SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Mar 12, 2015

YANGA SC DHIDI YA PLATINUM KIINGILIO POA BUKU TANO JUMAPILI TAIFA

Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
KIINGILIO ch chini katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika baina ya wenyeji, Yanga SC na Platinum FC ya Zimbabwe kitakuwa na Sh. 5,000 kwa jukwaa la viti vya rangi bluu na kijani, imeelezwa.
Yanga wataikaribisha Platinum FC ya Zimbabwe katika mchezo wa kwanza, Raundi ya Kwanza Kombe la Shirikisho Afrika Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro ameiambia BIN ZUBEIRY jioni ya leo kwamba, katika jukwaa la viti vya Rangi Chungwa itakuwa Sh, 7,000, VIP C Sh. 15,000, VIP B Sh. 20,000, na VIP A Sh 30,000.

Muro amesema tiketi zitaanza kuuzwa Jumamosi Saa 2:00 asubuhi katika vituo vya Karume (Ofisi za TFF), Mgahawa wa Steers (Posta Mpya), Oilcom (Buguruni), BigBon (Kariakoo), Olicom (Ubungo), Dar Live (Mbagala), Uwanja wa Uhuru, Kivukoni (Ferry) na Makumbusho (kituo cha mabasi).
Aidha, amesema magari yenye vibali maalum ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia ndani ya Uwanja siku ya Jumapili.
Yanga SC imefika hatua hii baada ya kuitoa BDF XI ya Botswana, wakati Platinum iliing’oa Sofapaka ya Kenya.
Wakati huo huo: Kikosi cha Platinum kilichotarajiwa kuwasili Saa 2:00 usiku wa leo, hakijawasili na wenyeji wao, Yanga SC wameshangaa kwa sababu hawana taarifa nyingine.
“Sasa hatujui tunafanya nini, walituambia watafika Saa 2:00 usiku, lakini tumefika mapema sana kuwasubiri, hawajafika na hatuna taarifa nyingine,”amesema Muro.
Kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) timu mgeni itajigharimia gharama za malazi ugenini, lakini mwenyeji atawajibika kuwagharamia usafiri wa ndani.

MATUMLA JR KUPIGANA NA MCHINA MACHI 27, AKISHINDA ATAPANDA ULINGO MMOJA NA MAYWEATHER, PACQUIAO MEI 2 LAS VEGAS

Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
BONDIA Mohamed Matumla anatarajiwa kupanda ulingoni Machi 27, mwaka huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam kupigana na Wang Xin Hua wa China.
Hilo litakuwa pambano la uzito wa Super Bantam, kuwania nafasi ya kugombea taji la dunia la WBF, Mei 2, mwaka huu mjini Las Vegas, Marekani siku ambayo Manny Pacquiao wa Ufilipino atapigana na Mmarekani Floyd Mayweather Jr.
Yaani mshindi wa pambano kati ya Matumla Jr na Xin Hua atapata tiketi ya kwenda kupigana katika pambano la utangulizi la Mayweather na Pacquiao Mei 2, Marekani. 

Pambano hilo litatanguliwa na mapambano kadhaa mengine, yenye mvuto, likiwemo kati ya Ashraf Suleiman wa Tanzania dhidi ya Mmarekani, Joseph Rabotte uzito wa juu taji la International WBF.
Mabondia wa Tanzania, Karama Nyilawila na Thomas Mashali watachapana katika pambano la uzito wa Super Middle kuwania taji la WBF Intercontinental, wakati Japhet Kaseba na Maada Maudo watachapana katika uzito wa Light Heavy kuwania ubingwa wa Taifa.    

OKWI AELEZA ALIVYOCHUKUA UAMUZI WA KUFUNGA BAO DHIDI YA BARTHEZ

Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi amesema alikuwa na asilimia nyingi kuwa mpira alioupiga langoni mwa Yanga ungeingia.

“Wakati nakimbia na mpira, niliona kipa akiwa amesogea juu kidogo. Kwa hesabu za haraka niliamini mpira ule ungeweza kuingia wavuni.
“Nilijua nitafunga, suala la kulenga ndiyo lilikuwa muhimu na nikafanya hivyo,” alisema Okwi.

Okwi raia wa Uganda, alifunga bao pekee lililoiwezesha Simba kuishinda Yanga kwa bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, Jumapili.

TANZANIA YAPAA FIFA KWA NAFASI SABA NA KUSHIKA NAFASI YA 100


Tanzania imepaa na kushika nafasi ya 100 katika viwango vya Ubora vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).


Tanzania imepanda hadi nafasi ya 100 baada ya kupanda nafasi saba mfululizo.

Wakati Tanzania iepanda nafasi hizo na kushika nafasi ya 100, Rwanda imezidi kupaa kwa kushika nafasi ya 64 baada ya kupanda nafasi nane.

Uganda nayo imepanda nafasi mbili na kushika nafasi ya 74 huku Kenya ikiendelea kusuasua katika nafasi ya 118.

NEW VIDEO: LINEX FT DIAMOND - SALIMA ITAZAME HAPA

Linex kwenye kolabo hii amesema kuwa haikuwa imepangwa yaani ni miongoni mwa kolabo ambazo yeye na Diamond haikupangwa,Diamond aliukuta wimbo studio akaupenda akamfahamisha Linex wakaamua kufanya kwa pamoja singo inaitwa Salima,hii ni singo ya pili kwa Linex kufanya na Diamond baada ya ile ya kwanza iliyoitwa Nitaificha wapi.
                    Bonyeza play kutazama wimbo huu.

ALEX FERGUSON KUTOA KITABU KINGINE TENA

Kocha mstaafu, Alex Ferguson yuko katika hatua za mwisho kutoa kitabu kingine.

Taarifa zimeeleza kitabu hicho zaidi kitalalia katika suala la ufundi uwanjani na nini alichofanya akiwa kocha.

Tayari wachambuzi wa soka Ulaya wameishaanza kusema kuwa kitabu hicho huenda kitakuwa msaada mkubwa kwa kocha wa sasa wa Man United, Louis van Gaal.

TENGA APIGA BAO ‘LAINIII’ CAF, MPINZANI WAKE AJIONDOA MWENYEWE UCHAGUZI WA APRILI 7

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
NAHODHA wa zamani wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Leodegar Chillah Tenga (pichani kulia) amepiga hatua moja mbele katika kuelekea kutetea nafasi yake ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Hiyo inafuatia aliyekuwa mpinzani wake, Rais wa Shirikisho la Soka Djibouti (DFF), Suleiman Hassan Waberi kujitoa kuwania nafasi hiyo.
Waberia ameandika barua ya kujitoa kwenye orodha ya wawania nafasi za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF kutoka Afrika Mashariki na Kati na sasa jina la Tenga pekee, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Vyama Vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), litakwenda Cairo.
Katika barua yake, Waberi amesema amefikia hatua hiyo baada ya kupokea ushauri kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa CECAFA wakimtaka amuachie Tenga nafasi hiyo.    
Mkutano Mkuu wa 37 wa mwaka wa CAF unatarajiwa kufanyika Jumanne ya Aprili 7, mwaka huu katika ukumbi wa Marriot uliopo ndani ya hoteli ya Zamalek mjini Cairo, Misri kuanzia Saa 3: 30 asubuhi.
Barua ya Waberi kujitoa uchaguzi wa CAF

PICHA: JUX AKISHOOT VIDEO YAKE MPYA

4X7A9979
‘Sisikii’ ni jina la wimbo ambao unafanya vizuri kwenye radio na TV pia, wimbo huo video yake yote ilifanywa China, ndani yake alionekana pia video queen msanii wa Bongo Fleva Vanessa Mdee.. Jux karudi tena location, safari hii kazi haijafanyika China tena na wala sio nje ya Bongo, mzigo unafanyika hapa Tz, walikuwa zao kwenye fukwe za bahari ya Hindi Dar es Salaam wakishoot video ya wimbo mpya wa staa huyo.
Wimbo unaitwa ‘Nikuite Nani’, tayari kazi ya kuandaa video imeanza muda wowote ikiwa tayari tutaiona, hapa nimekuwekea behind the scenes baadhi ya pichaz.. Vee Money ameonekana yuko nae kwa pembeni akicheki Jux na team ya Hanscana wakirekodi video hiyo ufukweni.
4X7A0007 2
4X7A0087
4X7A0171

Kingine nilichokishuhudia ni kwamba video iko simple kabisa yani, hakuna magari ya kifahari wala majumba yaliyotumiwa kushoot, muda mwingi picha za video zimerekodiwa wako zao tu ufukweni.
4X7A0201
4X7A0262
4X7A9865 2
4X7A9866 2
4X7A9870 2
4X7A9905
4X7A9965
4X7A9967 2
4X7A9979
440A8238 2

KITAMBI KOCHA MPYA AZAM FC

AZAM FC imemuajiri Dennis Kitambi (pichani kushoto), kuwa Kocha Msaidizi wa klabu hiyo bingwa Tanzania, chini ya Mganda, George ‘Best’ Nsimbe.
Kitambi aliyekuwa kocha wa Ndanda FC kabla ya kutimuliwa baada ya mechi tano msimu huu, ameanza kazi rasmi leo asubuhi.
Mwalimu huyo, mwenye leseni B ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) alishiriki kikamilifu programu ya mazoezi leo asubuhi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Tangu ameondoka Ndanda FC, Kitambi amekuwa mchambuzi wa soka katika Televisheni ya Azam FC ni uchambuzi wake kuhusu michezo na wachezaji uliowavutia mabosi wa klabu hiyo na kumuajiri.
Kitambi anaajiriwa Azam FC kiasi cha wiki mbili tangu kuondolewa kwa Mcameroon, Joseph Marius Omog na Msaidizi wake namba mbili, Mkenya Ibrahim Shikanda.

BAYERN MUNICH YAIADHIBU SHAKHTAR DONETSK 7-0


bayern-munich-celebration_3275483Na. Richard Bakana
Mabingwa watetezi wa klabu Bingwa barani Ulaya, Klabu ya Bayern Munich  usiku huu wamefanikiwa kusonga mbele katika michuano hiyo baada ya kuwafumua Shakhtar Donetsk kwa jumla ya mabao 7-0.
Mabao ya Bayern Munich yametupiwa kambani na Müller  katika Dakika ya 4 kwa mkwaju wa penati ikiwa ni bao la kwanza kabla ya dakika ya  51 ya mchezo huo kuiandikia timu yake bao la nne.
Naye Boateng aliiandikia timu yake bao la pili katika dakika ya 34, Ribéry akifunga goli la tatu katika dakika ya 49, Badstuber  alifunga bao la tano katika Dakika ya 63, Lewandowski akitupia la sita kunako dakika ya 75 kabla ya Götze kumaliza kazi kwa kufunga bao la saba katika dakika ya 87.
Hadi mwamuzi anapuliza kipenga cha mwisho Bayern Munich wamefanikiwa kuondoka kifua mbele kwa jumla ya mabao 7-0.
Kwa matokeo hayo sasa Wajermani hao wanakuwa wametinga katika hatua ya Robo fainali ya Klabu bingwa Ulaya kwa ushindi huo mnono.Thomas MullerThomas Muller akifunga bao lake usiku huu.

CHELSEA YAONDOLEWA UEFA NA PSG PUNGUFU

zlatan 1Na. Richard Bakana
Vinara wa ligi kuu ya England, Chelsea leo usiku wamejikuta wakiambulia majonzi baada ya kutolewa katika michuano ya klabu Bingwa barani Ulaya na Wapinzani PSG huku wakiwa mbele ya mashabiki wao kunano Uwanja wa Stamford Bridge  baada ya kulazimishwa sare ya 2-2.
Licha ya PSG kucheza wakiwa pungufu kwa kipindi kirefu kufatia Nyota wake Zlatan Ibrahimovic kupewa kandi nyekundi ya moja kwa moja baada ya kumfanyia madhambi Oscar katika dakika ya 32 kipindi cha kwanza, hawakuweza kuvunjika Moyo zaidi waliongeza nguvu na kusaka ushindi hatimaye sasa Wametinga hatua ya Robo fainali ya michuano hiyo mikubwa barani Ulaya kwa ngazi ya Vilabu.hazard  2
Chelsea ndio walianza kupata bao kupitia kwa Gary Cahill kunako dakika ya 80 kipindi cha pili kufatia kona iliyopigwa na mabeki wa PSG wakashindwa kuosha mbele ndipo mchezaji huyo akafumua shuti ambalo lilitinga kambani, Bila kukata tamaa Wafaransa hao (PSG) walikomaa na kujipatia bao la kusawazisha katika dakika ya 85 kupitia kwa David Luiz, ambapo hadi dakika 90 zinamalizika Chelsea ilikuwa imebanwa mbavu na PSG kwa kukubali sare ya 1-1.
Kama kawaida ziliongezwa dakika 30 ili kupatikana mbabe wa mchezo, Thiago Silva beki wa PSG  akanawa mpira katika eneo la 18 na muamuzi akawazawadia Chelsea Penati ambayo ilipigwa na Eden Hazard na kuipatia timu yake bao la 2 ikiwa ni dakia ya 95.silva 2
Lakini wahenga walisema kuwa “Siku ya kufa nyani miti yote huteleza” Thiago Silva akisawazisha makosa yaliyoipatia Chelsea bao la pili, Akawakata maini mashabiki na wapenzi wa The Blues baada ya kupiga kichwa safi kufatia mpira wa kona na kuiandikia PSG bao la kusawazisha ikiwa ni dakika ya 114 na kufanya kibao kisomeke 2-2.
Kufatia mchezo wa awali wa Februari 17 uliopigwa Ufaransa na timu hizo kutoka sare ya 1-1 sasa PSG wanakuwa wamesonga mbele katika hatua ya Robo fainali baada ya kutoka 3-3 na Chelsea.silvazlatan 2Chelsea v Paris St Germain (PSG), UEFA Champions League Round of 16 Football, Stamford Bridge, London, Britain - 11 Mar 2015

HIZI NDIO KURASA ZA MWANZO NA ZA MWISHO ZA MAGAZETI YA MICHEZO LEO MARCH 12

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.