TFF imeamka sasa baada ya kuamua kumfungia kitasa wa Mbeya City, Juma Said Nyosso.
Nyosso atakaa nje kwa mechi nane kwa kosa la kumdhalilisha mshambuliaji wa Simba SC, Elius Maguri timu hizo zilipokutana
Januari 28, mwaka huu.
Pamoja na Nyosso, beki wa Azam FC, Aggrey Morris
naye amefungiwa mechi tatu kutokana na lile sakata la kumpiga kiwiko mshambuliaji Emmanuel Okwi wa Simba.
Morris
amefungiwa mechi tatu baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga kwa makusudi
kisukusuku mshambuliaji wa SImba SC, Emmnauel Okwi timu hizo zilipokutana
Januari 25, mwaka huu.
Okwi
alipoteza fahamu baada ya kupigwa na Aggrey na kulazimika kukimbizwa hospitali
ya Rufaa ya Taifa, Muhimbili, Dar es Salaam kwa matibabu zaidi na taarifa za
Madaktari zilisema Mganda huyo angeweza kupoteza uhai siku hiyo kama si
kuwahiwa kwa huduma ya kwanza.
Mechi
zote hizo zilifanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba SC ikitoa sare ya
1-1 na Azam FC kabla ya kufungwa 2-1 na Mbeya City.
Katika
kikao chake cha awali, Februari 3, mwaka huu Kamati hiyo ya Nidhamu ilitoa
adhabu kwa watu tisa wakiwemo viongozi, wachezaji na kocha mmoja kwa kupatikana
na hatia ya makosa ya kinidhamu.
Okwi
alilazimika kukimbizwa hospitali baada ya kuanguka na kupoteza fahamu
na baadaye mikanda ya Azam TV ilionyesha Morris akimpiga.
Kwa
upande wa Nyosso, amebainika amefanya hivyo baada ya picha zilizopigwa
na gazeti namba moja la michezo nchini kumnasa akifanya vitendo hivyo
vya kipuuzi.
Lakini
tayari Nyosso ameomba msamaha kwa Maguri na Blog hii ilizungumza na
wote wawili lakini Maguri akasisitiza nanachotaka ni sheria kufuata
mkondo wake.
0 maoni:
Post a Comment