Jul 14, 2016

MHISPANIA WA AZAM FC ATAJA TOFAUTI YA MAKIPA WA HISPANIA NA TANZANIA

Na Haji Balou
KOCHA Mkuu wa makipa wa Klabu
Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam
FC, Jose Garcia, amesema kuwa makipa
aliowakuta ndani ya timu hiyo wapo
vizuri.

Kocha huyo hakusita kuelezea utofauti
wa makipa kutoka Tanzania na Hispania
mara baada ya kuwaona wa Azam FC,
ambapo alisema magolikipa wa hapa
wana nguvu sana lakini wanakosa mbinu.

“Watanzania wana nguvu sana, ila
wanakosa mbinu, lakini kwa upande wa
kule Hispania wako vizuri zaidi na
wanazo mbinu, na hicho ambacho
nimeongea na wenzangu ili tuweze
kukifanyia kazi,” alimalizia kocha huyo
mwenye umbile kubwa na mrefu
atayesaidiana majukumu hayo na Idd
Abubakar.

Ukiondoa makipa wa Azam FC, Aishi
Manula, Mwadini Ally na Metacha Mnata
aliyepandishwa kutoka timu ya vijana na
Kauju Agustino wa Azam B wanaendelea
kufanya maandalizi ya msimu mpya, kuna
makipa wengine wawili wa kigeni
wanawania nafasi moja ya kusajiliwa,
Daniel Yeboah (Ivory Coast) na Juan
Jesus Gonzalez (Hispania).

CHANZO WWW.AZAMFC.COM

0 maoni:

Post a Comment