basi hilo halina bima wala kibali cha barabarani.
Yanga SC ambayo kwa muda mrefu imekuwa haifiki mbali katika michuano ya kimataifa ikitolewa kwa matuta dhidin ya Al Ahly ya Misri katika hatua ya pili mwaka jana, inahitaji sare ya aina yoyote au kipigo kisichozidi bao 1-0 kusonga mbele.
Endapo timu hiyo ya Jangwani ikifanikiwa kuwang’oa maafande hao, itakutana na mshindi kati ya Sofapaka FC ya Kenya na Platnum FC katika hatua inayofuata. Wazimbawe walishinda 2-1 dhidi ya Sofapaka katika mechi ya kwanza iliyochezwa jijini Nairobi wiki mbili zilizopita.

BAADA YA KIPIGO, OZIL AISUSA JEZI YAKE KWA MCHEZAJI WA MONACO

WAKATI KIUNGO BERNADO WA AS MONACO ALIMFUATA MESUT OZIL WA ARSENAL WABADILISHANE JEZI BAADA YA MECHI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA KWENYE UWANJA WA EMIRATES, LONDON. ALIJIKUTA AKISUSIWA JEZI HIYO NA OZIL WALA HAKUTANA KUCHUKUA YA BENADO, HALFU HUYOOO AKAONDOKA ZAKE. ARSENAL ILILALA KWA MABAO 3-1.

ATLETICO MADRID YALALA BAO 1-0 DHIDI YA WAJERUMANI

.
FERNANDO TORRES (KULIA) AKIKIMBIA KUMLALAMIKIA MWAMUZI BAADA YA KIKOSI CHAKE KUFUNGA BAO LILILOKATALIWA. ATLTETICO MADRID IKIWA UGENINI IMELALA KWA BAO 1-0 DHIDI YA WENYEJI WAKE BAYER LEVERKUSEN.




ZIPO HAPA KURASA ZA MWANZO NA ZA MWISHO ZA MAGAZETI YA MICHEZO LEO FEB 26

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.