Neymar
(juu) akishangilia na Mbrazil mwenzake, Dani Alves baada ya kuifungia
mabao yote Barcelona jana katika ushindi wa 2-0 dhidi ya PSG ya Ufaransa
katika Robo Fainali ya pili Ligi ya Mabingwa jana Uwanja wa Camp Nou.
Barca sasa inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 5-1, baada ya awali
kushinda 3-1 Paris.
Mshambuliaji
wa Bayern Munich, Thomas Muller akishangilia na mchezaji mwenzake,
Thiago baada ya ushindi wa 6-1 dhidi ya FC Porto katika mchezo wa
marudiano wa Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya jana Uwanja wa Allianz
Arena mjini Munich, Ujerumani. Mabao mengine ya Bayern yalifungwa na Thiago, Boateng, Lewnadowski mawili na Alonso 88, wakati la Porto lilifungwa na Martinez,dakika ya 73. The Bavarians sasa wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 7-4 baada ya awali kufungwa 3-1 mjini Munich.