SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Feb 7, 2015

REAL MADRID NA RONALDO WAO, WAPIGWA 4-0


TIMU ya Atletico Madrid imeitandika mabao 4-0 Real Madrid katika mchezo wa La Liga jioni ya leo.
Mwanasoka Bora wa dunia, Cristiano Ronaldo alicheza kwa mara ya kwanza baada ya kumaliza adhabu yake, lakii alitoka uwanjani anazomewa na mashabiki wa wenyeji baada ya kipigo. 
 
Kiungo wa zamani wa Chelsea, Tiago alifunga bao la kwanza dakika ya 14, Saul Niguez akafunga la pili dakika ya 18, kabla ya Antoine Griezmann kufunga la tatu dakika ya 67 na Mario Mandzukic kufunga la nne dakika ya 89 kwa pasi ya Fernando Torres. 
 
Kikosi cha Atletico Madrid kilikuwa; Moya, Juanfran, Miranda, Godin, Siqueira, Tiago, Koke/Saul dk10/Garcia dk71, Gabi, Turan, Griezmann/Torres dk77 na Mandzukic. 
 
Real Madrid; Casillas, Coentrao, Nacho, Varane, Carvajal, Khedira/Jese dk46, Kroos, Isco/Illaramendi dk68, Bale, Ronaldo na Benzema/Hernandez dk73.
The former Chelsea midfielder watches as his effort beats Real Madrid captain Iker Casillas  Saul Niguez doubles Atletico's lead with a superb overhead kick just four minuted after the first goal 
Cristiano Ronaldo looks dejected after Real Madrid concede two goals inside the opening 20 minutes of the game 
Cristiano Ronaldo akiwa mnyonge baada ya Real Madrid baada ya Real kufungwa bao la pili katika kipigo cha 4-0 leo
Three-time Ballon d'Or winner Ronaldo looks annoyed after being fouled during the first half 
 
The victorious home side celebrate on the pitch following the final whistle in Madrid 

CHELSEA YA NG'AA ENGLAND

Chelsea wameibuka na ushindi wa goli 2-1 ugenini dhidi ya Aston Villa katika mchezo ulio kuwa mkali na wakusisimua. Chelsea ndio walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Eden Hazard dakika ya 8 kabla ya Okore kusawazisha dakika ya 48 na baadae Ivanovic Ivanovic strike seals Chelsea victory
Mfungaji wa goli la pili la Chelsea Blanislav Ivanovic akishangilia baada ya kuifungia timu yake y Chelsea.
Mchezaji  Eden Hazard akishangilia baada ya kuifungia goli la kwanza timu yake ya Chelsea.
 Aston Villa 1-2 Chelsea: Ivanovic the hero for Mourinho's menWachezaji wa Chelsea wakishangilia moja ya goli lao.

ALI KIBA AFUNGUKA BIFU NA DIAMOND NA MIPANGO YAKE KIMUZIKI

 
Hatimaye staa wa Bongofleva Ali Kiba amekiri kuwa yuko katika bifu na mwanamuziki mwenzie Diamond Platnumz kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.
Kauli hiyo ya Ali Kiba inapingana na ile ya hivi karibuni iliyowahi kutolewa na Mwenyekiti wa Kamati za bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe alisisitiza kuwa wanamuziki hao hawana tofauti zozote na kwamba ni watu tu ndio wanakuza suala hilo.
Hata hivyo, juzi Ali Kiba aliliambia gazeti Moja[Mwananchi] kuwa ni kweli kuna ugomvi baina yao, huku akisisitiza kwamba tofauti yao ilianza mwaka 2012. Wakati Ali Kiba akifunguka kuhusu bifu hilo hali imekuwa tofauti kwa Diamond ambapo amekaririwa mara kadhaa kuwa hana tofauti yeyote na mwanamuzi huyo ambaye wanatoka mkoa mmoja wa Kigoma na kuunganisha Kundi la Kigoma All Stars. Akizungumza wakati akijibu maswali mbalimbali katika mahojiano maalumu, mwanamuziki huyo pia alielezea mambo mengi kuhusu muziki wake na hii ni sehemu ya mahojiano hayo;
 
Swali: Nini chanzo cha bifu lako na Diamond?
Ali Kiba: Hakuna kiini kwa sababu nadhani hayo mimi aaah.…Kiukweli haya tuliyamalizaga muda mrefu …Labda watu wahisi kwamba kipindi kile alichonifuta katika wimbo wake (alisema bila kufafanua jina la wimbo) na yeye alivyosema kwamba nimemfuta katika wimbo wangu ‘Single Boy’, mimi sijawahi kurekodi na Diamond katika wimbo wangu hata mmoja na huo niliimba na Lady Jaydee.
Yeye ndiye aliyesema kwamba nilimfuta katika wimbo ule, ila ukweli ni kwamba hatukuwahi kuingia pamoja studio, nilimshauri tufanye wimbo mwingine lakini siyo ule kwa sababu nimeshaimba na Lady Jay Dee.
 
Swali: Umeshawahi kuwa karibu na Diamond?
Ali Kiba: Hapana yeye ndiyo alishawahi kuwa na ukaribu na mimi.
Swali: Unaweza kufanya kolabo na Diamond?
Ali Kiba: Ngoja nikwambie ukweli, sidhani kama ninaweza kuja kufanya kolabo na Diamond, ila nikipata wimbo ambao nadhani kwamba anastahili kuwapo, kiukweli nitamshirikisha lakini kama hastahili haitawezekana.
Kwa sababu kila wimbo unajielezea, kwa mfano kama mtu anataka kufanya Zouk akimtafuta Stara Thomas itawezekana kwani hayo ndiyo mambo yake, kwa hiyo kama nikitaka kufanya naye wimbo ambao nitaona kwamba unafaa nitamfuata na nitamweleza.

 
Swali: Utofauti kati yako na Diamond ni upi? 
Ali Kiba: Mimi naimba muziki mzuri na nina ‘hit song’, naye Diamond anaimba ‘hit song’, unaposema mimi sina hit song wakati mimi nina nyimbo nyingi kushinda yeye unakuwa unakosea, tangu nimeanza kuimba ni nyimbo mbili tu hazijawahi kuwa hit ikiwamo ‘My Everything’ na ‘Mali Yangu’ lakini nyingine zote zilivuma tangu nianze kufanya muziki.
 
Swali: Inasemekana katika Tamasha la TigoMusic kuna hirizi zilionekana Uwanja wa Leaders na wewe na Diamond mnatuhumiwa kuhusika, unalizungumziaje?
Ali Kiba: Yaani Mungu mmoja sina imani hiyo kabisa na mimi naamini Mungu na mambo ya hirizi na mimi ni tofauti. Nadhani watu wanasema hivyo kwa sababu wanadhani kwamba kuna bifu. Binafsi sina bifu na msanii yeyote labda kama wanaweza kuwa na bifu na mimi binafsi simchukii msanii yeyote na sina bifu na yeyote.
 
Swali: Video yako ya Mwana imezungumziwa na mashabiki kuwa haikuwa na uhalisia. Pia ilikuwa ya kawaida sana, wewe binafsi unalichukuliaje?
Ali Kiba: Video ilivyokuwa ndivyo ilipangwa iwe kwa sababu kila mtu alikuwa amejenga picha itakuwaje kwa hiyo ililazimika kufanya vile kwa kuwa watu walishapanga mpaka gharama kwa kuwa nilikaa muda mrefu pasipo kufanya. Ningefanya kitu ambacho watu walikifikiria kiukweli ingekuwa karaha, nilichozingatia mimi ni kuimba vizuri na kuonyesha fikra za wimbo husika.
 
Swali: Vipi uliandaa ‘skripti’ ya video au aliamua GodFather kuifanya vile ilivyotengenezwa?
Ali Kiba: Tulikuwa na ‘script’ yetu pia waongozaji wa video walikuwa na yao ambayo walitupatia. Hivyo tukakubaliana nao kwa sababu tulitaka kuleta utofauti na kila kitu kikakaa sawa.
 
Swali: Ni kweli kwamba una mpango wa kufanya kolabo na Chris Brown?
Ali Kiba: Uwezekano wa kufanya upo kwa sababu kila kitu ni mipango kwa hiyo naweza kufanya kolabo na wasanii wa kimataifa na mashabiki watarajie kufanya hivyo.
 
Swali: Kwa nini haujafanya video ya Kimasomaso na ulisema video ya Mwana ingefanyika Dar es Salaam kwa nini ulitengenezea Afrika Kusini?
Ali Kiba: Video ya ‘Kimasomaso’ ilishindikana kutokana na muda ulikuwa hautoshi, nilijikuta niko katika mambo mengi sana kwani nilikuwa nimeegemea katika video ya Mwana kwa hiyo nilipokuja kugeuka ikawa ni vigumu.
Nilisema kwamba nyingine ningefanya nje ya hapa lakini kwa ‘Mwana’ sijaelewa kwanini nifanye hapa, tofauti na hiyo nyimbo haikuwa na maana ya Dar es Salaam, maana yake ni mwanamke na mwanamume sikuona sababu ya kufanyia hapa jijini.
Ukitumia neno la Dar es Salaam ni kwa sababu ni jiji lenye changamoto kwa hiyo unapozungumzia hilo ina maana kwamba ni Joharnesburg, Nairobi, Kampala, London majiji ambayo yana changamoto mfano video ya Macmuga nilifanyia Marekani.

GOOOAAAAALLLLL

Ivanovic ameipatia goli la pili timu yake ya Chelsea 2-1 dhidi ya Aston Villa dakika ya 71

JAHAZI LA REAL MADRID LAZAMA

LIVE: Atletico Madrid 3-0 Real MadridTimu ya Atletico Madrid inaongoza goli 3-0 dhidi ya wapinzani wao Real Madrid dakika ya 71

CHELSEA HALI MBAYA

Aston Villa wamesawazisha na sasa matokeo ni 1-1 dhidi ya Chelsea

AZAM, MBEYA CITY ZABANWA LIGI KUU BARA


 
Kweli Ligi Kuu Bara ngumu, Azam FC na Mbeya City, kila moja ikiwa ugenini imebanwa na kujikuta ikiambulia sare.

Ruvu JKT 1-1 Mbeya City
Bao la JKT limefungwa na Ally Bilal katika kipindi cha kwanza wakati la Mbeya City limefungwa na Kenny Ally aliyesawazisha katika kipindi cha pili.
Polisi 2-2 Azam FC

Mabao ya Azam FC yamefungwa na pacha Kipre Tchetche katika dakika ya 10 na Kipre Bolou.

STAND UNITED YAKOMAA UGENINI


Ligi Kuu Bara imeendelea kuwa ngumu kwa karibu kila timu baada ya Stand United kukomaa ikiwa ugenini na kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya wenyeji wake Ndanda FC.

Ndanda FC 1-1 Stand United

Bao la wenyeji limefungwa na Nassor Kapama katika dakika ya 57 kabla ya wageni nao kukomaa na kusawazisha bao hilo.

JINAMIZI LA SARE LAENDELEA MSIMBAZI

COASTAL Union wamegoma kufungwa mechi ya pili mfululizo nyumbani, baada ya jioni ya leo kulazimisha sare ya 0-0 na Simba SC Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba ilijaribu kutengeneza mashambulizi ya mipira ya kutokea pembeni, lakini washambuliaji wake Dan Sserunkuma na Elias Maguri walibanwa na walinzi wa Coastal.
 
Hali kadhalika Coastal nayo ilitengeza mashambulizi yake kadhaa, lakini washambuliaji wake Iker Obinna na Rama Salim walibanwa na mabeki wa Simba SC.
Kiungo wa Simba SC, Abdi Banda akipasua katikati ya wachezaji wa Coastal Union, Abdulhalim Humud kushoto na Godfrey Wambura kulia

Hakukuwa na mchezo wa kuvutia sana kutokana na timu zote kucheza mipira mirefu kwa kuhofia ubovu wa Uwanja wa Mkwakwani, lakini hakukuwa na kupamiana kama ilivyokuwa Jumatano Coastal ikifungwa 1-0 na Yanga SC. 
Refa wa mchezo Simon Mbelwa aliyesaidiwa na Abdallah Mkomwa na Frank Kombo wote wa Pwani, kwa kiasi kikubwa walijitabhidi kuumudu mchezo huo.
 
Kwa matokeo hayo, Coastal inafikisha pointi 18, wakati Simba SC inatimiza pointi 17.
Kikosi cha Coastal Union kilikuwa; Shaaban Kado, Mbwana Hamisi, Othman Tamim, Abdallah Mfuko/Hamad Juma dk59, Juma Lui, Abdulhalim Humud, Joseph Mahundi/Itubu Imbem dk86, Godfrey Wambura, Bright Ike Obinna/Mohammed Mtindi dk66, Hussein Sued na Rama Salim.  

Simba SC; Ivo Mapunda, Kessy Ramadhani, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Juuko Murshid, Jonas Mkude, Simon Sserunkuma/Messi dk79, Abdi Banda, Dan Sserunkuma/Ibrahim Hajibu dk88, Elias Maguri na Emmanuel Okwi.
Kipa wa Simba SC, Ivo Mapunda akidaka mpira leo
Kipa wa Coastal Union, Shaaban Kado akidaka mpira mbele ya beki wake, Tumba Swedi ambaye yuko mbele ya mshambuliaji wa Simba SC, Dan Sserunkuma

USIKOSE KUFUATILIA WWW.HAJIBALOU,BLOGSPORT.COM KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI

MATOKEO KUTOKA ETIHAD STDIUM MAN CITY MAMBO MAGUMU

Hull City wakiwa ugenini wanaongeza 1-0 dhidi Man City dakika ya 39

REAL MADRID HALI MBAYA MECHI INAENDELEA


 LIVE: Atletico Madrid 1-0 Real Madrid
Atletico Madrid wanaingoza goli 2-0 dhidi ya Real Madrid dakika ya 20

HAYA NDIO MATOKEO YA CHELSEA MECHI INAENDELEA

Chelsea inaongoza 1-0 dhidi ya Aston Villa dakika ya 11

SIMBA BADO HALI NGUMU

Simba imetoka sare ya bila kufungana dhidi ya Coastl Union katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga

ARSENAL YALALA KWA TOTENHAM

Timu ya Totenham Hotspur imeibuka na ushindi wa goli 2-1 dhid ya Arsenal katika mchezo uliochezwa katika uwanja White Hart Lane mjini London Arsena walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Mesout Ozil dakika ya 11 kabla ya H.Kane kuzawazisha dakika ya 56 na baadae akafunga tena dakika ya 86 na kuihakikishia timu yake point tatu muhimu.
LIVE: Tottenham 2-1 ArsenalMfungaji wa mabao yote mawili  ya Totenham Kane akishangilia moja ya bao lake katika mechi ya leo dhidi ya Arsenal.

GOOOAAALLLL

Totenham wamesawazisha dakika ya 56 1-1 Arsenal

GOOOAAAALLLL; ARSENAL WANG'AAAA

Arsenal wanaongoza goli 1-0 dhidi ya Totenham sasa ni dakika ya 20

YANGA SC KUWEKA KAMBI JESHINI

YANGA SC imefuta mpango wa kwenda kuweka kambi Zanzibar kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya BDF XI ya Botswana.
Sasa, vigogo hao wa soka Tanzania wataingia kambini Jumatatu katika hoteli ya Tansoma, eneo la Gerezani, 

Dar es Salaam kwa maandalizi ya mchezo huo, unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wake.
Na timu hiyo inayofundishwa na Mholanzi, Mart Nooij anayesaidiwa na Mzalendo, Charles Boniface Mkwasa itakuwa ikifanya mazoezi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wiki yote kuelekea mchezo huo.
Hatua hiyo inafuatia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kukataa ombi la Yanga SC kutaka mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Mtibwa Sugar uahirishwe ili wapate fursa nzuri ya maandalizi ya mchezo wao na BDF XI.
 
Baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Jumatano, Yanga SC iliondoka asubuhi ya Alhamisi kwenda kuweka kambi Bagamoyo kuendelea na maandalizi ya mchezo mwingine wa ligi hiyo, dhidi ya Mtibwa Sugar.
 
Yanga SC watacheza mechi ya tatu ndani ya wiki moja kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya mabingwa wenzao wa zamani wa Ligi Kuu, baada ya Jumapili iliyopita kulazimishwa sare ya 0-0 na Ndanda FC na Jumatano kushinda 1-0 dhidi ya Coastal Union. 
Yanga SC ilipanda kileleni mwa Ligi Kuu katikati ya wiki kufuatia ushindi huo wa ugenini, Tanga kwa kutimiza pointi 22 baada ya kucheza mechi 12, moja zaidi ya mabingwa watetezi, Azam FC walioteremkea nafasi ya pili kwa pointi zao 21.
 
Shujaa wa pointi tatu za Yanga SC siku hiyo alikuwa ni Nahodha Nadir Haroub Ali ‘Cannavaro’, aliyefunga bao hilo pekee mapema tu kipindi cha kwanza, baada ya kupanda kwenda kusaidia mashambulizi. 
Ilikuwa ni dakika ya 12 ya mchezo, wakati Cannavaro alipomalizia kwa kichwa mpira mpira wa kurushwa wa beki Mbuyu Twite na kuipandisha kileleni Yanga SC. 

KIONGERA KUONDOKA SIMBA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgmFmXQGxpZZoDOsQxZ_ActHa0vPV1BGUxuZjC03wSalaX7FcyAly6gGsz9gSJ4l6-U7iFc49c6V6iLDV7bExXkjC1wL7KVZgoLxk0rXtiRjAJvYqE2SEdhLwtyrhq-y9s7ZgqSAmOkbO1x/s1600/k4.JPG

Kiungo Mkenya, Paul Raphael Kiongera ametishia kujiondoa mikononi mwa klabu ya Simba kama hakutakuwa na mabadiliko.



Kiongera ameliambia gazeti hili kuwa amechoshwa na kile alichokiita ‘uswahili mwingi’ ambapo anadai kutolipwa fedha yoyote tangu Desemba, mwaka jana.

Simba iliondoa jina la mchezaji huyo katika usajili wake wa msimu huu licha ya kuwa na mkataba naye, ambapo ilisema itaendelea kumlipa kama kawaida kwa kuwa itamhitaji baada ya kupona jeraha la goti lililokuwa likimsumbua na kusababisha akatibiwe nchini India ambapo Simba ndiyo iliyogharamia huduma zake.

Akizungumza kutoka jijini Nairobi, Kiongera amesema: 

 “Ni kweli nasubiri Februari hii iishe, nimalizane nao kwa mujibu wa mkataba wetu, wao ndiyo watakuwa wamekiuka masharti na wameuvunja.

“Naona Simba wananizingua tu. Ujue hawataki kunipa mshahara wangu.”

Lakini Simba imesisitiza kwamba inamlipa fedha zake na hadai chochote.

Mwenyekiti wa Usajili, Zacharia Hans Poppe, alisema: “Kweli Kiongera tuna dhamana ya kumlipa na binafsi najua analipwa fedha zake na hakuna madai yoyote juu yetu. Sina taarifa zozote juu ya yeye kutolipwa kwa kuwa mi najua analipwa kama kawaida, vinginevyo aulizwe katibu.”

CANNAVARO AOMBA RADHI

 
Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amemuomba radhi askari aliyemkimbilia na kwenda kumkumbatia dakika chache baada ya kufunga bao katika mechi dhidi ya Coastal Union.

Cannavaro alifunga bao hilo katika dakika ya 11, Jumatano iliyopita na kufanya kitendo hicho ambacho kilikuwa gumzo.
 Cannavaro alisema alimuomba askari huyo msamaha muda mfupi baada ya mechi hiyo ambapo aliamua kumfuata na kumueleza kuwa hakuwa na nia mbaya.
Cannavaro alisema anamshukuru askari huyo kwa kukubali maombi yake ya msamaha aliyoyatoa kwani hakutarajia hali hiyo kutokea kutokana na furaha aliyoipata baada ya kufunga bao hilo.
“Kiukweli nilifanya kosa kukimbia na kwenda kumkumbatia askari wakati nashangilia bao nililolifunga, nilijikuta ghafla nafanya kitendo kile bila kutarajia, sikukitarajia kabisa wala sikupanga iwe hivyo.

“Baada ya mechi kumalizika nilimfuata nikazungumza naye, pia walikuwepo baadhi ya viongozi wangu na wale wa polisi niliwaomba radhi kwa kitendo hicho nilichokifanya, 
nikashukuru wakanielewa na kulimaliza tatizo hilo,” alisema Cannavaro
USIKOSE KUFUATIIA WWW.HAJIBALOU.BLOGSPOT.COM KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI

HUU NDIO UBABE WA COSTA NA TERRY UWANJANI

Na Saleh Ally
TABIA za beki mkongwe wa Chelsea, John Terry, ni kupenda kujitambulisha kwa washambuliaji anaokutana nao wakati timu yake ikiwa uwanjani.
Terry, maarufu kama JT, hajitambulishi kwa kupeana mikono, badala yake maneno ya kibabe au kumgongagonga mshambuliaji anayekuwa anamkaba ili kumuonyesha siku hiyo shughuli ni pevu.

Nahodha huyo wa Chelsea amekuwa akifanya hivyo mara nyingi ikionekana kutaka kumtawala mapema kabisa kisaikolojia mshambuliaji anayemkaba kwamba ajue amekutana na kiboko yake au beki katili na asiyetaka mchezo na kazi yake.
Wakati akiwa Liverpool, mshambuliaji Fernando Torres aliwahi kusema kila walipokutana na Chelsea alifanya juhudi kubwa kuhakikisha anafunga kwa kuwa alitaka kumuonyesha Terry ambaye hakufurahishwa na ubabe wake mara kwa mara.
Huenda mara kadhaa, Terry amekuwa akibadili mbinu zake, lakini hiyo ni moja ya kubwa alizonazo. Wakati fulani, mpango huo wa Terry ulifeli.

Katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Atletico Madrid, Terry alianza mapema mipango yake ya kutaka kumuonyesha mshambuliaji Diego Costa kwamba yeye ni nani. Lakini majibu yalikuwa makali kuliko alivyotegemea na ndipo akagundua kuwa Costa ni namba nyingine na huenda mfumo alioutumia kwa mara ya kwanza haukuwa sahihi.
Kitendo cha Costa kuwakanyaga mabeki Emre Can na Martin Skrtel wa Liverpool kimewafanya wengi waamshe mjadala wa mshambuliaji huyo raia wa Hispania mwenye asili ya Brazil.
Maswali yamekuwa ni mengi, kama kweli anafaa kuichezea Chelsea, kama kweli wanastahili kuwa na mchezaji mkatili hivyo. Mwisho wengi wanahoji vipi awe mjeuri namna hiyo? Ingawa wanavutiwa na uwezo wa kazi zake maana ndiye anaongozwa kwa kutikisa nyavu katika Ligi Kuu England.
Costa ni mtoto wa Uswahilini, amekulia maisha hayo na hakuwahi kuishi maisha ya mafunzo ya soccer kwenye ‘academy’ kama ilivyo kwa wachezaji wengi wa Ulaya.
Ubabe wa mechi za mchangani ambazo alikuwa maarufu sana, bado uko kwenye damu yake, ndiyo maana anawapa tabu sana Wazungu.
Costa alizaliwa katika mji mdogo wa Lagarto katika Jimbo la Sergipe nchini Brazil. Miaka yote alikuwa akicheza soka la mchangani na alikuwa maarufu sana.
Hadi alipofikisha miaka 16, ndiyo alichukuliwa hadi jijini Sao Paulo na kujiunga na timu iliyokuwa na mafunzo sahihi ya mchezo wa soka.
Waliocheza naye soka katika Mji wa Lagarto kabla hajaondoka kwenda Sao Paulo, wanasema alikuwa mjeuri, mtu mwenye hasira na hakuwa na woga hata kidogo.
Lakini kituko cha kumpiga mchezaji halafu akakimbilia kumsukuma na kumghasi mwamuzi kilikuwa maarufu zaidi. Baadaye Costa alifungiwa miezi minne. Wakati huo alikuwa akiichezea Barcelona Esportiva Capella.
Aliwahi kubatizwa jina la Picardia, neno hilo la Kihispania lenye maana ya mpiganaji au mtu asiye na hofu na ndivyo anavyoonekana.
Hii inaonyesha kiasi gani uchezaji wa kibabe Costa hautakwisha na ataendelea kuwa namna hiyo kwa kuwa hakucheza soka la mafunzo linalomuonyesha afanye vipi kuonekana ni mwenye nidhamu.
Takwimu zinaonyesha hata kabla ya msimu kwisha, ameshasababisha tafrani za kawaida mara 22, amekwidana na mabeki mara tano, amewasukuma kwa kifua mara 13, amewasukuma kwa mikono mara 15 na amekutana na mabeki uso kwa uso na kutoa maneno ya kibabe mara 11.
Pamoja na kwamba ameshakutana na adhabu kutoka FA, lakini haimbadilishi yeye kuwa alivyo na wengi wamekuwa wakisema ni zawadi nzuri kwa mabeki wa England ambao wengi wamekuwa wababe kwa washambuliaji.
 Mara kadhaa, Costa ameonekana akiwa amechaniwa jezi au bukta. Lakini amekuwa akionyesha sehemu alizoumizwa na viatu vyenye njumu za chuma za mabeki hao ambao sasa wameanza kulalamika.
Hakuna ubishi tena unaweza kusema ubabe wa Costa ni dawa ya mabeki wababe wa England na karibu kila mchezo amekuwa akizozana nao na mara nyingi kuwafanya wadau wa soka kuwaonea huruma mabeki.
Kwa zaidi ya miaka 20, hakuna aliyewahi kulalamika mabeki wa Ligi Kuu England wamekuwa wakionewa hadi Costa alipotua England. Je, ataendelea hivyo hadi mwisho?
Mabao anayofunga anaonyesha ana uwezo na hilo alilidhihirisha Hispania kabla ya kutua England. Je, kuna mengi anafunga baada ya kuwatisha mabeki?
Jiulize, mabeki wa England hasa wale wa kati ambao wengi ni wakatili, wataendelea kumvumilia na kushitaki bila ya kumtafutia dawa?
Ila ukweli, mtoto wa Uswahilini anawapa shughuli mabeki hao licha ya wao kutamba kwamba England ndiyo kwa wababe.
Kwa sasa Costa ni kati ya burudani zinazovutia zaidi katika soka England. Kila anapokuwa anaitumikia Chelsea, wengi hupenda kuona anavyofunga na sasa imegeuka, wengi wanapenda kuona anavyopambana na mabeki wababe.

LEO DERBY KATIKA MAJIJI YA LIVERPOOL, LONDON

LONDON, England
UTAMU wa soka la Ulaya utaendelea wikiendi hii. Vita ya kusaka ubingwa wa England nayo itazidi kupamba moto katika mechi za leo na kesho, lakini kubwa zaidi linalozungumzwa kitaa ni ‘derby’ (mechi zinazohusisha timu zinazotoka mji mmoja) mbili kubwa nchini England.

Derby ya kwanza inatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa White Hart Lane ambayo itazikutanisha timu zinazotokea katika Jiji la London, yaani Tottenham Hotspur dhidi ya Arsenal katika mtanange wa kukata na shoka utakaochezwa kuanzia saa 9:45 alasiri.

Lakini baadaye saa 2:30 usiku, kutakuwa na derby nyingine itakayozikutanisha timu zinazotokea jijini Liverpool, yaani Everton na Liverpool FC ambazo zitapambana vikali kwenye Uwanja wa Goodison Park.
Tottenham vs Arsenal
Vita hii inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka sehemu mbalimbali duniani. Mechi itachezeshwa na mwamuzi mkongwe, Martin Atkinson, raia wa England.

Utamu wa mechi hii unatokana na timu zote kuwa kwenye kiwango bora katika mechi zake za hivi karibuni. Katika michezo yao mitano iliyopita, Tottenham wameshinda mitatu, wametoa sare mmoja na kupoteza mmoja, wakati Arsenal wenyewe wameshinda michezo yao yote mitano iliyopita.
Katika michezo yao mitano iliyopita waliyokutana, Arsenal imeshinda mara tatu, wakati Spurs imeshinda mara moja tu huku zikitoka sare mara moja.

Hata hivyo, pamoja na Arsenal kushinda mara nyingi dhidi ya wapinzani wao hao katika siku za hivi karibuni, bado mpambano unatarajiwa kutotabirika kutokana na kiwango cha sasa cha Spurs ambayo inawategemea zaidi washambuliaji wake Harry Kane na Christian Eriksen walio kwenye ‘fomu’ kwa sasa.

Supastaa wa Arsenal, Mchile, Alexis Sanchez, anatarajiwa kuukosa mchezo huo wa leo kutokana na kuendelea kusumbuliwa na majeraha ya nyama za paja yaliyomuweka nje ya uwanja katika ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Aston Villa wiki iliyopita, lakini kocha Arsene Wenger atashusha pumzi kufuatia kurejea kwa mpachika mabao wake, Danny Welbeck.
Timu zote hizi, zipo katika mapambano ya kuhakikisha zinakuwemo ndani ya nne bora ili zipate nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Kama Arsenal iliyo katika nafasi ya tano ikishinda kwenye mtanange huu, itakuwa imeingia hadi kwenye mbio za kuwania ubingwa wa England kwa kuwa itakuwa imebakiza pointi nane tu iwafikie vinara Chelsea ambao baadaye watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Aston Villa. Lakini Spurs ikifungwa itakuwa inazidi kujiweka pabaya katika vita ya kuingia ‘top 4’.

Kama Spurs iliyo katika nafasi ya sita ikishinda mchezo huo, itaipiku Arsenal kwenye nafasi ya tano na inaweza ikaingia moja kwa moja ndani ya nne bora na kusubiri matokeo ya Southampton ambayo itakuwa mgeni wa QPR baadaye jioni.

Liverpool vs Everton:
Huu ni mtanange mwingine ambao umeshaanza kuwa gumzo mjini. Liverpool iliyo nafasi ya saba, iliuanza msimu huu kwa kusuasua kutokana na kuonekana kummisi mpachika mabao wao aliyeondoka, Luis Suarez, lakini sasa inaonekana kuanza kuimarika, hasa kutokana na ubora unaoonyeshwa na viungo wawili wa timu hiyo, Raheem Sterling na Philippe Coutinho.

Kwa upande wa Everton wanaonekana kutokuwa sawa msimu huu, kwani wameshindwa kuonyesha makali yao ya msimu uliopita ambapo walikuwa wanapigania kuingia kwenye ‘top 4’.
Everton wapo katika nafasi ya 12 na wanatakiwa washinde ili kujiondoka kwenye hatari yoyote ya kushuka daraja na kujiongezea matumaini ya kutafuta nafasi ndogo waliyonayo ya kushiriki michuano ya Ligi ya Europa, lakini Liverpool bado wanapambana kuingia ndani ya nne bora.

Pambano hili litachezeshwa na mwamuzi Muingereza, Antony Taylor. Katika mechi zake tano zilizopita, Liverpool imeshinda mbili, imetoa sare mbili na kupoteza moja, wakati Everton wameshinda mechi moja tu kati ya michezo yao mitano iliyopita huku mingine wakitoa sare.

Takwimu zinaonyesha kuwa, kwenye mechi tano zilizopita baina ya timu hizo, Liverpool imeshinda mara moja huku matokeo mengine yakibaki kuwa ni sare. Ngoma itakuwa pevu leo na lolote linaweza kutokea.

HIVI NDIVYO ALIVYOPUMZISHWA NTAGWABIRA, KOCHA ALIYEFARIKI MWEZI TU BAADA YA KUTAKIWA NA SIMBA



Mchezaji wa zamani na kocha wa timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’, Jean Marie Ntagwabira amezikwa juzi katika makaburi ya kijeshi jijini Kigali, Rwanda.
WATOTO WA MAREHEMU WAKITOA HESHIMA ZAO ZA MWISHO


Mwezi mmoja kabla ya kifo chake, Ntagwabira aliwaniwa na Simba lakini mwisho nafasi yake akaitwaa Goran Kopunovic ambaye pia aliiambia SALEHJEMBE kushitushwa na kifo chake.
NTAGWABIRA WAKATI WA UHAI WAKE.
Mchezaji wa zamani na kocha wa timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’, Jean Marie Ntagwabira amezikwa juzi katika makaburi ya kijeshi jijini Kigali, Rwanda.

Ntagwabira ,41, amefariki dunia akiwa anasumbuliwa na ugonjwa wa mapafu uliofanya ashindwe kupumua.
Mazishi yake yalihudhuriwa na maofisa mbalimbali wa jeshi pamoja na wanamichezo mbalimbali wakiwemo makocha na wachezaji wa timu ya APR.
Wakati wa mazishi yake, Rais wa Shirikisho la Soka la Rwanda (Ferwafa), Vincent Nzamwita alitoa pole kwa wafiwa, wadau wote wa soka la Rwanda pamoja na familia ya marehemu.
 
WACHEZAJI WA APR
Lakini Shirikisho hilo pia likaahidi kuwasomesha watoto wa marehemu kwa kiwango chote cha elimu watakachofikia.
Ntagwabira ,41, amefariki dunia akiwa anasumbuliwa na ugonjwa wa mapafu uliofanya ashindwe kupumua.
Mazishi yake yalihudhuriwa na maofisa mbalimbali wa jeshi pamoja na wanamichezo mbalimbali wakiwemo makocha na wachezaji wa timu ya APR.
 
MAOFISA WA JESHI
Wakati wa mazishi yake, Rais wa Shirikisho la Soka la Rwanda (Ferwafa), Vincent Nzamwita alitoa pole kwa wafiwa, wadau wote wa soka la Rwanda pamoja na familia ya marehemu.
Lakini Shirikisho hilo pia likaahidi kuwasomesha watoto wa marehemu kwa kiwango chote cha elimu watakachofikia.

PEDRO KUONDOKA BARCELONA


Klabu za Liverpool na Arsenal zote za nchini England huenda zikapigana vikumbo mwishoni mwa msimu huu, kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Hispania, Pedro Rodriguez ambaye yu njiani kuachana na FC Barcelona.

Arsenal na Liverpool zinatajwa kuingia katika mvurugano wa kumuwania mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, kufuatia mipango iliyobainika huko mjini Barcelona ambayo inabainisha huenda Pedro akatemwa mwishoni mwa msimu huu kutokana na mapendekezo ya meneja wa sasa Luis Enrique.
Hata hivyo mkataba mshambuliaji huyo unatarajia kufikia kikomo mwaka 2016, lakini FC Barcelona wanahofia kumpoteza bila ya kupata faida ya ada ya uhamisho endapo ataondoka kama mchezaji huru, hivyo wameona ni bora kumuingiza katika mfumo wa kumuuza mwishoni mwa msimu huu.

Padro amekua na mafanikio katika klabu ya Barcelona ambayo ameitumikia kwa muda wa miaka 11 sasa, ambapo ameshwatwaa mataji manne ya ligi ya nchini Hispania pamoja na mataji mawili ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, ila amekua na wakati mgumu kwa msimu huu kutokana na kutumika mara 20 kikosini.

LIGI KUU ENGLAND KUENDELEA LEO

Shughuli pevu wikiendi hii Ligi kuu England
Ligi Kuu England itaendelea tena wikiendi hii ambapo michezo saba ya mzungo wa raundi ya 24 itapigwa katika viwanja tofauti.
katika uwanja wa White Hart Lane, Tottenham wataikaribisha Arsenal kwenye Dabi ya London ya Kaskazini, Arsenal wako nafasi ya tano wakiwa na pointi 42 huku Tottenham wakiwa nafasi ya sita kwa pointi 40.

Alexis Sanchez atakosa mchezo huu kutokana na kuwa majeruhi huku mshambuliaji Dany Welback atakua anarejea baada ya kuwa nje ya uwanja toka mwezi Desemba.
Vinara wa ligi hiyo Chelsea watashuka dimbani kuwakabili Aston Villa huku timu hiyo ikiendelea kukosa huduma za mshambuliaji wake Diego Costa.

Man City walioko nafasi ya pili kwa alama 48 alama 5 nyuma ya vinara Chelsea wao watakua na kibarua cha kuwania alama tatu muhimu kwa kuwakabili Hull city.
Majongoo wa jiji Liverpool watachuana na wapinzani wao wakubwa Everton katika kuwania pointi tatu muhimu.

Michezo mingine itakua ni kati ya timu inayoburuza mkia Leicester City dhidi ya Crystal Palace, huku QPR wakishuka dimbani kuwakabili Southampton
Mchezo wa mwisho wa ligi hiyo kwa siku ya jumamosi utakua ni kati ya Swansea na Sunderland

JAMES RODRIGUEZ ATEMBELEA MAGONGO

MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, James Rodriguez juzi ameanza kutembelea magongo baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti la mguu wake wa na anatarajiwa kuwa nje kwa miezi miwili.
Japokuwa klabu yake haijasema atakuwa nje kwa muda gani, lakini taarifa za ndani zinasema mchezaji huyo atakosekana kwa miezi miwili.
Rodriguez aliumia goti baada ya kuifungia bao la kuongoza Real Madrid katika ushindi wa mabao 2-1 kwenye mchezo wa La Liga dhidi ya Sevilla Uwanja wa Santiago Bernabeu na akatolewa kipindi cha kwanza baada ya madaktari kusema kwamba ameumia sana.
James Rodriguez was pictured on crutches at the hospital in Murcia as he underwent foot surgery
James Rodriguez was pictured on crutches at the hospital in Murcia as he underwent foot surgery
James Rodriguez pichani baada ya kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya Murcia 

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23, Rodriguez amefanikiwa kupata namba kwenye kikosi cha kwanza Real chini ya kocha Carlo Ancelotti, baada tu ya kusajiliwa msimu huu kufuatia kuifikisha timu yake ya taifa Colombia, katika Robo Fainali Kombe la Dunia hadi kuibuka mfungaji bora.
Amecheza mechi 33 kati ya 36 za Real Madrid msimu huu, akifunga mabao 12 na kusaidia upatikanaji wa mabao 10 zaidi.

PICHA; HUYU NDIO MTOTO WA SHAKIRA NA GERRAD PIQUE

sasha
Ni mara chache kwa mastaa wa kike wa muziki Marekani kuona wakiweka picha za watoto wao mara baada ya kutoka kujifungua.
Imewachukua muda mrefu mastaa kama Kim Kardashian, Beyonce, Kelly Rowland na wengine kuonyesha watoto wao wakiwa bado wachanga lakini kwa Shakira na mume wake Gerard Pique imekuwa tofauti kwani ni wiki moja tungu wapate ugeni katika familia yao na wameamua kuonyesha picha za mtoto wao.
sasha 2Katika picha hiyo wawili hao waliandika kuwa wanafuraha kubwa kumkaribisha mtoto wa pili Sasha katika familia yao na kuwashukuru mashabiki wao kwa kuwatakia heri.

PICHA ZA UTENGENEZAJI WA VIDEO YA BARNABA NA VANESSA MDEE


.
.
Vanessa Mdee na Barnaba Elias Feb 6, waliingia location kumalizia utengenezaji wa video mpya ya single yao iitwayo Siri, video hiyo imeongozwa na Hanscana kwenye kijiji cha Makumbusho Dar es Salaam.
Hizi ni baadhi ya picha ambazo nimekuchukulia baada ya kushuhudia utengenezaji wa video hiyo mpya, zicheki hapa zote mtu wangu.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
USIKOSE KUFUATILIA WWW.HAJIBALOU.BLOGSPOT.COM KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI