SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Mar 2, 2015

ALI KIBA AITABIRIA NGOMA YAKE MPYA

Embedded image permalink
Hit Maker wa Mwana ALI KIBA amesema kuwa ngoma yake Chekecha-Cheketua Itakuwa kali kuliko Mwana ambayo imefanya na Bado inafanya poa sana Afrika Mashariki.
Akipiga Stori na Kipindi cha DUNDO cha Mambo Jambo Radio Ali Kiba amepata kuyafunguka Hayo wakati akiwaweka sawa Mashabiki wake Maana halisi ya alichokiimba na kuwapanga Kuipokea Ngoma yake ambayo imetoka Rasmi  TAR. 27 February ambayo imefanywa Chini ya Studio za Chedaz Records na Producer Abby Daddy anaamini ni ngoma itayobamba zaidi kwani ana uhakika na mawe ambayo tayari ashayaweka kwenye manati tayari kwa ajili ya watu wake so mkae tayari.
Amesema Inatoka Audio kwanza then video itakuja soon..

AVEVA; SINA UGOMVI NA KABURU


1
Rais wa Simba, Evans Aveva
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam 
Rais wa Simba SC, Evans Aveva amesema kuwa ana maelewano mazuri na Makamu wa Rais wa klabu hiyo, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ na kwamba hana ugomvi wowote na kiongozi huyo wa wanamsimbazi.
Akizungumza katika mkutano mkuu wa wanachama wa Simba SC uliofanyika Ukumbi wa Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini hapa leo, Aveva amesema kuna taarifa zimekuwa zikielezwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba hana uhusiano mzuri na Kaburu, jambo ambalo amelikanusha vikali.
“Tumekuwa na matokeo mabovu na mwenendo wa kusuasua katika timu yetu. Ni matokeo mabaya ikilinganishwa na historia na jina la Simba Sports Club.
“Matokeo hayo yamekuwa yakiibua maswali mengi huku baadhi ya mitandao ya kijamii ikieleza kuwa mimi (Aveva) sina uhusiano mzuri na Kaburu.
“Ukweli ni kwamba mimi na Kaburu tunafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa, na si Kaburu tu, bali viongozi wote wa Simba SC. Hizi taarifa kwamba ni ugomvi na Kaburu si kweli,” amesema Kaburu.
Rais huyo pia ameeleza masuala mbalimbali yanayoihusu klabu hiyo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa uwanja, kuongeza idadi ya wanachama kwa kuleta mtambo maalum wa klabu kwa ajili ya kuchapisha kadi mpya za wanachama badala ya kuchapisha kwa watu binafsi ili kupunguza gharama.
Ukawa hawarudishwi Simba
Aveva amesema kuwa kamwe wanachama 72 waliofutiwa uanachama wa Simba SC hawatarudishwa kwa sababu walifukuzwa kwa mujibu wa katiba ya klabu hiyo ya Msimbazi jijini hapa.
Aveva amesema kuwarudisha kinyemela wanachama hao ni kukiuka misingi ya katiba kwani misingi ya katiba hiyo ilifuatwa wakati wa kuwafutia uanachama.

ZIPO HAPA KURASA ZA MWANZO ZA MAGAZETI YA MICHEZO LEO MACHI 2

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

YANGA SC KUKUTANA NA WAZIMBABWE KOMBE LA SHIRIKISHO


Na Vincent Malouda, ZVISHVAANE
VIGOGO wa ligi ya Tanzania bara, Yanga SC, watamenyana na klabu ya FC Platinum ya Zimbabwe katika raundi ya kwanza ya kombe la Shirikisho Afrika baada ya timu hiyo kuifumua Sofapaka FC ya Kenya na kusonga mbele kwa jumla ya magoli 4 – 2.
FC Platinum iliilaza Sofapaka 2 – 1 jana kwenye mechi ya mkondo wa pili iliyosakatwa alasiri ya leo katika uga wa Mandava mjini Zvishavane, Zimbabwe. Mshambulizi wa Sofapaka na Mburundi Fiston Abdoul Razak aliipa timu yake uongozi katika dakika ya nne lakini Wisdom Mtasa akazawazisha mambo baada ya robo saa.

Donald Ngoma wa Platinum (kushoto) amkimbiza Kevin Omondi wa Sofapaka

Timu zote zilipoteza nafasi za kuhesabika kabla ya refa wa katikati na Mbotswana Tirelo Mositwane kupuliza kipienga kuashiria mapumziko.
Katika kipindi cha lala salama, Mtasa alicheka na nyavu dakika ya 54 na kuua matumaini ya vijana wa kocha Mganda Sam Timbe kurejea mchezoni kwani walishindwa kufunga mabao manne ili kupenyeza awamu ijayo.
Platinum waliwazaba Sofapaka, maarufu kama Batoto ba Mungu 2 – 1 kwenye mkumbo wa kwanza uliyogaragazwa majuma mawili yaliyopita mjini Nairobi. Brian Muzondiwa na Donald Ngoma wakifunga katika mechi hiyo huku Fiston akisajili moja la kuvutia machozi.
Sofa sasa wanarejesha buti zao kutesa nyasi za nyumbani kwenye ligi kuu ya taifa, KPL, pindi tu mahakama itakaposikiza kesi iliyowasilishwa na kampuni inayosimamia ligi kuu kuhusu ombi la Shirikisho la Soka nchini, FKF, kusitisha ligi hiyo kuheshimiwa na kampuni hiyo ambapo hamna mechi zilizosakatwa katika ligi hiyo wikiendi hii.
Hayo yakijiri, ligi kuu ya FKF iliendelea siku ya jana mechi mbili zikipigwa katika viwanja tofauti. Bidco United iliwarambisha St. Joseph 3 – 0 sakafu katika uchanjaa wa Kaunti ya Thika, magoli ya Bidco yakifungwa na straika Hussein Puzzo, beki wa kushoto na mganda Patrick Senfuka na Simon Ng’ang’a dakika a 18, 54 na 78 mtawalia.
Katika uwanja wa Bukhungu mjini Kakamega, West Kenya iliandikisha ushindi wa 2 – 1 dhidi ya Kariobangi Sharks ya kutoka Nairobi. Peter Kihungi akiwazawidi West Kenya bao la kwanza kwa kujifunga kabla ya Johnson Indimuli na Rodgers Omondi kukamilisha mauaji.
Ligi hiyo inaendelea kesho Ligi Ndogo SC ikivaana na Modern Coast Rangers FC, FC Talanta na Finlays FC, zote ugani City, Nairobi. Zoo Kericho nyumbani baina ya Oserian FC kisha Agrochemicals FC ifunganye virago na Nairobi Stima kule Kisumu.

LIVERPOOL YAITANDIKA 2-1 MAN CIY ANFIELD

LIVERPOOL imeichapa mabao 2-1 Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa Anfield jioni ya leo.
Jordan Henderson aliifungia bao la kwanza Liverpool dakika ya 11 kwa shuti la umbali wa mita 20 baada ya kazi nzuri ya Steven Gerrard.
Edin Dzeko akafanikiwa kuisawazishia Man Cty dakika 15 baadaye, kabla ya Philippe Coutinho kuifungia bao la ushindi Liverpool dakika ya 75.
Kipigo hicho kinaifanya Man City ibaki na poitni zake 55 za mechi 27, wakati Liverpool imafikisha pointi 48 za mechi 27.
Kikosi cha Liverpool kilikuwa; Mignolet, Can, Skrtel, Lovren, Markovic/Sturridge dk76, Henderson, Allen, Moreno/KoloToure, Coutinho, Sterling na Adam Lallana.
Man City; Hart, Zabaleta, Kompany, Mangala, Kolarov, Nasri/Lampard dk83, Toure, Fernandinho/Bony dk78), Silva, Aguero, Dzeko na Milner dk58.
Coutinho is lost among a heap of his Liverpool team-mates as the Anfield side celebrate the Brazilian's winner against Manchester City
Coutinho akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kuikfungia bao Liberpool leoCoutinho leads the celebrations as Martin Skrtel and Joe Allen chase after him after his stunning winning strike 
 Henderson is mobbed by his Liverpool team-mates and Anfield boss Brendan Rodgers after his effort beat Hart all ends up
 

ARSENAL WAZINDUKA, WAICHAPA EVERTON 2-0

ARSENAL imezinduka kutoka kwenye kipigo cha Monaco Ligi ya Mabingwa, baada ya leo kuifunga mabao 2-0 Everton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Olivier Giroud alianza kufunga dakika ya 39 akimalizia pasi ya Mesut Ozil, kabla ya Tomas Rosicky kufunga la pili dakika ya 89.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger aliwatema kikosini Per Mertesacker baada ya kipigo cha Monaco.
Matokeo hayo, yanaifanya Arsenal itimize pointi 51 baada ya kucheza mechi 27, nyuma ya Manchester City yenye pointi 55 za mechi 27 na Chelsea pointi 60 za mechi 26.
Kikodi cha Arsenal; Ospina, Bellerin, Gabriel, Koscielny, Gibbs, Coquelin/Chambers dk89, Cazorla, Oxlade-Chamberlain/Rosicky dk82, Ozil, Alexis/Welbeck dk87 na Giroud.
Everton; Howard, Coleman, Jagielka, Stones, Garbutt, McCarthy, Besic/Naismith dk77, Barry/Gibson dk84, Mirallas/Lennon dk62, Barkley na Lukaku.
Giroud struggled in Arsenal's midweek defeat by Monaco but showed his delight at the Emirates after firing the Gunners in front
Giroud akishangilia baada ya kuifungia Arsenal leo

SIMBA SC WAENDA ZENJI KUIANDALIA DOZI YANGA SC

Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
KIKOSI cha Simba SC kimeondoka jana Dar es Salaam kwenda Zanzibar kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga SC Jumapili.
Simba SC ambayo juzi iliihadharisha Yanga SC baada ya kuitandika Prisons mabao 5-0 Uwanja wa Taifa, imekwenda Zanzibar kwa ajii ya maandalizi mazuri kama ilivyo ada yake unapowadia mchezo huo.
Zanzibar sasa ndiyo sehemu ambayo Simba SC wanaiamini zaidi kwa kambi za kujiandaa na mashindano mbalimbali na kuelekea mchezo wa Machi 8, 2015 wamerudi huko tena.
Kocha wa Simba SC, Goran Kopunovic akiwa mwenye furaha juzi timu yake ikishinda 5-0

Kocha Mserbia, Goran Kopunovic alikuwa mwenye furaha baada ya ushindi wa 5-0 dhidi ya Prisons Jumamosi Uwanja wa Taifa na akasema anaelekeza nguvu zake kwenye mchezo ujao.
Wakati Nahodha Joseph Owino amerejea kikosini, Waganda wenzake, Juuko Murushid na Simon Sserunkuma wamerejea kwao Uganda kwa matatizo ya kifamilia.
Lakini Simba SC inaonekana kuwa madhubuti hata bila ya Waganda hao wawili waliosajiliwa msimu huu.  
Upande wa pili, Mkutano Mkuu wa wanachama Jumapili ya jana ulirejesha hali shwari klabuni, kufuatia kuwapo taarifa kwamba Rais wa klabu, Evans Aveva ‘haivi’ na Makamu wake, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’.
Wawili hao wote walizungumza mbele ya wanachama wachache waliojitokeza mkutanoni kwamba hakuna tatizo baina yao na kuna mshikamano wa kutosha ndani ya uongozi.

CHELSEA NA MWALI WA CAPITAL ONE HAWA HAPA, MOURINHO AMWAGA CHOZI

WACHEZAJI NA KOCHA WA CHELSEA, JOSE MOURINHO WAKISHANGILIA BAADA YA KUTWAA UBINGWA WA CAPITAL ONE KWA KUITWANGA SPURS BAO 2-0.



MOURINHO ALISHINDWA KUJIZUIA, AKAMWAGA CHOZI.