SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

May 13, 2015

BAADA YA UPASUAJI MAREKANI, HATIMAYE PACQUIAO AREJEA KWAO UFILIPINO


  
Bondia nyota duniani, Manny Pacquiao amerejea kwao Ufilipino ikiwa ni siku chache baada ya kufanyiwa upasuaji katika bega lake nchini Marekani.

Manny alipokelewa na mashabiki na watu mbalimbali katika jiji na Manila.
Huku mkono wake ukiwa umefungwa, lakini bado alionekana ni mwenye furaha muda wote.

Bondia na mwanasiasa huyo, aliambulia kipigo kwa pointi dhidi ya bondia asiyepigika Floyd Mayweather.

Hata hivyo, Mayweather amekuwa akimshutumu Manny kwa kusema kwamba alipigana akiwa mgonjwa.








WAWILI WATEMWA SIMBA


sdf
Msimu umeisha wachezaji mbalimbali kutoka kwenye timu tofauti duniani wanahama kutoka kwenye timu moja hadi nyingine. Huko Ulaya mambo ni yamoto kwa upande wa kijana Pogba na hapa bongo hii ndio habari mpya.
Hawa ni wachezaji wawili wa Simba ambao wametoa taarifa kwenye page zao za social mediak kwamba hawatakuwa tena na Simba msimu ujao.

IMG-20150511-WA0031IMG-20150511-WA0027

HII NDIO IDADI YA MABAO YALIYOFUNGWA KWENYE LIGI YA VODACOM 2014/2015


DSFGHJ
Yanga imeongoza kwa kufunga mabao mengi msimu huu huku Simon Msuva akifunga mabao 17. Mabingwa wa Tanzania bara Dar Young Africans imefunga magoli 52 ambayo ni asilimia 15 ya mabao yote yaliyofungwa msimu huu.
kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi Jumla ya mabao 348 yamefungwa msimu huu na timu zote,  wakati huo huo Ruvu shooting na Polisi Morogoro ndio timu zilizofunga magoli machache Zaidi kwa kufunga mabao 16 kila moja ambayo ni sawa na asilimia 5.
Hata hivyo magoli ya msimu huu yameshindwa kufikia magoli ya msimu wa mwaka jana ambapo magoli 401 yalifungwa na Yanga pekee ilishinda magoli 61.

PLUIJM ATAJA KIKOSI BORA VPL 2014/2015 SIMBA NAO WAPO


DSC_0141
MSIMU wa 2014/2015 wa ligi kuu soka Tanzania bara umemalizika mwishoni mwa juma lililopita (Mei 9 mwaka huu) na kushuhudia Yanga wakitangazwa mabingwa, Azam nafasi ya pili, Simba nafasi ya tatu, Mbeya City nafasi ya nne, huku Ruvu Shooting na Polisi Morogoro zikishuka daraja.
MSIMAMO MZIMA HUU HAPA
Baada ya ligi kumalizika mtandao huu unafanya utafiti ambao matokeo yake na maana nzima vitawekwa bayani siku za usoni, lakini umeanza na kujua vikosi bora vya makocha wa timu za ligi kuu kwa msimu uliomalizika siku za karibuni.
Kila kocha anapewa nafasi ya kutaja wachezaji 11 kutoka timu zote ambao anaona wanaingia katika kikosi chake bora kabisa msimu mzima.
Leo tunaanza na kocha aliyetwaa ubingwa akiifundisha Yanga, Hans van der Pluijm ambaye amesema;
“Golini namuweka Ally Mustafa, nadhani amecheza vizuri sana, beki wa kulia ni Juma Abdul, mabeki wa katikati nawaweka Paschal Wawa na Nadir Haroub, kushoto Tshabalala kutoka Simba, sijui jina lake, najua jina lake la utani ni Tshabalala”.
“Safu ya kiungo ni Said Ndemla kutoka Simba, winga ya kulia ni Msuva, winga wa kushoto Emmanuel Okwi, kiungo cha mbele Niyonzima na washambuliaji wawili ni Amissi Tambwe na Kavumbagu’.
“Sikuwepo wakati ligi inaanza, nilianza kazi Yanga mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana, lakini kwa kipindi nilichoona ligi nimewaona wachezaji hao kuwa bora zaidi msimu huu”.
KIKOSI BORA CHA KOCHA WA YANGA, HANS VAN DER PLUIJM MSIMU WA 2014/2015 NA TIMU WALIZOTOKEA WACHEZAJI HAO
  1. Ally Mustafa (Yanga)
  2. Juma Abdul (Yanga)
  3. Mohamed Hussein ‘Tshabala’ (Simba)
  4. Nadir Haroub (Yanga)
  5. Paschal Wawa (Azam fc)
  6. Said Ndemla (Simba)
  7. Simon Msuva (Yanga)
  8. Haruna Niyonzima (Yanga)
  9. Amiss Tambwe (Yanga)
  10. Didier Kavumbagu (Azam fc)
  11. Emmanuel Okwi (Simba)
Kesho tutakuletea kikosi bora cha kocha wa Coastal Union, Jamhuri Kwhelo ‘Julio’, endelea kuwa nasi…..

SIKILIZA HII YA HANS POPPE KUHUSIANA NA KOPUNOVIC

HANS POPPE
Bosi wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema Kocha Goran Kopunovic ana kila sababu ya kuchagua, abaki au aende.

Hans Poppe amesema mazungumzo yao na Kopunovic ametaka dau kubwa hadi Sh milioni 28 kwa mwezi kama mshahara.

“Kweli bado hatujaelewana katika suala la maslahi. Sisi tunataka aendelee kubaki, lakini kwa fedha anayotaka hatuwezi kutoa.

“Kwa mwezi wadhamini wanatupa shilingi milioni 30 kwa mwezi kulipa wachezaji mishahara, yeye anataka achukue yote milioni 28.

“Hivyo tumemuachia yeye aamue kwa fedha ambazo tumemuambia. Kama hataweza basi atakwenda,” alisema Hans Poppe.

Taarifa za ndani ya Simba zimeeleza, kocha huyo ametaka mshahara wake upande kutoka dola 5,000 hadi dola 14,000 kwa mwezi.


Hali ambayo imeifanya Simba ishindwe kutoa fedha hizo na kusisitiza ikishindikana basi wataendelea kutafuta makocha wengine.

SUAREZ KUKOSA COPA AMERICA

cms-image-000008168

Mshambuliaji nyota wa timu ya Barcelona Luis Suarez atakuwa nje ya michuano ya mataifa ya Amerika ya kusini maarufu kama Copa America kutokana na kuendelea kutumikia adhabu ya kukosa michezo tisa kufuatia kosa la kumng’ata beki wa Italia Giorgio Chielini kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka jana .
Suarez atalazimika kuwatazama wenzie kwenye televisheni kutokana na adhabu hiyo ambayo imebakiza michezo saba kabla ya kumalizika .
Uruguay inayofundishwa na kocha mkongwe Oscar Washington Tabarez italazimika kumtegemea mshambuliaji wa PSG Edinson Cavani kwenye idara ya ushambuliaji huku ikimkosa pia Diego Forlan ambaye amestaafu kucheza timu ya taifa .
Forlan ambaye alistaafu mwezi machi mwaka huu amesema kuwa anaamini Uruguay ina wachezaji wazuri na wenye uwezo ambao wataziba pengo la Suarez na kufanya vizuri kwenye michuano ya mwaka huu .
Uruguay ndio mabingwa watetezi wa michuano ya Copa America ambayo waliitwaa mwaka 2011 nchini Argentina ambako waliwafunga Paraguay kwenye fainali na wanaingia kwenye michuano ya mwaka huu kama moja ya timu zinazopewa nafasi ya kufanya vizuri