SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Mar 11, 2015

MO COLA KUMWAGA MAMILIONI SIMBA

Simba iko katika hatua za mwisho kumaliza dili la kuingia mkataba wa udhamini na Kampuni ya Mohammed Enterprises.

Taarifa zinasema kampuni hiyo kupitia kinywaji chake cha Mo Cola huenda ikatoa hadi Sh milioni 500 kwa Simba.
Hata hivyo haijajulikana kiasi hicho kitakuwa kwa ajili ya mkataba wa miaka mingapi.

SALEHJEMBE inaendelea kufuatilia juhudi hizo za uongozi wa Simba kuikamata Mo Cola.

FALCAO ASHUSHIWA TIMU B, NAKO ACHEMSHA VILE VILE NA ‘KUPIGWA MKEKA‘

MSHAMBULIAJI Radamel Falcao anayesuasua tangu asajiliwe kwa mkopo Manchester United, ameteremshwa kikosi cha pili, kinachojumuisha vijana wa umri wa miaka 21.
Falcao jana alianzishwa katika U21 ya Manchester United iliyolazimishwa sare ya 1-1 na Tottenham Hotspur Uwanja wa Old Trafford na pia alitolewa kipindi cha pili bila kufunga bao, ingawa alionekana kutofurahia wakati anaitwa benchi na kocha Warren Joyce.  
Katika mchezo huo ambao, wachezaji wengine wa Man United ‘A’ Rafael, James Wilson na kipa Victor Valdes walichezeshwa, makosa ya Joe Rothwell yalimpa Kenny McEvoy wa Spurs nafasi ya kufunga bao la kwanza.
Rafael akaisawazishia United akitumia makosa ya kipa na kufanya sare ya 1-1.
Falcao ambaye alikaa benchi bila kutumika juzi United ikilala 2-1 mbele ya Arsenal, analipwa Pauni 250,000 kwa wiki na United ina hiari ya kumnunua moja kwa moja kwa Pauni Milioni 43.2 mwishoni mwa msimu.
Kocha Louis van Gaal hajawahi kuwapeleka wachezaji timu ‘B’, labda wawe wanatoka kwenye maumivu.
Falcao heads the ball towards goal but his drought goes on after another unsuccessful outing
Falcao aliendelea kukosa mabao ya wazi jana akiichezea Man United 'B', hadi akatolewa kipindi cha pili

CANNAVARO ASHONWA NYUZI SABA

CANNAVARO BAADA YA KUSHONWA NYUZI SABA, AKIWA NA BAADHI YA WAUGUZI WALIOMHUDUMIA...
Beki ngangari wa kati wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amejiondoa kwenye kikosi hicho kitakachoivaa Platinum ya Zimbabwe.

Timu hiyo, inatarajiwa kuvaana na Platinum katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika wikiendi hii kwenye Uwanja wa Taifa.

Cannavaro alisema amejiondoa kwenye kikosi hicho baada ya kupasuka juu ya jicho la kushoto na kusababisha ashonwe nyuzi saba.
KUMRADHI KWA PICHA: CANNAVARO WAKATI AKISHONWA...

Cannavaro alisema, nyuzi hizo alishonwa juzi Jumatatu asubuhi kwenye Hospitali ya Kilwa Road, Kurasini jijini Dar mara baada ya mechi hiyo kumalizika.

Aliongeza kuwa, hataweza kucheza kutokana na maumivu makali anayoyasikia kwenye jeraha hilo, hivyo ameona ni vyema akapumzika hadi jeraha hilo litakapopona kabisa kwa hofu ya kujitonyesha.

“Ujue nilitumia ujasiri sana kusimama na kuendelea kucheza mechi na Simba mara baada ya kugongana na mchezaji wa Simba ambaye sijamjua ni nani na nilidhani nimepasuka padogo kumbe ni pakubwa.

“Niligundua nimepasuka pakubwa mara baada ya kwenda hospitali na kugundulika jeraha ni kubwa na kutakiwa kushonwa nyuzi saba juu ya jicho langu, nilinyanyuka kuendelea kucheza kutokana na mapenzi yangu na Yanga.


“Nilitamani kucheza mechi na Platnum, lakini kutokana na jeraha hili kiukweli sitaweza kucheza, nimeona nipumzike kwa kuhofia kujitonyesha, nyuzi saba ni nyingi sana, yaani nina maumivu mara mbili ya kukosa fedha za ahadi kama tukiifunga Simba na maumivu haya niliyoyapata,” alisema Cannavaro kwa masikitiko makubwa.

KALUSHA BWALYA APINGANA NA LUIS FIGO KUWANIA URAIS FIGO

FIGO...
Mwanasoka nguli wa Zambia, Kalusha Bwalya, amesema anaamini kuwa ni mapema sana kwa  Luis Figo kupambana na rais wa sasa wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Sepp Blatter.

Figo, 42, ambaye aliwahi kuwa mchezaji bora wa duniani ni mmoja kati ya wagombea watatu wanaotaka kuwania urais huo kwenye uchanguzi utakaofanyika Mei 29, mwaka huu.
 
BWALYA
"Luis Figo alikuwa mchezaji mzuri sana, mchezaji wa kiwango bora zaidi duniani nilikuwa nafurahi kila nikimwona na jezi ya Ureno.
“Nafikiri kwa mtazamo wangu ni jambo zuri yeye kugombea, lakini naona kama vile amekwenda kwenye nafasi kubwa sana, nafikiri haukuwa muda wake, amewahi sana,” alisema Bwalya ambaye ni rais wa Shirikisho la Soka la Zambia.
Figo alikuwa mmoja kati ya wachezaji mastaa wa Real Madrid wakati huo akiwa na kina Roberto Carlos, Ronaldo de Lima pamoja na  Zinedine Zidane. Bwalya yeye alikuwa mchezaji bora wa Afrika mwaka 1988.

HIZI NDIO COLLABO ZINAZO SUBILIWA KWA HAMU TZ

https://www.facebook.com/DJMWANGA?ref=ts&fref=tsWasanii wengi wa muziki wameonesha kutaka kuutumia vyema mwaka huu kwa kuachia project zao mpya za kimuziki huku wengi walikuwa kimya kwa muda mrefu na wengine tulikuwa bado tunaziskiza kazi zao!!
Kati ya hizo hizi ni mbili ambazo bado hazijatoka ila zitatoka ndani ya mwezi March..!!
******
Like · · · 53502

RONALDO AWAPIKU MESSI, RAUL KUFUNGA MABAO MENGI ULAYA, REAL IKITINGA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA

REAL Madrid imeitoa Schalke 04 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, licha ya kufungwa mabao 4-3 nyumbani, Uwanja wa Bernabeu.
Real inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-4, baada ya awali kushinda ugenini, Ujerumani mabao 2-0.
Mwanasoka Bora wa dunia, Cristiano Ronaldo jana alimpiku Lionel Messi na Raul katika chati ya wafungaji bora wa kihistoria michuano ya Ulaya baada ya kufunga mabao mawili katika dakika za 25 na 45. Mreno huyo sasa anafikisha mabao 78 katika michuano ya Ulaya, akimpiku Raul aliyefunga mabao 76 sawa na Messi.
Aidha, Ronaldo sasa anamfikia Messi katika chati ya wafungaji wa mabao mengi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, wote 75 kila mmoja, wakifuatiwa na Raul mabao 71, Ruud van Nistelrooy 56 na Thierry Henry 50.
Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo sasa ndiye mchezaji aliyefinga mabao mengi zaidi michuano ya Ulaya

ORODHA YA WAFUNGAJI BORA MICHUANO YA ULAYA

78: Cristiano Ronaldo (Sporting Lisbon, Manchester United, Real Madrid) 
77: Raul (Real Madrid, Schalke)
76: Lionel Messi (Barcelona)
70: Filippo Inzaghi (Parma, Juventus, AC Milan)
67: Andriy Shevchenko (Dynamo Kyiv, AC Milan, Chelsea)
62: Gerd Muller (Bayern Munich)
62: Ruud van Nistelrooy (Heerenveen, PSV Eindhoven, Manchester United, Real Madrid, Hamburger)
59: Thierry Henry (Monaco, Arsenal, Barcelona)
59: Henrik Larsson (Feyenoord, Celtic, Barcelona, Helsingborgs)
56: Eusebio (Benfica)

PICHA: HUYU NDIYE MWIGIZAJI ALIYE JICHORA TATOO YA MESSI

Mwigizaji Nataliya Kozhenova kutoka nchini Ukrain ameonyesha mapenzi yake waziwazi baada ya kuchora tatoo yenye sura ya mchezaji wa timu Barcelona nchini Hispania Leonel Messi
Ukrainian actress Nataliya Kozhenova has a tattoo of Lionel Messi on her chest

Ukrainian actress Nataliya Kozhenova has a tattoo of Lionel Messi on her chest

Ukrainian actress Nataliya Kozhenova has a tattoo of Lionel Messi on her chest

Ukrainian actress Nataliya Kozhenova has a tattoo of Lionel Messi on her chest

BEKI KATILI ARUDI NA MKOSI, ALAMBWA KADI NYEKUNDU MOROGORO


Beki George Michael maarufu kama “Beki katili” amerejea na mkosi baada ya ukumbana na kadi nyekundu.

Michael amechapwa kadi nyekundu wakati timu yake ya Ruvu Shooting ikiwa inapambana na Polisi Moro kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro na mechi ikaisha kwa sare ya 0-0.
Michael alikutana na adhabu hiyo kwa madai alimpiga kiwiko mchezaji wa Polisi ingawa Msemaji wa Shooting, Masau Bwire amepinga hilo.

Beki huyo alikutana na tafrani kubwa kwa mara ya kwanza baada ya kumkaba Amissi Tambwe wa Yanga na picha za tukio kunaswa na gazeti maarufu la michezo la Championi.

VAN GAAL ‘AMPA MAKAVU’ DI MARIA, ASEMA ALIIPONZA TIMU KUFUNGWA NA ARSENAL

KOCHA wa klabu ya Manchester United, Louis Van Gaal amemponda winga wake Angel Di Maria kwa kosa la kupata kadi nyekundu katika mchezo wa jana wa robo fainali kombe la FA dhidi ya washika bunduki Arsenal uliopigwa katika dimba la Old Trafford.
Winga huyo aliyevunja rekodi ya usajili nchini Uingereza alipata kadi nyekundu baada ya kupewa kadi ya njano ya pili kwa kumsukuma mwamuzi Michael Oliver huku akiwa na kadi ya njano ambayo aliipata muda huo huo kwa kosa la kujiangusha baada ya kukabwa na kiungo wa Arsenal, Aaron Ramsey.

Van Gaal alisema mchezaji huyo alikosa umakini mpaka akapata kadi hiyo ambayo ilipelekea kuongeza ugumu wa mchezo na kufanya Arsenal kuongeza kasi ya mashambulizi langoni kwa mashetani hao.
"Di Maria anajua kuwa mchezaji haruhusiwi kumshika mwamuzi lakini hakulijali hilo.Alikosa umakini katika hilo kwani nilizingumza kabla ya mchezo kwamba kupata kadi nyekundu katika mechi kama hii ni rahisi sana ila hajazingatia hilo. " alisema Van Gaal.
Pia kocha huyo amesema alisikitishwa na kiwango kilichooneshwa na timu yake katika mchezo huo na sasa nguvu zote anazielekeza katika kuwania nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa msimu ujao.
Katika mechi hiyo ya robo fainali Arsenal iliibuka na ushindi wa 2-1, magoli ya Arsenal yakifungwa na Nacho Monreal na Danny Welbeck huku la Mashetani hao likifungwa na nahodha wao Wayne Rooney.
Hii ni mara ya kwanza kwa washika bunduki hao wa jiji la London kuifunga Manchester United katika uwanja wa Old Trafford tangu wafanye hivyo mwaka 2006.
Baada ya kutinga hatua ya nusu fainali Arsenal watacheza na mshindi kati ya Bradford City na Reading ambao wanataraji kucheza mechi yao ya marudiano jumatatu ijayo baada ya kutoka sare ya 0-0 katika mechi ya kwanza.


MADRID YAFUZU ROBO FAINALI KIMTINDO, YACHAPWA BAO 4-3 NA SCHALKE NYUMBANI


Real Madrid wamefuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya lakini "kimkanda mkanda" baada ya kuchapwa mabao 4-3 na wageni wake Schalke 04.



Madrid imefungwa nyumbani baada ya ushindi wa mabao 2-0 ugenini nchini Ujerumani hivyo kufanya ifuzu kwa jumla ya mabao 5-4.

Mashabiki wake, waliwazomea wachezaji hao wakati wakiboronga na kufungwa na Madrid walifanikiwa kusawazisha mara tatu, lakini wakashindwa kufanya hivyo mara ya nne.

Mshambuliaji wake, Cristiano Ronaldo alifanikiwa kufunga mabao mawili, lakini akashindwa kuonyesha cheche kabisa.

Mashabiki walionyesha kutofurahia uchezaji wa timu hiyo ambao ndiyo mabingwa watetezi kufuzu kwa hofu.



SABABU KWA NINI DANNY MRWANDA HAJAINGIA KAMBINI YANGA SC BAADA YA KIPIGO CHA SIMBA JUMAPILI

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI Danny Mrwanda hajaingia kambini kwa maandalizi ya mchezo dhidi ya Platinum ya Zimbabwe, kwa sababu hatacheza siku hiyo, akiwa anatumikia adhabu yake ya kadi nyekundu, Yanga SC imesema.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, Mrwanda alipewa kadi nyekundu katika mchezo wa marudiano, Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho dhidi ya BDF XI nchini Botswana, hivyo hatacheza Jumapili.
Yanga SC itamenyana na BDF XI Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza, Raundi ya Kwanza Kombe la Shrikisho Afrika na siku hiyo, Mrwanda atakuwa jukwaani.
Danny Mrwanda (kushoto) akitafuta maarifa ya kumtoka Ramadhani Singano 'Messi' (kulia) katika mchezo wa Jumapili

Pamoja na hayo, Muro amesema Mrwanda amepewa ruhusa maalum ya kutokuwa kambini, kwa sababu mke wake ametoka kujifungua.
Kauli hiyo ya Muro- moja kwa moja inazima tetesi kwamba mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba SC amesimamishwa.
Uvumi umekuwa ukiendezwa leo katika kurasa mbalimbali za watu za mitandao ya kijamii, kwamba Mrwanda amesimamishwa kwa sababu alicheza chini ya kiwango Jumapili Yanga ikifungwa 1-0 na mahasimu, Simba SC.
“Huo uzushi wanaoueneza wana nia ya kutuvuruga, lakini sisi kama timu tuko vizuri na wachezaji wetu. Danny ana kadi nyekundu na kila mtu anajua alipewa kadi Botswana, maana yake hatacheza Jumapili. Sasa kwa nini tumlazimishe kuwa kambini?”amesema Muro.
Mrwanda aliikosesha Yanga SC bao la wazi dakika ya 28 siku hiyo, baada ya kupewa pasi nzuri na Simon Msuva, lakini akazubaa na mpira ndani ya boksi hadi akapokonywa na Juuko Murushid.
Tukio hilo lilimkera kocha Mholanzi wa Yanga SC, Hans van der Pluijm ambaye alimtoa mchezaji huyo dakika mbili baadaye na nafasi yake kuchukuliwa na Hussein Javu na kipindi cha pili, Emmanuel Okwi akaifungia bao pekee Simba SC la ushindi katika mchezo huo wa Ligi Kuu.