SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Mar 31, 2015

YAYA TOURE AFIKIRIA KUIVUA 'KIMOJA' JEZI YA IVORY COAST

KIUNGO Yaya Toure amesema anafikiria kustaafu soka ya kimataifa baada ya kutimiza malengo yake.
Toure aliiongoza nchi yake kama Nahodha kutwaa Kombe la Mataifa ya Afrika, hilo likiwa taji la kwanza kubwa baada ya zaidi ya miongo miwili na sasa anaweza kufuata nyayo za kaka yake, Kolo kuvua jezi Ivory Coast.
Toure amesema atachukua siku kadhaa kuamua mustakabali wake, lakini amependekeza, kizazi kipya sasa lazima kipewe nafasi kikosi cha Tembo.
Toure was in action during the draw with Equatorial Guinea in Abidjan, Ivory Coast, on Sunday 
Toure aliichezea Ivory Coast ikitoa sare na Equatorial Guinea mjini Abidjan Jumapili katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa

"Mustakabali wangu?' aliuliza, alipoulizwa na BBC. "Inabidi usubiri. Sasa, malengo yangu yametimia. Tunapaswa kusubiri kwa siku kadhaa na kuona tutafanya nini,".
"Kaka yangu amestaafu, na Copa (Barry, kipa wa muda mrefu wa Ivory Coast) naye pia. Muda wa nyota wanaochipukia utafika karibuni. Tunahitaji kuwaachia wao.
Maneno haya ya Toure yanaweza kuwa habari njema kwa klabu yake, Manchseter City, ambayo ilikuwa katika wakati mgumu kwa kumkosa mchezaji huyo alipokuwa kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika nchini Equatorial Guinea.

DI MARIA AONGOZA MAUZO YA JEZI ENGLAND

HIZI ni habari njema ambazo zinaweza kumfariji Angel di Maria.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Argentina amekuwa ana msimu mgumu Manchester United uwanjani, lakini kiwango chake hakijaathiri umaarufu wake nje ya Uwanja kutokana na jezi kuongoza kwa mauzo katika Ligi Kuu ya England.
Kwa mujibu wa muuzaji wa reja reja wa duka la Sports Direct, ambaye anauza jezi za timu za Arsenal, Aston Villa, Chelsea, Liverpool, United, Manchester City, Tottenham na Newcastle, jezi ya Di Maria inauliziwa na mtu mmoja karibu katika kila wanunua jezi tofauti 10. 
Manchester United's record summer signing Angel di Maria tops the list of SportsDirect player shirt sales 
Mchezaji ghali wa Manchester United, Angel di Maria anaongoza kwa kuuza jezi katika orodha ya SportsDirect
Di Maria, Sanchez and Costa make up with top three with a combined share of 15.66 per cent
Di Maria, Sanchez na Costa ndio wamo kwenye tatu bora wote kwa pamoja wakiwa na asilimia 15.66

Jumla ya asilimia yake ni 9.59 ambayo inamfanya aongoze sokoni, akifuatiwa na nyota wa Arsenal, Alexis Sanchez, mchezaji huyo wa Chile akiwa nafasi ya pili kwa asilimia 3.8.
Di Maria amekuwa katika wakati mgumu uwanjani tangu asajiliwe kwa dau la Pauni Milioni 59.7 kutoka Real Madrid.

Mar 30, 2015

YANGA YAKODI 'MWEWE' WA SERIKALI KUWAFUATA WAZIMBABWE KOMBE LA SHIRIKISHO

MOJA YA NDEGE ZINAZOMILIKIWA NA SERIKALI YA TANZANIA.
Yanga inatarajiwa kwenda Zimbabwe Ijumaa, tayari kuivaa FC Platinum.

Kikosi cha Yanga kinatarajia kufanya safari yao ya Zimbabwe kwa kutumia ndege ya serikali.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya Yanga zimeeleza timu hiyo itasafiri na ndege hiyo baada ya Yanga kufanikiwa kupata kibali.

Uamuzi wa kupanda ndege ya serikali ni kupunguza gharama lakini pia uhakika kuepuka kutumia ndege za kawaida za abiria na kuwapa nafasi wenyeji wao kupanga mipango ya kuiangamiza.

Yanga inashuka dimbani dhidi ya Plutinum Jumamosi ikiwa ugenini baada ya kushinda mabao 5-1 katika mechi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho.

“Kweli, uongozi wa juu unaendelea kushughulikia suala la safari na tayari upande wa serikali umekubali kuikodisha ndege yetu,” kilieleza chanzo cha uhakika.


Yanga inahitaji sare ya aina yoyote ili kusonga mbele na ikifanikiwa itakutana kati ya Etoile du Sahel ya Tunisia au Benfica kutoka Angola.

Mar 26, 2015

MESSI NDIYE MWANASOKA 'MKUNJA MKWANJA MNENE' DUNIA NZIMA, MOURNHO ATISHA KWA MAKOCHA

MSHAMBULIAJI wa Bracelona, Lionel Messi ndiye mchezaji anayelipwa zaidi kwa sasa duniani, akiwa anaingiza karibu Pauni Milioni 1 kwa wiki kutokana na mshahara na mikataba ya udhamini.
Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina aliingiza pauni Milioni 47.8 mwaka 2014 za udhamini pamoja na mshahara wa klabu yake, Pauni Milioni 26.
Miongoni mwa wadhamini wa Messi ni Adidas, FIFA 15 na Turkish Airlines na hiyo inampandisha juu ya Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Ureno. Mreno huyo, Ronaldo, aliingiza Pauni Milioni 39.7, kwa mujibu wa taarifa zilizotoka sasa za Jarida la Wanasoka Tajiri.
Kwa upande wa makocha, Mreno Jose Mourinho wa Chelsea ndiye anaongoza pato lake la mwaka likiwa ni Pauni Milioni 13.2, akifuatiwa na Mtaliano wa Real Madrid, Carlo Ancelotti Pauni Milioni 11.4, Mspanyola wa Bayern Munich, Pep Guardiola Pauni Milioni 11.2, Mfaransa wa Arsenal, Arsene Wenger Pauni Milioni 8.3 na Mholanzi wa Manchester United, Louis van Gaal Pauni Milioni 7.3.
Messi tops up his salary with Barcelona by promoting various companies, including adidas 
Lionel Messi anaongoza kwa utajiri miongoni mwa wanasoka duniani  
Cristiano Ronaldo comes in second in the annual France Football list with earnings of £39.7m
Cristiano Ronaldo anashika nafasi ya pili kwa Pauni zake Milioni 39.7

WACHEZAJI WANAOLIPWA ZAIDI DUNIANI 

1. Lionel Messi Pauni Milioni 47.8
2. Cristiano Ronaldo Pauni Milioni 39.7
3. Neymar Pauni Milioni 26.8
4. Thiago Silva Pauni Milioni 20.2
5. Robin van Persie Pauni  Milioni 18.8
6. Gareth Bale Pauni Milioni 17.5
7. Wayne Rooney Pauni Milioni 16.5
8. Zlatan Ibrahimovic Pauni Milioni 15.8
9. Sergio Aguero Pauni Milioni 15.6
10. Robert Lewandowski Pauni Milioni 14.8 kwa mwaka 

MAKOCHA WANAOLIPWA ZAIDI DUNIANI 

1. Jose Mourinho Pauni  Milioni 13.2 kwa mwaka
2. Carlo Ancelotti Pauni Milioni 11.4
3. Pep Guardiola Pauni Milioni 11.2
4. Arsene Wenger Pauni Milioni 8.3
5. Louis van Gaal Pauni Milioni 7.3
6. Fabio Capello Pauni Milioni 6.6
7. Andre Villas-Boas Pauni Milioni 6.2
8. Sven-Goran Eriksson Pauni Milioni 5.9
9. Jurgen Klopp Pauni Milioni 5.3
10. David Moyes na Laurent Blanc Pauni Milioni 5.1 

Mar 25, 2015

MAGAZETI YA MICHEZO YA LEO MARCH 25 YAPO HAPA

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Mar 24, 2015

KURASA ZA MWANZO NA ZA MWISHO ZA MAGAZETI YA MICHEZO LEO MARCH 24 2015 ZIPO HAPA

.
.
.
.
DSC_0124
.
.

SAMATTA NA ULIMWENGU WAREJEA NYUMBANI JANA KUICHEZEA STARS DHIDI YA MALAWI MWANZA

Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
WASHAMBULIAJI wawili wa TP Mazembe ya DRC, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta watawasili usiku wa leo kwa ajili ya kujiunga na kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
Wawili hao wamo katika kikosi cha wachezaji 27 cha Stars kitakachoingia kambini leo kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Malawi utakaofanyika Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza Machi 29.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo asubuhi, Ulimwengu amesema wanatarajiwa kutua Dar es Salaam usiku kwa ajili ya majukumu ya kitaifa. “Tunatarajia kuwa Dar es Salaam usiku, tupo njiani hapa,”amesema. 
Samatta kushoto na Ulimwengu kulia watawasili usiku wa jana Dar es Salaam

Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, bia inayozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), inaingia kambini katika hoteli ya Tansoma kujiandaa na mchezo huo kabla ya kuelekea Mwanza machi 24 kwa maandalizi ya mwisho kabla ya mchezo.
Mbali na Samatta na Ulimwengu, wachezaji wengine walioitwa ni makipa Deo Munishi ‘Dida’ wa Yanga SC, Aishi Manula na Mwadini Ali, wote wa Azam FC, wakati mabeki ni Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Aggrey Morris (Azam FC), Mwinyi Haji (KMKM), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani, Nadir Haroub, Oscar Joshua (Yanga), Abdi Banda na Hassan Isihaka (Simba SC).
Viungo ni Frank Domayo, Salum Abubakar, Amri Kiemba, Mcha Khamis (Azam FC), Hassan Dilunga (Yanga), Said Ndemla (Simba), Haroun Chanongo (Stand United).
Washambuliaji Mwinyi Kazimoto (Al Markhiry - Qatar), Simon Msuva, Mrisho Ngassa (Yanga), John Bocco (Azam FC) na Juma Luizio (Zesco United - Zambia)
Malawi inatarajiwa kuwasili jijini Mwanza machi 27, 2015 ikiwa na kikosi kamili, wakiwemo wachezaji nane wanaocheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini, Msumbuji, Congo DR na Zimbambwe.
Malawi inashika nafasi ya 91 katika viwango vipya vya FIFA Duniani vilivyotolewa mwezi huu, huku Tanzania ikipanda kwa nafasi saba na kushika nafasi ya 100.

Mar 23, 2015

MALINZI AWAPONGEZA TWIGA STARS KUIADHIBU ZAMBIA

Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
RAIS wa Shrikisho la Mpira wa Miguu nchini –TF, Jamal Malinzi ametuma salama za pongezi kwa timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars) kwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya timu ya Taifa ya Zambia (The She-polopolo).
Katika salam zake Rais Malinzi amesema ushindi walioupata Twiga Stars katika mchezo huo wa awali, umetokana na maandalizi mazuri waliyoyapata chini ya kocha mkuu Rogasian Kaijage, benchi lake la ufundi na TFF.
Aidha Rais amewataka Twiga Stars kutobweteka kwa ushindi huo wa awali walioupata, bali wanapaswa kujiandaa vizuri zaidi kwa ajili ya mchezo wa marudiano ili waweze kupata ushindi na kuipeperusha vuzuri bendera ya Taifa ya Tanzania.
Nahodha Sophia Mwasikili aliifungia bao Twiga Zambia

Mchezo wa marduiano unatarajiwa kufanyika kati ya April 10,11 na 12, 2015, huu jijini Dar es alaam na mshindi wa jumla atafuzu moja kwa moja kwenye fainali za Afrika kwa Soka la Wanawake (All Africa Games Women)  zitakazofanyika Brazzavile Congo Septemba 3-18 mwaka huu.
Twiga Stars inatarajiwa kuwasili saa 7 kamili usiku (jumanne) jijini Dar es salaam kwa usafiri wa Shirika la Ndege la Ethiopia ikitokea nchini Zambia.
Kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu , Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), watanzania wote wanawapa pongezi  Twiga Stars kwa ushindi walioupata wa awali na kuwatakia maandalizi mema ya mchezo wa marudaiano.
Mabao ya Twiga Stars katika mchezo wa jana dhidi ya Zambia (The She-polopolo) yalifungwa na Asha Rashid (2), Shelder Boniface (1) na Sophia Mwasikili (1).

Mar 22, 2015

YANGA SC NA MGAMBO KATIKA PICHA JANA MKWAKWANI

Beki wa Yanga SC, Oscar Joshua akiwa hewani kuppiga mpira kichwa dhidi ya Salim Mlima wa Mgambo JKT katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jana Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Yanga SC ilishinda 2-0.
Kiungo wa Yanga SC, Haruna Niyonzima akimtoka Mohammed Samatta wa Mgambo
Simon Msuva wa Yanga SC, akimtoka Ramadhan Malima wa Mgambo
Amisi Tambwe wa Yanga SC akiwa ameruka kupiga mpira kichwa dhidi ya mabeki wa Mgambo
Beki wa Yanga SC, Kevin Yondan akiwa ameruka juu kugombea mpira na Malimi Busungu wa Mgambo
Mshambuliaji wa Yanga SC, Kpah Sherman akiwatoka mabeki wa Mgambo 

KURASA ZA MAGAZETI YA MICHEZO LEO JUMAPILI 22 MARCH ZIPO HAPA



.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Mar 21, 2015

MICHAEL CARRICK ASAINI MKATABA MPYA MAN UNITED

KIUNGO Michael Carrick amepata bonge la furaha Manchester United kuelekea mechi na mahasimu wao wakubwa, Liverpool baada ya kusaini Mkataba mpya mwaka mmoja Old Trafford.
Taarifa ya Manchester United iliyotumwa BIN ZUBEIRY imesema kwamba kiungo huyo anabaki kuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Louis van Gaal licha ya kukosa miezi miwili na nusu ya kwanza ya msimu kwa sababu ya kuwa maumivu ya kifundo cha mguu, alichoumia katika mazoezi ya kwanza ya Mholanzi huyo Agosti mwaka jana.
Van Gaal amempa Unahodha Msaidizi Carrick, baada ya kiungo huyo kuonyesha mchezo mzuri na kutengeneza bao la kwanza lililofungwa na Marouane Fellaini mwishoni mwa wiki katika ushindi wa 3-0 nyumbani dhidi ya Tottenham kabla ya yeye mwenyewe kufunga.
Carrick has made 17 appearances for Manchester United this season 
Michael Carrick ameichezea United mechi 17 msimu huu baada ya kuwa nje mwanzoni mwa msimu kwa sababu ya maumivu ya enka

Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 33, aliyejiunga na United kutoka Spurs kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 18.6 mwaka 2006, alitarajiwa kumaliza Mkataba wake mwishoni mwa msimu.

NGASSA APATA ‘GONJWA LA AJABU’ YANGA SC NA LEO HAWEZI KUCHEZA DHIDI YA MGAMBO

Na Mahmoud Zubeiry, TANGA
KIUNGO mshambuliaji wa Yanga SC, Mrisho Khalfan Ngassa amepata ugonjwa ambao yeye mwenyewe hauelewi na leo anaweza kukosa mechi dhidi ya Mgambo Shooting.
Yanga SC wanacheza na JKT Mgambo leo Uwanja wa Mkwakwani, Tanga katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, lakini Ngassa ambaye ni tegemeo kweli la timu hiyo hali yake tete.
Ngassa amesema kwamba alimaliza vizuri mechi dhidi ya Kagera Sugar Jumatano, Yanga SC ikishinda 2-1, lakini Alhamisi mambo yakageuka.
Mrisho Ngassa ameumia 'kiajabu ajabu' na leo hatacheza dhidi ya Mgambo Shooting Uwanja wa Mkwakwani, Tanga

“Nilikuwa napanda basi jana kwa safari ya kuja Tanga, mguu ukaanza kuuma. Maumivu yakazidi nikiwa kwenye basi. Tulipofika nikamuambia dokta. Ameanza kuhangaika nao tangu hapo, lakini wapi, hali bado tete,”alisema Ngassa jana usiku.
“Nimejaribu kuweka barafu kupoza maumivu, lakini hali bado si nzuri na sijui tatizo ni nini,”amesema Ngassa.
Wazi Yanga SC kumkosa Ngassa leo dhidi ya Mgambo ni pigo kubwa, kwa sababu mchezaji huyo amekuwa chachu ya ushindi katika klabu hiyo.
Wakati Yanga SC itaingia kwenye mchezo wa leo na kumbukumbu ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Kagera, Mgambo nao katika mchezo uliopita waliifunga 2-0 mjini hapa.


KURASA ZA MWANZO NA ZA MWISHO ZA MAGAZETI YA MICHEZO LEO IJUMAA

.
.
.
.
.
.
.
.

Mar 20, 2015

VAN GAAL AKUALI YAISHE ATANGAZA KUJIENGUA


Meneja wa klabu ya Man Utd, Louis van Gaal ametangaza kustahafu kufanya kazi aliyo nayo sasa mara atakapomaliza mkataba wake na klabu hiyo ya nchini England.
Van Gaal, sanjari na wachezaji wake mwishoni mwa juma hili watakabiliwa na mchezo muhimu katika ligi ya nchini England dhidi ya mahasimu wao wakubwa nchini humo Liverpool katika uwanja wa Anfield.
Meneja huyo kutoka nchini Uholanzi amethibitisha kukaa kwake pembeni katika mchezo wa soka kama meneja mara baada ya kumalizana na Man utd mwaka 2017, alipozungumza na vyombo vya habari kuelekea katika mchezo huo wa ligi uliopangwa kucheza siku ya jumapili.
Van Gaal, amesema kazi ya kukiongoza kikosi cha Man Utd ni ya mwisho kwake na hafikirii kuendelea kutokana na kuhitaji muda wa kupumzika baada ya kuutimikia mchezo wa soka kwa zaidi ya miaka 20 sasa.
'Nimeshazeeka sasa, hii Itakua kazi yangu ya mwisho' Alisema Van Gaal katika mkutano na waandishi wa habari.
'Nimeshazungumza na familia yangu na kuweka wazi msimamo huu, ambao utanisaidia kuwa karibu na watoto, wajukuu pamoja na mke wangu ambaye kwa kipindi kirefu amekua mpweke kutokana na shughuli nizifanyazo.' Aliongoza Van Gaal
Van Gaal alikubali kukichukua kikosi cha Man Utd baada ya kutimuliwa kwa David Moyes mwishoni mwa msimu uliopita, na alitarajiwa kuwa na mtazamo wa kukibadilisha kikosi cha klabu hiyo msimu huu, lakini mambo yamemuendea kombo.
Kabla ya kuikubali kazi ya Man Utd, Van Gaal alikua kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uholanzi ambayo ilishiriki fainali za kombe la dunia huko nchini Brazil na kuishi katika hatua ya nusu fainali, kabla ya kushika nafasi ya tatu kwa kuwafunga wenyeji.

CANNAVARO AREJEA MZIGONI, YU TAYARI KWA MGAMBO KESHO

CANNAVARO (WA TATU KUSHOTO) AKIWA NA WENZAKE WAKIJIFUA KWENYE UWANJA WA MKWAKWANI MJINI TANGA, LEO.
Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amerejea mazoezini na kuungana na wenzake mjini Tanfa.

Cannavaro ambaye alishonwa nyuzi saba baada ya kupasuka usoni wakati wa mechi ya watani wao Simba, leo amejifua na wenzake kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
Akionekana yuko fiti, Cannavaro amejifua na wenzake hali inayoonyesha ana nafasi ya kuitumikia Yanga itakapokuwa ikiivaa Mgambo, kesho.

Yanga ipo Tanga, tayari kuwavaa Mgambo ambao mechi iliyopita waliishinda Simba kwa mabao 2-0.

RATIBA ROBO FAINALI UEFA HII HAPA


Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) leo limekamilisha upangaji wa ratiba ya mechi za robo fainali huku Real Madrid ikipewa Atletico Madrid.


Wapinzani hao wakubwa kutoka nchini Hispania walicheza fainali ya mwaka jana ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Real Madrid kuibuka na ushindi, tena katika dakika za mwisho.

Barcelona wao watakutana na kiboko ya Chelsea, yaani PSG.

FC Porto wanakutana na mzigo wa Bayern Munich na Juventus wao watapambana na AS Monaco ya Ufaransa iliyoitoa Arsenal.

Mechi:
PSG Vs Barcelona
Atletico Madrid Vs Madrid
Porto Vs Bayern

Juve Vs Monaco

SSERUNKUMA YUPO SIMBA MILELE, WAKALA ASEMA

Na Vincent Malouda, NAIROBI
WAKALA wa straika la Simba SC Dan Sserunkuma, Ken Joseph, amesisitiza kuwa mteja wake yungali mchezaji wa Wekundu wa Msimbazi hadi mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa mwaka 2016.
Kumekuwepo na tetesi kuwa raia huyo wa Uganda tayari amewaandikia viongozi wa Simba barua akielezea azma ya kusitisha mkataba wake mwishoni mwa msimu huu kufuatia kutoridhishwa kwake kukalishwa kwenye benchi.
Sserunkuma hajarejea kambini baada ya kupewa ruhusa ya muda kushughulikia maswala ya kifamilia. Alitarajiwa kurejea Dar Jumamosi iliyopita baada ya kuondokea kwao Uganda pindi tu Simba ilipolazwa na Yanga taifa Machi 8.
Dan Sseunkuma kulia akiichezea Simba SC katika Ligi Kuu

“Naweza kukuthibitishia kwamba Dan Sserunkuma ni mchezaji wa Simba SC. Dan alipewa ruhusa ya siku chache na klabu kwenda nyumbani kisha arejee kambini. Ninachojua ni kwamba hakuna tatizo lolote kati ya Sserunkuma na Simba wala hajaniambia jambo lolote kuhusu kuondoka klabu hiyo, “ wakala huyo mzawa wa Uingereza na mwenye uraia wa Nigeria aliliambia BIN ZUBEIRY.
“Pia ijulikane kuwa Sserunkuma ni mchezaji mwenye hadhi ya juu jinsi wasifu kazi wake unavyosoma.”
Sserunkuma alisajiliwa Simba mwezi Desemba kutokea Gor Mahia ya Kenya alipomaliza mfungaji bora wa ligi kuu Kenya kwa magoli 16 na hadi kufikia sasa amecheka na nyavu mara tatu tu.
Amewahi kuzichezea Express FC na Victors FC za Uganda na vile vile Nairobi City Stars ya Kenya na pia kufanya majaribio nchini Armenia na Denmark.

ALICHOSEMA SSERUNKUMA KUHUSU UCHAWI SIMBA

http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/03/dan-serunkuma.jpg

Mshambuliaji wa klabu ya Simba pamoja na Timu ya Taifa ya Uganda, Dan Sserunkuma, amefunguka ya moyoni kuhusiana na ushirikina na kusema kuwa, Hajawahi kuambiwa na uongozi wa timu juu ya kutumia maswala hayo licha yakuwa Imani yake hairuhusu Ushirikina. 
Nyota huyo ambaye alikuwa ni mfungaji bora wa ligi kuu ya Kenya kwa misimu miwili iliyopita mfululizo akiwa Gor Mahia, Amesema hayo leo kupitia akaunti yake ya Twitter na kusema kuwa bado anaipenda Simba wala hafikilii kuondoka Msimbazi.
“Napenda kusema yafuatayo, Ninafuraha kuwa Simba, Sitaki kuondoka Simba, Sijawahi kulalamika kubaguliwa Simba, Sijawahi kulazimishwa na uongozi kutumia Uchawi kama ambavyo siamini” Ameandika Sserunkuma kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter.
facebook_1426798862337

KOCHA ENGLAND ATOA YAMOYONI KUHUSU HARRY KANE

 

Kocha wa timu ya taifa ya England Roy Hodgson amesema ingeshangaza sana kama mchezaji kinda wa klabu ya Tottenham Harry Kane asingejumuishwa katika kikosi cha Nchi hiyo kinachotarajiwa kumenyana na Lithuaniana na Italy.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, ni miongoni mwa wachezaji 24 wa kikosi cha England ambacho kimetajwa na Hodgson kucheza dhidi ya Lithuania mchezo ambao utapigwa katika dimba la Wembley mnamo march ,27 mwaka huu kwaajili ya mechi za kufuzu katika mashindano katika mataifa ya Ulaya yanayotarajia kufanyika mwakani. Kikosi hicho pia kinatarajia kuumana na Italy katika mchezo wa kirafiki utakaopigwa mjini Turin huko Italy tarehe 31 mwezi huu.

KILICHOANDIKWA KWENYE KURASA ZA MBELE NA ZA NYUMA MAGAZETI YA MICHEZO LEO IJUMAA.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.