SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Apr 8, 2015

AZAM FC WAUWEKA REHANI UBINGWA LIGI KUU, WALAZIMISHWA SARE 1-1 NA MBEYA CITRY

Frank Domayo wa Azam FC akifumua shuti katikati ya wachezaji wa Mbeya City leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam
MABINGWA watetezi, Azam FC wamekwaa kisiki nyumbani, baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Matokeo hayo yanawafanya Azam FC sasa wawe wanazidiwa pointi sita na vinara, Yanga SC wenye pointi 43 baada ya ushindi wa 8-0 dhidi ya Coastal Union leo.
Azam FC walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Kipre Michael Balou dakika ya 61 kwa shuti la umbali wa zaidi ya mita 25.
Haikuchukua muda mrefu, Mbeya City wakasawazisha kupitia kwa Raphael Alpha kwa penalti dakika ya 64, kufuatia Erasto Nyoni kumuangusha Deus Kaseke.
Baafa ya hapo, timu hizo zilishambuliana kwa zamani na kipyenga cha mwisho, hakuna timu iliyofanikiwa kupata bao zaidi.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, David Mwantika, Serge Wawa, Mudathir Yahaya, Himid Mao, Kipre Bolou/Gaudence Mwaikimba dk80, Frank Domayo/Amri Kiemba dk56, John Bocco na Brian Majwega/Farid Mussa dk74.
Mbeya City; Hannington Kalyesebula, Peter Richard, Hassan Mwasapili, Juma Nyosso, Christian Sembuli, Kenny Ally, Deus Kaseke/Hamad Kibopile dk84, Paul Nonga/Peter Mapunda dk70, Raphael Alpha, Themi Felix na Peter Mwilanzi.

TAMBWE APIGA NNE, SHERMAN AFUTA ‘MKOSI’ YANGA IKIUWA 8 - 0

Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
YANGA SC imezidi kujisogeza karibu na taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 8-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
Ushindi huo, unaifanya Yanga SC ifikishe pointi 43, baada ya kucheza mechi 20- ikifuatiwa na Azam FC, ambayo baada ya sare ya 1-1 na Mbeya City leo, inafikisha pointi 37, baada ya mechi 19. 
Mshambuliaji Mliberia, Kpah Sean Sherman ‘amefuta mkosi’ leo, akifunga bao moja na kutoa pasi za mabao matatu- wakati Mrundi Amisi Tambwe amepiga ‘hat trick’.
Amisi Tambwe aliifungia Yanga SC bao la kwanza dakika ya tisa, akimalizia pasi ya Sherman, baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na Oscar Joshua.
Amisi Tambwe amefunga manao manne Yanga ikishinda 8-0 leo dhidi ya Coastal Union Ligi Kuu 

Simon Msuva akaifungia Yanga SC bao la pili dakika ya 23 kwa shuti la mbali baada ya kupokea pasi ya Tambwe.
Dakika ya 34, Tambwe akaifungia Yanga SC bao la tatu akimalizia pasi ya Juma Abdul.  Tambwe tena akafunga bao lake la tatu katika mchezo wa leo na la nne kwa Yanga dakika ya 48, akimalizia pasi ya Sherman.
Sherman akaifungia Yanga SC bao la tano dakika ya 50 akimalizia pasi ya Tambwe. Mliberia huyo alimwaga machozi baada ya kufunga bao hilo na Mbuyu Twite akaenda kukipangusa kiatu chake kwa jezi yake. 
Msuva akaifungia Yanga SC bao la sita dakika ya 87 akimalizia pasi ya kichwa ya Tambwe. Msuva sasa ana mabao 13 katika Ligi Kuu akiwa anaongoza katika mbio za ufungaji bora, akifuatiwa na Didier kabumbangu wa Azam FC na Rashid Mandawa wa Kagera Sugar, wote wana mabao 10 kila moja.
Salum Telela akaifungia Yanga SC bao la saba dakika ya 88 kwa shuti kali akimalizia pasi ya Msuva, kabla ya Tambwe kufunga la nane dakika ya 90. 
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Oscar Joshua/Edward Charles dk77, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mbuyu Twite/Hassan Dilunga dk67, Salum Telela, Haruna Niyonzima, Amisi Tambwe, Kpah Sherman/Nizar Khalfan dk70 na Simon Msuva.
Coastal Union; Bakari Fikirini, Juma Hamad, Abdallah Mfuko, Yussuf Chuma, Bakari Mtama, Abdulhalim Humud, Mohamed Ally, Yahya Ayoub, Rajab Mohamed/Mohammed Shekuwe dk57, Ike Bright Obinna/Mohamed Mtindi dk64 na Rama Salim/Abbas Athuman dk46. 
Sherman amefuta mkosi kwa kutoa pasi za mabao matatu na kufunga bao moja

MECHI YA YANGA NA MBEYA CITY YAAHIRISHWA

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeingia katika majaribu ya kuivuruga tena ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara- na mchezo kati ya Yanga na Mbeya City Jumamosi wiki hii huenda usifanyike.
Mchezo huo unaweza kuahirishwa kupisha mchezo wa kirafiki wa wachezaji wa zamani wa Barcelona ya Hispania na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa ameiambia BIN ZUBEIRY asubuhi hii kwamba, kikao kinaendelea hivi sasa baina yao na waandajii wa mechi ya Barcelona na Taifa Stara wa zamani.  
Ligi Kuu inaendelea leo kwa mchezo kati ya Yanga na Coastal Union Uwanja wa Taifa

Kwa kuwa tayari magwiji wa Barcelona wamekwishaanza kutua Dar es Salaam na waandaaji wameingia gharama za matangazo ya mechi- wazi mchezo wa Yanga na Mbeya City Jumamosi hautakuwapo.
Badala yake, magwiji wa Barcelona wataingia uwanjani hapo kumenyana na Taifa Stars wa zamani.
Kwa sababu Jumapili pia, kuna mechi nyingine ya Ligi Kuu Uwanja wa Taifa, Simba SC watakuwa wanamenyana na Mgambo JKT ya Tanga.
Ligi Kuu inaendelea jioni ya leo kwa michezo miwili kati ya Yanga na Coastal Union Uwanja wa Taifa na Azam FC na Mbeya City Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

ILE ISHARA YA KUTULIZA, CHANONGO ASEMA ALIWATULIZA SIMBA


Kiungo mshambuliai wa timu ya Stand United, Haruna Chanongo, amewatuliza mashabiki wa Simba waliokuwa wakimzomea katika mchezo wa Stand United na Mtibwa Sugar baada ya kufanikiwa kuifungia timu yake bao pekee kwenye mchezo huo dhidi ya Mtibwa.

Mashabiki wengi wa Simba walikuwa jukwaani kwa kuwa kesho yake timu yao ilikuwa ikisubiri kupambana na Kagera Sugar.
Katika mchezo huo uliochezwa kwa siku mbili baada ya siku ya kwanza kuvunjika kutokana na mvua kubwa na kumalizika kesho yake, Chanongo alionyesha kiwango cha hali ya juu.
Hata hivyo, mashabiki hao ambao walikuwa wakizomea kila mchezaji huyo wa Simba aliyepelekwa Stand kwa mkopo alipogusa mpira, walinyamaza baada ya bao hilo.
Chanongo baada ya kufunga alikimbia kwenye jukwaani walilokaa na kuwaonyesha ishara ya mikono kuwa tulieni, hali iliyowafanya wawe wapole.
“Mimi sina ugomvi hata kidogo na Simba, nilishangaa kwa nini mashabiki wao walinizomea na kila mara nilikuwa nafikiria ni nini naweza kufanya ili niwatulize, nilipofunga ndiyo nikatumia ishara hiyo ya tulieni,” alisema Chanongo.

Aidha Chanongo amefafanua: “Mimi sijawakosea kitu mashabiki wa Simba lakini kitendo cha kunizomea kilinikosesha raha sana pale uwanjani na mimi nikajiuliza nifanye kitu gani ili waweze kunyamaza? Basi nilipofunga bao wakakaa kimya, hawakuzomea tena.”

ALICHOSEMA KAVUMBAGU KUHUSU USAJILI WAKE YANGA


Suala la usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Azam, Mrundi, Didier Kavumbagu, imechukua sura mpya baada ya kutoa kipindi cha muda wa mwezi mmoja ambapo ni sawa na siku 30, kabla hajajua kama atajiunga na Yanga ama la.

Kavumbagu ambaye amekuwa lulu katika kikosi cha Azam tangu atue msimu huu klabuni hapo akitokea Yanga, amekuwa akihusishwa mara kwa mara kurejea Jangwani, huku ikidaiwa kuwa tayari kuna mazungumzo ya siri kubwa yameanza baina yake na vigogo wa Yanga lakini yeye akasisitiza kutoa mwezi mmoja kabla ya kutangaza ameamua anakwenda wapi kwa ajili ya msimu ujao.

Mpaka sasa Kavumbagu amebakiza takriban miezi miwili ili kumaliza mkataba wake na Azam FC ambayo ilimsajili na kumpa mkataba wa mwaka mmoja.
Kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), mchezaji huyo kwa sasa anaruhusiwa kufanya mazungumzo na timu nyingine yoyote.
Kavumbagu amesema kuwa hilo suala la kutakiwa na Yanga amekuwa akilisikia lakini kwa sasa hawezi kulitolea sana ufafanuzi kwa kuwa bado anaendelea kutafakari na kisha baada ya kipindi cha mwezi mmoja kupita, atakuwa tayari ameshajua muelekeo wake na kila mmoja atafahamu kuwa atakuwa wapi msimu ujao.

Aidha, Kavumbagu aliyefunga mabao 10 mpaka sasa kwenye ligi akizidiwa moja na kinara Simon Msuva wa Yanga mwenye 11, ameongeza kuwa anaamini kipindi cha mwezi mmoja kinamtosha zaidi kuisaidia Azam katika kuubakiza ubingwa Chamazi kisha baada ya hapo na yeye ndiyo atageukia upande wa pili na kuangalia zaidi maslahi yake.

“Kwa sasa siwezi kuwa na jibu la moja kwa moja kuhusiana na Yanga au Azam kwa sababu bado kuna muda zaidi hapa katikati na baada ya mwezi mmoja nitakuwa tayari nimeshapata jibu kichwani kama nitabaki Azam au nitakwenda Yanga au sehemu nyingine.

“Kwa sasa nataka kutoa sana msaada kwa timu yangu ya Azam kuhakikisha tunautetea ubingwa msimu huu na kipindi cha mwezi mmoja kinatosha kabisa kufanya hivyo.

“Kwa sababu baada ya mwezi zitakuwa zimebaki kama mechi mbili kumalizika kwa ligi na kama ni nani anatwaa ubingwa itakuwa tayari imeanza kubainika, kwa hiyo na mimi sasa hapo naweza kuangalia mambo yangu ya msimu ujao kuona itakuwaje, niamini nachokwambia kwamba baada ya muda huo kila kitu kitakuwa wazi na hakutakuwa na maswali mengine tena,”  alisema Kavumbagu.

Pamoja na hayo lakini Yanga inaonekana kuwa na asilimia nyingi zaidi za kumrejesha mchezaji wao huyo waliyemsajili kwa mara ya kwanza msimu wa 2012/13 akitokea Atletico ya Burundi baada ya kocha wa timu hiyo, Hans van Der Pluijm, kukiri kuwa ‘target’ zake katika usajili huu ni kupata straika mwenye vigezo kama alivyonavyo Kavumbagu kwa ajili ya kukisaidia kikosi chake kwenye mapambano ya msimu ujao.

Hata hivyo, mbali na hayo, mashabiki wa Yanga pia wameonyesha hali ya kuhitaji huduma ya straika wao huyo baada ya kumueleza wazi kumtaka arudi nyumbani walipokutana naye jijini Tanga, Yanga ilipokuwa ikiumana na Mgambo Shooting na Azam ilipokwenda kucheza na Coastal Union.
Kwa upande mwingine Azam leo itapata pigo kwa kumkosa mshambuliaji wake huyo katika mchezo wao dhidi ya Mbeya City utakaopigwa kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar kutokana na kuwa na kadi tatu za njano.

KURASA ZA MAGAZETI YA MICHEZO LEO JUMATANO

DSC01077
DSC01078
DSC01079
DSC01080
DSC01081
DSC01082
DSC01083