Mar 6, 2015

HAWA NDIO WACHEZAJI MATAJIRI DUNIANI

MRENO Cristiano Ronaldo ndiye mwanasoka tajiri zaidi duniani akiwa na utajiri wenye thamani ya Pauni Milioni 152, ikiwa ni Pauni Milioni 7 zaidi ya hasimu wake mkubwa, Muargentina Lionel Messi.
Baada ya msimu mzuri wa 2014, ambao ilishuhudiwa Ronaldo akiiwezesha Real Madrid kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya naye akishinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia, maarufu kama Ballon d'Or, ameongeza idadi ya utajiri anaomzidi nyota wa Barcelona na Argentina.
Kwa mujibu wa Orodha ya Matajiri ya Goal.com, ilitotolewa leo, Ronaldo na Messi bado ndiyo wanasoka wanaofurahia zaidi kazi hiyo kuliko wenzao wote duniani.
The Portuguese retained his Ballon d'Or accolade in Zurich back in January
Cristiano Ronaldo akiwa na tuzo yake ya Ballon d'Or baada ya kukabidhiwa mjini Zurich, Uswisi Januari mwaka huu


ORODHA YA WACHEZAJI 10 TAJIRI ZAIDI DUNIANI 

1. Cristiano Ronaldo £152.3
2. Lionel Messi £145m
3. Neymar £97.9m
4. Zlatan Ibrahimovic £76.1m
5. Wayne Rooney £74.6m
6. Kaka £69.6m
7. Samuel Eto'o £63.1m
8. Raul £61.6m
9. Ronaldinho £60.2m
10. Frank Lampard £58m 
Barcelona's Lionel Messi was second on the Rich List with a personal wealth of £145m
Lionel Messi anashika nafasi yaa pili kwa utajiri wa thamani ya Pauni Milioni 145

0 maoni:

Post a Comment