
Kocha
wa Arsenal Arsene Wenger amekiri kwamba kutojua kizungu kwa beki mpya
wa timu hiyo Gabriel Paulista huenda kukaifanya timu hiyo kufungwa
mabao.
Beki huyo kutoka Brazil atashirikishwa katika mechi dhidi
ya Aston Villa siku ya jumapili baada ya kusajiliwa kutoka Villareal kwa
kitita cha pauni millioni 11.2.''Kwa sasa haongei hata neno moja la kizungu,na hiyo inaweza kukufanya ufungwe mabao ''alisema Wenger.

Kocha huyo pia amesema kuwa mchezaji Francis Coquelin anakaribia kuandikisha mktaba mpya ,lakini nahodha Mikel Arteta bado hajakubali kutia sahihi kandarasi mpya.
0 maoni:
Post a Comment