MSHAMBULIAJI
wa Newcastle United, Papiss Cisse amefungiwa mechi saba kwa kuhusika
kutemeana mate na beki wa Manchester United, Jonny Evans.
Evans
kwa upande wake, anaweza kufungiwa mechi sita kama atakutwa na hatia
baada ya Chama cha Soka England kuwafungulia mashitaka wote wawili.
Tukio
hilo liitokea Jumatano usiku wakati Man United ikishinda 1-0 dhidi ya
Newcastle katika mchezo wa Ligi Kuu ya England. Hatima ya Evans
inatarajiwa kutolewa leo na FA ya England, uwezekano mkubwa ukiwa ni
kufungiwa mechi sita.
Evans (kushoto) na Cisse wakigombana katika mchezo huo Uwanja wa St James' Park
0 maoni:
Post a Comment