May 7, 2015

MESSI AMFANYA KITU MBAYA GUARDIOLA CAMP NOU, APIGA MBILI BARCA IKIILAZA 3-0 BAYERN

BARCELONA imeanza vyema Nusu Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Bayern Munich, Uwanja wa Camp Nou nchini Hispania.

Lionel Messi akiruka juu kushangilia baada ya kuifungia Barcelona katika ushindi wa 3-0 usiku huu Uwanja wa Camp Nou
Bayern Munich sasa watatakiwa kushinda 4-0 katika mchezo wa marudiano Allinz Arena ili kutinga Fainali ambako watacheza na mshindi wa jumla kati ya Real Madird, mabingwa watetezi na Juventus. 
Lionel Messi alionyesha kiwango cha hali ya juu na kufunga mabao mawili katika mchezo huo, la kwanza dakika ya 77 na la pili dakika tatu baadaye. 
Neymar akafunga bao la tatu dakika 90 na kumtoa kinyonge Uwanja wa Camp Nou kocha wa zamani wa Barca, Pep Guardiola.
Kikosi cha Barcelona kilikuwa; Ter Stegen, Alves, Pique, Mascherano/Bartra dk89, Alba, Busquets, Iniesta/Rafinha dk87, Rakitic/Xavi dk82, Neymar, Messi na Suarez.
Bayern Munich; Neuer, Rafinha, Boateng, Benatia, Bernat, Lahm, Schweinsteiger, Alonso, Thiago, Muller/Gotze dk79 na Lewandowski.

0 maoni:

Post a Comment