SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Oct 16, 2015

BRENDAN RODGERS APATA KAZI MPYA BAADA YA KUFUKUZWA LIVERPOOL

rod
Ukishafanya kazi ya kuiongoza taasisi kubwa kama Liverpool mambo yako hayawezi kuwa mabaya hata kama umeachishwa kazi. Hivyo ndivyo imemtokea Brendan Rodgers ambae siku kadhaa zilizopita alifukuzwa kazi na club ya Liverpool na sasa hivi taarifa zimetoka kwamba ameshapata kazi mpya.
Kazi ya ukocha kwa sasa sio rahisi kwasababu club zote ndio kwanza zimeanza ligi na makocha wao. Kazi aliyopata Brendan Rodgers ni ya kuwa mchambuzi kwenye TV ya beIN Sports ya huko Qatar.
Rodgers anategemewa kuwa mmoja kati ya wachangiaji wa mechi za EPL ambazo zinaonyeshwa na channel hiyo aki ripoti kutoka kwenye studio zao huko Qatar. Mambo sio mabaya kwa Rodgers kwasababu warabu huwa hawana tabu kwenye swala la kuweka mzigo mzito kwa ajili ya watu wanaofanya kazi zao.

SIMBA SC WAILAUMU TFF WAMEJAA NA UYANGA

Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
KLABU ya Simba SC imelalamika kwamba, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) haliwatendei haki kwa sababu uongozi wake umesheheni watu wa Yanga SC.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE leo kwamba, imefikia TFF wamekata kabisa mawasiliano na klabu yao.
Poppe amesema kwamba TFF sasa hawajibu hata barua za Simba SC wanapoandika kuhoji au kuomba ufafanuzi wa jambo lolote.
Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) amesema kwamba imefikia wakati wanashindwa hata kujua namna gani wanaweza kupata haki zao nyingine za msingi, kutokana na ‘kuchuniwa’ na TFF.
Hans Poppe amesema TFF haiwatendeo haki kwa sababu viongozi wengi ni Yanga SC 

“Inafahamika kwamba Rais wa TFF (Jamal Malinzi), Katibu wake (Mwesigwa Selestine) wote ni Makatibu wa zamani wa mahasimu wetu, Yanga SC. Na bado wapo wengine wengi pale TFF ambao wametoka Yanga akina Baraka Kizuguto.
“Lakini kwa sababu wanaongoza chombo cha kitaifa, wanapaswa kutenda haki, yaani inaonekana kabisa TFF wanaikandamiza Simba na wanaibebea Yanga,”amelalamika Poppe.
Akifafanua, mfanyabiashara huyo maarufu nchini, amesema TFF hawajajibu barua yoyote ya Simba SC kwa mwaka huu na hawaelewei sababu ni nini.
“Watuonyeshe wao, ni barya ipi ya Simba SC wamejibu mwaka huu, malalamiko yetu ya mchezo dhidi Yanga hawakujibu, Suala la Messi (Ramadhani Singano) hawakujibu. Hata tunapojibu barua zao za adhabu wanazotuandika ili kuomba ufafanuzi, pia hawatujibu. 
“Labda watuambie basi kwamba barua zetu tunatakiwa kuzipitishia Yanga SC ndiyo watujibu, tutafanya hivyo, tutaandika na kuwapelekea Yanga waweke muhuri wao ipelekwe TFF, tujibiwe, hiyo ndiyo shida yetu,”amesema.
Hans Poppe amesema kwamba mchezaji wao Ramadhani Singano ‘Messi’ amehamishiwa Azam FC kinyume cha utaratibu na kila wapodai haki yao hawasikilizwi. “Mchezaji wa Yanga (Donald Ngoma) alimpiga kichwa mchezaji wetu (Hassan Kessy) na tukapeleka ushahidi wa picha za video, hakuchukuliwa hatua na wala hatukujibiwa,”. 
“Lakini Juma Nyosso (wa Mbeya City) alimdhalilisha John Bocco (wa Azam FC) akachukuliwa hatua baada ya saa 24 kwa ushahidi wa picha,”amesema.
Aidha, amesema kwamba Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), limeiamuru klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia iilipe Simba SC dola 300,000 za Kimarekani za manunuzi ya mshmbauliaji Emmanuel Okwi, lakini wanashindwa kufuatulia kwa sababu TFF haiwasikilizi tena.
“Kwa kweli tupo wakati mgumu mno, tunashindwa hata kuelewa tunacheza hii ligi kwa sababu gani, inaonekana tunawasindikiza watu ambao tayairi wameandaliwa kwa namna yoyote wawe mabingwa,”amesema

NIYONZIMA HATARINI KUIKOSA AZAM KESHO



Haruna Niyonzima akiwa na mkewe leo Kigali, Rwanda baada ya kufunga ndoa ya Kiserikali 
Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
UWEZEKANO wa kiungo Haruna Hakizimana Niyonzima kuichezea klabu yake, Yanga SC Jumamosi Dar es Salaam dhidi ya Azam FC ni mdogo.
Nahodha huyo wa Rwanda, amefunga ndoa na mkewe leo Kigali, baada ya kurejea kutoka Morocco kuichezea timu yake ya taifa.
Katibu wa Yanga SC, Dk. Jonas Tiboroha ameithibitishia BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE usiku huu kwamba, Niyonzima bado hajawasili.
“Niyonzima hajawasili, nadhani anaweza kuja kesho, kwa sababu walikuwa Morocco na timu yao ya taifa,”amesema Dk. Tiboroha.
Katibu huyo wa Yanga SC amesema mshambuliaji Mrundi, Amissi Tambwe amewasili tangu juzi na leo amefanya mazoezi na wenzake Uwanja wa Boko Veterani, Dar es Salaam.
Yanga SC imeweka kambi hoteli ya Kiromo, Bagamoyo mkoani Pwani na inafanya mazoezi, uwanja wa Boko Veterani nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam FC Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
Aidha, kiungo Mnyarwanda wa Azam FC, Jean Baptiste Mugiraneza naye pia hajarejea Dar es Salaam, hivyo yuko hatarini kuikosa mechi hiyo ya kukata na shoka.
Niyonzima akiwatoka wachezaji wa Azam FC, Erasto Nyoni (kulia) na Khamis Mcha (kushoto) katika moja ya mechi zilizopita kuzikutanisha timu hizo

BOBAN ATAMBA SIMBA ITAFIA SOKOINE KESHO


Na Mwandishi Wetu, Mbeya
Mbeya City inatarajiwa kuikaribisha Simba, kesho Jumamosi katika Ligi Kuu Bara lakini ujio wa kiungo Haruna Moshi ‘Boban’ umeongeza nguvu kwenye kikosi cha Mbeya City ambapo amesema anaamini timu yake itaibuka na ushindi.


Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu
 yake hiyo, jana kwenye Uwanja wa Sokoine, Boban alisema kwa 
jinsi alivyowaona wenzake katika muda mfupi, anaamini
 ushindi utapatikana.

“Hii imekuwa siku nzuri kwangu, nimegundua timu yetu ina
 kikosi bora, vijana wana vipaji na uwezo mkubwa wa kucheza
 soka, binafsi hili limenishangaza na kunipa imani kuwa Simba
 hawana nafasi kwetu Jumamosi, tutawafunga,” alisema Boban.

Wakati huohuo, mchezo huo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa 
kwenye Uwanja wa Sokoine, umesababisha kuwe na gumzo
 kubwa mkoani hapa, ambapo umekuwa ukizungumzwa katika
 vijiwe vingi vya soka.

Kutokana na hali hiyo, ulinzi ulikuwa mkali katika mazoezi ya Mbeya City ambayo ipo chini ya Kocha Meja Abdul Mingange.