SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Feb 1, 2015

MATOKEO KUTOKA NOU CAMP BARCELONA

Sasa ni  mapumziko  Barcelona 1 - 1 Villareal

GOOOOOOAAAAALLLLLL

Ivory coast 1 - 1 Algeria dakika ya 55

RUVUSHOOTING WANG'AA LIGI KUU BARA



 Ruvushootingi imeendeleza ubabe katika ligi kuu Tanzania bara baada ya kuifunga Stand United goli 2-1 katika uwanja wa mabatini uliopo Mlandizi Mkoani Pwani.
Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua, Ruvu walikuwa wa kwanza kufunga kupitia kwa Juma Nade dakika ya tano , kabla ya Khamisi Thabiti kusawazisha dakika ya 53.
Yahya Tumbo ndiye alie ihakikishia ushindi Ruvushooting katika Uwanja wa nyumbani baada ya kufunga goli la pili dakika ya 89

WATAKAO ANZA BARCELONA DHIDI YA VILLAREAL HAWA HAPA

KIKOSI CHA BARCELONA KITAKACHO ANZA LEO DHIDI YA VILLAREAL



Timu ya Barcelona imetoa kikosi chake cha kwanza kitakacho pambana na Villareal usiku huu.



 13 Bravo 

22 Alves 

3 Piqué 

14 Mascherano 

18 J.Alba 

5 Sergio

8 Iniesta 

12 Rafinha

 11 Neymar 

9 Suárez 

10 Messi

CHRISTIAN ATSU AIBEBA GHANA AFCON

Football - 2011ACQ - Ghana v Swaziland - Accra Sports Stadium

Michuano ya kombe la mataifa ya Afrika imeendelea hii leo kwa kushuhudia mchezo mmoja wa hatua ya robo fainali ukizikutanisha Ghana pamoja na Guinea .
Katika Mchezo huo Ghana walifanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali wakiwafunga Guinea kwa mabao matatu bila .
Ghana walianza kazi mapema wakifunga bao mapema kwenye dakika ya nne kupitia kwa winga Christian Atsu .
Black Stars walipata bao la pili kwenye kipindi cha kwanza mfungaji akiwa Kwessi Appiah bao ambalo liliua matumaini ya Guinea .
Mwanzoni mwa kipindi cha pili Ghana walifunga bao la tatu mfungaji akiwa Christian Atsu tena na kuikatia timu yake tiketi ya kufuzu hatua ya nusu fainali .
Nafasi ya mwisho kwenye hatua ya nusu fainali itafahamika saa chache zijazo wakati mchezo wa mwisho wa roo fainali utakaowakutanisha Ivory Coast na Algeria utakapopigwa .
Hadi sasa timu tatu tayari zimefuzu hatua ya nusu fainali nazo ni wenyeji Equatoarial Guinea , Ghana pamoja na Jamhuri ya kidemokrasi ya kongo .

DE GEA MGUU NDANI MGUU NJE MAN UNITED

David-De-Gea-of-Manchester-United-gestures

Tetesi kuhusu mustakabali wa kipa Mhisapnia David De Gea ndani ya klabu ya Manchester United zimezidi kuibuka ambapo kila siku ameendelea kuhusishwa na kujiunga na mabingwa wa ulaya Real Madrid ambao wametajwa kuwa na mpango wa kumsajili kipa huyo .
Taarifa toka England na Hispania zinasema kuwa wawakilishi wa kipa huyo wanataka kuwepo na kipengele kinachoruhusu kipa huyo kuuzwa ndani ya mkataba mpya ambao anatarajiwa kuusaini .
De Gea amebakiza miezi 18 kabla ya kumaliza mkataba wake wa sasa na United na klabu hiyo imekuwa katika mkakakati wa kuhakikisha kipa huyo anasaini mkataba mpya ambao una maslahi yaliyoboreshwa tofauti na mkataba wake wa sasa .
United imemsajili kipa wa zamani wa Barcelona Victor Valdez ambaye huenda akawa mrithi wa David De Gea endapo atakimbilia Real Madrid.
United imemsajili kipa wa zamani wa Barcelona Victor Valdez ambaye huenda akawa mrithi wa David De Gea endapo atakimbilia Real Madrid.
Katika kuhakikisha kipa huyo anabaki United , timu hiyo imejiandaa kumfanya De Gea kuwa kipa anayelipwa fedha nyingi kuliko wote duniani kwa mshahara wa paundi laki mbili kwa wiki lakini wawakilishi wa kipa huyo wamekuwa kikwazo kwa harakati hizi za United .
De Gea kwa mbali amekuwa mchezaji bora kwa timu yake ambapo kwenye michezo kadhaa amekuwa akiikoa huku akionyesha kiwango cha juu hali ambayo imemfanya atajwe kuwa moja ya makipa bora duniani .
Real Madrid kwa muda mrefu wamekuwa na shauku ya kumsajili Mhispania huyu ambaye kwa upande mwingine ameonyesha dhamira ya kurudi nyumbani kwao jijini Madrid .
Kitendo cha United kumsajili kipa wa zamani wa Barcelona Victor Valdez kimeongeza fununu za kuondoka kwa De Gea na mpaka sasa bado uongozi wa United unahaha kuhakikisha unambakiza kipa huyo

YANGA YABANWA NA NDANDA LEO TAIFA



yanga

Ligi kuu ya soka Tanzania Bara imeendelea hii leo kwa michezo miwili iliyopigwa jijini Dar-es-salaam pamoja na huko mkoani pwani ambako timu nne zilikuwa viwanjani zikisaka pointi tatu muhimu .
Jijini Dar-es-salaam uwnaja wa taifa ulishuhudia mchezo kati ya mabingwa wa zamani wa ligi hiyo Dar-es-slaam Young Africans dhidi ya timu iliyopanda daraja msimu huu ya Ndanda Fc toka Mtwara .
Mpaka kipenga cha mwisho kinapulizwa kuashiria mchezo huo kumalizika hakukuwa na timu iliyoweza kumtambia mwenzie baada ya timu hizo mbili kutoka sare ya bila kufungana .
Hata hivyo Yanga watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kuondoka na ushindi baada ya kutengeneza nafasi kadhaa za wazi ambazo kama washambuliaji wake wangekuwa makini basi Yanga ingeweza kushinda .
 Yanga Sc Vs Ndanda FC imemalizika. Matokeo na Pichaz nimekusogezea hapa…
Katika mchezo mwingine uliopigwa huko mkoani Pwani kwenye uwanja wa Mabatini wenyeji Ruvu Shooting waliwafunga Stand United kwa mabao mawili kwa moja .
Ruvu   Shooting walifunga mabao yao kupitia kwa Juma Mpakala kwenye dakika ya tano ya mchezo huku bao la ushindi likija kupitia kwa Yahya Tumbo kwneye dakika ya 89 na Stand United wakafunga kupitia kwa Hamis Thabit .
Matokeo ya michezo ya leo yanawafanya Yanga washindwe kuwafikia Azam Fc kwenye kilele cha msimamo wa ligi ya Tanzania Bara ambapo hadi sasa wana pointi 19 wakiwa wamezidiwa kwa pointi mbili na Azam wenye pointi 21 .

ARSENAL WAFANYA MAUAJI KWENYE EPL

ARSENAL

Washika bunduki toka jijini London Arsenal hii leo (jumapili) wamefanikiwa kuwafunga Aston Villa kwa ushindi mnono wa 5-0 katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Emirates katika muendelezo wa ligi kuu ya England .
Arsenal walianza mchezo huo kwa kasi wakifunga bao la haraka kwenye dakika ya 8 mfungaji akiwa mshambuliaji raia wa Ufaransa Olivier Giroud baada ya pasi ya beki Per Mertersecker .
Arsenal walifunga bao la pili kupitia kwa kiungo mshambuliaji Mesut Ozil ambaye alipokea pasi ya Giroud na kuukokota mpira kabla ya kupiga shuti dogo lililompita kipa wa Aston Villa Brad Guzan .

Theo Walcott aliifungia Arsenal bao la tatu kwenye dakika ya 63 baada ya kupewa pasi na Santi Cazorla ambaye alikuwa moja kati ya wachezaji waliong’aa katika mchezo wa leo .
Bao la nne lilifungwa kwa njia ya penati baada ya kipa wa Aston Villa Brad Guxzan kumchezea vibaya mshambuliaji chipukizi Chupa Akpom , Santi Cazorla alipiga penati hiyo na kuipa timu yake bao linguine huku Aston Villa wakiendelea kupata wakati mgumu .
Theo Walcott alifunga bao la pili kwenye mchezo dhidi ya Aston Villa.
Theo Walcott alifunga bao la tatu kwenye mchezo dhidi ya Aston Villa.
Wakati mchezo ukielekea mwishoni , beki wa kushoto Hector Bellerin alifunga karamu ya mabao baada ya kuipa Arsenal bao la tano .
Ushindi huu unawafanya Arsenal kushupa hadi nafasi ya tano wakiwa na pointi 42 , pointi moja nyuma ya Man United walioko kwenye nafasi ya nne .

BREAKING NEWS;

WAPENDWA WASOMAJI, BLOG HII ITA BADILISHWA JINA NA SASA UTAIPATA KUPITIA WWW.HAJIBALOU.BLOGSPORT.COM TUNAOMBA RADHI KWA USUMBUFU UTAKAO JITOKEZA.

FULL TIME; ARSENAL RAHA TUPU

Arsenal imeibuka na ushindi wa goli 5-0 dhid ya Aston Villa

KUTOKA EMIRATES ; GOOOOAAALLL

Arsenal 4-0 Aston Villa  dakika ya 76

KUTOKA TAIFA FULL TIME

Yanga     0-0    Ndanda Fc

LINEX AMEANZA KUSHOOT VIDEO YAKE MPYA ALIYO MSHIRIKISHA DIAMOND TAZAMA PICHA HAPA

.
.
Diamond Platnumz na Linex Jan 31, waliingia location kutengeneza video ya wimbo wao mpya uitwayo Salima.Video hiyo mpya iliyotengenezwa kijijini imeongozwa na director Adam Juma.
Hizi ni baadhi ya picha za utengenezaji wa video hiyo mpya.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC_0147
.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC_0069
.
DSC_0104
.
.
.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Huyu ndie mrembo aliyevaa uhusika wa Salim.
.
.
.
.
DSC_0259

MATOKEO KUTOKA EMIRATES

Arsenal  1 -0 Aston villa dakika ya 39

KISIGA AJITOA SIMBA

Kiungo mshambuliaji wa Simba Shabani Kisiga "Malone" amejitoa katika klabu ya Simba Sc kwa sababu ambazo bado hajaziweka  wazi .
Kisiga alibeba vitu vyake baada ya kuisha mechi ya Mbeya City jumatano Uwanja wa Taifa na kuwaambia wenzake kama anaondoka na azima simu zake zote ili akipigiwa asipatikane.
Katika mchezo huo Simba alilala kwa goli 2-1 Kisiga aliingia kipindi cha pili akitokea benchi.Sikuzote kisiga anatokea benchi na kubadili mchezo lakini jumatano alishindwa kuisaidia timu yake na kuepuka kipigo kutoka kwa Mbeya City.

l

ALICHOSEMA BEN POL KUHUSU NYIMBO YA SOPHIA

 Star wa muziki wa R&B hapa Bongo, Ben Pol ametoa ya moyoni kuwa kwa namna flani, ngoma yake mpya ya SOPHIA ni rekodi ambayo ameifanya maalum kwaajili ya mtu wake wa karibu sana.


 

Ben Pol
Pol amesema kuwa mambo yakifanikiwa kuwa rasmi atamuweka wazi kwa watanzania ili wajue.
Ben ambaye katika ngoma hii ndani yake pia ameelezea uzuri wa mji wa Dodoma ambapo ndipo anapotokea, amesema kuwa ana imani mambo yatakuwa vizuri hapo baadaye kwaajili ya kumleta mwanadada huyo mbele ya mashabiki zake, ikiwa sasa mambo yao yanaendelea chini ya kapeti tu.

SIMBA YA PIGWA FAINI YA SH MILIONI 3


Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeipiga klabu ya Simba faini ya sh. milioni tatu kutokana na timu yake kuvaa jezi ambazo hazikuwa na nembo ya mdhamini wa Ligi Kuu, kampuni ya Vodacom wakati wa mechi yao dhidi ya Kagera Sugar.

Mechi hiyo namba 50 ya Ligi Kuu ya Vodacom ilichezwa Desemba 26 mwaka jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 13(7) ya Ligi Kuu inayotaka klabu kuheshimu masharti ya udhamini wa Ligi Kuu kwenye mechi zake.
Nayo Polisi Tabora imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa mujibu wa kanuni ya 28(4) kwa kusababisha mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kati yake na Toto Africans iliyochezwa Januari 14 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kuvurugika.

Kutokana na mchezo huo kuvurugika, Toto Africans imepewa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu. Uamuzi huo umefanywa kwa kuzingatia kanuni ya 28(1) inayotawala ligi hiyo.

PLUIJIM ATAKA YANGA WAFUTE MAKOSA LEO TAIFA


https://encrypted-tbn2.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcTzfVZWSloHuX7jesy8LIVqg7xlQkLEMfFR3YBSNoDzAjR-aQG7
 
Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema mechi ya leo dhidi ya Ndanda ni sahihi kwao kujirekebisha na kuyafanyia kazi waliyojifunza kwa zaidi ya siku 7.


Yanga inaikaribisha Ndanda FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, leo.

Pluijm raia wa Uholanzi amesema ni wakati mwafaka kuyafanyia kazi mambo walioyokosea katika mechi iliyopita.

"Ushindi ndiyo jambo muhimu, lakini hatuwezi kushinda kama hatujayafanyia marekebisho matatizo yetu.

"Ninaamini wachezaji watafanya hivyo na itakuwa njia ya kuendelea kufanya vizuri zaidi," alisema.

Pluijm amesema anaamini ana kikosi kizuri kinachoweza kuifumua Ndanda lakini lazima nafasi zitakazopatikana zitumiwe kwa asilimia angalau 70.

Yanga imekuwa ikiongoza kwa kutengeneza nafasi nyingi, pia kupoteza nyingi katika Ligi Kuu Bara.

HII NDIO ZAWADI ALIYOPEWA KOCHA WA SIMBA



Mabao mawili aliyofunga Danny Sserunkuma wakati Simba ikiimaliza Ruvu JKT kwa mabao 2-1 leo, amezawadiwa Kocha Goran Kopunovic.

Wachezaji Simba wameamua kumzadia kocha huyo mabao hayo kwa kuwa leo ni siku yake ya kuzaliwa, anafikisha miaka 48.
Kabla ya mchezo huo, Kopunovic aliwaomba wachezaji hao kumzawadia kitu kizuri kwa ajili ya sikukuu yake ya kuzaliwa.
“Kweli kocha aliwaambia anaomba msaada wao, aliwaambia angependa kusherekea siku yake ya kuzaliwa akiwa na amani.
“Hivyo aliwaomba kuifunga Ruvu JKT ili Wanasimba wafurahi naye awe na amani hiyo kesho.

“Kweli utaona wachezaji wamejituma sana licha ya mechi kubwa ngumu na mwisho wamefanikiwa kushinda na baada ya hapo wamemzawadia mabao hayo mawili ya Sserunkuma,” kilieleza chanzo.

Huo ni mchezo wa tatu wa Kopunovic akiwa na Simba katika Ligi Kuu Bara na amefanikiwa kushinda mechi mbili na kupoteza mmoja.

MSIMAMO LIGI KUU ENGLAND

                                           BAADA YA MECHI ZA JANA

                         Premier League

Pos
Team P               W               D              L          GS GA         +/-              Pts
1 Chelsea FC Chelsea 23 16 5 2 52  20 +32 53
2 Manchester City FC Manchester City 23 14 6 3 46 23 +23 48
3 Manchester United FC Manchester United 23 12 7 4 39 22 +17 43
4 Southampton FC Southampton 22 13 3 6 37 16 +21 42
5 Tottenham Hotspur FC Tottenham Hotspur 23 12 4 7 35 30 +5 40
6 Arsenal FC Arsenal 22 11 6 5 39 25 +14 39
7 Liverpool FC Liverpool 23 11 5 7 33 27 +6 38
8 West Ham United FC West Ham United 23 10 6 7 35 27 +8 36
9 Stoke City FC Stoke City 23 9 5 9 26 28 -2 32
10 Swansea City AFC Swansea City 22 8 6 8 26 30 -4 30
11 Newcastle United FC Newcastle United 23 8 6 9 29 35 -6 30
12 Everton FC Everton 23 6 8 9 31 34 -3 26
13 Crystal Palace FC Crystal Palace 23 5 8 10 25 34 -9 23
14 Sunderland AFC Sunderland 23 4 11 8 21 33 -12 23
15 West Bromwich Albion FC West Bromwich Albion 23 5 7 11 20 32 -12 22
16 Aston Villa FC Aston Villa 22 5 7 10 11 25 -14 22
17 Burnley FC Burnley 23 4 8 11 21 38 -17 20
18 Hull City AFC Hull City 23 4 7 12 20 33 -13 19
19 Queens Park Rangers FC Queens Park Rangers 23 5 4 14 24 42 -18 19
20 Leicester City FC Leicester City 23 4 5 14 21 37 -16 17