Beki wa klabu ya Sporting Lekeren
ya nchini Ubeligiji,Gregory Mertens amefariki dunia leo siku tatu tangu
aanguke uwanjani wakati akikichezea kikosi cha akiba cha timu hiyo
dhidi ya Genk.
Mchezaji huyo aliyewahi kuiwakilisha ubelgiji katika timu chini ya miaka 21,alianguka kufuatia kusumbuliwa na matatizo ya moyo.
Beki huyo ,24, alianguka uwanjani
dakika 15 baada ya mechi hiyo kuanza na hivyo kupatiwa huduma ya kwanza
kabla ya kukimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi .
Msemaji wa Lokeren Herman Van De
Putte amesema kuwa ,hili ni pigo kwa wachezaji,familia yake, mashabiki
na familia ya soka kwa ujumla
Taarifa kutoka katika klabu hiyo
inasema ” Licha ya matibabu mazuri yaliyotolewa na madaktari wa
timu,madaktari wa hospitali lakini ilionekana hali ilizidi kuwa mbaya
zaidi “
Wachezaji mbalimbali ,Romeu
Lukaku,Fabrice Muamba,Jelle Vossen na wengine wengi wameandika katika
akaunti zao za twita,instagram ujumbe wa kumuombea mchezaji huyo kwa
mungu.
0 maoni:
Post a Comment