SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Nov 12, 2014

WASANII WA TANZANIA WAMUOMBEA RAIS JAKAYA KIKWETE.

Staa wa muziki wa Bongo fleva Nasib 'Abdul Diamond'.

SIKU chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kufanyiwa pasuaji wa tezi dume (prostrate), mastaa mbalimbali wameguswa na kuunganisha nguvu ya pamoja kumfanyia maombi mazito kiongozi huyo wa nchi ili aweze kupona haraka.Rais Kikwete alifanyiwa upasuaji huo Novemba 8, mwaka huu katika Hospitali ya John Hopkins iliyopo Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani.Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, mastaa wamesema wameguswa na kuumwa huko kwa rais lakini wameshukuru kwamba upasuaji umefanyika salama hivyo wanamuombea apone haraka ili aweze kurudi katika afya yake ya kawaida.
“Mungu asaidie upone haraka baba…tunaumwa nawe,” aliandika Aman Temba ‘Mh. Temba’ mtandaoni huku Esterlina Sanga ‘Linah’ akiandika:“Furaha ya moyo wangu inakamilika na mengi lakini kubwa kuliko yote ni kuona tabasamu lenye afya na uzima tele kwako baba, shujaa rais wangu. Get well soon my shujaa.”
Staa wa filamu Bongo, Jackline Wolper.
Mbali na wasanii hao, wengine walioonesha kuguswa na kuumwa kwa rais na kuandika hisia zao ni Diamond, Linex, Wolper, Shetta, Shilole na MwanaFa.
Mbali na wasanii wananchi mbalimbali wa kawaida kwa nyakati tofauti walieleza hisia zao kupitia gazeti hili:
“Nilipopata tu taarifa kwamba mheshimiwa rais amefanyiwa upasuaji, nilishtuka kidogo lakini baada ya hapo mimi pamoja na wenzangu tukafanya maombi maalumu ya kumuombea rais wetu aweze kupona haraka na kuendelea na majukumu yake ya kawaida.
Msanii wa Bongo Fleva, Shetta.
“Niwaombe Watanzania wote tuungane kwa pamoja kumuombea rais wetu maana maombi yetu yana maana kubwa mbele za Mungu,” alisema Mazula, mkazi wa Tabata.
Tezi dume ni nini?
Tezi dume ipo kwa binadamu wa kiume ambapo ina muonekano kama wa yai (oval shape) na upana wake huwa ni CM4 na unene CM3 ingawa kwa mujibu wa madaktari, vipimo hivyo vinatofautiana kwa kila mwanaume.
Estelina Sanga 'Linah'.
Tezi dume inazunguka shingo ya kibofu cha mkojo na kuzunguka mrija unaopeleka mkojo nje, kwa kawaida tezi hii ina umbo la wastani na huongezeka ukubwa kadri umri wa mtu unavyozidi kuongezeka.

CAF yahaha kutafuta mbadala wa Morocco.


Shirikisho la kanda kanda barani Africa CAF linaendelea kuchambua ni nchi gani itakayookoa jahazi ya kuwa mwenyeji wa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2015 baada ya kuthibitisha Morocco kuondolewa rasmi kuandaa fainali hizo.
Nchi ya Morocco imeondolewa kutokana na kukataa kuwa mwenyeji ya mashindano hayo mwakani kwa hofu ya ugonjwa wa Ebola.
Mwandishi wa habari anasema fainali hizo zinaweza sasa kupelekwa Angola nchi iliyokuwa mwenyeji wa fainali hizo miaka minne iliyopita.
Nchi nyingine zinazodhaniwa kuweza kuandaa mashandano hayo ni Gabon na Nigeria. Shirikisho la kanda kanda barani Afrika linasema litatoa uamuzi ni nchi ipi itakayoandaa mashindano hayo haraka iwezekanavyo.

Lewis Hamilton atang'ara Abu Dhabi

                             Lewis Hamilton

Nguli wa zamani wa dunia wa mbio za magari Nigel Mansell amesema Lui Hamilton anayo nafasi moja iliyosalia kufanya vyema na kutinga fainali huko Abu Dhabi November 23.
Katika mahojiano maalumu na BBC Radio 5 Mansell anasema nafasi ya ushindi iko wazi mbele ya Lui na sasa ni uamuzi wake kuamua kushindwa ama kushinda!
Hamilton anaiongoza timu ya Mercedes kwa pointi 17, na nafasi ya kufanya maajabu anayo mikononi mwake.
Awali ni awali ,mwaka 1986 huko Australia kwenye
Mbio za Langa langa zilishuhudia William akiukosa ushindi hivi hivi baada ya kupata pancha . lakini yeye anasema hana tofauti na bata, mzoefu wa kupata,!
Alisahau maumivu ya tairi kukosa upepo na kuukosa ushindi pale alipojiona ana bahati ya mtende kuota jangwani baada ya kupata tuzo ya Sports Personality of the Year zitolewazo na BBC kakosa huku kapata kule!
Kama wewe ni shabiki sugu wa michezo!Tuzo hizo zimewadia tena ingia katika mtandao wa BBCSWAHILI.COM utapata maelekezo ya namna ya kupiga kura kumchagua mchezaji umtakaye, akwae tuzo hiyo ya BBC SPORTS PERSONALITY OF THE YEAR, na Mshindi atatangazwa baadaye mwezi ujao kazi kwako

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI

.
.
.
.

MRISHO NGASSA AJITOA TAIFA STARS, KISA…


Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI Mrisho Khalfan Ngassa hajasafiri na kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, kilichoondoka alfajiri ya leo kwenda Afrika Kusini kuweka kambi ya siku mbili kabla ya kwenda Swaziland Novemba 13, mwaka huu.
Ngassa aliomba ruhusa baada ya kuorodheshwa kwenye kikosi cha Mholanzi, Mart Nooij cha wachezaji 24 kwa ajili ya mechi ya kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) dhidi ya Swaziland itakayochezwa Novemba 16, mwaka huu mjini Mbabane.
Ngassa ametoa ‘udhuru’ wa matatizo ya kifamilia na Mholanzi huyo amemuelewa na kumuacha safarini.

Wachezaji wengine walioitwa kwenye kikosi hicho ni makipa Aishi Manula (Azam) na Deogratias Munishi (Yanga). Mabeki ni Abubakar Mtiro (Kagera Sugar), Aggrey Morris (Azam), Emmanuel Simwanda (African Lyon), Hassan Isihaka (Simba), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Osacr Joshua (Yanga), Said Moradi (Azam), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) na Shomari Kapombe (Azam).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Haruna Chanongo (Simba), Himid Mao (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Said Ndemla (Simba) na Salum Abubakar (Azam).
Washambuliaji ni Juma Luizio (ZESCO, Zambia), Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR Congo).
Mara ya mwisho, Stars iliifunga 4-1 Benin katika mchezo wa kirafiki unaotambuliwa na FIFA pia, Oktoba 12, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
11

VAN PERSIE KUIKOSA MECHI YA UHOLANZI NA MEXICO LEO

MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Robin van Persie ataikosa mechi ya kirafiki ya kimataifa baina ya nchi yake, Uholanzi dhidi ya Mexico Jumatano ya leo baada ya kocha Guus Hiddink kuthibitisha hayuko fiti kiasi cha kutosha.

Van Persie akiwa Nahodha wa Uholanzi, aliiongoza hadi nafasi ya tatu katika Fainali za Kombe la Dunia mwaka huu nchini Brazil, lakini kikosi cha Hiddink kimekuwa na wakati mgumu tangu baada ya michuano hiyo, kikishinda mchezo mmoja tu katika mechi zao tatu za awali za kufuzu kwa Euro.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31, ambaye alicheza dakika zote 90 klabu yake Man United ikimenyana na Crystal Palace mwishoni mwa wiki iliyopita, anaweza akarejea kwa wakati kuivaa Latvia Jumapili.
Robin van Persie leaves the Dutch training session with fitness coach Rene Wormhoudt on Tuesday
Robin van Persie akiondoka kwenye mazoezi ya Uholanzi na kocha wa mazoezi ya viungo, Rene Wormhoudt jana

HUU NI WAKATI WA RONALDO, ANGALIA ANAVYOZIDI KUTESA

Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amezidi kung’ara.Cheki alivyopokea tuzo yake ya mfungaji bora wa La Liga msimu uliopita maarufu kama Pichichi.
Halafu akapokea tuzo nyingine ya mchezaji bora wa La Liga maarufu kwa jina la Di Stefano. Kweli hiki ni kipindi chake.


WASHINDI:
TUZO YA PICHICHI
2009-10 Lionel Messi
2010-11 Cristiano Ronaldo 
2011-12 Lionel Messi
2012-13 Lionel Messi
2013-14 Cristiano Ronaldo 

TUZO YA DI STEFANO:
2009-10 Lionel Messi
2010-11 Lionel Messi
2011-12 Cristiano Ronaldo
2012-13 Cristiano Ronaldo
2013-14 Cristiano Ronaldo