Sep 1, 2016

KIUNGO MTANZANIA APATA TIMU AFRIKA KUSINI

Na Haji balou
KIUNGO wa zamani wa
Simba SC na Azam FC,
Abdulhalim Humud ‘Gaucho’
amejiunga na klabu ya Real
Kings FC ya Ligi Daraja la
Kwanza Afrika Kusini.

Humud ambaye msimu
uliopita alichezea Coastal
Union ya Tanga iliyoshuka
daraja kutoka Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara,
amesaini mkataba wa
mwaka mmoja kujiunga na
timu ya Durban, Kwazulu-
Natal.

Real Kings walipanda Ligi
Daraja la Kwanza mwaka
huu na wakafanikiwa kufika
fainali ya ligi ya ABC
Motsepe League.

Wakala aliyefanikisha
Humud kusaini Real Kings,
amesema leo kwa simu
kutoka Durban kwamba ana
matumaini mchezaji huyo
atafanya vizuri Afrika
Kusini.

0 maoni:

Post a Comment