SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Feb 16, 2015

MSIMAMO LIGI KUU BARA HUU HAPA

Pos                 Team                   Pld     W     T     L     Goals    Diff        Pts
1     •     Logo     Azam                    13     7     4     2          22          10    25
2     •     Logo     Yanga                  13     7     4         2         15          8        25
3     ↑     Logo     Kagera Sugar       15     5     6     4     12     1                  21
4     ↑     Logo     Simba                   14     4     8          2        15        4         20
5     ↓     Logo     Mtibwa Sugar        14     4     7     3     15    1                  19
6     •     Logo     Ruvu Stars            14     5     4           5         10      -1     19
7     •     Logo     Coastal                  15      4     7     4     10    1        19
8     ↓     Logo     JKT Ruvu              15       5     4     6     14    -1        19
9     ↓     Logo     Polisi Moro                15     4     7     4         12      -1       19
10     •     Logo     Mbeya City                14     4     5          5    9      -2       17
11     •     Logo     Ndanda               15     4     4     7              13     -5        16
12     •     Logo     Stand Utd               15     3     6            6   13      -5      15
13     •     Logo     Mgambo              13     4     2             7       7       -8      14
14     •     Logo     Prisons               13     1             8     4         10    -2       11

WALICHO SEMA YANGA BAADA YA KUFIKA MBEYA

mashabiki-yanga
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Baada ya kuwachapa ‘Makhrikhri’ BDF XI FC ya Botswana, kikosi cha Yanga SC tayari kimo jijini Mbeya kusaka pointi sita za Ligi Kuu Tanzania Bara kabla ya kuwafuata maafande wa BDF XI FC mjini Gaborone, Botswana.
Wakiwa jijini Mbeya jioni hiui, Yanga SC wametamba kuchukua pointi zote sita katika mechi mbili za Ligi Kuu jijini humo dhidi ya timu ‘kibonde msimu huu’, Tanzania Prisons na Mbeya City FC.
Jerry Muro, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, ameuambia mtandao huu muda mfupi uliopita kuwa wachezaji wametua jijini Mbeya salama wakitokea jijini hapa.
Muro, mwandishi bora wa habari nchini miaka minne iliyopita, wachezaji wametinga jijini Mbeya kwa mafungu, baadhi wakisafiri kwa ndege na wasiopenda usafiri huo wa anga wamesafirishwa kwa basi.
“Tumeingia Mbeya kwa malengo mawili; kwanza kuchukua pointi zote sita katika mechi mbili zijazo dhidi ya Prisons na Mbeya City ili tukae vizuri katika msimamo wa Ligi Kuu. Pili, kufanya maandalizi ya mechi ya marudiano na BDF XI FC nchini Botswana,” amesema Muro.
Kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Alhamisi Yanga SC itashuka Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya kuwakabili Prisons kabla ya kuchuana na wababe wa Simba SC, Mbeya City FC kwenye uwanja huo Jumapili.
Baada ya mechi dhidi ya City FC, Yanga SC wataanza safari kuelekea mjini Gaborone, Botswana kwa ajili ya mechi yao ya marudiano dhidi ya ‘Makhrikhri’ BDF XI FC ya hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika Februari 27.
Kikosi cha Mdachi Hans van der Pluijm cha Yanga SC kiliinyuka timu hiyo ya Jeshi la Ulinzi la Botswana mabao 2-0 katika mechi ya kwanza Uwanja wa Taifa jijini hapa juzi (Jumamosi).
Shukrani kwa mabao ya mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita, Mrundi Amisi Tambwe, yote akiyafunga kwa vichwa na kufikisha mabao manne katika mashindano yote msimu huu.
Wachezaji wawili, kiungo Nizar Khalfan na beki wa kati Pato Ngonyani, ambao wamebaki jijini hapa kutokana na maradhi.
Yanga SC kwa sasa inakamata nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 25, sawa na mabingwa Azam FC ambao wako kileleni mwa msimamo kwa faida ya tofauti nzuri ya mabao ya kutupia na kufungwa.
Azam FC inayonolewa na Mcameroon Joseph Omog, imefunga mabao 22 na kufungwa 12 wakati Yanga SC imetikisa nyavu za wapinzani mara 15 huku safu yake ya ulinzi inayoongozwa na Nahodha, Mzanzibar Nadir ‘Cannavaro’ imeruhusu mabao saba.

DOKII AIBWAGA YANGA SC, ATUA AZAM FC

Msanii nyota Tanzania, Ummy Wenceslaus maarufu kwa jina la Dokii (kushoto) jana alikuwa miongoni mwa Watanzania waliojitokeza Uwanja wa Azam Complex kuishangilia Azam FC ikimenyana na El Merreikh ya Sudan katika mchezo wa kwanza Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika. Azam ilishinda 2-0.
Lakini katika michuano ya Kombe la Mapinduzi Januari mwaka huu visiwani Zanzibar, Dokii (katikati ya rafiki zake) alikuwa akiishangilia Yanga  SC japokuwa Azam FC ilikuwepo pia. 
Dokii ni shabiki mzuri wa soka na husafiri hadi nje ya nchi kwenda kuishangilia timu ya taifa inapocheza. Hapa alikuwa Mombasa, Kenya mwaka juzi kwenye Kombe la Challenge akiishangilia timu ya Bara ikimenyana na Uganda katika Robo Fainali ya Kombe la Challenge na kushinda kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 2-2.

PICHA MATUNGULI YALIYOBEBWA NA MASHABIKI YA SIMBA JANA MOROGORO

2 
KIKUNDI Maarufu cha wanachama walioasi wa klabu ya Simba, Simba Ukawa, jana kilikuja na matunguli katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro, Mnyama akishinda mabao 2-0 na hali hiyo ilisababisha Simba wenyewe kwa wenyewe wapigane wakipinga imani hizo za kishirikiana.
Matunguli hayo yaliyokuwa yanatisha kuyatazama yalikamatwa kabla ya mechi na kuzua tafrani miongoni mwa wadau wa soka waliofurika uwanja wa Jamhuri. Huu ni muendelezo wa imani za kishirikina katika soka la Bongo.
 Wadau wakiwa wameyakamata Matunguli
Mzigo ulikuwa hatari sana wadau

SHUTI LA BAHANUZI ‘LAMPOFUA’ JICHO IVO MAPUNDA


Said Bahanuzi alimbabua shuti Ivo jana
Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
KIPA wa Simba SC, Ivo Mapunda sasa jicho lake halioni kabisa kwa sasa baada ya jana kupigwa na shuti la la mshambuliaji wa Yanga SC, Said Bahanuzi, Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Bahanuzi alikuwa akiichezea Polisi Moro alipotolewa na Yanga SC kwa mkopo wa kumalizia msimu na jana alikutana na mpira uliopanguliwa na Ivo Mapunda baada ya kona na kuurudisha kwa shuti kali lililombabua jichoni kipa huyo. 
Ivo hakuweza kuendelea na mchezo baada ya tukio hilo dakika ya 58 na kutokana na hali mbaya aliyokuwa nayo alikimbizwa hospitali ya mkoa wa Morogoro kwa matibabu zaidi.
Taarifa kutoka hospitali ya Morogoro zinasema Ivo alitoka hapo jana akiwa haoni kabisa baada ya matibabu.
Baada ya matibabu ya jana, Ivo anatarajiwa kuongozana na Daktari wa Simba SC, Yassin Gembe leo katika hospitali hiyo tena kwa ajili ya uchunguzi ili kujua atahitaji muda gani kabla ya kuanza tena kazi.
Ivo Mapunda baada ya kutibiwa hospitali jana mjini Morogoro


Baada ya kuumia, Simba SC ikiwa inaongoza bao 1-0, nafasi ya Ivo ilichukuliwa na kipa chipukizi, Peter Manyika ambaye alimalizia sehemu iliyobaki ya mchezo na timu ikashinda 2-0.
Mabao ya Simba SC jana yalifungwa na Ibrahim Ajibu kipindi cha kwanza na Elias Maguri kipindi cha pili.

MESSI APIGA HAT TRICK YA TANO MSIMU HUU


BARCELONA imeshinda mechi ya 11 mfululizo, baada ya kuilaza Levante mabao 5-0  katika mchezo wa La Liga usiku wa jana Uwanja wa Camp Nou.
Lionel Messi amefunga hat trick yake ya tano katika msimu huu wa La Liga kwa mabao yake ya dakika za 38, 59 na 65 kwa penalti, wakati mabao mengine yamefungwa na Neymar dakika ya 17 na Suarez dakika ya 73.
Huo ni ushindi wa 11 mfululizo kwa Barcelona katika mashindano yote msimu huu.
Kikosi cha Barca kilikuwa: Bravo, Montoya, Bartra, Mascherano, Adriano; Busquets, Xavi, Rakitic/Roberto dk62, Pedro, Messi na Neymar/Suarez dk67.
Levante; Marino, Ivan Lopez/Jason dk 71, Navarro, Ramis, Tono, Diop/Mari dk78, Simao, Xumetra, Barral, Morales na Uche/Victor dk62.
The Argentinian (left) was superb throughout and scored his fifth La Liga hat trick of the season 
Messi kushoto akishangilia baada ya kupiga hat trick yake ya tano La Liga msimu huu
Luis Suarez scored a wonderful bicycle kick after coming off the bench for Luis Enrique's side
Luis Suarez amefunga bao zuri la tik tak leo

MAGAZETI YA MICHEZO LEO JUMATATU