SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Mar 9, 2015

KURASA ZA MWANZO ZA MWISHO MAGAZETI YA MICHEZO LEO MARCH 9

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

10 BORA YA WACHEZAJI WANAOONGOZA KUPIGA CHENGA NA KUTOA PASI BARANI ULAYA RONALDO HAYUPO HATA 20 BORA


messi26032014Naposema “kufanikiwa au kukamilisha chenga” namaanisha kuwa unampiga mtu au watu chenga halafu unafanikiwa kuumiliki mpira bila kupokonywa na kisha kumpasia mwingine au kufunga au kufanya vyovyote vile, Yaani unapiga chenga bila kupokonywa mpira, Sasa hapo nadhani umenipata kwa ufafanuzi huo ili usije kubakia ushangaa hapa. 
Sasa twende kazi…
Najua haujui ila nitakujuza hapa aisee…
Lionel Messi ndie mchezaji aliepiga chenga nyingi kwa mafanikio barani Ulaya kwa zaidi ya misimu miwili iliopita kuliko mchezaji yeyote.
Messi amepiga chenga 258 bila kupokonywa mpira, Kwa hiyo, Messi ndio top dribbler in Europe zaidi ya misimu miwili iliopita.
Eden Hazard wa Chelsea anafuatia kwa ukaribu zaidi akiwa amezidiwa chenga nne tu na Messi.  Hazard ana chenga 254.
Hazard ni mmoja kati ya wachezaji wawili kutoka kwenye Ligi Kuu ya Uingereza kuingia kwenye 10 bora hiyo.Eden Hazard
Mwingine ni Raheem Sterling wa Liverpool mwenye chenga 172 akishika nafasi ya nane.
Lakini katika hali ya kushangaza, mchezaji bora duniani Cristiano Ronaldo hayupo kwenye 10 bora hiyo na wala kwenye 20 bora ya waliopiga chenga na wakakamilisha chenga zao.
Cristiano Ronaldo yeye hajafikisha hata nusu ya chenga za Messi na Hazard kwa hiyo zaidi ya misimu miwili.
Cristiano amepiga chenga 99 kwa kipindi hicho zaidi ya misimu miwili, ambapo imemfanya kuwa nje ya 20 bora kwenye orodha iliotolewa.
Takwimu hizo zinaonyesha jinsi wachezaji wafupi kina Messi, Hazard na Sterling walivyo wachezaji hatari kwenye timu zao kama wachezeshaji wakubwa.
Na hapa ndipo wachezaji kutoka Ligi Kuu ya Ujerumani wanapotamba. Bundesliga imetoa wachezaji sita katika kumi bora ya wapiga vyenga bora barani Ulaya.
Hapa utawakuta kina Arjen Robben (172) na Frank Ribery (175) wote wa Bayern Munich.

Kuna winga Roberto Firmino (244) wa Hoffenheim, Raffael (222) wa Borussia Monchengladbach, Karim Bellarabi (206) wa Bayer Leverkusen, na Eric Choupo-Moting (200) wa Schalke 04.
Lucas Moura wa Paris Saint Germain (PSG) anafunga kumi bora akiwa amepiga chenga 167.
Hakuna mchezaji yeyote kutoka Ligi Kuu ya Italia alieingia kwenye kumi bora ya orodha hiyo.

PICHA; HIVI NDIVYO SIMBA VS YANGA ZILIZYOONYESHANA UBABE MSIMABAZI WAKIIBUKA KIDEDEA

SIMBA IMEIBUKA NA USHINDI WA BAO 1-0 DHIDI YA YANGA KATIKA MECHI YA LIGI KUU BARA KWENYE UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR, LEO. HIZI NI SEHEMU YA PICHA ZA PAMBANO HILO KAMA HII, 'MUUAJI' WA LEO, EMMANUEL OKWI ALIVYOKUWA AKIPAMBANA NA KELVIN YONDANI...


TAMBWE AKIPAMBANA NA JONAS MKUDE WA SIMBA...

KESSY WA SIMBA AKIMILIKI MPIRA MBELE YA JAVU WA YANGA, KUSHOTO NI NDEMLA WA SIMBA.

IVO MAPUNDA WA SIMBA AKIFANYA YAKE...

BEKI MGANDA WA SIMBA, JUUKO MURISHID AKILONGA NA MWAMUZI WA MECHI HIYO, MARTIN SAANYA...

TAMBWE AKIJARIBU KUWATOKA MESSI NA KESSY...

YONDANI WA YANGA AKIRUKA JUU KUMKWEPA KIPA WAKE ALLY MUSTAPHA HUKU MESSI WA SIMBA AKIANGALIA....


CANNAVARO WA YANGA AKIMWANGUKIA MESSI WA SIMBA,....


OKWI AKIJARIBU KUMTOKA CANNAVARO WA YANGA... 

ILIANZA YANGA B KUSHUGHULIKIWA, IMEPIGWA NNE NA SIMBA B

TIMU ya vijana ya Simba SC imewafunga wapinzani wao, Yanga SC mabao 4-2 katika mchezo uliofanyika mchana wa leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo huo wa utangulizi kabla ya timu za wakubwa za klabu hizo kumenyana katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ulishuhudiwa na maelfu ya wapenzi wa timu hizo waliowahi uwanjani.
Mabao ya Simba SC inayofundishwa na kiungo wa zamani wa klabu hiyo, Nico Kiondo yalifungwa na Ibrahim Suleiman dakika ya tatu, Issa Abdallah dakika ya 41 na 51 na Mbarak Yussuf dakika ya 72.
Kiungo wa Simba B, Mohammed Kijiko akipasua katikati ya wachezaji wa Yanga B leo Uwanja wa Taifa
Mohammed Kijiko akimtoka beki wa Yanga B, Issa Ngao 
James Msuva wa Simba B akimtoka beki wa Yanga B
Makocha wa Yanga B, Salvatory Edward kulia na Nsajigwa kushoto katia benchi lao leo

Mabao ya Yanga SC inayofundishwa na kiungo wake wa zamani, Salvatory Edward anayesaidiwa na beki wa zamani wa timu hiyo, Nsajigwa Shadrack yamefungwa na Amos dakika ya 57 na Sospeter dakika ya 72. 

LIVERPOOL YABANWA NYUMBANI KOMBE LA FA NA BLACKBURN ROVERS

Mario Balotelli came on in the second half for Liverpool but was unable to find a way through the Blackburn defence
Mshambuliaji wa Liverpool, Mario Balotelli akimtoka beki wa Blackburn Rovers, Conway katika mchezo wa Robo Fainali Kombe la FA usiku wa leo Uwanja wa Anfield. Timu hizo zilitoka sare ya 0-0 na sasa zitarudiana Uwanja wa Ewood Park kusaka timu timu ya kwenda Nusu Fainali.

BARCA YAPAA KILELENI LA LIGA BAADA YA KUIFUMUA VALLECANO 6-1, MESSI APIGA TATU, SUAREZ MBILI

BARCELONA imepanda kileleni mwa La Liga, baada ya ushindi mnono wa mabao 6-1 dhidi ya Rayo Vallecano jana jioni Uwanja wa Nou Camp.
Barca sasa inafikisha pointi 62, baada ya mechi 26, ikiishushia nafasi ya pili, Real Madrid yenye pointi 61, baada ya jana kufungwa 1-0 na Athletic Bilbao.
Luis Suarez alianza kuifungia Barca dakika ya sita, kabla ya Gerard Pique kufunga la pili dakika ya 49.
Barcelona walipata penalti na Tito akatolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kucheza rafu kwenye boksi.
Lionel Messi alipiga mara ya kwanza penalti akakosa, lakini refa akamuambia arudie ndipo akafunga dakika ya 56, kabla ya kufunga tena dakika za 63 na 68 kukamilisha hat-trick yake leo.
Alberto Bueno aliifungia bao la kufutia machozi Vallevano kwa penalti dakika ya 81 na Dani Alves akatolewa kwa kadi nyekundu kwa kucheza rafu iliyozaa penalti hiyo, kabla ya Suarez kuhitimisha ‘pati la mabao’ la Barca kwa bao la dakika ya 90.
Kikosi cha Barcelona kilikuwa: Bravo, Pique, Xavi, Pedro, Iniesta/Rafinha dk66, Suarez, Messi, Mascherano/Rakitic dk66, Alba/Adriano dk76, Alves na Mathieu.
Rayo Vallecano: Alvarez, Tito, Amaya, Ba, Insua, Trashorras, Lica/Aquino dk71, Jozabed/Quini dk66, Bueno, Kakuta, Baptistao/Manucho dk83.
Barcelona moved top of La Liga with their impressive win against 10-man Rayo Vallecano on Sunday
Luis Suarez amefunga mabao mawili katika ushindi wa 6-1 wa Barcelona dhidi ya Rayo Vallecano
 

HIVI NDIVYO KUPONOVIC ALIVYO SHANGILIA GOLI LA OKWI

Kocha wa Simba SC, Goran Kopunovic raia wa Serbia akishangilia bao la Emmanuel Okwi lililoipa timu yake ushindi wa 1-0 dhidi ya mahasimu, Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Anavuta kasi kurusha ngumi hewani
Tayari ameutandika upepo 'right-hook' ya maana, hizo ni furaha za bao la Okwi