KIUNGO wa zamani wa klabu ya Manchester United, Paul Scholes (pichani)
amesema kuwa timu hiyo inaonekana kucheza katika kiwango cha chini kwa
msimu huu kuliko msimu uliopita licha ya kuwa kocha Louis Van Gaal
ametumia kiasi kikubwa katika kufanya usajili.
Kiungo huyo ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka katika kituo kimoja cha televisheni huko nchini Uingereza amesema kuwa kocha huyo mholanzi anaonekana kuridhika na kufurahishwa kwa timu yake kushika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi nchini humo.
Scholes ambaye alitundika daruga mwaka 2013 baada kucheza kwa muda mrefu aliyasema hayo jana mara baada ya Manchester United kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Newcastle United huku pia akionekana kutoridhishwa na aina ya ufundishaji ya kocha Louis Van Gaal.
"Anaonekana anafuraha kushika nafasi ya nne lakini timu hii inahitaji kuwepo katika mbio za ubingwa kwa sababu ametumia paundi milioni 150 katika usajili " alisema Scholes.
Aidha Scholes amesema kuwa haipaswi kumlaumu sana kocha huyo kwa msimu huu kwani ndiyo msimu wa kwanza lakini kwa msimu ujao inabidi awaridhishe mashabiki wa timu hiyo ambao wamekuwa wanyonge tangu Sir Alex Ferguson astaafu mwaka 2013.

0 maoni:
Post a Comment