Mar 7, 2015

KOPUNOVIC: MBINU ZA PLUIJM ZIPO KWENYE KIGANJA CHA MKONO WANGU

Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
SIMBA SC ipo Zanzibar wakati wowote kuanzia leo usiku inaweza kurejea tayari kwa mchezo wao dhidi ya Yanga lakini kocha wao Goran Kopunovic ametamka kwamba hana wasiwasi na mbinu za mwenzake wa Yanga Hans Pluijm.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY, Kopunovic raia wa Serbia amesema wamefanya maandalizi ya nguvu kuelekea mchezo huo ambapo kwake hana wasiwasi na mbinu za kiufundi za Pluijm kwa kuwa dawa anayo.
Kopunovic amesema wataingia katika mchezo kwa kucheza mpira kwa staili yao waliyojiandaa katika kambi yao ya Zanzibar ambayo timu hiyo imekuwa ikijifua katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Chukwani visiwani humo.
Kocha wa Simba SC, Goran Kopunovic amesema mbinu za mpinzani wake, Hans van der Pluijm anazijua

"Hii ni mechi kubwa hapa Afrika,najua kwamba kutakuwa na presha tofauti katika mchezo huu lakini hakuna kingine tunachotaka zaidi ya kutaka kuona ushindi,"amesema Kopunovic.
"Naijua Yanga,najua mbinu za kocha wao Mholanzi,tunawaheshimu lakini tunamalengo na pointi tatu za mchezo huo tutacheza soka letu litakalotipatia ushindi.

0 maoni:

Post a Comment