Feb 16, 2015

MESSI APIGA HAT TRICK YA TANO MSIMU HUU


BARCELONA imeshinda mechi ya 11 mfululizo, baada ya kuilaza Levante mabao 5-0  katika mchezo wa La Liga usiku wa jana Uwanja wa Camp Nou.
Lionel Messi amefunga hat trick yake ya tano katika msimu huu wa La Liga kwa mabao yake ya dakika za 38, 59 na 65 kwa penalti, wakati mabao mengine yamefungwa na Neymar dakika ya 17 na Suarez dakika ya 73.
Huo ni ushindi wa 11 mfululizo kwa Barcelona katika mashindano yote msimu huu.
Kikosi cha Barca kilikuwa: Bravo, Montoya, Bartra, Mascherano, Adriano; Busquets, Xavi, Rakitic/Roberto dk62, Pedro, Messi na Neymar/Suarez dk67.
Levante; Marino, Ivan Lopez/Jason dk 71, Navarro, Ramis, Tono, Diop/Mari dk78, Simao, Xumetra, Barral, Morales na Uche/Victor dk62.
The Argentinian (left) was superb throughout and scored his fifth La Liga hat trick of the season 
Messi kushoto akishangilia baada ya kupiga hat trick yake ya tano La Liga msimu huu
Luis Suarez scored a wonderful bicycle kick after coming off the bench for Luis Enrique's side
Luis Suarez amefunga bao zuri la tik tak leo

0 maoni:

Post a Comment