Mchezo
wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Azam FC dhidi ya Mgambo
Shooting uliokuwa ufanyike kesho Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga sasa
nao umesogezwa hadi Jumamosi.
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) limeipatia tahfifu Yanga SC baada ya kuifutia
mchezo wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliokuwa uchezwe kesho
dhidi ya JKT Ruvu ili kuipa wasaa mzuri wa kujiandaa na Kombe la
Shirikisho Afrika. Yanga SC watakuwa wenyeji wa Platinum
FC Jumapili katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika
Raundi ya Kwanza, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kikosi
kizima cha timu hiyo kimeingia kambini leo katika hoteli ya Tansoma kwa
maandalizi ya mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa timu hiyo.
Yanga
SC iliitoa BDF XI ya Botswana katika Raundi ya Awali kwa jumla ya mabao
3-2, baada ya kushinda 2-0 nyumbani na kufungwa 2-1 ugenini. Mwishoni
mwa wiki, Yanga SC ilipoteza mchezo wake wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara mbele ya mahasimu wa jadi, Simba SC kwa kufungwa 1-0,
hivyo kupunguza idadi ya pointi wanazowazidi mabingwa watetezi, Azam FC
kutoka nne hadi moja (31-30). Ligi hiyo, inaendelea leo
Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, wenyeji timu ya Polisi Morogoro
watawakaribisha Ruvu Shooting kutoka Mlandizi mkoani Pwani. Mchezo
kati ya Azam FC dhidi ya Mgambo Shooting uliokuwa ufanyike kesho Uwanja
wa Mkwakwani mjini Tanga sasa nao umesogezwa hadi Jumamosi.